Wednesday, 2 July 2014
IDADI YALFAJIRI WAFIKIA WANNEA WATU WALIOKUFA KATIKA AJALI YA NDEGE YA MIZIGO JOMO KENYATTA LEO
Askari
wa Jeshi la Kenya wakiwa eneo la tukio wakijaribu kutoa msaada katika
Ndege ya mizigo iliyoanguka leo asubuhi katika eneo la Utawala kwenye
Uwanja wa Jomo Kenyatta, jijini Nairobi.
Taarifa
kutoka Kenya zinasema kuwa mpaka sasa imefahamika kuwa jumla ya watu
wanne akiwamo Rubani, waliokua kwenye ndege hiyo wameripotiwa kufa baada
ya ndege hiyo kuanguka dakika chache tu baada ya kupaa kutoka kwenye
uwanja huo ikielekea Moghadishu, Somalia.
Ajali
hiyo imetokea alfajiri ya leo ambapo imeelezwa kuwa ndege hiyo ilikua
iondoke mapema kusafirisha zao la Mirungi na bidhaa nyinginezo kuelekea
Somalia.
Akithibitisha
ajali hiyo Mkuu wa Polisi wa Jiji la Nairobi, Benson Kibue, amesema
kuwa kuwa Ndege hiyo yenye nambari 5Y-CET ilianguka kwenye paa la jengo
la kibiashara wakati likijaribu kutua ghafla baada ya kutokea hitilafu
katika ndege hiyo na kushika moto kisha kuanza kuteketea na watu wanne
waliokua ndani.
Aidha
kwa mujibu wa Mkuu wa Polisi wa Jijini Nairobi, Benson Kibue, amesema
kuwa katika ajali hiyo walinzi wawili walijeruhiwa mmoja ametibiwa na
kuruhusiwa kurejea nyumbani huku mmoja akilalazwa katika hospitali ya
Mama Lucy.
Polisi wanaendelea na uchunguzi kwenye mabaki ya ndege hiyo kuona iwapo kuna waathirika zaidi.
LOWASSA ASHIRIKI SHEREHE ZA JUBILEI YA MIAKA 25 YA ASKOFU MKUU WA JIMBO LA IRINGA, MHASHAMU TARCISIUS NGALALEKUMTWA
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akisalimiana na Askofu Mkuu wa Jimbo la Iringa,Mhashamu Tarcisius
Ngalalekumtwa wakati wa Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wake,iliyofanyika
Julai 01,2014 kwenye Kanisa Kuu la Katolini Mjini Iringa.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akisalimiana na Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania,Mhashamu
Severini Niwemugizi wakati wa Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wa Askofu
Mkuu wa Jimbo la Iringa,Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa,,iliyofanyika
Julai 01,2014 kwenye Kanisa Kuu la Katolini Mjini Iringa.
Rais
Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa akisalimiana na Askofu Mkuu
wa Jimbo la Iringa,Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa wakati wa Jubilei
ya Miaka 25 ya Uaskofu wake,iliyofanyika Julai 01,2014 kwenye Kanisa Kuu
la Katolini Mjini Iringa.

Askofu
wa Jimbo la Tabora,Mhasamu Paul Ruzoka akizungumza machache wakati wa
Sherehe za Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wa Askofu Mkuu wa Jimbo la
Iringa,Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa,iliyofanyika Julai 01,2014
kwenye Kanisa Kuu la Katolini Mjini Iringa.
Askofu
Mkuu wa Jimbo la Iringa,Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa akiwa na
wasaidizi wake wakati wa Sherehe za Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu
wake,iliyofanyika Julai 01,2014 kwenye Kanisa Kuu la Katolini Mjini
Iringa.
Askofu Mkuu wa Jimbo la Iringa,Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa akiongoza ibada maalum ya Jubilei hiyo.
Makamu
wa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania,Mhashamu Severini Niwemugizi
akizungumza katika sherehe hizo,wakati alipokuwa akitoa salamu za Baraza
hilo kwa Serikali.
SSEBO NAYE ATIMKIA E FM YA MKUDE SIMBA
Mtangazaji
maarufu nchini wa vipindi vya Radio na Television Dennis Busulwa a.k.a
Ssebo amejiunga na Radio
ya E FM ambayo imekwishajizolea umaarufu mkubwa jijini Dsm kwa kipindi
kifupi tu kutokana na staili yake tofauti ya urushaji matangazo nchini.
Ssebo mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka
mitano kwenye vituo mbalimbali vya Radio na TV amejizolea sifa na
mashabiki lukuki katika tasnia hii ya utangazaji kutokana na staili na
vituko vyake awapo
hewani.
"Mashabiki
wangu watarajie mengi mazuri kutoka kwangu nikiwa na E FM",alisema
Ssebo.Ssebo anakutana na timu ya watangazaji wengine wakongwe kama Dj
Majey, Dizzo One na Sos B waliokwisha anza kusikika
Radioni hapo.
