Friday, 4 April 2014

NJOO TUCHEZE STYLE YA "YACHUMA CHUMA" NA SKYLIGHT BAND LEO NDANI YA KIOTA CHA THAI VILLAGE.


Aneth Kushaba AK47 (wa pili kushoto) akiongoza waimbaji wa Skylight Band kutoa burudani burudani kwa mashabiki wao kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
Skylight Band na staili yao ya “Yachuma chuma” kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
Mashabiki wa Skylight Band wakisebeneka ndani kiota Thai Village usikose burudani ya kipekee leo usiku kuanzia saa 9:30.

Umati wa mashabiki wakishuhudia burudani ya Skylight Band ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.

Tuesday, 1 April 2014

KUFURU...UTAJIRI WA MASANJA MKANDAMIZAJI UNATISHA AISEEE....!JIONEE MWENYEWE HAPA....!!



 

  • Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ akiwa mbele ya usafiri na mjengo wake.

     HABARI MEZANI

    UTAJIRI wa komediani maarufu Bongo,  Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ ni kufuru! Tena unatisha na sasa anaonekana kuwa miongoni mwa wasanii wanaomiliki fedha na mali nyingi Bongo, Risasi Mchanganyiko linakupa zaidi. 
    Awali, habari kuhusu utajiri wa Masanja ilitua mezani mwa gazeti hili kama kidokezo, hapo mwandishi wetu akaingia mzigoni na kuanza kuchunguza kwa kina mali anazomiliki msanii huyo na kugundua kuwa ni kati ya mastaa mabilionea Bongo.

     “Masanja sio yule tena. Ana mpunga (fedha) mrefu sana. Hakuna msanii wa maigizo Bongo anayeweza kumfikia kwa sasa. Hao wengine ni mbwembwe tu, lakini pesa imelala kwa Masanja,” kilipasha chanzo chetu.
     Kikaongeza: “Kwanza ana ghorofa lipo Tabata, hapo ndipo anapoishi. Pia ana magari kibao ya kifahari, mashamba ya mpunga na Kampuni ya OK Security inayolinda sehemu mbalimbali zikiwemo taasisi nyeti nchini.

    Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ akiwa kwenye pozi na miongoni mwa magari yake.
     “Ni msanii gani mwenye kampuni kubwa kama ya Masanja? Wengi wanaishia kudai wanatayarisha filamu ambazo hata matunda yake hayaonekani.”
     RISASI MZIGONI
    Mdogomdogo, Risasi Mchanganyiko likajitupa mtaani kuchimba kuhusu madai hayo ambayo awali liliyatilia shaka kama si wasiwasi.

     Uchunguzi wetu ulibaini ukweli wa mali za msanii huyo na mambo mengine mengi yanayoingia kama vyanzo vya mapato yake.
     MAGARI SITA
    Ilibainika kuwa, Masanja anamiliki magari sita, yakiwemo ya kifahari. Baadhi ya magari hayo ni Toyota Land Cruiser V8, Nissan Hardboad na Toyota Verossa.
     
    NYUMBA TATU BONGO
    Pia, mkali huyo wa kuvunja mbavu, anamiliki nyumba tatu za maana jijini Dar es Salaam, moja ni ghorofa ipo Tabata, nyingine Kigamboni na nyingine haifahamiki eneo rasmi ilipo.
    Hata hivyo, imebainika kuwa mbali na mijengo yake hiyo iliyopo jijini Dar, nyumbani kwao Mbarali, Mbeya ana mjengo wa maana.
     
    MASHAMBA KIBAO
    Msanii huyo hayupo nyuma kwenye kilimo, ana mashamba kadhaa Kigamboni jijini Dar es Salaam lakini linalotia fora ni lile lililopo Mbarali lenye ukubwa wa hekari 50 ambalo analima mpunga.
     
