Wednesday, 13 November 2013
*RAIS JAKAYA KIKWETE AIFARIJI FAMILIA YA DKT. SENGONDO MVUNGI, MWILI KUWASILI IJUMAA NOV 15
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo
nyumbani kwa aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na
kiongozi mwandamizi wa chama cha NCCR Mageuzi, marehemu Dr. Sengondo
Mvungi huko Mbezi Kibamba jijini Dar es Salaam leo mchana.
***************************************
***************************************
*Mwili wa Dkt. Sengondo Mvungi kuwasili Ijumaa, Novemba 15, 2013
Tume
ya Mabadiliko ya Katiba inawafahamisha wananchi kuwa taratibu za
kuusafirisha mwili wa Mjumbe wake, Dkt. Sengondo Mvungi aliyefariki
nchini Afrika Kusini zimekamilika na mwili wake unatarajia kuwasili
nchini siku ya Ijumaa, Novemba 15, 2013.
Baada ya kuwasili, mwili huo utahifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Aidha,
siku ya Jumamosi, Novemba 16, 2013 kutafanyika Ibada ya mazishi katika
Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam kuanzia saa
4:00 asubuhi. Baada ya misa, marehemu ataagwa katika Viwanja vya
Karimjee kuanzia saa 6:30 mchana siku hiyohiyo ya Jumamosi, Novemba 16,
2013.
Aidha,
Marehemu Dkt. Mvungi anatarajiwa kusafirishwa siku ya Jumapili, Novemba
17, 2013 kwenda Kisangara Juu, Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro kwa
ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika siku ya Jumatatu, Novemba 18,
2013.
Dkt.
Mvungi alifariki jana (Jumanne, Novemba 12, 2013) katika Hospitali ya
Millpark jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini alikopelekwa kwa ajili
ya uchunguzi na matibabu zaidi akitokea Kitengo cha Mifupa Muhimbili
(MOI) aliokuwa amelazwa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake Kibamba, wilaya
ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na watu waliomjeruhi vibaya kichwani
usiku wa kuamkia siku ya Jumapili, Novemba 3, 2013.
Wakati huohuo,
Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakiongozwa na Mwenyekiti wake
Jaji Joseph Warioba leo (Jumatano, Novemba 13, 2013) wameungana na
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete kufika nyumbani kwa marehemu Dkt. Mvungi eneo la Kibamba jijini
Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa pole kwa familia, ndugu na jamaa wa
marehemu Dkt. Mvungi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiifariji familia ya Marehemu Dkt.Sengondo
Kikwete akataa zawadi ya dhahabu
KATIKA hali ambayo watu wengi
wasingetarajia, Rais Jakaya Kikwete amekataa zawadi ya dhahabu aliyopewa
na Kampuni ya Nyamigogo Grand Vezir Holdings ya mkoani Geita.
Badala yake ameelekeza dhahabu hiyo safi
yenye uzito wa gramu 227 na yenye thamani ya Sh milioni 16 iuzwe na
fedha zake zitumike kusaidia watoto yatima.
Rais alitoa maelekezo hayo juzi baada ya
kukabidhiwa zawadi hiyo wakati wa sherehe ya kuzindua mgodi wa
uchenjuaji dhahabu wa kampuni hiyo, nje kidogo ya mji mdogo wa Kharuma
yaliko makao makuu ya wilaya mpya ya Nyang’hwale, Geita.
Baada ya kukabidhiwa zawadi hiyo, Rais
Kikwete aliuliza: “Sasa nifanye nini na zawadi hii? Nawarudishieni hii
dhahabu, iuzeni popote mnakotaka na fedha itakayopatikana tutawapa
watoto yatima.”
Akizungumza na wananchi katika mgodi
huo, Rais Kikwete aliupongeza uongozi wa mgodi huo akisema umeongeza
thamani ya dhahabu na ya maisha ya wananchi katika eneo hilo nje ya mji
huo.
Hata hivyo, Rais aliushauri uongozi wa mgodi huo kufanya jitihada za kuboresha teknolojia inayotumika.
“Mmefanya vizuri sana na mgodi huu ni
mradi wa maana sana kwa kuongeza thamani ya dhahabu na kuboresha maisha
ya wananchi katika eneo hili. Ubunifu huu unastahili pongezi.”
