Tuesday, 15 October 2013

Washindi wa Chomoka na Mwananchi wapera zawadi zao


 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya MCL akifungua hafla ya ukabidhi wa zawadi kwa washindi wa shindano la Chomoka na Mwananchi, shughuli iliyofanyika katika makao makuu ya kampuni ya mwananchi, wacvhapishaji wa magazeti ya Mwananchi, mwanaspoti na The Citizen
 Mkurugenzi wa kampuni ya MCL, Tido Mhando, akimkabidhi ufunguo wa gari, mshindi wa gari Bw Benedict Mgoo kutoka Dodoma, anayeshuhudia ni mke wa mshindi huyo Bi Fortunata
 
 Bw benedict, akifungua gari lake huku akishuhudiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Limited
 ..hapa akiwa ndani ya gari na Familia yake
 Hapa akitoa ushuhuda kwa wanahabari
 Hapa Bw benedict akijibu maswali ya wanahabari
Hii ni picha ya Bw benedict akiwa na wanafamilia waliomsindikiza kwenda Mwananchi kupokea zawadi yake
 Meneja Maendeleo ya Biashara wa  Mwananchi Communication Limited (MCL), Theophil Makunga  akimkabidhi hundi ya Shilingi Milioni moja Mshindi wa Promosheni ya Chomoka na Mwananchi, Benedict Masija Mkazi wa Kigamboni jijini Dar es Salaam
 Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Mwananchi Communication Limited (MCL) Francis Nanai, akimkabidhi hundi ya Shilingi Milioni moja mshindi wa promosheni ya  Chomoka na Mwananchi, Cletus Mubezi Mkazi wa Temeke  jijini Dar es Salaam
 Mkurugenzi Mtendaji  wa Mwananchi Communications Limited(MCL),Tido Mhando(kushoto) akimkabidhi hundi ya Shilingi Milioni moja Mshindi wa
Promosheni ya Chomoka na Mwananchi,  Dk Andrew Lwali Mkazi wa Kibaha mkoa wa Pwani
 Mhariri Mtendaji wa  Gazeti la Mwananchi ,Dennis Msacky (kushoto)akimkabidhi  hundi ya Shilingi Milioni moja mshindi wa Promosheni ya Chomoka na Mwananchi, Edna Maro Mkazi wa Tegeta  jijini Dar es Salaam
 Mhariri Mtendaji  Mtendaji wa Mwananchi  Communications Limited(MCL)Bakari Machumu akimkabidhi  hundi ya Shilingi Milioni moja mshindi wa Promosheni ya Chomoka na Mwananchi, Stephen Shembata  Mkazi wa Tegeta  jijini Dar es Salaam
 Mkurugenzi Mtendaji  wa Mwananchi Communications Limited(MCL),Tido Mhando(kushoto) akimkabidhi hundi ya Shilingi Milioni moja Mshindi wa
Promosheni ya Chomoka na Mwananchi ,Mashaka Msuya  Mkazi wa Buguruni jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji  wa Mwananchi Communications Limited(MCL),Tido Mhando akimkabidhi hundi ya Shilingi Milioni moja Mshindi wa Promosheni ya Chomoka na Mwananchi, Levina Nyambo  Mkazi wa Mabibo jijini Dar es Salaam 
 Washindi wote kwa pamoja wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa MCL

