Mashindano ya mbio za Mitumbwi mkoa wa Kagera ya Kampuni
ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager
zimefanyika leo katika fukwe za Spice Hotel mjini Bukoba, washindi
kupatikana na kukabidhiwa vitita vya zawadi. Ambapo Fainali ya kanda
yatafanyika Jijini Mwanza mwezi ujao tarehe 7 december, 2013.

Huduma ya kutoa vifaa kwa ajili ya kujikinga ikiendelea kabla ya mashindano kuanza

Vijana
kazi wakianza kujiandaa kabla ya mtanange huo mkali wa kusaka washindi
wa kuwakilisha kwenye huko jijini Mwanza tarehe 7/12/2013

Mitumbwi ikishakaguliwa na hapa ni kuingia tu kuanza mashindano rasmi

Katika
kuchukua matukio ya bukobasports.com ilibidi na mimi nivae kama
mwanamshindano ili niweze kuchukua picha vizuri tayari kufukuzana na
mashindano hayo makubwa ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia
yake ya Balimi Extra Lager.

Kazi imeanza...

Ilichukua muda wa dakika kama 40 kwenda mpaka mwisho na kugeuza kurudi walipoanzia

Mgeni
rasmi RPC Kagera(katikati) ACP-Philip Kalangi (katikati), kulia ni
Mwenyekiti Makasia mkoa wa Kagera Bw. Faraji Mugaye na (kushoto) ni
Mwenyekiti Makasia Taifa Bw. Richard Mgabo

Mashindano yakiendelea pia kulikuwa na burudani safi zikiendelea hawa ni Vijana wa hapa Bukoba wanajulikana kwa jina la wasafi..

Kila mtumbwi ulitaka ushinde na kunyakua kitita

Burudani ikiendelea..

Wanawake nao walikuwepo kwenye mtanange huo mkali wao raundi yao walikuuwa na mitumbwi 12

Sehemu ya mwishoni lazima upite nje ya bendela hiyo nyeupe na kutafuta nyingine na kugeuka ulipotoka!

Wanawake wakiwajibika kutaka kupata ushindi hapa

Wanawake hao wakipiga Kasia kwa kwenda mbele!!

Wazungu nao walikuwepo kushuhudia mitanange hiyo

Ilikuwa ni patashika!!.

Jamal Kalumuna kulia akiwa na kiongozi

Mdau wa Michezo na Mwana Bukoba Veteran Bw. Ernest Nyambo nae alikuwepo

Wadau

Picha ya pamoja ya Wadau.

Sehemu ya meza kuu.

Bingwa mtetezi ni Kagera, Kombe la mwaka 2012 na sasa lilikabidhiwa kwa Mgeni rasmi

Washindi
wa Mwaka jana nao walikuwepo kushiriki mashindano hayo na bingwa
mtetezi alitoka mkoa huu wa Kagera wa mwaka jana 2012 hivyo mashindano
hayo yatakayo fanyika mwanza mwezi ujao tarehe 7 december nao watashiriki
mashindano hayo. Ambapo washindi wanne wamepatikana.

Wakikabidhi kombe la mwaka jana 2012 kwa Mgeni Rasmi RPC Kagera(katikati) ACP-Philip Kalangi

Wakati wa Zawadi

Wanawake walioshinda ni wale waliokuwa wanaongozwa na Levina Constantine na Salome Ernest.

Ushindi
mtamu: Mshindi wa kwanza kwa wanawake alipewa kitita cha Tsh:
700,000/= hapa ilibidi wacheze ngoma ya Saida Maana walifurahi sana.

Picha
ya pamoja ya washindi Wanawake na viongozi ambapo walioshinda ni
mtumbwi uliokuwa na mkuu wao Bi. Levina Costantine kutoka Bushasha
Bukoba Vijijini. Mshindi wa pili ni Bi. Salome Ernest kutoka Musila

Washindi wakionesha vitita vyao

Ushindi raha jamaniiii..

Picha ya pamoja washindi Wanaume na Viongozi,
Wanaume walioshinda ni Delius Kiiza, Eliud Prosper, Zaidock Kaiza,
Emmanuel Petro, Dastan Petro, Eliakim Zaidock, Nashow Bakuza, Frolence
Kiiza, Edwin John na Johansen Paulo wa Izigo Muleba.

Picha ya pamoja ya Viongozi.
Zawadi zilikuwa hivi:-
Mshindi wa kwanza kwa
Wanaume Wanawake
1- 900,000/= 700,000/=
2- 700,000/= 600,000/=
3- 500,000/= 400,000/=
4- 400,000/= 300,000/=
No comments:
Post a Comment