Tuesday, 4 March 2014

SHOGA ACHOMWA MOTO MCHANA KWEUPEE...NI BAADA YA SHERIA KUPITISHWA NA RAISI MUSEVEN WA UGANDA

http://4.bp.blogspot.com/-rTL48nrSTQU/UxV6VbozVHI/AAAAAAAAN5Y/hQLlExyKa_E/s1600/TWITTER.jpg
uganda waanza harakati za kukomesha mashoga na hyu ndio miongoni mwa mashoga aliye chomwa moto ,kazi kweli kweli sidhani kama wengine wataendelea maana hii ni dawa tosha sasa sijui kwa sehemu kama mombasa ,kenya na Tanzania utaratibu huu si utafaa sana maana tabia hizi zinashamiri sana, hebu serikali iangalie hii njia pengine itakuwa msaada

Monday, 3 March 2014

KARAMBI KATA KIMWANI MULEBA WAMLILIA MASILINGI,WAELEZA NI KAMA WATOTO YATIMA,MATATIZO NA MIGOGOLO YA ARDHI YAKOSA UFUMBUZI

 Picha ya Balozi Wilson Masilingi iliyobandikwa nyumbani kwa mwananchi Karambi kata ya Kimwani Jimbo la Muleba Kusini
 Mzee George Bwahama( Diwani mstaafu na mwenyekiti wa mtaa) ambae ameeleza kilio cha wananchi wa Karambi kuhusiana na kero za wananchi kutokuwa na ufumbuzi,amesema matatizo yanayowakabiri wananchi yamekosa majibu na ufumbuzi kwa kushindwa kuonana na mwakilishi wao waliomchagua na kusababisha kukata tamaa na kupelekea wananchi wengi kumkumbua alie wahi kuwa mbunge wao Wilsoni Masilingi ambae kwa sasa ni Balozi, Bw George amesema katika kipindi cha uongozi wa Masilingi  alikuwa akipata muda wa kukaa na wanachi na kuskiliza kero zao na kuzitaftia ufumbuzi,kitu ambacho kwa sasa ni kama ndoto nma wao kuonekana kama wametengwa, amesema ipo migogoro ya ardhi,matatizo ya huduma za afya, miundombinu, maswala ya elimu nk, yote haya ni kero kwa wananchi ya karambi, akiongelea swala la elimu, amesema katika kipindi cha Masilingi aliweza kuwajengea shule ya sekondari kwa kuchangia kwa asilimia kubwa kutafuta wafadhili na nguvu za wananchi, na akasema shule hiyo ndio mkombozi kwa wananchi wa Karambi.
 Eneo la kijiji cha Karambi
 Tatizo la maji katika kijiji cha Karambi
 Mazingira ya shule ya Sekondari Karambi ambayo ujenzi wake ni nguvu ya Balozi Masilingi
 Majengo ya Sekondari ya Karambi ,jitihada za Balozi  Wilson Masilingi kufanikisha ujenzi
 Mazingira ya shule
 Moja ya eneo korofi Karambi
 Wananchi wa Karambi wakiburudika
Wananchi baadhi wa Karambi, walioelezea mgogolo wa ardhi uliopo eneo la  Burigi lililovamiwa na wahamiaji haramu,walieleza kilikaa kikao kati ya wananchi na Waziri wa  Ardhi, Nyumba na Makazi Prof Anna Tibaijuka tarehe 4-4-2013 mpaka sasa ufumbuzu haujapatikana,japo Waziri alihaidi kutatua mgogolo huu hakuwahi kurudi tena,huwa tunasikia amekuja  anahishia muleba kwake huku haji( NI  MAELEZO YA MMOJA WA WANANCHI)