*RAIS KIKWETE USO KWA USO NA LISSU ALIPOKUTANA NA VIONGOZI WA VYAMA VYA UPINZANI IKULU JIJINI DAR LEO


Rais Dkt.Jakaya Kikwete akisalimiana na Mhe.Tundu Lissu CHADEMA Nyuma ni Mhe.James Mbatia NCCR Mageuzi.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mhe. John Mnyika.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Viongozi wa Vyama vya Siasa nchini,waliofika ikulu jijini Dar es Salaam leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha ikulu kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni Mh.Freeman Mbowe mara baada ya mazungumzo nao leo ikulu jijini Dar es Salaam.Nyuma kushoto ni Kiongozi wa NCCR Mageuzi,Mh. James Mbatia na Professa Ibrahim Lipumba wa CUF.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya Pamoja na Viongozi wa Vyama vya upinzani muda mfupi kabla ya kuanza mazungumzo kuhusu rasimu ya katiba ikulu jijini Dar es Salaam.Wengine katika picha kutoka kushoto Isaack Cheyo UDP, James Mbatia NCCR Mageuzi, Professa Ibrahim Lipumba CUF, Freeman Mbowe CHADEMA, Philip Mangula CCM, na Bibi Nancy Mrikaria aliyemwakilisha Mwenyekiti wa TLP Mhe.Agustine Lyatonga Mrema.
*******************************************
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Vyama vya upinzani na wasaidizi wao waandamizi muda mfupi kabla ya kuanza mazungumzo kuhusu rasimu ya katika ikulu jijini Dar es Salaam leo.Kutoka kushoto mbele Isaack Cheyo UDP, James Mbatia NCCR Mageuzi, Professa Ibrahim Lipumba CUF, Freeman Mbowe CHADEMA, Philip Mangula CCM, na Bibi Nancy Mrikaria aliyemwakilisha Mwenyekiti wa TLP Mhe.Agustine Lyatonga Mrema.Waliosimama Nyuma kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu CUF Bwana Julius Mtatiro,Mhe. Tundu Lissu CHADEMA, Bwana Martin Mng’ong’o NCCR Mageuzi ,Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu na Bunge William Lukuvi, Mhe.Habib Mnyaa CUF, Mbunge wa Ubungo Kwa tiketi ya CHADEMA Mhe.John Mnyika, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Mhe.Steven Wassira na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Mathias Chikawe

*RAIS JAKAYA KIKWETE ATOA ZAWADI YA EDI EL HAJJ KWA MAKUNDI MAALUM


 RAIS Jakaya Kikwete  msaada wa vyakula  wenye thamani ya Sh. milioni 5.5 kwa makundi maalum ambayo ni wazee  na wasiojiweza, watoto yatima na watoto walio katika  mkinzano na  kisheria kwa ajili ya kusherekea sikukuu ya Edi El Hajj.

 Msaada huo ulitolewa leo  kwa niaba ya Rais  Kikwete , na Kaimu Kamishna  wa Usatawi wa Jamii Rabirira Mushi   katika hafla fupi iliyofanyika kwenye mahabusu ya watoto iliyopo Regency  jijini Dares Salaam  kwa  vituo na makazi 12 ya makundi hayo yaliyopo hapa nchini.

“ Mhe. Rais  ametoa zawadi ya mbuzi, mchele na mafuta ya kupikia  ili kuona kwamba watoto na wazee hawa wanajumuika  na wanajamii wengine katika  sherehe hii,” alisema  Rabirira.

 Alivitaja vituo  vilipokea msaada huo kuwa ni  kituo cha watoto Dar  Al arkam na Nunge  vyote viko(Temeke), Msongola Orphaned  Centre(Ilala), Furaha(Kinondoni)  Mother Theresa(Mburahati), Malaika Kids Home(Mkuranga) na makazi ya wazee na wasiojiweza cha Kilima(Bukoba Vijijini).

Vituo vingine ni  Mahabusi ya watoto(Arusha Mjini), mahabusi ya watoto(Tanga Mjini), makazi ya wazeee Mwanzange(Tanga), makao ya watoto Istikana (Pemba ) na makazi ya wazee Sebuleni(Unguja).

Akizungumzia kuhusu msaada huo kwa niaba ya wenzake Mwenyekiti wa kituo cha Msongola Orphaned Trust Fund, Shanta Deus   alimshukuru Rais Kikwete kwa moyo wake wa kujitolea kwa  makundi hayo huku akiwataka watu wengine kuiga mfano.
“Ninawaomba watu wengine, sekta binfasi na kampuni mbalimbali kuiga mfano huu ili kuweza kuwasaidia watoto yatima na wanaoshi katika mazingira hatarishi pamoja na makundi maalum kwa kutoa misaada mbalimbali,”alisisitiza Shanta.

Naye Sista  Oliver  Paulo  ambaye ni mlezi wa  makao ya watoto ya yatima, kijiji cha Furaha  aliishauri jamii iwe tabia ya kushirikiana na makundi hayo katika sherehe mbalimbali na kuwasaidia.

*RUKAMBURA JERA MIAKA 20 KUTOJIHUSISHA NA SOKA, SHAFII WAFUNGI HADI ALIPE FAINI YA SH. M. 1


Kamati ya Rufani ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imewaadhibu walalamikiwa watano kati ya saba baada ya kufanya mapitio (revision) kwa uamuzi wa Kamati ya Maadili kutokana na maombi ya Sekretarieti, huku Richard Julius Rukambura akifungiwa miaka 20 kujihusisha na mpira wa miguu.

