Tuesday, 14 May 2013

CAMERA YETU BARABARA YA ARUSHA MANISPAA YA BUKOBA

Takribani miaka ya 2010-2012 barabara ya arusha ilikuwa maarufu kwa vibanda vya wauza kuku na maduka ya spea za baiskeli,Lakini ghafla mwishoni mwa mwaka 2012 kasi ya mabadiriko ya maduka na shughuli za kibiashara kushamili kwa muda mfupi na barabara hiyo kuonekana muda mwingi kuwa na msongamano wa watu na magari. Baada ya kutembelea sehemu mbalimbali za biashara hatukusita kuhoji baadhi ya wafanyabiashara ambao tumewakuta katika maeneo ambayo hapo siku za nyuma yalikuwa na makazi ya watu kuishi lakini sasa yanatumika kwa shughuli za kibiashara,mfanyabiashara mmoja aliejitambulisha kwa jina Miraji hussen alisema mapema mwezi wa kwanza mwaka huu 2013 wafanyabiashara wengi waliomo soko kuu bukoba walikuwa watoke kwa ajili ya ujenzi wa soko,hivyo wengi wao walifanya jitihada binafisi kutafuta maeneo ya kuamishia shughuli zao,ndo maana kwa ajili hiyo nyumba nyingi zilizokuwa maeneo ya barabara ya arusha wamiliki walizibadilisha na kuwa za biashara kwa hiyo ndio sababu kubwa ya mabadiliko, japo tunasikia kuwa mpango wa uvunjaji wa soko umesitishwa mpaka hapo badae,miraji husseni alisema.

Mitaa hii watu huja kutengeneza pikipiki na kunywa kahawa



Dada Lucy akiwa saloon,barabara ya Arusha




Duka la spea za baiskeli kwa ngugu Miraji Hussein

Ndugu Ramadhani anauza vifaa vya umeme

Kitambo dada huyu anafanya biashara barabara hii ya Arusha


Barabara ya Arusha hiko busy muda wote





Vibanda vya wauza kuku,hapa ndio soko kuu kwa bukoba ukihitaji kuku



Kitambo nyumba ya wageni ipo mitaa hii,wengi wenu mmepita hapa


Dada Jovensi ni mmoja wa waanzilishi wa maduka katika barabara ya Arusha

Amir Hamza ni wakala wa kusambaza sukari kutoka katika kiwanda cha sukari kagera,huduma hii imechangia kwa kiasi kikubwa barabara ya Arusha kuwa na msongamano wa magari wakati wakipakia sukari

ndugu Mwinyi akiwa kazini





Miaka ya 2011 katika barabara ya Arusha lilikuwepo duka la ndugu Abasi tu, leo yapo kibao

Maduka ya nguo za kike na kiume yapo mengi sana maeneo hayo





Nilikutana na huyu dada barabara ya Arusha nikiendelea na kazi, mtaa huko busy na magari saa zote



maeneo yote haya ya maduka,saloo yalikuwa makazi ya watu barabara ya Arusha





Manywele design duka jipya ,mwanzoni ilikuwa nyumba ya kuishi sasa ni duka





Takribani yapo maduka matano kwenye kwenye jengo hili, ni nyumba mama nyamwihura ilikuwa nyumba ya kuishi sasa ni maduka, barabara ya Arusha

Monday, 13 May 2013

USIKOSE REDD'S MISS MULEBA2013 ,WAISUKA 31-5-2013,DAYNA NYANGE ATATOA BURUDANI,WAR EMBO 12 WATACHUANA VIKALI NA WAREMBO 3 WATAINGIA KWENYE KINYANG'ANYIRO CHA REDD'S MISS KAGERA 2013

KARIBUNI SANA

BANDARI YA BUKOBA YAZIDI KUBORESHWA ILI KUTOA HUDUMA BORA KWA MTEJA

      Leo camera yetu ilitembelea bandari ya Bukoba na kukuta shughuli zikiendelea vizuri, na hali ya mazingira ikionekana katika hali ya usafi na kuvutia,viwanja vya bandari hiyo kwa sasa vimeboreshwa kwa kuwekewa sakafu ambayo imeondoa kabisa ile hali ya tope kipindi cha mvua na vumbi kipindi cha kiangazi,Lakini pia upo ujenzi wa mzani unaendelea 'mzani huu utakao kuwa ukipitisha gari iliyobeba mzigo na kuwezesha kutambua uzito wa mzigo kwa haraka zaidi.  Pia camera yetu ilienda eneo la meli ya victoria ilipotia nanga,shughuli za upakiaji mzigo ulikuwa ukiendelea vizuri,.


 Shughuli za upakiaji mizigo  zikiendelea katika bandari ya bukoba mjini

 Meli ya mv victoria ikiwa imetia nanga bandari ya bukoba,na shughuli za upakiaji mizigo zikiendelea
 Wafanyabiashara wa ndizi wakishusha ndizi bandari ya bukoba kwa ajili ya kupelekwa Mwanza


 Upakiaji mizigo melini hutumia craine ili kurahisisha upakiji kwa haraka na usalama zaidi wa mizigo na wabebaji mzigo

 baharia shomari akiwa kazini
 trector hutumika kuvuta tela  la mizigo kusogeza eneo la kupakia


 kapteni mwasa  wa victoria (kushoto) akiwa katika mazingira ya bandari ya bukoba akiangalia shughuli zinavyoendelea 

 Kijana Bunduki akiwa na  ndugu akida kwenye dirisha la tiketi


 Dada Akida akiendelea na kazi zake

 Ndizi mbivu zinazopelekwa mwanza kibiashara
 Mama mjasiriamali akisubiri kupakia ndizi zake mbivu kupeleka Mwanza
 Abiria wanaokwenda kwenda Mwanza wakikata tiketi dirishani

 ndugu Methew Mathias(passenger Argent) bandari ya bukoba

 Upimaji wa mizigo ukiendelea,mzani mkubwa unaojengwa kwa sasa utakapokamilika upimaji wa mizigo utakuwa rahisi zaidi


 Eneo la bandari ya bukoba linavyoonekana,tope na vumbi kwa sasa ni historia.

 Eneo la abiria kukaa na kusubiri kuingia melini limeboreshwa bandari ya bukoba
 abiria wakisubiri muda wa kuingia melini kuelekea mwanza
 Hapa ndio unajengwa mzani mkubwa bandari ya bukoba
 MZANI HUU UKIKAMILIKA UTARAHISISHA UPAKIAJI WA MIZIGO KIRAHISI
 ENEO LA GETI LA KUINGIA BANDARINI
TUNAIPONGEZA SERIKALI,WIZARA NA MAMLAKA YA BANDARI KWA KUBORESHA BANDARI YA BUKOBA ILI KUMUWEZESHA ABIRIA.MTEJA KUTUMIA HUDUMA ZA BANDARI YA BUKOBA. KWA HABARI ZA UHAKIKA ANGALIA jamcobk.blogspot.com