Ilikuwa ni shangwe na vifijo katika kata ya Marangu Mwika Moshi katika ukumbi wa Mamba Complex wakati wa kumuaga Bi Aduent Mariki ambae tarehe 28-10-2016 anatarajia kufunga pingu za maisha na mme wake mtarajiwa Bw Vijisenti almaarufu.( katika mkoa wa Kagera wilaya ya Misenye.katika picha Bi Aduent akiwa na mme wake mtarajiwa).
Mwanamke kujiamini.
Kushoto Bw VIJISENT katika ubora wake.
Thursday, 20 October 2016
Tuesday, 11 October 2016
HONGERA SHIRIKA LA NYUMBA,KWA KUTAMBUA TATIZO LA TETEMEKO KWA WAPANGAJI WENU BUKOBA.
Camera yetu imepita mitaa mbalimbali katika manisipaa ya Bukoba ,ikiwa ni takribani mwezi mmoja sasa tangu litokee tetemeko la kihistoria katika mkoa wa Kagera na kusababisha uharibifu mkubwa wa makazi ya watu, maeneo ya biashara na wengine kupoteza maisha. Mpiga picha wetu akiwa katika mitaa alikutana na mhanga aliejitambulisha kwa jina moja Gozi maeneo ya soko kuu alisema ameushukuru uongozi wa shirika la nyumba Bukoba kwa namna walivyotambua umuhimu wa wapangaji wao, baada ya kuzungumza na wafanyabiashara wapangaji wamekubaliana kukarabati kwa haraka majengo yao yalioathilika na sasa ujenzi unaendelea vizuri.
Moja ya jengo la NHC ambalo ukarabati wake unaendelea vizuri.
Moja ya jengo la NHC ambalo ukarabati wake unaendelea vizuri.
Subscribe to:
Posts (Atom)