    NI MSANII WAMAIGIZO TAJIRI ZAIDI?
    Kwa utajiri huo, ipo minong’ono kuwa, nyota huyo anaweza kuwa kwenye namba za juu za wasanii wa maigizo wenye mkwanja mrefu.
    Wengine wanaotajwa kwenye orodha ya waigizaji matajiri Bongo ni Husna Posh ‘Dotnata’, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ na Amri Athumani ‘Mzee Majuto’.
     MATAJIRI BONGO FLEVA
    Katika muziki wa Bongo Fleva, wasanii wanaoaminika wana utajiri mkubwa zaidi ni Judith Wambura ‘Lady Jaydee’, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Joseph Haule ‘Profesa Jay’.
    Wasanii hao wanamiliki mijengo ya maana, achilia mbali magari ya kifahari na miradi kadhaa.
     
    MASWALI KUHUSU MASANJA
    Utajiri wa Masanja umeonekana kuibuka ghafla huku vyanzo vyake vya kumwingizia kipato vikijulikana ni sanaa ya uigizaji, muziki na huduma ya uchungaji.
    Je, kwa uigizaji tu katika Kundi la Orijino Komedi ‘OK’ ndiko alikopata mkwanja huo na kuanzisha miradi hiyo mikubwa?

     Kama ndiyo, kwa nini memba wenzake ndani ya kundi hilo hawana maendeleo makubwa kama yeye?
    Kazi nyingine ya Masanja ni muziki wa Injili ambapo kwa sasa albamu yake ya Hakuna Jipya iko sokoni. Je, albamu hiyo na shoo anazofanya zinaweza kuwa chanzo cha utajiri huo?

     Lakini pia Masanja ni mchungaji ambaye anahudumu katika Kanisa la Evangelist Assemblies of God Tanzania (EAGT) ‘Mito ya Baraka’ lilicho chini ya Askofu Bruno Mwakiborwa. Je, mshahara anaoupata kutokana na huduma hiyo unaweza kuwa chanzo cha mapato yake?
     Risasi Mchanganyiko halikutaka kupasua kichwa, juzi lilimsaka Masanja kwa simu na kumhoji juu ya mali zake ambapo kwanza alithibitisha kweli anamiliki mali hizo na nyingine ambazo hakupenda kuzitaja.
     “Ni kweli nina nyumba tatu hapa mjini, kampuni ya ulinzi na mashamba ya mpunga eka 50 nyumbani Mbarali, Mbeya. Kuhusu magari pia ni kweli kabisa. Mimi ni mtumishi sitakiwi kusema uongo,” alisema Masanja.
     RISASI: Lakini mbona utajiri wako umekuwa wa haraka sana mtumishi, vipi vyanzo vya mapato yako?
    MASANJA: Orijino Komedi ndiyo chanzo cha vyote... pale ndipo kwenye koki.

     RISASI: Kuchekesha tu kaka? Au kwenye muziki wa Injili pia kunalipa?
    MASANJA: Injili na uchungaji ninaotumika kanisani ni huduma kaka, sitegemei mapato kutoka huko. Nipo kwa ajili ya kulisha kondoo wa Bwana.

    RISASI: Wasanii wenzako wa Orijino Komedi wanachukuaje mafanikio yako?
    MASANJA: Wanafurahia, wananiunga mkono maana ni sehemu ya mafanikio yao pia. Sisi tunaishi kama ndugu. Kwa hiyo kuna baadhi ya aidia ni zao, hivyo wanajivunia sana mafanikio yangu.
    Tuituitui! Simu ikakatika! Risasi likaenda mtamboni.

    VURUGU ZILIZOTOKEA MECHI YA KAGERA SUGAR NA RUVU SHOOTING, KRFA WAMEJIPANGAJE KWENYE MECHI YA KAGERA SUGAR NA SIMBA JUMAMOSI 5-4-2014 KAITABA?



    Kijana wa  Kimasai alisababisha vurugu akiwa amezibitiwa na Polisi akiwa chini ya ulinzi

    Wakati zikiwa zimesalia siku chache kufanyika mtanange mkali wa Kagera Sugar na Simba ligi kuu  vadacom  katika uwanja wa Kaitaba siku ya Jumamosi  5-4-2014 chama cha mpira  Mkoa wa Kagera kimejipangaje kuhakikisha kinathibiti vurugu zinazoweza kutokea na kusababisha kuhatarisha usalama wa mashabiki,Katika mechi ya Kagera Sugar na Ruvu Shooting iliyochezwa jumapili 30-3-2014 tumeshuhudia  vurugu zilizozukiwa na  Kijana mmoja wa kimasai aliemvamia shabiki mmoja alietambulika kwa jina la Moses Nyama  ambae ni msanii katika bend ya muziki ya Kakau kumpiga  akishilikiana na wenzake kwa fimbo huku wakiwa na siraha za visu viunoni na kumjerui kabla ya mashabiki kuingilia kati kumnusuru na badae Polisi kufika wakiwa wakitazama mpira badala ya usalama wa raia. Ili kuzibiti hali hii ya mashabiki kuingia uwanjani na fimbo, visu, mikuki nk KRFA na Jeshi la Polisi mmejipanga vipi katika mtanange wa Kagera Sugar na Simba Jumamosi 5-4-2014 ?

    Huyu ni Mmasai ambae ni miongoni mwa waliojerui akiwa na sime kiunoni akizibitiwa na  Askari waliovaa kilaia






    Mashabiki wanahitaji Amani wakati wote uwanjani


    Shabiki nguli wa Simba MSHAMU




    Mmasai akiwa kapandisha mzuka anataka kupiga mtu na wengine wakiwa wamedhibitiwa na Mashabiki







    Wote hawa wamasai walivamia mtu mmoja kwa fimbo zao ,na kumjerui


    Mwenye kaunda suti ni Katibu wa KRFA Salumu Chama alilazimika kuingilia kati sakata hili




    Baada ya dakika kadha Polisi waliokuwa wakiangalia mpira walikuja baada ya mashabiki kupiga kelele . Na hapa ndio swala la kujiuliza na kufanyiwa kazi, je Polisi anapoingia uwanjani ni kwa ajili ya kuangalia mpira au usalama wa mashabiki? swali kwa wahusika.


    Je kuingia na fimbo na visu uwanjani  ni sahihi?



    Kulia ni Moses Nyama alipata kipigo kutoka kwa Wamasai Japo nae si haba MWANZONI alikabiliana nao.