Monday, 30 June 2014
KAGASHEKI CUP 2014: TIMU YA KAGONDO YAITUNGUA BUHEMBE FC BAO 1-0
Timu ya Kagondo FC imejipatia Alama tatu muhimu kwenye Mtanange wao dhidi ya timu ya Buhembe FC leo kwenye Uwanja wa Kaitaba Bukoba Mjini kwenye Michuano ya Kombe la Kagasheki. Bao hilo la pekee lilifungwa na Mchezaji namba tisa Mgongoni Abduratif Khamis katika kipindi cha kwanza dakika 37. Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa bao hilo 1-0 na kipindi cha pili timu zote mbili hakuna iliyoziona nyavu za mwezake timu licha ya kushambuliana mara kwa mara. Mwamuzi alipuliza kipenga dakika 90 kumaliza mtanange huo na Timu ya Kagondo FC wakiibuka na ushindi huo wa bao 1-0. Mapema leo Mchana Timu ya Nshambya na Kibeta ziliumana na timu zote mbili zilimaliza mtanange kwa sare ya bila kufungana kwa kutoka 0-0. Kesho Ligi hii inaendelea tena kwa siku ya nne na kutakuwepo na michezo miwili, Mapema ni Nyanga vs Kitendaguro na Jioni saa 10:00 ni Wagonga Nyundo "Ijuganyondo Vs Kahororo".
Kikosi cha Timu ya Kagondo Fc
Kipute kilianza kwa Timu ya Buhembe kwa kasi sana
Kipa wa Kagodo chupuchupu afungwe bao hapa katika kipindi cha pili. Kipindi cha pili hakuna aliyeziona nyavu za mwenzake bao hilo lilidumu mpaka dakika za mwisho
Hatari: Kipa wa Kagondo Fc akidaka mpira wa Kona
Kipindi cha Pili dakika za mwishoni Timu ya Buhembe FC ilipata kona mbili lakini haikuweza kusawazisha bao, licha ya kuliandama lango la wenzao Kagondo Fc.
Sunday, 29 June 2014
KAGASHEKI CUP 2014: KASHAI 3 vs BAKOBA 0, MAJANGA!! MAHASIMU BAKOBA HOI KWA WENZAO, WAKUBALI YAISHE!! MASHABIKI WANUNA KAITABA!
Na Faustine Ruta, BukobaMichuano ya Kagasheki Cup 2014 imeendelea tena leo kwenye Uwanja wa Kaitaba ulipo Bukoba Mjini kwa siku ya pili na kushuhudia mahasimu wawili Mmoja akimliza mwenzake bao 3-0.
Mtanange wa leo hii Jumapili ulizikutanisha timu mbili matata kwenye hii ligi za Kashai na Bakoba FC na kushuhudia Timu ya Bakoba ikifungwa bao 3-0 bao zilizofungwa kipindi cha kwanza mbili na kipindi cha pili moja.
Timu ya Kashai FC walianza kuifunga timu ya Bakoba bao la kwanza katika dakika ya 8 bao likifungwa na Joha Johansen.
Bao la pili lilifungwa na Msengi Gerard katika dakika ya 38 kipindi cha kwanza na kufanya bao kuwa 2-0 dhidi ya mahasimu wao wakubwa Bakoba FC ambao mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika walikuwa hawajapata kitu.
Kipindi cha pili licha ya timu zote mbili kukamiana kwa sana timu ya Bakoba ilipata nafasi kama tatu lakini haikuweza kuifunga timu ya Kashai na hatimaye Kashai kupata bao lao la tatu katika dakika ya 60 kipindi cha pili bao lililotiwa nyavuni na Mchezaji wa Kashai FC Shamte Odilo na Kipute kumalizika kwa dakika 90 Kashai ikiibuka kwa bao 3-0.
Michuano hii itaendelea tena kesho Jumatatu na kutakuwa na Mitanange miwili wakwanza utachezwa saa nane kati ya Nshambya FC ikiumana na timu ya Kibeta Fc saa 8:00 mchana na mtanange wa saa 10:00 ni baina ya Kagondo Fc na Buhembe Fc.
Mchezaji wa Shamte wa Timu ya Kashai akishangilia bao lake
Shamte na Joha Johansen wakishangilia bao
Mashabiki wa timu ya Bakoba wakiwa awaamini macho yao, timu ikipigwa bao la pili katika dakika ya 38
Mashabiki wa Kashai Fc usipime!!
Chinja!! Chinja!!! Mashabiki wa Kashai wakiipamba timu yao ili iendelee kutoa dozi kwa maasimu wao!
Kipute kikiendelea...
Mchezaji wa Bakoba akikimbia na mpira kwenda kufunga...
Patashika wachezaji wakichuana kugombea mpira
Mchezaji wa Kashi Fc akimbana mwenzake wa Bakoba
Jukwaa kuu mashabiki wa Bakoba, hawana hamu!!! wengi mikono kichwani!! na wengine wakijiuliza kunani?? Na hapa ilikuwa na mapumziko Bakoba walienda kupumzika wakiwa nyuma ya bao 2-0.
Kwa wengine mambo safi!
Vijana wakitokelezea kwenye Camera
Mwanadada Shabiki wa timu ya Kashai
Kipute kikiendelea...
Vijana wa Kashai wakiwabana wenzao Bakoba Fc ili wasiweze kurudisha hata bao moja
Mabeki wa kulia na kushoto wa timu ya Kashai wakimbana mchezaji mmoja wa Bakoba
Pamoja sana!!
Wazee nao hawakukosa!
Mama Shabiki wa Bakoba Fc akiwa hana ili wa lile!! leo kakamatika!Dakika 90 zimemalizika...Kashai 3 vs Bakoba 0
Subscribe to:
Posts (Atom)



























