Thursday, 9 January 2014

DADA WA KAZI ANAVAA HIVI , MAMA MWENYE NYUMBA UPO UNAANGALIA TU, UNATEGEMEA NINI?


Wapo watu ambao bado hawajajua
madhara ya mavazi, mavazi yanaweza
kuharibu nyumba, dada wa kazi
akijiachia namna hii na mwenye
nyumba unaangalia tu madhara ni
makubwa labda kama mnaishi wawili
tu hapo ndani ila kama unaishi na
mumeo kazi unayooo..!!

Tuesday, 7 January 2014

*PICHA YA KUFUNGUA MWAKA 2014 WAFUASI WA CHADEMA WALIPOCHAPANA KAVU KAVU JANA


  Mfuasi wa Chadema akiwa chini baada ya ‘kukatwa mtama’ na mfuasi mwenzake wa chama hicho baada ya kutokea vurugu baina ya wafuasi wanaounga mkono uongozi na wale wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, baada ya kuahirishwa kwa hukumu ya kesi ya mbunge huyo katika Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam jana. Picha na kwa hisani ya Mwananchi.com 
**************************************
Dar es Salaam.Wafuasi wa Chadema wanaomuunga mkono aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe na wanaounga mkono uongozi wa juu, jana walitwangana tena muda mfupi baada ya kuondoka eneo la Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam.
Tukio hilo limetokea huku Mahakama hiyo ikiahirisha hadi leo, kutoa uamuzi wa maombi ya Zitto kuzuia kujadiliwa na Kamati Kuu ya Chadema.
Katika maombi hayo namba 1 ya mwaka 2014, Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, anaiomba Mahakama iizuie Kamati Kuu ya Chadema kumjadili na au kuchukua uamuzi wowote kuhusu uanachama wake hadi kesi yake ya msingi aliyoifungua mahakamani hapo itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
Uamuzi wa maombi hayo ulipangwa kutolewa jana na Jaji John Utamwa ambaye hata hivyo, alisema alikuwa hajamaliza kuandika uamuzi huo na kuahirisha shauri hilo hadi leo mchana.
Maombi hayo ya Zitto ya zuio la muda la kujadiliwa na kuchukuliwa uamuzi wowote kuhusu uanachama wake yametokana na kesi ya msingi aliyoifungua mahakamani hapo Januari 2, 2014, dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema na Katibu Mkuu wa chama hicho.
Katika kesi hiyo, Zitto pia anaiomba Mahakama Kuu imwamuru Katibu Mkuu wa Chadema ampatie mwenendo na taarifa za kikao cha Kamati Kuu za kumvua nyadhifa zake zote alizokuwa nazo ndani ya chama na iwazuie walalamikiwa kumwingilia katika utekelezaji wa majukumu yake ya ubunge wa Kigoma Kaskazini.
Mapigano
Baada ya kuahirishwa kwa shauri hilo, wanachama wa makundi yote waliondoka eneo la Mahakama wakiendelea kuimba na kushangilia lakini walipofika eneo la Mahakama ya Rufani ghafla walianza kupigana ngumi na mawe. Baadhi yao walikamatwa na askari kutokana na vurugu hizo.
Awali, wafuasi hao walifika mapema asubuhi katika viwanja vya Mahakama tayari kusikiliza uamuzi huo.
Ulinzi ulikuwa umeimarishwa na askari polisi wakiwamo wale wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), waliokuwa na silaha pamoja na mabomu ya machozi walikuwa wametanda.
Pia kulikuwa na askari wa Kikosi cha Mbwa pamoja na gari la maji ya kuwasha.
Licha ya kuwahi, ni wafuasi wachache walioruhusiwa kuingia ndani ya u`kumbi wa Mahakama tena baada ya kuandikisha majina yao huku wakitambuliwa na viongozi wao waliokuwapo.
Baada ya idadi iliyokuwa ikihitajika kutimia, wafuasi wengine waliambiwa wasubiri kutapata taarifa za uamuzi huo baadaye.
Wakiwa wanasubiri, walikuwa wakitambiana kwa maneno na nyimbo.
Kundi la Zitto lilikuwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali wa kumsifu na bendera za chama hicho pamoja na ngoma huku likikejeli kundi linalounga mkono uongozi wa chama hicho.
Baadhi ya mabango yalisomeka ‘Zitto kama Mandela’, ‘Zitto Mkombozi.’
Baadhi ya maneno waliyokuwa wakiyatamka katika nyimbo zao ni pamoja na `Zitto Kwanza’, chama (Chadema) baadaye.
Wafuasi wa uongozi nao walikuwa na mabango yaliyosomeka: ‘Hongera Mbowe kwa ujasiri,’ ‘Kunguru hafugiki’ na ‘Zitto rudisha kadi yetu’.
Awali, kundi linalounga mkono uongozi lilidai kwamba wanaomuunga mkono Zitto si wanachama halali wa chama hicho, bali wamenunuliwa kwa lengo la kwenda mahakamani.
Tofauti na siku ya kwanza ya kusikilizwa kwa maombi ya Zitto, ambayo kundi linalounga mkono uongozi lilidai kuwa wafuasi wa Zitto wameandaliwa na CCM, jana liliwatuhumu kuwa wameandaliwa na CUF.
Baadhi ya viongozi wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha), walisikika wakilalamika kwa askari kuwa wafuasi hao wametoka mitaani na wengine ni wa CUF.
CUF wakana tuhuma
Hata hivyo, CUF jana kimekana kuhusika na mgogoro huo unaoendelea Chadema. Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Julius Mtatiro alisema jana kuwa kuna taarifa zimesambaa kuwa CUF kilikuwa kimeandaa vijana wa kwenda mahakamani jana kwa ajili ya kufanya vurugu.
“Wadau, waandishi wengi wa habari walinipigia nithibitishe ikiwa CUF iliandaa makundi ya wanachama wakamshabikie ZZK (Zitto) mahakamani leo (jana) hii. Taarifa ya namna hii pia imeenea mitandaoni.
“Pia viongozi kadhaa wa Chadema wamenipigia kunijulisha kuwa intelijensia yao imegundua kuwa vijana wa CUF wamepenyezwa na kwamba wamevishwa T-shirt (fulana za M4C na mapanga,” alisema Mtatiro na kusisitiza kuwa CUF hakijapanga wala kutuma makundi ya vijana kwenda kumshabikia Zitto.
Alisema ikiwa wanachama wa CUF wameonekana mahakamani itakuwa ni kwa utashi na matakwa yao.
“Hatujawahi kukutana, kupanga wala kutuma vijana wa CUF wakasimamie upande wowote katika mgogoro huu.
Wakati wa fukuto la Hamad Rashid na CUF watu wengi tu raia walifika mahakamani, hatukuhoji na kutafuta vyama vyao, tuliamini ni Watanzania tu,” alisema Mtatiro na kuongeza:
“Ni vigumu kwa CUF kukataza wanachama wake wasihudhurie kesi maarufu kama ile ya Babu Seya, Sheikh Ponda, Zitto Kabwe, Samaki wa Magufuli na nyinginezo.” CHANZO MWANANCHI

