Friday, 30 January 2015

DC WA MULEBA NA WENZAKE WASALIMIKA KATIKA DHORUBA WA UPEPO MKALI ZIWA VICTORIA.

Tunapenda kuwajulisha kuwa mkuu wa Wilaya Muleba Bw Lembrose Kipuyo na ujumbe aliokuwa nao walipatwa na dhoruba ya upepo mkali ziwa victoria wakiwa na mtumbwi wao wakielekea kwenye maafa yaliyotoke katika kisiwa cha Goziba, Mtumbwi wao umepatikana wakiwa salama, Na wameendelea na safari kwenda klisiwa cha Goziba kuangalia wahanga wa dhoruba ya upepo mkali uliosababisha uharibifu mkubwa katika kisiwa hicho.

BREAKING NEWS:DC MULEBA NA UJUMBE WAKE WAPOTEA NDANI YA ZIWA VICTORIA,BOTI YAO YAPIGWA DHORUBA

 
Habari zilizotufikia ni kwamba mkuu wa wilaya ya Muleba Lembrose Kipuyo(pichani) na ujumbe wake wamepotea na boti yao katika ziwa victoria baada ya mtumbwi waliokuwa wakisafiri nao kuelekea katika kisiwa cha goziba kujionea madhara ya dhoruba iliyokikumba kisiwa hicho kupoteza mwelekeo ambapo tangu waondoke muleba asubuhi hadi saa 3:00 usiku walikuwa hawajafika muleba,simu zao hazipatikani na wala hawajulikani walipo.

Vikosi mbalimbali vya serikali vipo ziwani kuwasaka.

Tunaendelea kufuatilia habari hii kwa undani baki nasi......

Thursday, 29 January 2015

TALGWU YATOA VITANDA KWA AJILI YA MAMA WAJAWAZITO,MASHINE KWA VITUO VYA AFYA BUKOBA.

 Chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa (TALGWU) kimetoa vifaa vya huduma ya afya vitanda maalumu kwa ajili ya mama wajawazito kujifungua na mashine kwa ajili ya kusaidia kutoa uchafu watoto wachanga wanapozaliwa,vifaa vyote vilivyotolewa vina thamani ya milioni kumi na mbili,vifaa hivyo vimetolewa katika vituo vya afya Manispaa ya Bukoba na Bukoba vijijini,Uongozi wa TALGWU Taifa ulikabidhi vifaa hivyo kwa katibu tawala wa Mkoa wa Kagera Bw Nassor Mnambila ambae alikuwa mgeni rasmi katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya Manispaa ya Bukoba.
 Mkuu wa wilaya Bukoba Bi Zippola Pangani akiwa na viongozi wa TALGWU Taifa.
 Kaimu mkurugenzi Manispaa ya Bukoba Bw Chibhunu Lukiko akisalimiana na mwenyekiti wa Talgwu Taifa Suleiman Abdalah Kikingo(kushoto)
 Mwenyekiti wa Talgwu Taifa akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkugenzi Manispaa ya Bukoba.
 Mgeni rasmi akiwasili.
 Mc wa hafla akiongoza ratiba.
 Wanachama wa TALGWU.
 wimbo wa shime tujiunge pamoja ukaimbwa.
 Dk Musa akifurahi na camera yetu.
 Wanachama wa TALGWU.
 Mwenyekiti wa TALGWU Taifa  Suleiman Abdalah Kikingo akieleza kwa kifupi umuhimu wa kusaidia mama wajawazito na watoto.
 Mgeni rasmi katibu tawala Mkoa wa Kagera Nassor Mnambila akitoa hotuba yake,amesema thamani ya msaada huu wa vifaa kwa ajili ya kusaidia mama wajawazito wakati wa kujifungua na mashine ni zaidi ya thamani ya fedha,maana watakaonufaika na vifaa hivi ni wamama wengi sana na hivyo kufanya thamani ya vifaa hivyi kuwa kubwa zaidi, pia amewataka wafanyakazi wa vituo vya afya kuvitunza vifaa hivyo.
 Mganga mkuu wa Mkoa wa Kagera Dk  Thomas Rutachunzibwa akisibitisha ubora wa vifaa vilivyoletwa.
 Katibu tawala wa Mkao akimbabidhi Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa Bukoba vifaa kwa ajili ya vituo vya afya katika eneo lake.
 MWANDISHI WA HABARI WA CLOUDS TV Audax Mtiganzi akifanya mahojiano.
Jamcobukoba.blogspot.com kwa habari za uhakika,tupigie simu namba 0788-707027, 0754-757157.