AFYA YA MWANDISHI WA HABARI WA STAR TV NA RFA YAZIDI KUBOREKA,WADAU WAMTEMBELEA NYUMBANI KWAKE KARAMBI NGOTE MULEBA

 Hali ya afya ya mwandishi wa habari wa Star TV na RFA  Raymond Owaman  inaendelea vizuri,  pichani kama unavyomuona akionyesha maendeleo ya afya yake,kwa muda mrefu sasa alipatwa na ugonjwa wa kiharusi uliosababisha baadhi ya viungo vya mwili kupooza na kushindwa kutembea na kukosa nguvu kabisa,kwa sasa hali yake inazidi kuboreka na kuonekana mwenye furaha na kuweza kuongea na kutamka vizuri, kitu ambacho mwanzoni hsakuweza hata kuongea na kutambua,
 Wadau wakiwasili nyumbani kwa Bw Raymond Owaman
 Mmiliki wa jamcobukoba.blogspot.com  Jamal Kalumuna (Jamco) akisalimiana na Mwandishi Raymond Owaman nyumbani kwake  Karambi Ngote Muleba
 Bw Raymond alijisikia faraja sana na furaha yake akaionyesha wazi,maana hakutegemea kama anaweza kupata wageni ghafla bila taarifa.
 Mke wa Bw Raymond Owaman
 Wadau waliofika kumjulia hali
 Akielezea hali ya maisha yake tangu ameugua na hali halisi ya maisha ya kijijini
 Hii ni picha ya ajari ya ndege iliyotokea 1-5-1997, ni moja ya matukio aliyoripoti kwenye vyombo vya habari, akiwa katika hekaheza za kazi zake
 Picha ya pamoja
 Picha ya pamoja wadau waliokwenda kumtembelea Bw Raymond Owaman
jamcobukoba.blogspot.com inawaomba wadau mbalimbali wafike kumtembelea na kumjulia hali Bw Raymond Owaman, kumfariji na kumpa moyo

HAFRA FUPI YA UJIO WA MKOMBOZI COMMERCIAL BANK BUKOBA.

Mc wa Hafra hiyo Bw. Andrew Kagya akiwakaribisha wageni Ukumbini, Ukumbi wa Hoteli ya Coffee Tree iliyopo Bukoba Mjini, ambayo maandalizi yake yote yamegharimikiwa na kampuni yetu kupitia kinywaji maridadi cha Climax na Windhoek.
Taswira ya Vinywaji maridadi vya Climax na Windhoek.
Waimbaji wa Hapa Mjini Bukoba, Kapotive Star Singers-Bukoba walikuwa tayari kutumbuiza kwenye hafra hiyo ambayo lengo kuu la hafla hiyo ni kupata fursa ya kubadilishana mawazo wakati maswala ya kufungua tawi la benki la Mkombozi Commercial Bank hapa Bukoba.Bwana Respicius Didace wa Mabibo Beer wines & Spirits LTD akifunguka, Kwa niaba ya Kampuni yetu ya Mabibo Beer wine and Spirits, kupitia kinywaji chake cha kimataifa cha Windhoek Premium Lager 100% Pure African Beer na kinywaji kisicho na kilevi cha Climax Non Alcoholic Herbal Energy Welcome Drink, tunawakaribisha sana jioni ya leo kwenye hafla fupi ambayo ni muhimu sana kwetu wana Bukoba.

Leo tumebahatika kuwa na Mkurugenzi wa Mkombozi Commercial bank ambae ataweza kutumegea machache kuhusu benki hii, na pia hata sisi tutapata nafasi kumuuliza maswali ambayo tunadhani yatasaidia katika kuongeza uelewa wetu kuhusu benki hii. Pia atatuonesha fursa zinazotokana na uwepo wa benki hii hapa Bukoba hasa kwa kununua hisa zake.