ZITTO KIDEDEA, AIBWAGA CHADEMA MBELE YA TUNDULISU MAHAKAMA KUU LEO


 HONGERA: Wakili wa CHADEMA Tundu Lisu (kulia) akilazimika kumpongeza aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe baada ya Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, John Mkamwa, kuridhia zuio la Zitto asijadiliwe na ngazi yoyote ya maamuzi ya Chadema, hadi kesi ya msingi aliyofungua dhidi ya chama hicho itakapomalizika. Jaji huyo amekubali kesi ya msingi iungurume na itaanza kusikilizwa Februari 13, mwaka huu.
 Zitto akitoka kwa msaada wa mabaunsa wake katika chumba cha mahakama kuu baada ya uamuzi huo wa  Mahakama kuu leo jioni.
Tundu Lisu na wapambe wake wakionekana kutoka kwa aibu Mahakamani baada ya kubwagwa

 Tundulisu aklizungumza na waandishi nje ya mahakama
 Wakili wa Zitto akizungumza na waandishi nje ya mahakama kuu
 Wafuasi wa Chadema wanaomuunga mkono Zitto wakishangilia abaada ya ushindi wa kiongozi huyo

MABIBO BEER WINES AND SPIRITS LTD WAZINDUA WINDHOEK NA CLIMAX WALKGARD TRANSIT BUKOBA

 Ni mwonekano na mandhali ya usiku wa Windhoek na Climax katika hotel ya Walkgard Transit Bukoba
 Wadau mbalimbali wakipata chakula cha usiku kilichoandaliwa na kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd yenye makao makuu jijini Dar-es-salaam ,chini ya mkurugenzi mkuu James Rugemalira
 Ni mwonekano wa kinywaji cha Climax,Ni kinywaji laini hakina kilevi unapokitumia kinakufanya kuwa mchangamfu na mwenye nguvu mwilini.
 Ni wageni mbalimbali wakiwasilikwenye Hafla ya usiku wa Windhoek na Climax,  Mlangoni unapewa Climax moja wakati ukisubiri utaratibu mzima.
 Bw Bushira akiangalia kwa makini kinywaji cha Climax baada ya kusikia utamu wake hakina alcohol.
 Mh  Janat Musa Kayanda (Katibu wa ccm Manispaa ya Bukoba) akifurahi
                                                Mwakilishi kutoka Coffee Hotel Bukoba
 Mgole shop akiburudika na Windhoek taratibu
 Jamco akiwa na Jerome Rugemarila(Mkurugenzi Mtendaji wa Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd
  Mwana libeneke Bukobawadau Mc Baraka na Bw Jorome Rugemarila
 Mwenyekiti wa Mahotel ya Walkgard na Transit Bw Robert Matungwa (katikati) akifurahia Windhoek
 Mkurugenzi mtendaji wa Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd Jorome Rugemarila akiwakaribisha wageni kwenye uzinduzi na usiku wa Windhoek na Climax.
Bw     Basibila  sambamba na cha Windhoek
 SuperMkude akiwa na Bw George
 Haya ndio mambo ya usiku wa Windhoek na Climax
 Bi Modesta Kainami aka Kibengwe,Lilian Peter,sambamba na Nyamwiza (Mama Hasani)
 Basibila alikikubari kinywaji cha Windhoek akiwa na Jorome(kushoto)
 Lilian Peter amewakubali Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd

 Bw Audax (kulia) na Bw Brandes Meneja wa Bukoba Coop Hotel
 Bw Mandela
 Bw WillyKiroyera akiwa na Mh Kiraja
 MwlMarius(Rugambya sekondar, kulia) na Bw Shamsu
                                           Bw Edigar Rutarakana Dada Gode Bayona
 Bw Kamala sambamba na mdau wa Windhoek  kutoka Ujerumani
Mr & Mrs Deo Rugaibura
 Bw Twaha Msoke , kulia ( Meneja Lake Hotel) na Bw Alistides Musheshe ( Meneja wa Bukoba Hotel E.L.C.T)
  Bw  Mandela akifurahia usiku wa Windhoek
Huo ndio ulikuwa usiku na uzinduzi wa Windheok na Climax Walkgard Transit Bukoba