Aliongeza: “Lakini lazima tuboreshe
teknolojia. Teknolojia inayotumika kwenye mgodi huu bado ni ya zamani
kidogo. Hii ni sawa na hadithi ya mtu mwenye chongo katika jamii ya
vipofu watupu. Yeye anaonekana kama mfalme.”
Mgodi wa Nyamigogo ambao ni wa marudio
kwa maana ya kuzalisha dhahabu kutokana na mchanga ambao huko nyuma
ulifukuliwa na kutoa dhahabu, ulianzishwa mwaka 2011 na mpaka sasa
zimewekezwa Sh bilioni 1.6 katika uendelezaji wa mgodi huo.
Risala ya uongozi wa mgodi ilisema mgodi
huo unaozalisha kiasi cha gramu kati ya 500 na 600 kwa mwezi unaajiri
watu 45 wakiwamo wanawake 10.
Tangu kuanzishwa kwake, mgodi umekuwa
unaunga mkono shughuli za jamii inayouzunguka, ikiwa ni pamoja na
kujenga zahanati na madarasa ya shule katika vijiji viwili.
Rais Kikwete alizindua mgodi huo, ikiwa
ni sehemu ya kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo katika ziara yake
rasmi ya kikazi katika mkoa wa Geita, moja ya mikoa minne ambayo
aliianzisha mwaka jana. Mingine ni Simiyu, Njombe na Katavi.
Tuesday, 12 November 2013
MVUNGI AFARIKI DUNIA
Mjumbe
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba aliyekuwa akipatiwa matibabu nchini Afrika
Kusini amefariki dunia leo..
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw.
Assaa Rashid leo jioni (Jumanne, Novemba 12, 2013), Dkt. Sendongo Mvungi majira
ya saa 8:30 mchana kwa saa za Afrika ya Kusini akiwa katika Hospitali ya
Milpark.
“Kwa
masikitiko makubwa, Tume inawafahamisha wananchi kuwa Mjumbe wake, Dkt.
Sengondo Mvungi aliyekuwa akipata matibabu katika Hospital ya Milpark iliyopo
jijini Johannesburg nchini
Afrika Kusini amefariki dunia leo (Jumanne, Novemba 12, 2013) saa 8:30 mchana
kwa saa za Afrika ya Kusini,” amesema Bw. Rashid katika taarifa yake fupi ya
awali na kuongeza:
“Taratibu
za kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka nchini Afrika Kusini kuja nchini kwa
mazishi zinaendelea na taarifa zaidi zitatolewa kesho (Jumatano, Novemba 13,
2013),” ameongeza.
Marehemu
Dkt. Mvungi alisafirishwa siku ya Alhamisi, Novemba 7, 2013 kwenda nchini
Afrika Kusini kwa uchunguzi na matibabu zaidi akitokea Kitengo cha Mifupa
Muhimbili (MOI) aliokuwa amelazwa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake Kibamba,
wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na watu waliomjeruhi vibaya kichwani
usiku wa kuamkia siku ya Jumapili, Novemba 3, 2013.
Katika
taarifa yake, Tume pia imewaomba watanzania wote kuungana na familia, ndugu,
jamaa na marafiki wa marehemu Dkt. Mvungi katika kuomboleza msiba huo.
UWANJA WA KAITABA BUKOBA WAFUNGIWA KUCHEZEA LIGI KUU
BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPL Board) imefungia
viwanja saba vilivyokuwa vikitumiwa na timu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na
Ligi Daraja la Kwanza (FDL) hadi vitakapofanyiwa marekebisho ili kukidhi
mahitaji ya mechi za mpira wa miguu.
Uamuzi huo umefikiwa na TPL Board katika kikao chake
cha kwanza kilichofanyika juzi (Novemba 10 mwaka huu) jijini Dar es Salaam
ambapo pamoja na mambo mengine kilipitia ripoti za mechi za VPL na FDL katika
mzunguko wa kwanza.
Viwanja vilivyofungiwa na marekebisho yanayotakiwa
kufanyika kwanza ili viruhusiwe kutumika tena ni Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba
(majukwaa yake yamechakaa, hivyo kuhatarisha usalama wa watazamaji), na Uwanja
wa CCM Mkwakwani jijini Tanga (vyumba vya wachezaji kubadilishia nguo (dressing
rooms) havina hadhi).
Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya (sehemu
ya kuchezea- pitch ni mbovu), Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid
jijini Arusha (pitch ni mbovu), Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi (vyumba vya
kubadilishia kutumika kwa ajili ya shule ya awali), Uwanja wa Majimaji mjini
Songea (pitch ni mbovu) na Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro (pitch ni mbovu).
Klabu ambazo timu zake zinatumia viwanja hivyo
zimeshaarifiwa rasmi juu ya uamuzi huo ambapo ama vinatakiwa kuwasiliana na
wamiliki wa viwanja hivyo ili wafanye marekebisho au kutafuta viwanja vingine
vya kuchezea mechi zao.
Kwa upande wa ripoti za mechi za VPL; Mbeya City
imepigwa faini ya sh. 500,000 na kupewa onyo kali kwa timu yake ya U20
kutocheza mechi ya utangulizi walipocheza na Yanga. Pia wanatakiwa kulipa
gharama za uharibifu baada ya washabiki wao kuvunja kioo cha basi la Yanga
baada ya gharama hizo kuthibitishwa na Bodi ya Ligi.
Pia Mbeya City imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa
washabiki wake kushambulia basi la wachezaji wa Tanzania Prisons baada ya mechi
dhidi yao, na kulipa gharama za uharibifu baada ya kuthibitisha na Bodi ya
Ligi.
Coastal Union imepigwa faini ya sh. 500,000 kutokana
na vurugu za washabiki wake ilipocheza na Azam kwenye Uwanja wa Mkwakwani
ambapo mwamuzi msaidizi Hassan Zani alishambuliwa kwa mawe na kujeruhiwa
mkononi na kichwa, tukio lililosababisha mchezo kusimama kwa dakika tatu.
Beki wa Coastal Union, Hamad Khamis wa Coastal Union
amepigwa faini ya sh. 500,000 kwa kumpiga kichwa kwa makusudi Kipre Tchetche wa
Azam. Kitendo hicho kilisababisha refa amtoe nje kwa kadi nyekundu, hivyo
atakosa mechi tatu zinazofuata za timu yake.
Mchezaji Cosmas Lewis wa Ruvu Shooting alifanya
kitendo cha utovu wa nidhamu kwa kupiga kelele wakati mgeni rasmi akisalimia
timu na kukataa kupeana mkono na kamishna kwenye mechi dhidi ya Rhino Rangers,
hivyo amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000.
Mtunza vifaa (Kit Man) wa JKT Ruvu, Selemani Oga
aliondolewa kwenye benchi la ufundi wakati wa mechi yao dhidi ya Mbeya City kwa
kosa la kutoa lugha chafu kwa refa, hivyo suala lake litapelekwa katika Kamati
ya Maadili.
Kocha Msaidizi wa Oljoro JKT, Fikiri Elias amepigwa
faini ya sh. 500,000 na kufungiwa mechi tatu kwa kumshambulia kwa matusi refa
wakati wa mechi yao dhidi ya Ashanti United. Naye mtunza vifaa wa timu hiyo
Elas Justin amepelekwa Kamati ya Maadili kwa kumshambulia refa kwa matusi ya
nguoni.
Simba wamepigwa faini ya sh. 500,000 kutokana na
vurugu za washabiki wake wakati wa mechi dhidi ya Kagera Sugar.
Katika FDL, mchezaji Ally Mtoni wa Villa Squad
amepigwa faini y ash. 200,000 na kufungiwa mechi tano. Kosa lake ni kujisaidia
haja ndogo golini wakti wa mechi dhidi ya Ndanda FC iliyochezwa mjini Mtwara.
Kamishna Paul Opiyo wa mechi ya FDL kati ya Villa
Squad na Transit Camp kwa kutokuwa makini. Katika ripoti yake ameeleza kuwa
Transit Camp ilichelewa kufika uwanjani, lakini hakusema ilichelewa kwa muda
gani.
