Friday, 22 November 2013

JENGO LA RAS KAGERA LINALOTUMIWA NA BARAZA LA ARDHI NA NYUMBA BUKOBA LAFANYIWA UKARABATI

 Mwenyekiti wa baraza la Ardhi na nyumba bukoba mh Renatus Leonard Chenya , amesema jengo la Ras Kagera linalotumiwa na Baraza la Ardhi na nyumba kwa ajili kutatua kesi na migogoro mbalimbali inayohusu Ardhi na nyumba linafanyiwa ukarabati na wizara ya Ardhi, nyumba na makazi kwa kusimamiwa na  National Housing and Building Research Agency(NHBRA) katika kuboresha huduma za jamii, Bw Renatus ameeleza pia ukarabati huu umeshafanyika katika baadhi ya wilaya mkoani kagera zikiwemo za  Muleba,Karagwe na Ngara.
                                          Muonekano sehemu ya mbele
                              Sehemu ya mbele ya  Balaza la Ardhi na Nyumba Bukoba
                                                                     Ukarabati unaendelea
                                                         Muonekano sehemu ya nyuma
                                 Jengo hili linalofanyiwa ukarabati,limejengwa kipindi cha mkoloni

MAFURIKO YA SENENE BUKOBA LEO

 Ni mafurushi yaliyosheeni senene  leo katika maeneo ya soko kuu bukoba, hali hii inaashilia msimu wa senene kuanza.
                                                 watu wakiwa busy kununua senene
 Barabara ya jamhuri soko kuu leo ilikuwa watu wanapishana kwa shida , watu wakinunua senene
                                                                     Hii ndio hali halisi
                Bw richard leo mwenye upara mkurugenzi wa kasibante redio nae akinunua senene
 Magari yamekuwa yakipishana kwa shida asubuhi ya leo kutokana na mrundikano  wa watu
 senene wameuzwa kati ya 500 na 1000 kwa kiganja, na wengine wamekuwa wakiuza kwa jumla
                                                                              mafuriko si mchezo.....

                                                    Mama na fuko la rambo ,anaelekea home

Thursday, 21 November 2013

NDOA YA PACHA WA P-SQUARE YAINGIA DOSARI


Jumapili ya November 17, 2013, jiji la Lagos, Nigeria lilishuhudia harusi kubwa ya kitamaduni kati ya muimbaji wa kundi la P-Square, Peter Okoye na mchumba wake Lola Omotayo, lakini cha ajabu, kaka yake mkubwa, Jude Okoye hakuwepo.
 
Msemaji wa kundi hilo Bayo Adetu alisema Jude hakuwepo kwenye harusi kwakuwa alikwama nchini Ghana.
Jude_okoye-2 Jude Okoye
P-Square walikuwa wametumbuiza jijini Accra, Ghana kwenye show ya ‘Glo and Bounce Slide‘ siku moja kabla ya harusi na hivyo Adetu akadai kuwa Jude alikosa ndege na hivyo kushindwa kurejea Lagos kushuhudia harusi hiyo iliyohudhuriwa na mastaa kibao akiwemo Diamond Platnumz.
 
Lakini chanzo cha sehemu ya kundi la wasanii wengine walioenda Ghana kwenye show hiyo kilisema Jude hakwenda Ghana. 
 
‘Hatukumuona, mapacha hao walikuwa hapa na bendi yao lakini hatukumuona Jude‘, chanzo hicho kilisema.
 
Vyanzo vya ndani kwenye familia ya Okoye vimedai kuwa Jude Okoye na wanafamilia wengine hawakuiunga mkono ndoa ya Peter na mama wa mwanae Lola Omotayo. Vyanzo vingine vimedai kuwa marehemu mama yao naye hakuwa akiuunga mkono uhusiano huo.
dc6c29ec506111e387720e8e429886c3_8 Lola
‘Jude na wengine hawampendi. Hawakutoa baraka zao kwa ndoa hiyo. Hata Paul pia, lakini ni pacha wake. Hata ndugu wengine walikuwepo pale walikuwa wagumu pia kuhudhuria. Jude hakwenda kwasababu hakuwa ameliunga mkono wazo hilo tangu siku ya kwanza,’ chanzo cha familia hiyo kilisema.
LolaOmotayoMakeupLook2_that1960chickdotcom  Lola ni mrembo haswaa
Baadhi ya wanafamilia wa Okoye walienda mbali zaidi na kudai kuwa Lola Omotayo anadaiwa kumsaliti Peter Okoye mara kwa mara. Inadaiwa kuwa walikuwa wanadai vifanyike vipimo vya DNA kubaini kama kweli Cameron na Aliona ni wa Peter kweli ama kashikishwa tu.