    Monday, 31 March 2014

    BUKOBA VETERAN WAZINDUA KATIBA NA KUKABIDHIWA JEZI KUTOKA UJERUMANI,HAFLA YADHAMINIWA NA KINYWAJI CHA CLIMAX

     Bukoba Veteran baada ya kukamilisha mchakato ulioanza siku nyingi zilizopita za kuandaa Katiba  hatimae wamezindua Katiba itakayowaongoza,lakini pia wamekabidhiwa Jezi kutoka Ujerumani, mgeni rasmi alikuwa  Sakina Sinda Wakili wa Serikali Mfawidhi wa Mkoa wa Kagera.
     Kapten akipokea jezi
     Wazee wa busara
     Chezea Climax weweeeeeee
     Hafla imedhaminiwa na kinywaji cha Climax
     MCJerry akichombeza
     Mgeni rasmi akiwasili ukumbi wa Lina's
     Katibu wa Bukoba Veteran Raksoni Kahabuka akiongerea mchakato wa Katiba ya Bukoba Veteran
     Climax ni kinywaji  bora viwango vya kimataifa
     Wakipata kinywaji cha Climax
     Mdau Didas Zimbile akiwa na Mainda E
     Optat Katibu
     Wanaveteran
     Bw Wily Kiroyera akieleza jinsi alivyofaamiana na  Fr Gerald Rugumila kupitia mtandao wa Facebook mpaka kuifaamu Bukoba Veteran na  sasa kuwa marafiki na timu kubwa  ya Mainz 05 inayocheza  BUNDESLIGA NA INAYOMILIKI  UWANJA  unaochukua watazamaji 34,036 huko  Ujeruman
     Fr Gerald Rugumila akieleza namna alivyoweza kuijua Bukoba Veteran kupitia kwa Bw Wily Kiroyera
     Mwenyekiti wa Bukoba Veteran Ernest Nyambo akiongea na wadau kuhusiana na siku muhimu na ya kihistoria katika umoja wa Bukoba Veteran
     Fr Mloso wa Ntungamo Seminary akitoa neno
     Bw Kagya Mratibu wa tamasha kubwa litakalofanyika siku ya pasaka Lina;s . Kapotive singles watawasha moto wakiwa na wasanii wa injili wakubwa Tanzania
     Katibu wa KRFA Salumu Chama akiongea na wana Bukoba Veterani
     Chezea Bukoba Veteran weweeee
     UZI wa Mainz 05
     Fr Gerald Rugumila mkazi wa manispaa ya Bukoba Nshamya anaehishi Ujerumani akikabidhi jezi  kwa kapten wa timu Mwinyi ,  Fr Gerald ni shabiki nguli wa Mainz 05 ya Ujerumani inayoshiriki ligi kuu ya BUNDESLIGA, Fr Gerald amekuwa na urafiki wa karibu na Bw Wily Kiroyera kupitia mtandao wa Facebook akiwa Ujeruman na sasa kuwa kiunganishi na Bukoba Veteran
     Baadhi ya wanakamati wa liofanikisha katiba kuwepo
     Mh Matete akifafanua vipengele vya katiba
     Hii ndio Katiba
     Fr Gerald Rugumila akivaa Tshirt aliyopewa kama  zawadi
     Mwenyekiti akieleza kwa ufupi jinsi T.shirt ya Bukoba Veteran itakavyowawakilisha ujerumani
     Mwenyekiti akiwa na Moses wakionyesha uwezo wa kusakata bolingo
     NI NGWASUMA KWA KWENDA MBELEEEE
     Afisa Utamaduni Manispaa ya Bukoba Rugeiyamu akimkaribisha mgeni rasmi
     Mgeni rasmi Sakina Sinda  Wakili wa Serikali Mfawidhi Mkoa wa Kagera akitoa neno katika uzinduzi wa katiba ya Bukoba Veterani katika ukumbi wa Lina's
     Mkurugenzi wa Lina's Mtensa akitabasamu na camera yetu
     Kijana mwiba akionyesha nembo ya Mainz 05 ya ujeruman akiwa na Capten Mwinyi wa Bukoba Veteran
     Rahimu akiwa na Kagya
     Mwenyekiti wa Bukoba Veteran Ernest Nyambo akiongea na wadau akisisitiza kutambua na kuthamini mchango mkubwa wa  kinywaji cha Climax kufanikisha hafla
     Bw Bube mkurugenzi wa shule ya watoto wadogo Leoleo akisoma katiba ya Bukoba Veteran kwa umakini mkubwa akiwa na Super Mkude  mkurugenzi wa shule ya Karume
     Bw Endrew Kagya akielezea ubora wa kinywaji cha Climax kwa niaba ya  wakala  wauzaji wa  Climax mkoa wa Kagera ambao ndio wamedhamini hafla hii
     Kwa raha zetuuuuu
     Hii ndio katiba ya Bukoba Veteran
    Kushoto Fr Gerald Rugumila, Fr Mlosa na  mgeni rasmi Mh Sakina Sinda
     Mgeni  Rasmi akipata chakula
     FR Gerald Rugumila akipata chakula, kiunganishi kikuu kati ya Bukoba Veterani na  timu ya Mainz 05 ya Ujerumani kupitia kwa Wily Kiroyera
     Katibu wa KRFA Salumu Umande Chama akipata chakula
     Wily Kiroyera akipata msosi
     Kamati ya T.shirts za Bukoba Veteran  umekuja mzigo mpya Popote ulipo duniani au Tanzania, Kagera  au Bukoba changia timu kwa kununua T.shirt kwa 20,000 tu .
     Kijana Rakson Kahabuka ndani ya uzi  wa Mainz 05 ya Ujeruman
    Ongera Bukoba Veretan chini ya uongozi wa mwenyekiti Ernes Nyambo kwa hatua kubwa mliyopiga jamcobukoba.blogspot.com tunawatakia ufanisi zaidi.