Kocha wa Polisi Dar es Salaam, Ngelo Nyanjabha na
Meneja wa timu hiyo Mrimi Masi wamepigwa faini ya sh. 200,000 na kufungiwa
mechi tatu kila mmoja kwa kuongoza kundi la washabiki kumvamia refa wa mechi
yao dhidi ya Villa Squad iliyochezwa Dar es Salaam.
Pia Bodi ya Ligi imeagiza Polisi waandikiwe barua ya
onyo kwa vile wakati waamuzi wanapigwa walikuwepo lakini hawakutoa msaada kwa
wakati.
Kocha wa Friends Rangers, Kheri Mzozo amepigwa faini
ya sh. 200,000 na kufungiwa mechi sita kwa kosa la kumtukana refa na kutishia
kuhamamisha washabiki waingie uwanjani kufanya fujo kwenye mechi dhidi ya Villa
Squad.
Naye Kocha msaidizi wa timu ya Transit Camp, Haji
Amiri amepigwa faini ya sh. 200,000 na kufungiwa mechi sita kwa kutoa lugha ya
matusi kwa mwamuzi wa akida wakati wa mechi dhidi ya Friends Rangers.
Adhabu zote zimetolewa kwa mujibu wa kanuni. Pia Bodi ya Ligi imeahirisha kufanya uamuzi wa mechi kati ya Stand United na Kanembwa JKT iliyochezwa Uwanja wa Kambarage ili kukusanya taarifa zaidi. Mechi hiyo haikumalizika. Bodi ya Ligi itakutana tena Jumapili (Novemba 17 mwaka huu).
Monday, 11 November 2013
ANGALIA PICHA ZA AJALI MBAYA KATIKA MSAFARA WA RAIS KIKWETE HUKO GEITA NA ILIYOJERUHI WATU 5
Msafara
wa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk JakayaKikwete mkoani
Geita, leo umeingia dosari baada ya gari moja lilokuwa kwenye msafara
huo kupinduka na kujeruhi watu watno.Gari
la Bohari ya Dawa (MSD) lililopata ajali likiwa na meneja wa MSD Kanda
pamoja na waandishi wa habari.Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani
Geita Lenard Paul ajali hiyo imetokea leo saa 3 na dakika 45 asubuhi katika eneo la Nyankumbu kilomita 3 kutoka makao makuu ya mkoa wa geita.Kamanda
Paulo amesema gari hilo namba DFP.9730 aina ya Toyota Landcruzer
lililokuwa likiendeshwa Yungi Mkwati, mali ya Bohari kuu ya Madawa
(MSD), lilipinduka baada ya kuteleza kwenye lami iliyomwagwa barabarani
hii leo.
Amewataja Waliojeruhiwa katika
ajali hiyo kuwa ni mwandishi Peter Makunga wa Radio Kahama Fm na Radio
Free Afrika, Peter Fabian wa Gazeti la Rai, Frederick Katulanda
Moderator wa Tovuti ya mabadiliko.com, meneja wa MSD kanda ya Ziwa
Byekwaso Tabura pamoja na dreva wa gari hilo Yungi Mkwati.
Kamanda Paulo amesema majeruhi
wote wamefikishwa katika hospitali ya wilaya ya Geita kwa ajili ya
matibabu na kisha kuruhusiwa huku Mwandishi Peter Makunga akiwa bado
amelazwa hospitalini hapo na hali yake inaendelea vizuri.
Askari akilikagua gari.
Mwandishi Peter Makunga akiwa anaendelea kupatiwa matibabu baada ya ajali hiyo, hospitali ya wilaya ya Geita.
Gari la Bohari ya Dawa (MSD) lililopata ajali likiwa na meneja wa MSD Kanda pamoja na waandishi wa habari.
HAYA NDIYO MANENO YA DIAMOND KWA WEMA

RAIS wa Wasafi Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’, juzikati alifunguka kuwa kwenye maisha yake ya ndoa atakayoingia siku chache zijazo, aliyekuwa mchumba wake wakamwagana na kurejeana hivi karibuni, Wema Sepetu asitegemee kuolewa naye.
