Sunday, 20 October 2013

UTATA MPYA UJIO WA ALEX MASSAWE





HATUA za kumrejesha nchini mfanyabiashara maarufu, Alex Massawe, aliyefikishwa mahakamani nchini Dubai, Falme za Kiarabu (UAE) kwa tuhuma za mauaji, zimegubikwa na utata mkubwa, huku Tanzania ikidaiwa kushindwa kutimiza masharti ya Shirika la Polisi la Kimataifa (Interpol).

Kwa mujibu wa chanzo chetu kutoka Dubai, Interpol iliipa Tanzania hadi kufikia Septemba 4, mwaka huu, iwe imewasilisha vielelezo vya kuthibitisha tuhuma zake.

Chanzo hicho kiliongeza kuwa muda huo umemalizika bila Tanzania kuwasilisha uthibitisho huo na kwamba Massawe ameachiwa huru nchini humo.

Massawe alikamatwa Dubai kati ya Juni 20 na 25. Kwa mujibu wa Mkuu wa Interpol, Tawi la Tanzania, Gustav Babile, ombi la kumleta mhalifu nchini kutoka nje ya nchi (extradition request) lina hatua ndefu.

Alisema kuwa kuna mlolongo wa taratibu za kutekeleza ili Massawe aletwe, akasisitiza kuwa ilikuwa ni lazima kwanza Polisi wa Tanzania watoe tangazo kwa Interpol kuhusu kumsaka mtu huyo ili aletwe.

Jeshi la Polisi nchini limekanusha taarifa hizo za kuachiwa kwa Massawe, likisema halina taarifa za suala hilo, na kwamba taratibu za kisheria zinaendelea kufanyika.

Msemaji wa jeshi hilo, Advera Senso, alisema: “Mambo ya kusikia sisi hatuyafanyii kazi, kwanza vyanzo vingine vya habari ni vya kutiliwa shaka. Sisi tukijiridhisha tukawa na taarifa kamili tutawaambia.”

*MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA MKUTANO WA MABUNGE YA SADC MJINI ARUSHA LEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua mkutano wa siku 11 wa 34 kwa Mabunge ya Nchi wanachama wa Jumuiya ya SADC katika ukumbi wa AICC jijini Arusha leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Pandu Ameir kificho kabla ya kufungua mkutano wa siku 11 wa 34 kwa Mabunge ya Nchi wanachama wa Jumuiya ya SADC leo katika ukumbi wa A I C C jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mbunge wa Arusha mjini Mhe. Godbles Lema nje ya ukumbi wa mikutano wa A I C C Arusha, Baada ya kufungua mkutano wa siku 11 wa 34 kwa Mabunge ya Nchi wanachama wa Jumuiya ya SADC katika ukumbi wa A I C C mjini Arusha leo. Kushoto Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Pandu Ameir kificho kabla ya kufungua mkutano wa siku 11 wa 34 kwa Mabunge ya Nchi wanachama wa Jumuiya ya SADC leo, katika ukumbi wa A I C C mjini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia vikundi vya sanaa vya ngoma za aina mbalimbali alipowasili katika Jengo la Ukumbi wa mikutano A I C C mjini Arusha kwa ajili ya kufungua mkutano wa siku 11 wa 34 kwa Mabunge ya Nchi wanachama wa Jumuiya ya SADC leo.

*SIMBA WASHANGILIA USHINDI WA SARE YA 3-3 DHIDI YA YANGA

 Beki wa Yanga, Nadir Haroub 'Canavaro', akiwania mpira na kipa wa Simba Abel Dhaira, wakati wa kipindi cha pili cha mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliomalizika hivi punde kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam. 
Katika mchezo huo timu hizo zimetoka sare ya mabao 3-3, ambapo Yanga ilipata mabao yake katika kipindi cha kwanza kupitia kwa wachezaji Mrisho Ngasa, aliyetupia katika dakika ya 15, Hamis Kiiza 36 na 45. 

Mabao ya Simba yalifungwa kipindi cha pili kupitia wachezaji wake, Betram Mwombeki, katika dakika ya 54, Joseph Owino katika dakika ya 57 na Gilbert Kaze, katika dakika ya 83. 
Baada ya Simba kusawazisha mabao yote matatu viongozi na mashabiki wa timu hiyo walionekana kushangilia sare hiyo, ambayo kila mmoja aliyekuwapo uwanjani hapo hakuweza kuamini kilichotokea kuanzia mashabiki, wachezaji wa Yanga na hata wa Simba.
 Mashabiki wa Simba, walikuwa kama wamemwagiwa maji, wakiwa na huzuni katika kipindi cha kwanza baada ya kufungwa mabao 3-0.
 Mshambuliaji Mrisho Ngasa, (kulia) akimtoka beki wa Simba, Joseph Owino, katika kipindi cha pili.
 Mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu (kulia) akiwatoka mabeki wa Simba, Joseph Owino na Gilbert Kaze, katika kipindi cha kwanza.
 Mrisho Ngasa, akiruka kwanja la beki, Gilbert Kaze.
 Mashabiki wa Yanga ilikuwa ni furaha kama hivi, ambapo baadaye furaha hii ilizimika ghafla.
 Katika mtanange huo, mashabiki kadhaa walizimia, ambapo shabiki huyu wa Yanga, akibebwa kutoka jukwaani baada ya kuzimia, huku mashabiki saba wa Simba na wawili wa Yanga walizimia.
 Mshabiki wa Simba walizinduka na kushangweka kama hivi, baada ya kupata bao la pili.
Mrisho Ngasa, akishangilia bao lake la kwanza alilofunga katika dakika ya 15, kipindi cha kwanza.

