Saturday, 28 October 2017

MVUA KUBWA NA UPEPO MKALI VYASABABISHA MAAFA MAKUBWA BUGANDIKA WILAYA MISSENYE BUKOBA.


Mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali imesababisha maafa makubwa ya nyumba kuezuka na mazao mbalimbali kuharibika mashambani  katika kata ya Bugandika wilaya ya Missenye Mkoa wa Kagera,Upepo mkali na Mvua zilizonyesha 28-10-2017 zimeacha vilio na hali ya masikitiko kwa baadhi ya familia katika kata ya Bugandika, Hali hii inatokea baada ya siku moja kutolewa taarifa kutoka Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania  kuwa vipindi vya mvua kubwa vinatarajiwa katika baadhi ya maeneo ya ukanda wa ziwa victoria na magharibi mwa nchi kwa mikoa ya  Mara , Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Geita, Kagera,Kigoma, Tabora, Katavi na Rukwa,na hali hii itatokea tarehe 28-10-2017 na 29-10-2017.
 
Ni vizuri kuchukua tahadhari kwa maeneo yaliyotajwa.

Thursday, 12 October 2017

CRDB BENKI BUKOBA WATAMBUA NA KUSHUKURU WATEJA WAO.

 Katika maadhimisho ya kilele cha wiki ya huduma kwa wateja, CRDB Benki tawi la Bukoba wameandaa hafla ya chaakula na mazungumzo na wateja wao , katika hotel ya Cofee iliyoko Bukoba Manispaa. Meneja wa tawi  Bw Sendwa wakati akiongea na wateja aliwashukuru wateja wote wa CRDB Benki kwa kuwawezesha kufanya kazi kwa faida na ndio maana wameona umuhimu wa kukutana nao na kuzungumza mafanikio na changamoto zinazowakabiri, ili wote kwa pamoja washirikiane na kusonga mbele.(katika picha , Meneja wa tawi akitambulisha wafanyakazi)
 Kushoto, mgeni rasmi akiwasili ukumbini.
 Katika burudani, live bendi ilihusika.
 Kulia ni Bw Alfred Ngatunga na Bw Rashid Shehe wafanyakazi wa CRDB Bukoba ngazi ya viongozi.
 Kulia Bw  Daniel Nyamuvugwa kutoka makao makuu CRDB na Bw  Manesa Mbaga Meneja Masoko CRDB Bukoba.
 Bw Manase Mbaga akiongea na wateja.
 Wafanyakazi wa  CRDB Bukoba.
 Utambulisho wafanyakazi wa CRDB
 Wateja wa CRDB


 Mgeni rasmi (kushoto) akifungua muziki)
 Wahenga utawajua tu, mambo ya twistiiiii
Kulia ni Meneja wa tawi akisakata rhumba na mgeni rasmi.