Wednesday, 31 December 2014

AJALI MBAYA YATOKEA MAENEO YA ROUND ABOUT YA RWAMISHENYE JIONI HII.

 Ni Lori la kubeba vifusi ambalo lilitambulika kumilikiwa na kampuni inayochimba visima vya maji na kutengeneza mtandao wa mabomba ya maji Manispaa ya Bukoba leo jioni liliacha njia maeneo ya mzunguko wa Rwamishenye, njia ya kuelekea Mutukula,Kwa mujibu wa maelezo ya walioshuhudia inasemekana Lori hilo inawezekana lilikatika breki likiwa limepakia kifusi cha udongo,Hata hivyo inasemekana dereva wa gari hili alionekana amelewa na kupelekea kushindwa kumudu kuendesha gari hilo. Hakuna aliepoteza maisha.

Huyu ndio inasemekana alikuwa dereva wa lori lililopata ajari , na inasemekana alikuwa amelewa kwa mujibu ya watu walioshuhudia tukio.Alipambana na askari wa usalama barabarani akigoma kupanda gari ya polisi akidai yeye si dereva wa hilo gari, baada ya kupambana polisi walifanikiwa kumzibi na kumpeleka kituoni.

Tuesday, 30 December 2014

MIAKA 50 YA NDOA YA TA SIMFORIAN RWEIKIZA MWAMI NA MA IRIDA KALIKWENDWA WA KANAZI BUKOBA.

 Ni nyuso zenye furaha na zilizosheeni upendo wa dhati wakatio wa ibada takatifu ya kumshukuru mungu kwa kutimiza miaka 50 ya ndoa.Ibada ya misa takatifu ya kuadhimisha miaka 50 ya ndoa ilifanyika nyumbani kwao na ibada iliongozwa na Fr Longino.
 Ni picha ya wajukuu, matunda ya miaka 50 ya ndoa.
 Wagole wakiingia ukumbini.
 Fr Longino akiendelea na ibada.
 Somo likisomwa.
 Watoto wa wanajubilee ya dhahabu ya ndoa.
 Wakivishana tena pete ya miaka  50 ya ndoa.
 Wajukuu wakiwapongeza.
 Pia ulifanyika ubatizo wa wajukuu wawili.
 Kulia Bw Griflin baba wa ubatizo wa mtoto.
 Wajukuu wakitoa maombi wakati wa ibada.
 Picha ya ndugu na jamaa.
 Keki ya jubilee ya dhahabu.
 OMUTOMAAAA.
 Hapana chezee mama Poroje.
 Neno la familia.
 LYAO AKAKEKI MUSHAIJA WANGEEE(kARIBU KEKI MME WANGU.)
 NYWAO MUKAZIWANGE(Kunywa mke wangu)
 Zawadi time.
 Fr Longino anaeishi Tabora akitoa zawadi.
 Mr Poroje kwa mbali.
Mr Poroje akitabasamu na camera yetu. Jamcobukoba.blogspot.com inawatakia maisha mema  ya ndoa.