Sekretarieti ya TFF iliwasilisha maombi ya mapitio kwa Kamati ya Rufani ya Maadili ili kupata mwongozo kwa vile kulikuwapo mkanganyiko kwenye uamuzi wa Kamati ya Maadili, hivyo kuiwia vigumu kwake kuutekeleza.

Uamuzi huo wa mapitio umesomwa leo jioni (Oktoba 15 mwaka huu) mbele ya waandishi wa habari na wajumbe wa Kamati hiyo wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti Victoria Makani.

Rukambura amefungiwa miaka 20 baada ya kupeleka masuala ya mpira wa miguu katika mahakama za kawaida kinyume na Ibara ya 75 ya Katiba ya TFF na kifungu cha 73(3)(b) cha Kanuni za Maadili za TFF toleo la 2013. Adhabu yake itamalizika Oktoba 15, 2033.

Kabla ya kutoa adhabu hiyo, Kamati imejiridhisha kuwa Rukambura ni mwanafamilia wa TFF kwa vile aliwahi kuwa Mwenyekiti wa klabu ya Pamba ya Mwanza, na fomu zake za kuomba uongozi TFF ziliidhinishwa na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Shinyanga. Vilevile ni ‘Leadership Aspirant’ kwa mujibu wa kifungu cha 2(v) cha Kanuni za Utii za TFF toleo la 2013.

Pia imesema kwa Msajili wa Klabu na Vyama vya Michezo kusajili Katiba ya TFF inayokataza masuala ya mpira wa miguu kwenda katika mahakama za kawaida, na kutaja vyombo vya haki vitakavyoshughulikia masuala hayo (judicial organs), Kamati ya Maadili ilikosea kutomtia hatiani mlalamikiwa kwa kuegemea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Naye Shaffih Dauda, Kamati imebaini kuwa mwanafamilia wa TFF kwani ni Mwenyekiti wa Bombom FC, fomu yake ya kuomba uongozi ilipitishwa na klabu ya Simba na pia ameshakuwa kiongozi katika ngazi mbalimbali ndani ya Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kinondoni (KIFA), hivyo yeye ni ‘Leadership Aspirant’ kwa mujibu wa kifungu cha 2(v) cha Kanuni za Utii za TFF toleo la 2013.

Hivyo Dauda amepatikana na kosa la kimaadili kwa kutotekeleza maagizo rasmi ya TFF ya kutosambaza barua iliyotoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwenda kwa Rais wa TFF, Leodegar Tenga.

Kamati ya Rufani ya Maadili imempa onyo kali na faini ya sh. milioni moja anayotakiwa kuilipa ndani ya siku tatu ambapo akishindwa kufanya hivyo atafungiwa mwaka mmoja. Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa kifungu cha 6(1)(a),(c) na (h) cha Kanuni za Maadili za TFF toleo la 2013.

Akilipa faini ataweza kuendelea na mchakato wa kugombea nafasi ya uongozi aliyoomba.

Nazarius Kilungeja amepatikana na kosa la kimaadili kwa mujibu wa kifungu cha 73(8)(a) cha Kanuni za Maadili za TFF toleo la 2013, kwani akijua kuwa ana adhabu ya kinidhamu ya kufungia miaka mitano na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Rukwa (RUREFA) iliyoanza 2009 alichukua fomu kuomba uongozi TFF.

Hivyo, amefungiwa miaka mitatu, adhabu ambayo itakwenda sambamba na ile ya RUREFA ambapo kifungo chake sasa kitamalizika Oktoba 15, 2016.

Sekretarieti ya TFF imepewa onyo kali kwa kupokea fomu yake ya kugombea na malipo wakati akiwa amefungiwa. Onyo hilo pia limetolewa kwa Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA) Mkoa wa Rukwa kwa kuidhinisha fomu yake ya kugombea.

Naye Wilfred Kidao Mzigama ambaye ni mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF amepatikana na kosa la kimaadili kwa kuwa na nyaraka la Kamati ya Utendaji bila kibali na kukiuka taratibu za kuwasilisha malalamiko kwa mujibu wa Ibara ya 12(2) na Ibara ya 50(1) na (5) ya Katiba ya TFF.

