Friday, 19 June 2015
BERNARD MEMBE KUTUA BUKOBA 20-6-2015 JUMAMOSI KUPATA WADHAMINI.
Wednesday, 17 June 2015
DK DIODORUS KAMALA AFUNGA FAINALI ZA DIWANI CUP KATA YA KASHENYE.
Balozi Diodorus Kamala amefunga rasmi mashindano ya mpira wa miguu katika kata ya Kashenye wilaya ya Missenye yalioandaliwa na Diwani wa hiyo Omurangila Rugaibula,Akiongea na wananchi wengi waliojitokeza amemshukuru diwani kwa kutambua na kuthamini michezo na kuona umuhimu mkubwa wa kuandaa mashindano hayo,Balozi kamala ambae tayari ametangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Nkenge amewazawadia mabingwa wa kombe hilo, mshindi wa pili na watatu.zawadi zilizotolewa ni mipira, jezi na pesa taslimu.
ENDELEA KUANGALIA JAMCOBUKOBA.BLOGSPOT.COM
ENDELEA KUANGALIA JAMCOBUKOBA.BLOGSPOT.COM
Monday, 15 June 2015
KATIKA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS LA UJENZI WA MAABARA,DIWANI WA KATA YA KASHENYE KANYIGO AANDAA HARAMBEE.
Mh Diwani wa kata ya Kashenye Kanyigo wilaya ya Missenye Omurangira Adeodatus Rugaibura akisoma taarifa ya kata kwa kipindi cha 2010-2015,ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi.Mh Diwani aliandaa harambee kwa ajiri ya ujenzi wa maaabara ya shule ya sekondari Kashenye,Viongozi,wananchi wa eneo hilo wanaoishi na wasio ishi walishirikishwa,zaidi ya kiasi cha 80 milioni kinahitajika kukamilisha ujenzi wa maabara.
Mwl Maburuki(kushoto) na mwenzake walishiriki tukio la kihistoria.
Wadau wa maendeleo kata Kashenye.
Wananchi waliojitokeza.
Zoezi la harambee likiendelea.
Bw Matunda nae akachukua mic kutangaza alichonacho.
Ujumbe wa Bw Divo nao ulikuwepo.
Wa pili kulia ni Balozi Diodorus Kamala ambae amewahi kuwa mbunge wa jimbo la Nkenge(na safari hii anatarajia kutangaza nia) nae alichangia mifuko hamisini ya saruji,Bw Julius rugemarila ambae nae ameshatangaza nia ya kugombea(alituma mwakilishi, na Bw Kyombo ambae nae ni mgombea nae alichangia.Zaidi ya milioni 11 zilikusanywa ikiwa bado marengo hayajakamilika, kupitia jamcobukoba.blogspot.com inatoa wito wadau wote wa elimu wa ndani na nje kuchangia maabara kwa nia ya watoto wetu wapate elimu bora,zikiwa zimebaki siku chache kabla ya tarehe ya mwisho kufika utekelezaji wa agizo la rais Kikwete.

LOWASSA MAPOKEZI YAKE BUKOBA LEO,WANASEMA MAFURIKO HAYAZUIWI NA VIGANJA,AJIZOLEA WADHAMINI RUKUKI.
Waziri mkuu mstaafu Bw Edward Lowassa amefika makao makuu ya mkoa wa Kagera, Bukoba Manispaa na kupokelewa na maelfu ya wananchi katika uwanja wa ndege wa Bukoba na kumsindikiza kwa kidedea kuelekea makao makuu ya ccm Mkoa kwa ajiri ya kupata wadhamini katika mchakato mzima wa kuomba ridhaa katika chama cha ccm kupererusha bendera ya nafasi ya uraisi mwezi wa kumi mwaka huu,Mh Lowassa ambae anaonyesha kuwa na mvuto kwa wananchi kila anapofika katika mikoa mbalimbali ,amekuwa akipokelewa na wananchi wengi sana.Kwa Bukoba watu wazima na vijana wameonekana kumuunga mkono kwa wingi,akiongea na wananchi wengi waliojitokeza kwenye ofisi za ccm mkoa mh Lowassa pamoja na kuwashukuru wananchi ameongea sababu zilizomfanya aombe nafasi ya urais,amesema umefika wakati wa kuwa na serikali yenye kutoa maamuzi na kuyatekeleza, tena maamuzi magumu,Amesema anauchukia sana umasikini, hivyo anataka watu wachape kazi na wapewe hongera ya kazi sio pole ya kazi.
Ni ndege anayotumia Mh Lowassa.
Mh Lowassa akisalimiana na Murungi kichwabuta uwanja wa ndege Bukoba.
Bw Mzee Kabaka akisalimiana na mh Lowassa.
Umati uliojitokeza kumpokea.
Katibu wa ccm Bukoba Vijijini akimkabidhi orodha ya wanachama waliomdhamini.
Mh Lowassa akiongea na wananchi.
Endelea kuangalia Jmcobukoba.blogspot .com

Subscribe to:
Posts (Atom)