Thursday, 2 January 2014

MAREHEMU SADICK SUED KAGASHEKI AZIKWA LEO NYUMBANI KWAKE MARUKU KANYANGEREKO BUKOBA

 Picha ya marehemu Sadick Sued Kagasheki aliezikwa leo mchana nyumbani kwake Marukuku Kanyangereko, marehemu amefariki 1-1-2014 na kuzikwa leo 2-1-2014, ameacha wajane watatu , watoto 16 na wajukuu 32, Innahlilah wainalijiuni.
                Watu mbalimbali wakiwasili nyumbani kwa marehemu Maruku Kanyangereko leo
                                    Marehemu Sadick Sued Kagasheki akiswaliwa
                                                 Jeneza la marehemu likiletwa kaburini
                                                            Mazishi yakiendelea
                                                              Dua baada ya mazishi
                                             Mh Amida Adamu Kagasheki
                                                        Bw Kabaka
                         Kaimu  Shekhe wa Mkoa Kagera Haruna Kichwabuta akitoa mawaidha
                      Alhaji Abubakari Kagasheki akitoa neno la shukrani kwa niaba ya familia
Abdul Kagasheki Mnec Ccm Bukoba mjni akisikiliza mawaidha ya shekhe Haruna Kichwabuta

Wednesday, 1 January 2014

WAZIRI MGIMWA AFARIKI DUNIA NCHINI AFRIKA YA KUSINI


Habari zilizoufikia mtandao huu hivi punde zinasema kuwa aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dkt. William Mgimwa amefariki dunia mchana wa leo huko nchini Afrika ya Kusini alikokuwa amelazwa katika Hospitali ya Mediclinic Kloff. 

Habari zaidi kuhusu msiba huu zitawajia kdri zitakavyokuwa zikipatikana. Mungu ilaze roho ya marehemu, Dkt. Mgimwa mahala pema peponi, Amina.

*NJEMBA YAGOMA KUSHUKA KUTOKA JUU YA MNARA WA SIMU UBUNGO JIJINI DAR AKIHITAJI KUONANA NA RAIS(HII NI FUNGA MWAKA 2013)

 Askari wa Kikosi cha Zima moto na Uokoaji Wakiwa wamepanda juu ya Mnara wa Simu Uliopo Ubungo Jijini Dar Es Salaam Muda mfupi uliopita kwaajili ya kumuokoa kijana mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Hassan Ambaye alipanda juu ya mnara huo kwa lengo la kufikisha Ujumbe wa kutaka kuonana na Raisi Kikwete ili aweze kumwelezea kwa kile anachodai kuwa jeshi la polisi lilimbambikia kesi na hatimaye kuhukumiwa kifungo cha Miaka 6 kwenda jela

 Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji wakiendelea na zoezi la kumuokoa Kijana Hassan kwaajili ya kutojirusha kutoka Juu ya Mnara wa Simu Muda mfupi uliopita Ubungo Jijini Dar Es Salaam Leo
Hapa akishushwa na askari wa Kikosi Cha Zimamoto na Uokoaji
Hapa Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji akiwa amemuweka begani na Kushuka nae chini Mara baada ya kufanikiwa Kumshika vizuri kwaajili ya kumteremsha chini bila kupata madhara
 Kijana aliyefahamika kwa jina moja la Hassan akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kushushwa juu ya Mnara wa Simu na Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji muda mfupi uliopita Ubungo jijini Dar
 Tukio likiendelea huku wakazi wa jiji la Dar Wakiendelea kushuhudia. 
 Raia wakishuhudia tukio hilo
 Wakazi wa Jiji la Dar wakishuhudia tukio hilo lililotokea muda mfupi uliopita Ubungo Jijini Dar leo
Gari la Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji likiwa limetia timu eneo la tukio kwaajili ya Kuokoa

Wakazi wa Jiji la Dar wakishuhudia gari la Polisi likiondoka na Kijana Hassan ambaye alipanda juu ya Mnara leo Ubungo jijini Dar Es Salaam.

RAIS KIKWETE AMWAPISHA IGP MPYA PAMOJA NA NAIBU WAKE LEO IKULU


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Ernest Mangu katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpatia nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Naibu  Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Abdulrahman Kaniki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali na Katibu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Ernest Mangu na naibu wake Naibu IGP Afande Abdulrahman Kanini katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali Mawaziri na Katibu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Ernest Mangu na naibu wake Naibu IGP Afande Abdulrahman Kanini katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na IGP mpya Afande Ernest Mangu,  Naibu  Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Abdulrahman Kaniki pamoja na IGP mstaafu Afande Saidi Mwema katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na IGP mpya Afande Ernest Mangu,  Naibu  Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Abdulrahman Kaniki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam