Friday, 27 February 2015

NDEGE YATEKETEA MWANZA


Taarifa inasema kuwa ni ndege ya jeshi la wananchi JWTZ, ambayo imeanguka katika viwanja vya jeshi wilayani Ilemela mkoani Mwanza, ambapo hakuna aliyepoteza maisha.

Inasemekana ndege hiyo ambayo hatujapata namba yake, imeteketea kabisa, huku rubani aliyekuwa ndani yake amenusurika katika ajali hiyo na hakuna aliyepoteza maisha kwasababu alikuwa pekee kwenye ndege hiyo...................


Ni ndege hiyo ya  ya Jeshi ambayo hubeba mabomu, ilikua kwenye mazoezi ya kawaida ambayo hufanyika mara kwa mara. Lakini kwa leo haikuwa na mabomu na ilikuwa na Rubani pekee, ambaye inasemekana amepata majeraha kidogo baada ya kuruka na mwavuli na kukimbizwa hospital ila ndege yote imeteketea kwa moto.
Na Mwanaharakati.

Wednesday, 25 February 2015

AJARI YA BASI LA ADVENTURE MJINI KIBONDO,KAPTEN MWASA ANUSURIKA NA WENZAKE.

 Basi la Adventure linalofanya  safari za Mwanza - Kigoma limeacha njia na  kupinduka na baadhi ya abiria kujeruiwa,chanzo cha habari yetu ajari imesababishwa na moja ya lori lililokuwa speed  katika makutano maeneo ya Kibondo, na  katika hali ya kulikwepa na kusalimisha  maisha ya abiria Basi likaacha njia,.
 Ni watu mbalimbali wakisaidia kuwatoa abiri kwenye gari ,baada ya ajari kutokea.
 Kapten Mwasa mmoja wa wahanga walionusulika  katika ajari.

Jamcobukoba.blogspot.com inatoa pole kwa majerui wote.

COSAD WAANDAA SEMINA YA KUWAFUNDA WASANII WA MUZIKI,WATAKIWA KUWA NA NIDHAMU WATAFANIKIWA.

 Mkurugenzi wa Cosad Tanzania Bw Smart Baitan akiongea na wasanii  wa muziki katika semina iiliyoandaliwa na Cosad, iliyofanyika katika viwanja vya eneo la studio za kurekodi za Cosad maeneo ya Kashura Kitendaguro Bukoba,Bw Smart amewataka wasanii kuwa na nidhamu na maadili ili waweze kufanikiwa,UKIBEBWA BEBEKA, NI maneno aliyoyatumia sana kwenye hotuba yake,Cosad ni shirika lisilo la kiserikali linalotoa huduma kwa jamii. Katika jitihada za kusaidia wasanii ,Cosad imefungua studio ya kisasa ya kurekodi kazi za wasanii wa muzii kwa gharama nafuu sana.
 Bw Smart akiwa na  Bw Izrael Kagaruki ambae ni Kipofu akieleza kwa kumtolea mfano kuwa  katika maisha usikate tamaa,Huyu Bw Izrael ni  kipofu  lakini ameshakuja marekani  mara mbili na akaendesha semina kubwa huko Marekani, kwa hiyo  kama wewe ni mkamilifu wa kila kitu kwa nini ulalamika na kushindwa maisha? Aliuliza bw Smart.
 Wafanyakazi wa Cosad.
 Mgeni rasmi akiwasili.
 Kwaya ya Tumaini ya Rwamishenye wakiimba moja ya nyimbo iliyorekodiwa katika studio za Cosad.
 Ma MC wakiendelea na utaratibu wa ratiba.
 Kushoto ni Mkurugenzi wa Kiroyera Tours Bi Ngonzi , mmoja wa wakufunzi waliotoa somo kwa wasanii.
 Msanii Teso boy akionyesha uwezo wake katika fani ya usanii wa filamu.
 Bw Teso boy muandaaji wa Mashindano ya NANI MKALI ambayo fainali zake zitafanyika siku ya pasaka na mgeni rasmi atakuwa Mbunge wa Bukoba Mjini Balozi Khamis Kagasheki.
 Mgeni rasmi akiongea na wasanii.
 Balozi Kagasheki akiongea na  Bi Victoria Kiwanuka ambae ni  Muuguzi mkuu katika dispensary ya Cosad iliyo Nyamkazi,alikuwa akifanya kazi huko Marekani na sasa amerudi kusaidia nyumbani.
 Bi Ngonzi Karikawe  Mkurugenzi wa Kiroyera Tours.
 Msanii Babu Rweyemamu akiteta na Mh Kagasheki.
Endelea kuangalia jamcobukoba.blogspot.com

Tuesday, 24 February 2015

HAFRA FUPI YA KUMUAPISHA MKUU WA WILAYA YA MISSENYE,KUKARIBISHA WAPYA NA KUAGA WANAOONDOKA.

 Mkuu wa Mkoa wa Kagera John Mongella  akimuapisha Mkuu wa wilaya ya Missenye Fadhil Nkurhu,Hafla hii fupi ilifanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
 Kaimu Ras Bw Anyosise akitoa maelekezo ya utaratibu .
  Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Bw Jackson Musome.
 Mkuu wa wilaya ya Rombo Bw Lembris Kipuyo alikuwa wilaya ya Muleba akiwa na Kanal mstaafu Issa Njiku mkuu wa wilaya ya  Mlele Katavi alikuwa wilaya ya Missenye.
Bw Yahya Kateme Mwenyekiti wa vijana ccm Mkoa Kagera akiwa na katibu wake wa uvccm Mkoa Didas Zihimbile.
Meneja wa Tawi la NMB Bukoba.
Shekhe wa Mkoa Kagera Haruna Kichwabuta akisoma dua.
Mkuu wa Mkoa john Mongella akiwa na Mwenyekiti wa ccm Mkoa Costancia Buyiye.
Baba Askofu Buberwa akiomba dua.
Baba Askof Methodius Kilain.
 Bw Varelian akiwa na Mh Kanal mstaafu Issa Njiku.
Endelea kuangalia jamcobukoba.blospot.com