Tuesday, 26 April 2016

MWENYEKITI WA CCM , RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AWASILI NCHINI AKITOKEA CHINA



 Mwenyekiti a CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa na Katibu wake, Suleiman Mwenda baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, leo akitokea nchini China alikokuwa katika ziara ya kikazi kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC).
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akilakiwa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida
 Mwenyekiti wa CC,M Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa na Madabida
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akizungmza na  baadhi ya viongozi  
 Jk akiingia ukumbini kuzungumza na waandishi
 Jk akiwa tayari kuzungumza na waandishi wa Habari
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akizungumza na Waandishi wa Habari leo baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere mjini Dar es Salaam, akitoa nchini China alikokuwa katika ziara ya kikazi. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam.

Monday, 25 April 2016

DAVID ISAYA NA EDINA KOKUMANYIKA WAFUNGA PINGU ZA MAISHA,BONGE LA SHEREHE LAFANYIKA.

 Ilikuwa ni vifijo , nderemo, hoihoi na shangwe kwa familia, ndugu , jamaa na marafiki pale ziliposikika sauti za wanandoa, pale padre alipowauliza kwa sauti unakubali kumuoa/ kuolewa.. na kila mmoja akajibu nakubali na nitamuheshimu, nitakuwa nae katika raha na shida, na baada ya hapo wakawa mwili mmoja Bw na Bibi David Isaya,baada ya hapo msafara ukazunguka maeneo ya mji wa Bukoba kuelekea kwenye eneo la kupiga picha linalomilikiwa na Mama Ardventina Matungwa lililopo kata ya Kitendaguro nyumbani kwake, na baadae  shangwe zikaamia katika ukumbi wa coffee Tree Inn Bukoba Manispaa.
 Wakitamka agano la ndoa.
 Wakipata mkate wa bwana.
 Sasa ni mwili mmoja.
 Hongera best.
 Wakakabidhiwa hati za ndoa.
 Mwenyekiti wa usafiri Bw Optat akiandaa msafara wa maharusi.
 Garden ya Mama Matugwa, kazi ya kufotoa ikaanza.
 Mahaba niue.
 Aisee nilichagua duh..
 Naombaaaaa...
 USIANGAIKE LAAZIZI WANGU NAKUVISHA KIATU.
 Shangwe zikaamia ukumbini.
Tutaendelea kuwaletea kilichojili ukumbini coffee Tree Inn.

Sunday, 24 April 2016

FAMILIA YA BW LACTO RWEZAURA WAWEKA IBADA YA KUMSHUKURU MUNGU KWA MEMA ANAYOWAJALIA.

 Ni Bw Lacto akiwa na mkewe  mama Kemi mwenye miwani wakati wa misa ya shukrani iliyofanyika nyumbani kwao Muleba Karutanga Magata ikiwa ni shukrani kwa mungu kumnusuru Bw Lacto Rwezaura kwenye ajali mbaya ya gari aliyoipata mwaka jana,pia kubariki nyumba yao mpya.
 Bi Anitha akiteta neno na baba yake mzazi Bw Lacto.
Waalikwa wakiwa kwenye ibada ya misa ya shukrani.
 Bw Jamal Kalumuna akiongoza ratiba ya shughuli nzima.
 Marafiki kutoka Mwanza.
 Baba paroko akieleza mafundisho kuhusiana na madhumuni ya tukio husika.
 Nyumba ikibarikiwa.
 Bw Lacto akitoa neno la shukrani.
 Bw Jamal  (Jamco) akiwa na Anitha.
 Wadada kutoka Mwanza wakitoa zawadi.
Jamcobukoba.blogspot.com inawatakia maisha ya furaha na kumtumaini mungu.