Saturday, 9 June 2018

UZINDUZI WA PASIPOTI ZA KIELECTRONIKI MKOA WA KAGERA WAFANA.

 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustaph Kijuu amewataka watumishi wa Jeshi la Uhamiaji Mkoa wa Kagera kufanya kazi kwa weredi,uhaminifu na kujituma kuhudumia wananchi katika zoezi la utoaji wa pasipoti za kielectroniki,Akisoma hutuba kwa niaba yake katika uwanja wa Uhuru Bukoba Manispaa ,Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kagera  Mh Deodatus Kinawiro amewataka wananchi wanachi kujitokeza kwa  wingi na kuchangamkia huduma  hii ya pasipoti,huku akitaja faida mbalimbali za kuwa na pasipoti hii. kwa  mujibu wa idara ya Uhamiaji mpaka sasa tayari Jeshi la Uhamiaji limekwisha toa  jumla ya pasipoti 17,598 zikiwemo pasipoti za kawaida, Utumishi, Diplomasia na Diplomasia maalum tangu zoezi hili lilipozinduliwa Rasmi na  Januari 31 mwaka huu, na Mh Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli.(katika picha kushoto mgeni rasmi Kaimu Mkuu wa Mkoa Kagera Deodatus Kinawiro akimkabidhi  pasipoti  ya Kieletroniki Mwenyekiti wa CCM Bukoba Mjini Mh Joas Muganyizi  Zachwa.)
 Kamishna wa pasipoti na  Uraia   Gerlad Kihigi akisalimiana na wageni, wakiwemo viongozi wa dini katika hafla ya uzinduzi wa pasipoti za Kieletroniki.
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bkoba Chief Kalumuna akisalimiana na viongozi wa dini.
 Shekhe wa Mkoa wa Kagera Haruna Kichwabuta akifungua kwa Dua.
 Mwenyekiti wa ccm Bukoba Mjini Joas Muganyizi Zachwa akitoa salamu kwa niaba ya mwenyekiti wa Mkoa ccm.
 Kushoto Kamishna wa Pasipoti na Uraia Gerlad Kihiga akimkabidhi pasipoti ya Mkuu wa Mkoa Kagera iliyopokelewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa Deodatus Kinawiro.
 Baba ASKOF Rwoma akipokea pasipoti yake.
 Mzee Joseph Masabala akitoa neno kwa niaba ya wanachi waliofika katika hafla ya uzinduzi.
Kwa matukio mbalimbali ya kijamii ,burudani nk angalia blog yetu.

Thursday, 17 May 2018

WAZIRI JAFO AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA WODI YA MAMA NA MTOTO, ZAHANATI YA MARUKU BUKOBA VIJIJINI.

 Ilikuwa na shangwe , nderemo na vifijo katika kijiji cha Maruku Bukoba vijijini pale Waziri wa Nchi,ofisi ya Rais,tawala za Mikoa na Serikali za mitaa Selemani Said Jafo alipofika na kujumuika na wananchi na kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa wodi ya mama na mtoto katika Zahanati ya Maruku.(Katika picha kushoto ni Mkuu wa Mkoa Kagera Meja jenerali mstaafu Salum Kijuu,  Mbunge wa  Bukoba Vijijini Jason Rweikiza na Waziri wac Tamisemi Suleimani Said Jaffo.)
 Muonekano wa jengo la wodi ya mama na mtoto.
 Fundi akiendelea na kazi.
 Kazi ikiendelea.
 Bw Kamuntu Mc wa shughuli.
 Wananchi waliojitokeza kwenye hafla.
 Kamati ya maandalizi ikiweka mambo sawa.
 Waziri Jafo akiwasili eneo la tukio.
 Viongozi wa dini akifungua kwa sara na dua.
 Mh Mbunge wa jimbo la Bukoba  Vijijini Jason Rwaikeza.

Endelea kufuatilia jamcobukoba.blogspot.com.