Diamond ambaye ni staa wa Bongo Fleva aliyasema hayo mbele ya
paparazi wetu Novemba 7, mwaka huu jijini Dar kufuatia kuulizwa
anamchagua nani wa kumuoa kati ya Wema Sepetu na mchumba wake wa sasa,
Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Swali kwa Diamond liliibuka baada ya kuzagaa kwa tetesi kwenye
mitandao ya kijamii kwamba yu mbioni kumvisha pete ya uchumba mmoja wa
mademu zake.
Swali hilo lilimfanya Diamond afunguke kwa kusema kwamba anachokijua
yeye na ambacho kipo kwenye mikakati yake, mke wake mtarajiwa ni Penny.
“Najua wengi wanahisi mimi ninaweza kuoa mwanamke zaidi ya mmoja
kutokana na dini yangu kuruhusu lakini jambo hilo mimi silifikirii hata
kidogo kwa kuwa kwenye maisha yangu nilishapanga nitaoa mke mmoja tu,”
alisema Diamond.
Diamond akiwa kwenye pozi katika kiwanja cha ndege cha Mwalimu Julius Kambalage Nyerere siku chache wakati alipokuwa akitokea nchini china,ambapo walidaiwa kukutana na Wema na kuwafanya warejee kwenye penzi lao.

Akaendelea: “Watu wanasema mengi juu yangu na Wema, wengi wao hawajui nafsi yangu inataka mwanamke yupi, ninachoweza kusema na watu wakasikia na kunielewa basi wajue kwamba Penny ndiye mke wangu, Wema asitegemee kuolewa na mimi.”
Diamond alikwenda mbele zaidi kwa kumwanika Penny kwamba ana sifa ya kuwa mke kwani ni mvumilivu sana na anaonesha upendo wa dhati kwake.
“Kwa maana hii basi hakuna mwanamke mwenye jina kubwa wala sura nzuri zaidi ya Penny ninayeweza kumwita mke wangu. Najua kila mtu ana namna yake ya kuchagua ampendaye, ndiyo maana utaona watu wanasema hili mara lile, lakini hawajui nafsi yangu inataka mwanamke wa aina gani,” alisema Diamond na kuongeza:
Kama kuna demu anayejipa matumaini hayo basi asitegemee hata siku moja kwa sababu kuoa kwangu kutazingatia mke mwema na si bora mke, Penny pekee ndiye mwenye sifa za kuwa mke wangu,” alisema Diamond.
Akaendelea: “Watu wanasema mengi juu yangu na Wema, wengi wao hawajui nafsi yangu inataka mwanamke yupi, ninachoweza kusema na watu wakasikia na kunielewa basi wajue kwamba Penny ndiye mke wangu, Wema asitegemee kuolewa na mimi.”
Diamond alikwenda mbele zaidi kwa kumwanika Penny kwamba ana sifa ya kuwa mke kwani ni mvumilivu sana na anaonesha upendo wa dhati kwake.
“Kwa maana hii basi hakuna mwanamke mwenye jina kubwa wala sura nzuri zaidi ya Penny ninayeweza kumwita mke wangu. Najua kila mtu ana namna yake ya kuchagua ampendaye, ndiyo maana utaona watu wanasema hili mara lile, lakini hawajui nafsi yangu inataka mwanamke wa aina gani,” alisema Diamond na kuongeza:
Kama kuna demu anayejipa matumaini hayo basi asitegemee hata siku moja kwa sababu kuoa kwangu kutazingatia mke mwema na si bora mke, Penny pekee ndiye mwenye sifa za kuwa mke wangu,” alisema Diamond.
Juzi Ijumaa Wikienda lilimpigia simu Penny ili kutaka kupata maoni yake kuhusu tamko la Diamond, lakini muda mrefu simu hiyo ilikuwa ikiita bila kupokelewa.
Baada ya kumkosa Penny, Ijumaa Wikienda lilimtwangia simu Wema, naye kama Penny, simu yake iliita mara kadhaa lakini haikupokelewa.
AFISA USALAMA FEKI ANASWA KWENYE MSAFARA WA RAIS MJINI GEITA
GEITA: Katika hali ambayo inazidisha mashaka juu ya Usalama wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, Mtu mmoja ambaye hajatambulika nia yake, amefanikiwa kujipenyeza katika msafara wa Rais na kujifanya miongoni mwa walinzi wa msafara.