Amepigwa faini ya sh. milioni moja anayotakiwa kuilipa ndani ya siku tatu ambapo akishindwa atafungiwa mwaka mmoja. Akitekeleza adhabu hiyo ataweza kuendelea na mchakato wa kugombea uongozi kwa nafasi aliyoomba.

Vilevile Kamati hiyo imetoa onyo kali kwa Sekretarieti ya TFF na wajumbe wa Kamati ya Utendaji kwa kushindwa kudhibiti nyaraka muhimu za vyombo vyao.

Pia Kamati ya Rufani ya Maadili imempata na kosa la kimaadili Kamwanga Tambwe kwa mujibu wa kifungu cha 73(8) cha Kanuni za Maadili za TFF toleo la 2013, kwa kuingia kwenye mchakato wa uchaguzi wakati ana adhabu ya kinidhamu inayomalizika 2014.

Hivyo, amepewa adhabu ya kufungiwa miaka mitatu ambayo itakwenda sambamba na ile ya kinidhamu na kumalizika Oktoba 15, 2016. Pia Sekretarieti ya TFF, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Ruvuma (FARU) na Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT) Mkoa wa Ruvuma wamepewa onyo kali kwa kupokea na kuidhinisha fomu zake za kugombea uongozi wakati akitumikia adhabu ya kufungiwa.

Kamati ya Rufani ya Maadili imewakuta kutokuwa na hatia ya makosa ya maadili kama ilivyobaini Kamati ya Maadili walalamikiwa Riziki Juma Majala na Omar Isack Abdulkadir, hivyo wana haki ya kugombea uongozi kwa kufuata Katiba na Kanuni za TFF.



Kwa mujibu wa kifungu cha 74(4) cha Kanuni za Maadili za TFF toleo la 2013, uamuzi wa Kamati ya Rufani ya Maadili hauna fursa ya rufani wala marekebisho kutoka chombo kingine chochote isipokuwa FIFA na Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS).

*RAIS KIKWETE KATIKA SHEREHE ZA KILELE CHA MBIO ZA MWENGE WA UHURU, KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE NA WIKI YA VIJANA


 Rais Jakaya Kikwete, Mama Salma, Waziri wa Habari, Dkt. Fenela Mukangara, Mkuu wa Mkoa Iringa, Ishengoma na Mangula, wakifurahia kwa pamoja wakicheza muziki wakati wa sherehe za Kilele cha Mbio za Menge wa Uhuru zilizofanyika kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa leo mchana.
 Rais Jakaya Kikwete akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2013 Bw.Juma Ali Simai leo katika uwanja wa CCM Samora mjini Iringa.
 Rais Jakaya Kikwete, akihutubia katika sherehe hizo.
 Rais Kikwete, akimkabidhi Kikombe Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ishengoma.
 Rais Jakaya Kikwete (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wakimbiza mwenge wa Uhuru 2013 leo mjini Iringa.
Rais Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa na...

Monday, 14 October 2013

TUNAKUKUMBUKA DAIMA

Taifa laadhimisha miaka 14 ya kifo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Kutokana na hekima na busara zako CCM na Serikali yake bado ipo imara ,CCM Inaamini  katika misingi ya Umoja,Amani na Mshikamano.

*AKUTWA AMEJINYONGA KWENYE MTI MKOANI MOROGORO


Askari akipanda juu ya mti kwaajili ya kuushusha mwili wa marehemu.

Sunday, 13 October 2013

UFOO SARO AFANYIWA UPASUAJI WA KUONDOLEWA RISASI MWILINI ALAZWA WODI 12 YA KIBASILA. ... JIONEE HALI ILIVYOKUWA

 Ufoo Saro baada ya kufanyiwa upasuaji huo.
 Muuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), akimpeleka wodini Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Ufo Saro,  baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuondolewa risasi kufuatia kushambuliwa kwa silaha ya moto nyumbani kwa mama yake  Kibamba jijini Dar es Salaam leo na mtu aliyedaiwa ni mchumba wake ambaye pia alimuua mama yake na kisha kujiua.
 Wanahabari wakimpiga picha Ufoo Saro baada ya kuondolewa chumba cha upasuaji.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakimsindikiza Ufoo Saro wakati akipelekwa wodini