Tuesday, 28 May 2019

BW RAHIM KABYEMELA FUTURISHA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM,MKUU WA WILAYA BUKOBA AWAOMBA WADAU WENGINE KUSAIDIA.

 Bw Rahim Kabyemela Mkazi wa Manispaa ya Bukoba amefuturisha watoto wenye mahitaji maalum wa Shule ya Mugeza Viziwi,Shule Ya Msingi Mugeza Mseto yenye wanafunzi walemavu wa viungo,macho na Albino,Katika hafla hiyo mgeni rasmi Mh Mkuu wa Wilaya Bukoba Deodatus Kinawilo amewataka wadau wengine kuwa na moyo wa huruma kama  Ndugu Rahim kusaidia watoto wenye mahitaji maalum,viongozi mbalimbali wa dini,kisiasa na serikali walishiriki futari na watoto hao.























Thursday, 11 October 2018

CLUB YA WAFANYABIASHARA WA NMB BUKOBA WAKUTANA,UONGOZI WA JUU WA NMB WAAHIDI KUBORESHA ZAIDI HUDUMA.

 Club ya Wafanyabiashara wa NMB Bukoba wamekutana na uongozi wa juu wa NMB Benki katika Mkutano wao wa kawaida unaofanyika kila mwaka katika ukumbi wa ELCT Bukoba hotel.Katika mkutano huo  wanaclub ya Wafanyabiashara Bukoba walipata fursa ya kuongelea changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika biashara na kushauri baadhi ya mambo kufanyiwa marekebisho ili waweze kufanya biashara vizuri,Viongozi wandamizi wa NMB Benki walipta wsa wa kujibu changamoto mbalimbali zilizotoliwa na Club ya Wafanyabishara,Pia Mkurugenzi  wa Mikopo NMB Benki Bw Tom  Borghols aliwaomba wafanyabiashra kushauri nini kifanyike ili uongozi wa juu uweze kuona namna bora ya NMB Benki kutoa huduma bora kwa wateja wake.Mbali na mazungumzo yaliyofanyika, pia wana club ya wafanyabiashara wa Bukoba walipata mafunzo mbalimbali ya kukuza biashara .


 Mwenye kipza sauni ni Bw Donatuss Richard, Mkuu wa  Idara ya Biashara ndogo na kati akizungumza na Club ya Wafanyabiashara.
 Mfnyabiashara akieleza moja ya changamoto anazokutana nazo katika biashara.
 Bw Abraham Augustino Meneja wa Kanda ya ziwa  NMB Benki akizungumza.

 Bw Rama mfanyabiashara alietunukiwa cheti na NMB Benki kutambua namna anavyofuata taratibu za Benki.
 Mwenyekiti wa Club ya Wfanyabishara Bukoba Bw  Faustine Karugendo akiongea.

 Mkurugenzi wa  Mikopo NMB Bank PLC Bw Tom Borghols akizungumza na wanaclub Mkoa Kagera katika ukumbi wa ELCT Bukoba hotel.