Tuesday, 18 March 2014

MAWAZIRI WASITOKANE NA WABUNGE





Mwenyekiti aw Tume ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba ameliambia bunge Maalum la Katiba linaloendelea mkoani Dodoma kuwa Rasimu ya Katiba mpya inapendekeza Mawaziri wasitokane na wabunge.

Amesema hatua hii inamuondoa Rais kwenye bunge kwani kwa kuwa na Mawaziri ndani ya bunge Hilo kunalifanya bunge kushindwa kuisimamia serikali ipasavyo kwa kuwa serikali ni sehemu ya bunge Hilo.
Amesema Mawaziri watateuliwa na na Rais NA kuthibitishwa na bunge . Aidha , rasimu ya Katiba inapendekeza kuwa Rais achaguliwe kwa kupata kura zaidi ya asilimia 50 ya kura zote .

Rais Mara baada ya uchaguzi na kutangazwa na Tume ya uchaguzi anaweza kufikishwa mahakama ya rufaa kuhoji uhalali wake na mgombea yeyote wa kiti hicho aliyeshindwa na Shauri hilo kuamuliwa ndani ya mwezi mmoja.

Jaji Warioba amesema Rasimu ya Katiba inapendekeza kuwepo NA ukomo wa wabunge wa miaka 15 ya kukalia kiti hicho mfululizo ili kuondoa dhana ya umiliki wa ubunge na kuimarisha uwajibikaji.

Hakutakuwepo na uchaguzi mdogo endapo Mbunge atafariki badala yake nafasi hiyo itazibwa na jina litakalokuwa kwenye orodha zilizoandaliwa NA vyama vya siasa vyenye wabunge husika na kuwasilishwa kwa Tume ya Uchaguzi.
Aidha, Spika na Naibu Spika hawatatokana na Mawaziri, Naibu Waziri NA wabunge ili kupata viongozi ambao hawataelemea upande wowote.

Monday, 17 March 2014

MAKONDA WASIO-OGA NA KUNUKA KWA KUTOA HARUFU ,WAOGESHWA KWA LAZIMA HADHARANI ..JIONEE HAPA


Hii unaambiwa imetokea Kisumu Ndogo, Donholm nchini Kenya Ijumaa iliyopita. Makonda hao walilazimishwa kuoga hadharani kwa   kile kinachaodaiwa   kuwa  walikuwa  wananuka. Wateja wamekuwa wakilalamika kwamba makonda hawa
wananuka na hivyo kuathiri biashara. Makonda hao waliogeshwa huku wadau wakishushudia na kuhakishiwa usafi kwa makonda itakuwa ni swala la lazima.

Sunday, 16 March 2014

CCM YAIBWAGA CHADEMA KALENGA,USHINDI WA ZAIDI YA ASILIMIA 70


Mashabiki wa CCM wakimbeba aliyekuwa mgombea wa CCM jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini Godfrey Mgimwa, baada ya kupata matokeo ya awali ya CCM kuongoza kata 11 kati ya kata zote13 katika matokeo ya awali yasiyo rasmi ya  uchaguzi uliofanyika leo. Shamrashamra hizo zilifanyika Ofisi ya CCM mkoa wa Iringa
Mashabiki wa CCM wakimwayamwaya kwa furaha baada ya kupata matokeo hayo ya awali

BASI LA YANGA LAPATA AJALI LEO ASUBUHI MAENEO YA MIKESE MOROGORO



Kocha wa Yanga  HANS VAN PLUIJM (kulia), akifanya mawasiliano baada ya basi la timu yake kupata ajali eneo la Mikese. Kushoto ni Kocha wa Makipa, Juma Pondamali.
Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga kimepata msukosuko baada ya basi lao kutumbukia msingini katika eneo la Mikese mkoani Morogoro.
Basi hilo limepata ajali leo asubuhi wakati kikosi hicho kikiwa safarini kurejea jijini Dar, baada ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar uliopigwa jana jioni kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini humo, na kutoka sare ya bila kufungana.
Taarifa zinasema hakukua na majeruhi lakini baadhi ya wachezaji walilazimika kujiokoa baada ya basi hilo kulikwepa basi jingine ambalo lilikuwa linalifuata hilo la Yanga.

Friday, 14 March 2014

SHIDA HAINA MWENYEWE, MALAYSIA YATUMIA WAGANGA WA JADI KUTAFUTA NDEGE ILIYOPOTEA



https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjCyu4OncJGxkOo_n-ny9PzS-D6H9aUB9uGj2HU3zkm9Iem6vipwHqgkALBCsh7smKXlY-RKvj5YTLYB7obHe_B9V6DckF-5yKQNNllB2TzxG9-SKTkv49h9Yg2lkeB81ygIe2HbNKoDug/s1600/malysia.pngWakati ambapo China imepeleka angani satellite 10 kuitafuta ndege ya Malaysia Airlines iliyopotea, serikali ya Malaysia imewaomba waganga wa kienyeji kusaidia zoezi hilo.
Mganga maarufu nchini humo Ibrahim Mat Zin anayejulikana kama ‘Raja Bomoh Sedunia Nujum VIP’ alifanya tambiko kwenye uwanja wa ndege Kuala
Lumpur Jumatatu hii kusaidia kuitafuta ndege hiyo ya MH370. Anadaiwa kuitwa na viongozi wa juu wa serikali.