Wednesday, 28 January 2015

KAGASHEKI: CCM KAZI IPO MWAKA HUU

Dar es Salaam. Hofu kuhusu nafasi ya CCM kwenye Uchaguzi Mkuu ujao inazidi kuongezeka baada ya mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki kukitabiria chama hicho tawala “kazi kubwa”, akisema hali ya sasa “siyo ile iliyokuwa nayo miaka mitano iliyopita”.
Kagasheki pia alikitahadharisha chama hicho dhidi ya kuzidi kukua kwa nguvu ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) akisema iwapo umoja huo utamchagua mgombea makini, CCM itakuwa na kazi ngumu.
Balozi Kagasheki, ambaye alikuwa Waziri wa Maliasili na Utalii kabla ya kujiuzulu kutokana na sakata la Operesheni Tokomeza, alisema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa mahojiano maalum na gazeti la Mwananchi.
Kauli yake inaungana na za vigogo wengine wa CCM waliotahadharisha mwenendo wa chama hicho dhidi ya ongezeko la nguvu ya upinzani, akiwamo Waziri Mkuu wa zamani, Fredrick Sumaye, ambaye alisema rushwa inakimaliza chama hicho, na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba, ambaye alisema kuwa chama hicho kisitegemee ushindi wa kishindo.
Akijibu swali la maoni yake kuhusu Uchaguzi Mkuu ujao na nafasi ya CCM, Kagasheki alisema: “Ipo kazi, nafasi ya CCM sasa... Jamii imeanza kuwa na maswali mengi kuhusu chama chetu, viongozi wachukue hili kwa umakini, wakifuatilia watajua.”
Mbunge huyo alisema kuwa matokeo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa hivi karibuni yametokana na wananchi kuona CCM imeshindwa kuisimamia vizuri Serikali.
Katika uchaguzi huo uliofanyika Desemba mwaka jana CCM ilishinda kwa asilimia 79.81 (vijiji) na 79.83 katika vitongoji, wakati kwenye mitaa mingi ikiwa maeneo ya mijini kimeshuka kikipata asilimia 66.66, ikilinganishwa na ushindi wa asilimia 89.2 katika mitaa, asilimia 91 katika vitongoji na asilimia 91.6 katika vijiji katika uchaguzi huo mwaka 1999.
Kwa mujibu wa matokeo hayo, kulikuwa na ongezeko kubwa la ushindi wa wapinzani kwenye baadhi ya maeneo, hasa kutokana na kusimamisha mgombea mmoja chini ya Ukawa inayounganisha vyama vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD.
“Mengine yametokana na CCM kutoisimamia vizuri Serikali au kutotimiza wajibu. Wapo wananchi wanaosema CCM inakumbatia waovu. Kama inataka kuendelea kuaminika na kutumainiwa, CCM isibweteke, isione aibu kuikosoa Serikali.
“Hapa natambua juhudi za Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana kuwa karibu na watu. Ipo haja kwa CCM kujitazama upya, itazame mikakati yake, inaweza kujipanga kurudisha imani.” Kauli hiyo ya Balozi Kagasheki imekuja siku chache baada ya Makamba, ambaye ni mbunge wa Bumbuli kuwataka wanachama wa chama hicho kikongwe kujiandaa kisaikolojia kwa matokeo yoyote yanayoweza kutokea katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.
“Wana-CCM wanatakiwa kujiandaa kisaikolojia kwani walizoea ushindi wa asilimia 90 au 80, huu ulikuwa ushindi wa nyuma. Tusishangae tukipata ushindi wa asilimia 50, 60, 57 au 70 ni kitu cha kawaida kutokana na kukua kwa demokrasia, hususan ushindani wa vyama vingi vya siasa kuanza kuimarika,” Makamba alisema katika kipindi cha Power Breakfast cha Radio ya Clouds.

Tuesday, 27 January 2015

RAIS KIKWETE AHANI MSIBA WA MFALME WA SAUDI ARABIA, AWASILI BERLIN, UJERUMANI, KWA ZIARA YA KIKAZI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa mkono wa pole kwa watawala na familia mjini Riyadh, Saudi Arabia Jumapili, Januari 25, 2015, alipofika kuhani kuhani kifo cha Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud aliyefariki Alhamisi na kuzikwa Ijumaa ya wiki iliyopita. Baada ya kuhani msiba wa Mfalme Abdullah, Rais Kikwete ameendelea na safari
yake kwenda nchi za Ujerumani na Ufaransa kwa ziara za kikazi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Bi Fawzia Rasheed, Mkuu wa Sera wa Global Alliance for Vaccines and Immunization (Gavi Alliance) alipotua mjini Berlin, Ujerumani, leo Jumatatu 26, 2015 kuungana na viongozi mbali mbali duniani kujadili jinsi ya kuboresha mipango ya utoaji chanjo kwa watoto wadogo hasa katika nchi zinazoendelea. 
PICHA NA IKULU