Kampuni yetu ya Mabibo Beer & Spirits Ltd inaamini katika kuwaleta watu pamoja, ndio maana wakati wa maandalizi ya hafla yetu hii, tumeawaalika wafanyabiashara wanaochipukia, wafanyabiashara wakubwa kwa kadiri ya mji wetu, viongozi wa dini, viongozi wa serikali, wawakilishi wa baadhi ya shule maarufu hapa Bukoba, wawakilishi wa wananchi kwenye kata (Madiwani) n.k. Hii ni fursa ya kufahamiana na watu mbalimbali katika nyanja mbalimbali wakati tunaendelea kuburudika na vinywaji vyetu vya Windhoek, na kwa wale ambao hawatumii kilevi wakifurahia Climax (Non Alcoholic Energy Drink).
Mr. Nicholas Mokirya-Branch Manager Mwanza Branch nae alikuwepo kwenye hafra hii na hapa alikuwa akitoa neno.Mheshimiwa mgeni rasmi, Mama Edwina Lupembe, Mkurugenzi wa “Mkombozi Commercial Bank" akiwamegea machache kuhusu benki hiyo ya Mkombozi
Kulia ni Fr. Vitus Mrosso nae alikuwa tayari kwenye meza kusikiliza wito huo kwenye hafra hiyo swala zima likiwa ni kununua Hisa za Mkombozi commercial Bank ili kuweka akiba binafsi.
Wadau wakifuatilia kwa makini...
Bi. J. Murungi na Mr. Bube wakiteta jambo hapa wakati wa hafra hiyo
Mr. Bigambo (kushoto) nae alikuwepo mahala hapo
Lengo kuu la hafla hii ni kupata fursa ya kubadilishana mawazo wakati tunapoelekea kufungua tawi la benki la Mkombozi Commercial Bank hapa Bukoba.
Baadhi ya wafanyabiashara wa hapa Mjini Bukoba wakifuatilia kwa makini
Askofu Msaidizi Methodius Kilaini wa Jimbo Katoliki la Bukoba akisalimiana naWaziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka.
Kapotive Star Singers-Bukoba wakiendelea kuimba nyimbo mbalimbali
Kapotive Star Singers-Bukoba wakicheza Ngoma  wakati wa hafra hiyo
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Edwina Lupembe akiteta jambo.
Taswira Ukumbini hapo Coffee Tree Hotel katika hafra hiyo iliyokuwa chini ya ya Uzamini wa Udhamini wa Windhoek and Climax.
Fr. Vitus Mrosso akiuliza swali kuhusu swala zima la Benki hiyo ya Mkombozi na Mikopo yake
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka(kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Edwina Lupembe (kulia) wakifurahia jambo kwenye meza kuu wakati wa hafra hiyo.
Meza kuu
Bi. Jeniffer Murungi Kichwabuta nae akiuliza swali kuhusu Hisa za Benki hiyo
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Edwina Lupembe(katikati) akijibu maswali
Bi. Edwina Lupembe hakuishia hapo kujibu maswali tu aliendelea pia kuwapa faida za benki hiyo ya Mkombozi na kuwataka wakazi wa Bukoba kuendelea kununua Hisa kwa wingi zaidi.
Askofu Msaidizi Methodius Kilaini wa Jimbo Katoliki la Bukoba (kulia) akitoa neno, Benki ya Mkombozi ni sauti ya kinabii inayolenga kuwaletea watanzania ukombozi wa kweli. Benki ya Mkombozi iliyozinduliwa mwaka 2009, kwa kianzio cha mtaji wa Shilingi Bilioni sita nukta nane, mchango wa waamini wa Kanisa Katoliki, inalenga kuwasaidia watu wa kipato cha chini kuinua hali yao ya maisha na wawekezaji kupanua kiwango chao cha kuwekeza kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania wote pasipo na ubaguzi.Askofu Msaidizi Methodius Kilaini wa Jimbo Katoliki la Bukoba (kulia) akionesha juu kwa wale ambao hawatumii kilevi wakitumie Climax (Non Alcoholic Energy Drink). Ambapo maandalizi yote yamegharimikiwa na kampuni kupitia kinywaji maridadi cha Climax na Windhoek.
Hata na mimi natumia kinywaji hiki cha Climax  (Non Alcoholic Energy Drink) Askofu Msaidizi Methodius Kilaini wa Jimbo Katoliki la Bukoba akikinanga kinywaji hicho!
Askofu Msaidizi Methodius Kilaini wa Jimbo Katoliki Bukoba, ni kati ya wajumbe wa Kikosi kazi, waliopewa dhamana kushughulikia mchakato wa uanzishwaji wa Benki ya Mkombozi nchini Tanzania. Hii ni sauti ya kinabii, katika mapambano dhidi ya umaskini. Ninakualika sasa uweze kujiunga na Askofu Msaidizi Kilaini kwa ufafanuzi zaidi kuhusu dhamana ya Kanisa ndani ya Jamii na Benki ya Mkombozi.
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka nae aliguswa na Kinywaji hicho cha Climax
Rahim Abdul Rahim Kabyemela akipongezwa na Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka  kwa kazi nzuri anayoifanya hapa Bukoba akiwa yeye ndie Balozi na msambazaji wa Vivywaji hivyo vinavyopendwa hapa Kagera.