Wednesday, 14 January 2015

HONGERA JAMAL MALINZI,KAITABA STADIUM UMEITENDEA HAKI.


 Nakumbuka mapema mwaka jana katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa Wa Kagera,mara baada ya kuwasili akitokea jijini Dar Mwenyekiti wa chama cha mpira Kagera  KRFA Jamal Malinzi baada ya kuchaguliwa kuwa  rais wa chama cha mpira nchini TFF alitamka kuwa uwanja wa Kaitaba utawekewa nyasi bandia na kujengwa jukwaa kubwa moja,Wengi wa wapenzi wa soka Mkoa wa Kagera walipokea kauli hiyo kwa shangwe na furaha kubwa,lakini baadhi yao walizani ni ahadi hewa walizozoea kuhaidiwa na hazitekeleziki, Kwa Jamal Malinzi imekuwa tofauti amehaidi na sasa utekelezaji umeanza,Jamcoblog tumetembelea uwanja wa kaitaba na kukuta kazi ikiendelea kwa kasi ya kuridhisha,Uwanja  huu wa kaitaba unaofadhiliwa na FIFA kwa asilimia mia moja tunaamini utakapokuwa umekamilika kwa kuwekewa nyasi bandia utakuwa umeuweka mkoa wetu  katika ramani ya dunia ya kuwa na viwanja bora nchini na kuweza kuleta mechi kubwa kuifanya Bukoba kujulikana na kuongeza wageni au utalii na kipato cha wananchi kukua na uchumi wa Mkoa kwa ujumla, Hongera Jamal Malinzi Hatukukosea kukuchagua.
 Hiyo ndio hali halisi matengenezo yakiendelea.

 Blogger wa Jamcoblog katika harakati za kuchukua  matukio.
 Mtaalamu kutoka FIFA akiwa kazini.

 Unaona, Kaitaba hiyo nyasi bandia zajaaaa.
 Mtaalamu kutoka FIFA katika harakati za kikazi.
Narudia maneno ya kihaya ( Eofisi etainamu wawe Ebaekomile) Asante Jamal Malinzi tunajivunia uwepo wako.

Tuesday, 13 January 2015

YALIYOJIRI NDANI YA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM ZANZIBAR

TANGAZO LA KAZI

NAFASI MOJA YA KAZI, FOOD SCIENTISTS AND TECHNOGISTS,  MAOMBI YATUMWE info@nkbottlers.co.tz   au   adhamadia@yahoo.co.uk   au piga simu ya mkononi namba 0787936122 kwa maelezo zaidi.nafasi ni moja tu.

RIDHIWANI KIKWETE AKABIDHI AMBULANCE KITUO CHA AFYA CHALINZE




 Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete (katikati) akikabidhi gari jipya la kubebea wagonjwa (Ambulance), kwa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo,Dk. Mastidia Rutaihwa kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Chalinze, katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Chalinze jioni hii. Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Mganga Mkuu wa kituo hicho, Dk. Bamba Victor na Diwani wa Kata ya Bwilingu, Nasa Karama. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
 Muumini wa Dini ya Kikiristo, Heema Said akitoa neno la shukrani kwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Kikwete 9aliyevaa koti kushoto) alipokabidhi ambulance hiyo. Ridhiwani alisema kuwa yeye hivi sasa ni mbunge wa vyama vyote jimbo humo hivyo ambulance aliyoitoa itoe huduma kwa wakazi wote wa jimbo hilo bila kubagua watu kutokana na itikadi zao. Pia aliuasa uongozi wa kituo hicho cha afya na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kuhakikisha wanatunza vizuri gari hilo.
 Dok Rtaihwa akimkabidhi ufunguo wa gari hilo Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Chalinze, Dk.Victor baada ambulance hiyo kukabidhiwa na Mbunge Ridhiwani.
 Dk. Victor akitoa shukurani kwa Mbunge Ridhiwani kwa msaada huo wa ambulance
 Wakifurahia kwa pamoja kupata usafiri huo muhimu kwa wagonjwa
 Mbunge Ridhiwani Kikwete na Dk. Rutaihwa wakiangalia ndani ya ambulance hiyo
 Wakiwa na furaha baada ya kuangalia samani zilizomo ndani ya ambulance hiyo
 Ridhiwani  pamoja na viongozi wa dini ya kiislamu wakiliombea dua gari hilo. Kutoka kulia ni Alhaji  Sheikh Hussein Fuko na Alhajj Khamis Magula
 Ridhiwani 9katikati) na Mbuunge wa Jimbo la Mtera, Lusinde wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Kituo cha Afya cha Chalinze akiwemo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Dk. Rutaihwa.
 Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Dk.Mastidia Rutaihwa akitoa shukurani kwa Ridhiwani kwa msaada wa Ambulance na kuahidi kuitunza
 Ridhiwani akipongezwa na wananchi kwa kuwapatia ambulance
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya Hafsa Kazinja akicheza muziki na mmoja wa wazee wa Chalinze alipotumbuiza katika mkutano huo
 Ridhiwani akihutubia katika mkutano huo
 Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria makabidhiano ya ambulance katika viwanja vya miembe saba mjini Chalinze leo
 Mbunge wa Jimbo la Mtera, Dodoma, Lusinde ambaye alikuwa safarini akitokea Dodoma kwenda Dar kwenye vikao vya Kamati za Bunge, aliamua kushiriki kwenye mkutano huo ambapo alimsifia Mbunge Ridhiwani kwa kipindi kifupi alichoaguliwa kuwa mbunge miezi sita iliyopita kutekeleza kwa kiasi kikubwa ahadi alizozitoa wakati wa kampeni ikiwemo ambulance hiyo, ujenzi wa visima katika vijiji mbalimbali na ujenzi wa barabara pamoja na zahanati
Lusinde akikumbatiana kwa furaha na Ridhiwani baada ya mkutano huo kumalizika

Sunday, 11 January 2015

MBUNGE WA MBEYA MJINI, JOSEPH MBILINYI ‘SUGU’ APATA AJALI YA GARI MLIMA KITONGA

Sugu Mbeya
Mheshimiwa Joseph Mbilinyi akiwa amesimama mbele ya gari alilopata nalo ajali

Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amenusurika katika ajali ya gari  ambayo imetokea jana mchana(Jan.10)   eneo la Mlima Kitonga, wilaya ya kilolo mkoani Iringa.
Chanzo cha ajali hiyo kinatajwa kuwa ni kufeli kwa break hali iliyopelekea gari hilo kuanguka kichwa chini miguu juu wakati mbunge huyo akitokea Mbeya kuelekea Mikimu mkoani Morogoro kwenye mkutano wa hadhara.
Katika gari hilo aina ya Totoya Land Cruiser ambalo lilikuwa likiendeshwa na mheshimiwa Sugu, lilikuwa limebeba   watu wanne ambao wote walisalimika na kutoka salama licha ya michubuko ya mkononi aliyoipata mbunge huyo wa Mbeya Mjini.
Sugu apata ajali
Gari la Mheshimiwa Sugu baada ya kupata ajali eneo la Mlima kitonga
sugu Mr.Sugu
muonekano wa gari la mheshimiwa Sugu mlima Kitonga mkoani Iringa
Sugu Mr 2
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ akiwa amefungwa bandeji kwenye bega baada ya kunusurika katika ajali