SHULE YA SEKONDARI ACHILEUS MULEBA YAAZIMISHA MAHAFALI YA KWANZA KIDATO CHA NNE,MUASHAMU BABA ASKOF RWOMA JIMBO LA BUKOBA AWA MGENI RASMI

 Picha ya pamoja muashamu baba askof wa jimbo la bukoba Desderius rwoma akiwa na viongozi wa shule na wanafunzi waliohitimu kidato cha nne kwa mara ya kwanza tangu kuwepo kwa shule
                          mmojawapo ya wazazi waliofika kushiriki mahafali ya watoto wao wanaohitimu
 mkurugenzi wa shule padre achileus kianuka akiwa na furaha kwa shule yake wanafunzi kuhitimu kidato cha nne kwa mara ya kwanza
                                                                  wanafunzi wakiimba
                                      bwana bina na mkewe wakiwa na mtoto wao aliehitimu
                                            bi Anitha lacto akiwa kabeba  zawadi za kumpongeza mwanae
                                                            hakika wazazi walipendeza pia
                                                                         karibuni chakula
                                                      wakati wa vinywaji na kufurahi
                                                bwana stivin baypot nae katika pozz
                                     muashamu baba askof rwoma akinena na wenzake meza kuu
                                                         wageni waalikwa katika pozz tofauti
                                                                       keki ikakatwa
                  baba askofu desderius rwoma akikata keke na mwanafunzi mhitimu  Aniset bujune
                                                aniseti bujune akiwa na furaha kuhitimu
                                              wahitimu wakiimba na kufurahi kwa kuhitimu
                                          ukafika wakati wa wazazi kushare love na watoto wao
bi anitha akiwa na ndugu jamaa na marafiki wakimpongeza mtoto wa anitha  aniseti bujune mwenye maua, jamcobukoba.blogspot.com naupongeza uongozi wa shule na wazazi wote kwa hatua mliyofikia ongerani sana.

MKUU WA MKOA KAGERA KANAL FABIAN MASSAWE AZINDUA KITABU CHA MAISHA YA MZEE PIUS NGEZE BAADA YA MIAKA 70

mwonekano wa kitabu cha maisha ya mzee pius ngeze kilichozinduliwa na mkuu wa mkoa kagera kanal Fabian Massawe, kinapatikana kwenye maduka ya vitabu kwa shilingi kumi na nne elfu tu.
mzee galiatano na mkewe rafiki mkubwa wa mzee ngeze nae alishiriki hsafla ya kumpongeza

Padre Privatus Karugendo mwandishi wa kitabu cha maisha ya mzee ngeze katika kipindi cha miaka 70 akieleza kwa nini aliamua kuandika kitabu hiki  mbele ya mgeni rasmi na wageni waalikwa waliohidhulia hafla ya kumpongeza mzee ngeze
                   mkuu wa mkoa kagera akielezea jinsi alivyomjua na kumfahamu mzee pius ngeze
mkuu wa mkoa wa kagera kanal Fabian Massawe akizindua kitabu cha maisha ya mzee pius ngeze baada ya miaka 70.kitabu hiki kimeandikwa na Padre Privatus Karugendo kinachoelezea maisha ya mzee ngezi , kielimu, kikazi, kisiasa mpaka kustaafu kwake.
mtoto wa mzee piusi ngeze, willim ngeze akimshukuru baba yake kwa niaba ya wenzake kwa malezi bora na safi waliyopewa na wazazi wao kwa kuwasomesha na sasa ni watu wazima na wanashuhudia baba yao akitimiza miaka 70. wanampa sifa mungu na kumshukuru
                                                             mama kanati mgeni mwalikwa
                                                                               picha ya pamoja
mzee ngeze akimpokea prof Anna Tibaijuka waziri wa Ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi akiingia katika ukumbi wa hafla lina's
                    mzee ngeze akieleza na kushukuru wageni walioudhuria hafla ya kumpongeza
                                                      familia ya mzee ngeze wakifurahia
Mzee Pius Ngeze na mke wake wakimlisha keki mtoto wao william Ngeze kwenye hafla ya kumpongeza mzee ngeze kutimiza miaka 70 iliyofanyika katika ukumbi wa lina's bukoba