Mtu huyo ambaye baada ya kunaswa amekutwa na vitambulisho bandia, alifanikiwa kujipenyeza katika mkutano wa kwanza wa ziara ya Rais wilayani Bukombe mkoani Geita, ambapo kulikuwa na sherehe za uzinduzi wa barabara ya Lami ya Bwanga hadi Uyovu Lunzewe yenye urefu wa km 45 ambayo ujenzi wake ulizinduliwa na Rais Jakaya Kikwete siku hiyo Novemba 9 mwaka huu.
Akiwa kama afisa usalama alikuwa akizuia baadhi ya watu kufika maeneo maalum yaliyoandaliwa mahususi kwa ulinzi, lakini pia alikuwa akipitapita kukagua baadhi wa watu wakiwamo na waandishi wa habari huku akiwapanga namna ya kukaa vyema kabla msafara wa Rais kuwasili eneo la tukio.
Katika mkutano huo wa kwanza alifanikiwa kupita salama kwani baada ya mkutano huo kumalizika, aliweza kupata usafiri na kuondoka na msafara umbali wa km 53 na kufika Ikulu ndogo ya Bukombe, ambako msafara uliitulia kwa muda na wageni kupata chakula, kisha kuelekea katika mkutano wa pili wa hadhara mjini Ushirombo.
Hata hivyo, huko hakuweza kufanikiwa, Jeshi la Polisi mkoani Geita kwa shirikiana na Maofisa Usalama wa Taifa, lilifanikiwa kumtia mbaroni mtu huyo kama inavyoonyesha (Pichani Juu) akiwa ameshikwa chini na Ulinzi wa Askari polisi na afisa usalama akitolewa katika ya mkutano wa Rais Kikwete uliofanyika katika Uwanja wa Kituo cha mabasi Ushirombo.
Mtu huyo ametambulika kwa jina la Kwamani Juma anakadiriwa kuwa na umri kati ya 43-46, alikamatwa Novemba 9 mwaka huu, eneo la Ushirombo katika mkutano wa hadhara akiwa amejipanga kama maaofisa Usalama karibu na jukwaa kuu alilokuwa amekaa Rais Jakaya Kilwete.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita Leonard Paul amethibitisha kukamatwa kwa afisa huyo bandia, alisema "Ndiyo… amekamatwa, si umeona kwenye mkutano kilichotokea, sasa unataka nieleze nini zaidi," alielza Kamanda Paul
Kukamatwa kwake kulifanya wanaomjua kuanza kueleza wasifu wake na mmoja wapo akiwa ni Afisa Utamaduni wa Wilaya ya Bukombe, Julius Kambarage ambaye kutokana na kumfahamu mtu huyo alistajaabu kumuona akiwa amejipenyeza jukwaani hali ambayo ilimfanya kutoa taarifa kwa wahusika.
"Mimi nilikuwa MC, pale kwenye uzinduzi wa Barabara (Lunzewe) nilipomuona niliwaeleza watu wa usalama, sikujua walifanyiaje kazi, lakini nlistajaabu amefika tena Ushirombo, ila safari hii nilimuona wakati akikamatwa, naona atakuwa Tapeli huyu" alieleza Afisa utamaduni huyo.
Mtu huyo mpaka akikamatwa alionekana akiwa mtanashati, aliyevalia Kaunda Suti, miwani na kuonekana nadhifu, ina anadaiwa katika ukaguzi kitambulisho alichokutwa nacho kilikuwa kimeandikwa jina lake na huku kikuonyesha kuwa na Muhuri unaosomeka ‘Ulinzi na Usalama wa Taifa’.
Naye Diwani wa Kata ya Uyovu Yusufu Fungameza (Chadema), alieleza kumtambua mtu huyo na kudai ni mkazi wa Kata yake lakini amekuwa akitajwa na kulalamikiwa kuhusika na matukio ya utapeli kwa wananchi.
"Huyu bwana namfahamu sana, ni mkazi Kata yangu lakini amekuwa akinihusisha na vote do vya utapeli, yapo matukio kadhaa ya kulalamikiwa kutapeli watu pale Uyovu amewahi kumtapeli mfanyabiashara mmoja," alieleza.
Subscribe to:
Posts (Atom)
