 
Peter akiwa na mwanae Cameron
‘Ni serious kabisa, wanadai kuwa Lola hulala na wale anaowaita ‘wajomba’ na wanataka vifanyike vipimo vya DNA, wanataka kumlinda kaka yao.’
   
 

AFANDE SELE APOKELEWA KWA SHANGWE BAADA YA KUJIUNGA CHADEMA







Mwanamziki mashuhuri Tanzania, anayejulikana kama Afande Sele Amejiunga na M4C, kwa kuingia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo. Mji wa morogoro ulirindima vifijo wakati Afande akizunguka na Msafara wa Piki Piki kuwaaga rasmi wale wasio na misimamo thabiti Kisiasa, kama inavyoonekana katika picha. 

kwa upande mwingine wapenzi wa CCM walionekana kuwa nahofu na uchungu, na walihisi sasa mambo yanazidi kuwa magumu sana kwao.

Kata ya mafiga wa upande wake ilionekana kutekwa kabisa na CHADEMA, huku katika mkutano wa Ndani Afande Sele alichaguliwa kushika nafasi ya Uenyekiti wa kata hiyo, katika kipindi hiki cha kushusha chama kwa wananchi (Program ya Chadema ni msingi), ambayo imekuwa mwiba mkali kwa CCM.

WASHIRIKI WA TANZANIA TOP MODEL KUPIGA KAMBI GIRAFFE OCEAN VIEW HOTEL


 Mkurugenzi Tanzania Top model Ysufu George akiongea na wanahabari kuhusu ujio wa kuweka kambi ya siku 17 ya wanamitindo hao katika Hoteli ya Giraffe ocean view iliyomo Frikana jijini Dar.
 Wanamitindo wakiwasili leo mapema Giraffe Ocean View Hotel wakitokea Tamar Hotel walikokuwa wameweka kambi ya siku mbili baada ya kutokea hotel ja Jb Bekmont.
Giraffe ocean View Hotel ,hoteli yenye hadhi ya nyota nne,karibu Giraffe upate huduma zilizo sawa na thamani ya pesa zako,inasifika kwa ukarimu uliopita kiwango.

Wednesday, 20 November 2013

JICHO LA CAMERA YETU BUKOBA MAENEO TOFAUTI LEO

 Ni maeneo ya Jamuhuri road karibu duka la vifaa vya ujenzi kwa Bandari dukani kwa Mh Murungi Kichwabuta akiwa na Mwl Bishanga(mwenye nguo nyekundu)wakiwa na mmliki wa  jamcobukoba.blogspot.com
 Enkonjwa au Gonja ni chakula kinachopendwa  na watu wengi sana, Aidha waweza kuzitengeneza kwa namna tofauti, waweza kuzichoma zikiwa mbivu, kuzikaanga au kuzichesha, au kuzichanganya na vyakula vingine.
                            Camera yetu maeneo ya soko kuu senene wameanza kupatikana
 Camera yetu maeneo ya kashai ,barabara iendayo kahororo  ni utaalamu wa kukamata senene,kama uonavyo ni teknologia ya kisasa inayotumika kukamata senene inayohitaji mtaji kwa kiasi fulani  kwa ajili ya kununua taa kubwa zenye mwanga mkali, mabati,mapipa au majaba makubwa, nishati ya umeme na rasilimali watu kwa ajili yakukusanya wanapokamatwa,kwa kipindi hiki watu wengi uingia katika biashara hii ambayo ukiifuatilia kwa karibu ni biashara ambayo inalipa na watu kujipatia kipato kikubwa ambacho kwa hali ya kawaida si rahisi kugundua kwa haraka.
 Camera yetu katika kanisa la mchungaji King James wa kashai ambae amejenga kanisa kubwa na la kisasa maeneo ya kahororo kyamaizi,Mchngaji King James amejizolea sifa rukuki kwa maubili yake na uponyaji kiroho na kwa muda mfupi kanisa lake kuwa na waumini wengi sana.
                           Mchungaji James (mwenye kofia) akiwa na Ramadhani kambuga
                                      waitu banyegere, jamani karibuni senene fresh wa leoleo
                                     kipindi hiki mabucha ya nyama hupata wakai mgumu
                                                          senene wakiwa wameshamenywa
                                              Kijana akiwajibika kumenya,akiwa katika ajira
                                                 Stand ya Tax soko kuu kwenye senene
 Vitu adimu maeneo mengine, lakini bukoba vinapatikana kwa wingi, entura,pilipili,namaharage mabichi
                Mh Murungi Kichwabuta akiwa amenunua pilipili mbuzi kwa matumizi ya nyumbani
 Wadada hao wawili wamejiajili kwa kutembeza ,pilipili.maharage,entura,entongo na vitu vingine kwenye maduka ya watu mbalimbali
                                                   Ongereni wadada kwa kujiajiri na kujitafutia kipato