Friday, 27 January 2017

RAIS DK. MAGUFULI KUWA MGENI RASMI MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA NCHINI




Rais John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Sheria nchini zitakazofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao katika viwanja vya Mahakama jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Kaimu Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Hamis Juma amesema mahakama itawaelimisha wananchi jitihada mbalimbali ilizochukua zenye lengo la kuboresha huduma zake kupitia mpango mkakati wa miaka mitano inaoutekeleza katika kutoa haki kwa wakati na kuwezesha ukuaji wa uchumi.

Amesema kabla ya kilele cha maadhimisho hayo, mahakama itafanya matembezi maalum yatakayoongozwa na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi  na yataanzia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kuishia katika viwanja vya Mnazi mmoja.

Katika matembezi hayo Rais Mstaafu Mwinyi atazindua rasmi maadhimisho ya wiki ya elimu ya sheria ikiwa ni sehemu ya sherehe za kuelekea maadhimisho ya kilele cha siku ya sheria nchini.

Aidha ametoa rai kwa wananchi kutembelea sehemu zote zilizoandaliwa kwa ajili ya utoaji elimu ya sheria nchini kwa ajili ya kujifunza na kupata huduma mbalimbali za Kisheria.

Alizitaja huduma hizo ni pamoja na taratibu za ufunguaji mashauri katika ngazi mbalimbali za mahakama, taratibu za kesi za mirathi, taratibu za kesi za dhamana, taratibu za rufaa, ndoa na talaka, taratibu za kupokea na kushughulikia malalamiko na Msaada wa Kisheria.

Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini hufanyika kila mwaka mwanzoni mwa mwezi wa pili na mwaka huu yamebeba ujumbe wa Umuhimu wa Utoaji Haki kwa Wakati Kuwezesha Ukuaji wa Uchumi.

MWENYEKITI MSTAAFU WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI JAJI DAMIAN LUBUVA AKABIDHI TAARIFA YA UTENDAJI WAKE WA KAZI WA MIAKA 5 KWA MWENYEKITI WA SASA WA NEC JAJI WA RUFAA SEMISTOCLES KAIJAGE


 MAKABIDHIANO: Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kulia) akimkabidhi  Mwenyekiti wa sasa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage (kushoto) taarifa ya utendaji Kazi wake kwa kipindi miaka 5 alichokuwa madarakani.

 Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damian Lubuva akizungumza na Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Sekretarieti ya Tume hiyo mara baada ya kukabidhi taarifa ya utendaji Kazi wake kwa kipindi miaka 5 alichokuwa madarakani

 Mwenyekiti wa sasa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage akizungumza na Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Sekretarieti ya Tume hiyo mara kupokea taarifa ya utendaji Kazi wa Mwenyekiti Mstaafu wa Tume hiyo Jaji Damiani Lubuva jijini Dar es salaam.

 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Bw. Ramadhan Kailima akizungumza jambo wakati wa makabidhiano hayo jijini Dar es salaam.Katikati ni Mwenyekiti Mstaafu wa Tume Jaji Mstaafu Damian Lubuva na Kulia ni  Mwenyekiti wa Sasa wa NEC, Jaji wa Rufaa, Semistocles Kaijage.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti Mstaafu wa Tume Jaji Damiani Lubuva , Wajumbe wa Tume na Secretarieti ya Tume hiyo.

Friday, 20 January 2017

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA MABALOZI SITA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akimuapisha Dkt. Emanuel Nchimbi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Brazili, Ikulu jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Januari 20, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. James Msekela  kuwa Balozi wa Tanzania Geneva –Umoja wa Mataifa, Ikulu jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Januari 20, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Mbelwa Kairuki kuwa Balozi wa Tanzania nchini China, Ikulu jijini Dar es salaam leo Ijumaa Januari 20, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. George Madafa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia leo Ijumaa Januari 20, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Elizabeth Kiondo kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uturuki leo Ijumaa Januari 20, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Fatma Rajab  kuwa balozi wa Tanzania nchini Qatar, Ikulu jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Januari 20, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza machache baada ya kuwaapisha mabalozi hao Ikulu jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Januari 20, 2017. Picha na IKULU

WAZIRI NAPE AKUTANA NA WADAU SEKTA YA FILAMU


Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akiongea na wadau katika sekta ya filamu alipokutana nao kujadili changamoto za sekta hiyo na jinsi ya kupambana na maharamia wa kazi za wasani na kuwatoa hofu juu ya wasiwasi wao wa Mali zilizowahi kukamatwa kuwa zimerudishwa kwa wahusika.
Wadau wa Sekta ya Filamu wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye alipokutana nao  Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akimsikiliza Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Bw. Simon Mwakifamba


Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akiangalia kazi haramu za wasanii zilizokamatwa kwa wasambazaji zilizopo katika ghala la kampuni ya madalali ya YONO iliyopo Ilala Bungoni.
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akiangalia mashine ya kudurufu santuri za muziki na video wasambazaji zilizopo katika ghala la kampuni ya madalali ya YONO iliyopo Ilala Bungoni.

Monday, 16 January 2017

BONGE LA SHEREHE SERENA HOTEL DAR,EMMANUEL SAKWANDA NA JUDITH JUSTIN LAMBERT HONGERENI,UFUNGUA UJIONEE MWENYEWE..
















































 Katika burudani Saida na kundu lake walitumbuiza.

 Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi mh Rashid Othuman akitoa neno la shukrani kwa waalikwa.
 Kamati ya maandalizi ikitambulishwa.
 Jodarn Lambert katika ubora wake.
 Bendi kutoka Tanga ikawainua waalikwa.

 Balozi Mberwa Kairuki akiwa na mkewe mh waziri Angela Kairuki.
 Burudani
 Bw Anic Kashasha(MSHENGA) akipata kitu supu.
 Muonekano na mpangilio ilikuwa ni kivutio tosha cha utalii.
 Bw Harusi na Bi harusi katika muonekano wa vazi tofauti.

 Bw Kashasha akiwa na mke wake akicheza ngoma ya saida Kaloli akiwa live.
 Blogger akaweka kamera chini , nae akapigwa picha akicheza ngoma ya saida Kaloli,ilikuwa ni shidaaa..

 Wafanyakazi wa Junaco katika ubora wao.



 Bibi akitoa zawadi.
 Balozi Diodorus Kamala(kulia) akiwa na Dr Frank.
 Kushoto ni Mh Marsha akiwa na mh mbunge wa baraza la wawakilishi Zanzibar.
 Familia ya Bw Anic Kashasha.
 Mh Jaji mkuu wa Tanzania Othuman Chande akiwa na Bw Anic Kashasha katika ukumbi wa Serena hotel, ni miongoni mwa wageni maarufu walioudhuria.
 Bw Robert Matungwa akisalimiana na jaji mkuu wa Tanzania.
 Mrs Justin Lambert(kulia) akifurahia kitu.
 Wajumbe wa kamati.
 Mh Protas Ishengoma katika ubora wake.
 Bw Justin Lambert akiwa na Jaji mkuu wa Tanzania.