“Nadhani ndege bado ipo angani ama ilianguka baharini,” alisema Ibrahim Mat Zin. 

Thursday, 13 March 2014

SAMIA SULUHU HASSAN ACHAGULIWA KUWA MAKAMU MWENYEKITI WA BUNGE MAALUMU LA KATIBA


 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Samia Suluhu Hassan akitoa shukrani zake kwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba baada ya Kuteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo.
 Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samia Suluhu Hassan akimkumbatia Mwenyekiti wa Bunge Hilo Samwel Sitta Leo Mjini Dodoma.
 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Mwenyekiti Mteule wa Bunge hilo Bw. Samwel Sitta akibadilishana Mawazo na Mjumbe wa Bunge Hilo Mohamed Seif Khatib ndani ya Ukumbi wa Bunge leo Mjini Dodoma.
 Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Thomas Kashilila akieleza wajumbe juu ya utaratibu wa upigaji kura kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti leo Mjini Dodoma.
 Mgombea wa Nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la katiba Bi. Amina Abdallah akinadi Sera zake  kwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba.
 Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la katiba wakibadilishana Mawazo na Mwenyekiti wa Bunge Hilo Samwel Sitta(Aliyekaa).Leo mjini Dodoma.
Mgombea wa Nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la katiba Bi. Amina Abdallah akimpongeza Bi. Samia Suluhu Hassan baada ya Kutangazwa kuwa Makamu mweyekiti wa Bunge Maalum la Katiba. 

SITA AIBUKA KIDEDEA KWA KURA 487 KATIKA UCHAGUZI WA MWENYEKITI WA KUDUMU BUNGE LA KATIBA


 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na aliyekuwa Mgombe katika nafasi ya Uenyekiti Bw. Samwel Sitta akinadi Sera zake kwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kabla ya zoezi la Upigaji kura kwa nafasi hiyo Leo Mjini Dodoma.
 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na aliyekuwa Mgombe katika nafasi ya Uenyekiti Bw. Hashim Rungwe akinadi Sera zake kwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kabla ya zoezi la Upigaji kura kwa nafasi hiyo Leo Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Edward Lowasa akiweka karatasi ya Kura yake ya Kumchagua Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba leo Mjini Dodoma 
Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Wakipiga Kura Kwa ajili ya Nafasi Ya Mwenyekiti wa Bunge Hilo Iliyokuwa Ikiwaniwa na Bw. Edward Lowasa na Bw. Hashim Rungwe leo Mjini Dodoma.
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba,ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Urambo Mashariki, Mh Samwel Sitta ameibuka kinara kwenye nafasi aliyowania ya kuwa Mwenyekiti wa kudumu wa Bunge Maalum la Katiba, baada kumbwaga mpinzani wake,Wakili wa Kujitengemea, Hashim Rungwe. 

Sitta ameibuka kinara na kuichukua nafasi hiyo ya kuwa Mwenyekiti wa Kudumu wa Bunge hilo Maalum katika kinyang'anyiro cha uchaguzi huo uliofanyika leo jioni mjini Dodoma.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Muda, Mh Ameir Pandu Kificho, amekabidhi madaraka hayo kwa mwenyekiti mpya Samuel Sitta baada ya kumaliza rasmi muda wake wa kuliendesha bunge hilo leo. 

Jumla ya Kura zilizopigwa ni 563 na zilizoharibika ni 7,kufuatia idadi hiyo ya Kura Ndugu Hashim Rungwe amepata kura 69 na Mh.Samwel Sitta ameibuka na kura 487,kwa Matokeo hayo imetangazwa kuwa Mh.Samwel Sitta ndiye mshindi wa kuanza kupambana na misukosuko ya bunge hilo ambalo kwa sasa litaanza kuendeshwa kwa kanuni.
 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Stephen Wasira akiwa na Mjumbe mwenzie wakielekea katika ukumbi wa Bunge kwa Ajili ya Upigaji kura YA Nafasi Mwenyekiti Leo Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Augustino Mrema akiwa na moja ya mjumbe wa bunge hilo wakielekea katika ukumbi wa Bunge kwa Ajili ya Upigaji kura YA Nafasi Mwenyekiti Leo Mjini Dodoma. 
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na aliyekuwa Mgombe katika nafasi ya Uenyekiti Bw. Samwel Sitta akiteta jambo na Mjumbe wa Bunge hilo ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Anna Tibaijuka wakati zoezi la upigaji kura likiendelea Leo Mjini Dodoma.

Wednesday, 12 March 2014

SITTA ACHUKUA FOMU KUWANIA UENYEKITI BUNGE LA KATIBA



Mgombea Uenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta akipokea Fomu kutoka kwa Ofisa wa Bunge Bi. Lidya Mwaipyana Katikati ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Mbunge wa Nzega Hamisi Kigwangala.
Mgombea Uenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta akionesha fomu ya uenyekiti aliyochukua leo Kushoto niMjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Mbunge wa Nzega Hamisi Kigwangala na Kulia ni Mjumbe wa Bunge hilo Bw. Paul Makonda.
Mgombea Uenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta akiongea na waandishi wa habari Mara baada ya Kuchukua fomu hizo na kuahidi kufanya kazi kwa Kasi naViwango.