Wednesday, 18 September 2013

PICHA: OMMY DIMPOZ..ALIPOWASILI WASHINGTON DC KWA STYLE TAYARI KWA SHOW YAKE ITAKAYOANZA JUMAMOSI HII WASHINGTON DC.


DIMPOZ AKIPATA UKODAKI NA PROMOTER WAKE "MR DMK"  PAMOJA NA AKINA DADA WALIOKUWEPO KUMPOKEA KATIKA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA WASHINGTON DC.KULIA NI MLIMBWENDE ALIYEWAHI KUTWAA TAJI LA MISS TEMEKE NA KUSHOTO NI MLIMBWENDE MWINGINE KUTOKA TZ.


OMMY NDANI YA LIMO KUELEKEA HILTON.

LUNCH TIME AT THE HILTON.
OMMY DIMPOZ AKIWA NA DESIGNER MISS TEMEKE NA GAUNI LAKE LA KWETU FASHION.

JK ATEMBELEA CAPITOL HILL


 Rais Dkt Jakaya Kikwete akiongozana na Mhe. BernardWaziri Membe na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula tayari kuelekea Capitol Hill  kuendelea na ziara yake nchini Marekani. Rais Kikwete aliwasili Washington, DC  leo Jumatano Sept 18, 2013 asubuhi  akitokea California
Rais Dkt Jakaya Kikwete akiongea na Halima Mamuya na H.V. Street wamiliki wa AmeriTan International ya Louisiana

Juu na chini ni Rais Dkt Jakaya Kikwete akijiandaa kuingia kwenye gari kuelekea Capitol Hill kuendelea na ziara yake nchini Marekani
Gari lililomchukua Rais Dkt. Jakaya Kikwete likiondoka kuelekea Capitol Hill.

Tuesday, 17 September 2013

MKATABA WA KUFUA UMEME KATIKA MAPOROMOKO YA MAJI YA RUSUMO MKOA WA KAGERA WASAINIWA LEO

 Mawaziri wa nchi tatu wa kwanza kulia  waziri wa miundo mbinu wa rwanda Silas Rwakabamba, waziri wa Nishati na madini wa Tanzania Sospeter muongwa, na waziri wa  Nishati wa Burundi Manirakiza C'ome katika picha ya pamoja katika viwanja vya bukoba hotel E.L.C.T bukoba
                                       mkutano wa kuwekeana mkataba umefanyika bukoba hotel
                          wajumbe kutoka katika nchi ya Tanzania, Burundi na Rwanda
                                                             mawaziri wa nchi tatu
                                      bw seifu mwakilishi kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa kagera
  Eng Innocent Luoga Naibu kamishina msaidizi wa nishati  Tanzania akieleza mchakato wa mradi
 Bw  Paul Baringanire mwakilishi wa benki ya dunia ambao  ndio wafadhili wakubwa wa mradi wametoa dora za kimarekani milioni 340 kwa ajili ya kufua umeme  wa rusumo
 Bi Stella Mandago mwakilishi wa benki ya maendeleo ya Afrika ambao watagharamia usambazwaji wa umeme wa rusumo katika nchi tatu, Tanzania,Burundi na Rwanda
 waziri wa Burundi Manrakiza c'ome ambae alikuwa akiongea kwa kifaransa na kutafsiriwa na mkalimani akieleza namna walivojipanga katika mradi
 Waziri wa  miundo mbinu wa rwanda Silas rwakabamba akieleza mikakati ya nchi yake katika utekelezaji wa mradi.
 waziri wa nishati na madini wa Tanzania pro peter muongwa akieleza jinsi Tanzania ilivyojipanga katika mapinduzi ya nishati, amesisitiza nchi zote kuwa makini katika utekelezaji wa mradi huu ambao zaidi  ya miaka arobaini iliyopita umeshindwa kutekelezwa.amesisitiza hakuna maswala ya kujuana na siasa katika mradi huu, kila nchi ihakikishe inaweka watendaji makini ambao watachapa kazi , na maswala ya rushwa ni mwiko katika mradi
                                                  picha ya pamoja mawaziri na wafadhili wa mradi
                                              picha ya pamoja mawaziri , wafadhili na management ya nchi tatu

                                                        waziri wa Tanzania akisaini mkataba
                                       mawaziri  wa nchi tatu wakiwa na mikataba yao
                                                     waziri wa rwanda akisaini mkataba
                                                    mawaziri wa nchi tatu wakiwa na wajumbe wa bodi

Monday, 16 September 2013

DAYNA ASEMA MADAI YA SHEDY KWAMBA YA YEYE ALIKUBALI DEMO YAKE KUTUMIWA NA DIAMOND SI YA KWELI

DAYNA

Msanii wa kizazi kipya Dayna ambaye hivi karibuni kumeibuka malumbano yanayodai Diamond kutumia beats ya wimbo wake wa Naumia alioutengeneza kwa prodyuza Shedy na Prodyuza alipoulizwa alisema Dayna alikubali Beats za wimbo wake zitumiwe na Diamond huku akidai kwamba Dayna alikua hajalipia beats ya wimbo wake na hivyo kuamua kumuuzia Diamond ambaye nae bila kuchelewa ameishatoa wimbo wake wa My number one ambao unatamba sasa hivi kwenye vituo vya radio na vituo vya luninga.

LOWASSA AENDESHA HARAMBEE YA UJENZI WA SHULE YA MSINGI YA KANISA LA AICT WILAYANI KAHAMA, ZAIDI YA SH. MIL. 212 ZAPATIKANA

 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono waumini wa Kanisa la AICT (Africa Inland Church Tanzania) Pastoreti ya Kahama Mjini,wakati alipokuwa akiwasili kwenye kanisa hilo kwa ajili ya kuendesha Harambee ya Kuchangia Ujenzi wa Shule ya Msingi ya Kanisa hilo.
 .Pichani chini na juu, Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikata utepe na kufungua pazia katika jiwe la msingi ikiwa ni ishara ya Ufunguzi rasmi wa Jengo la Madarasa ya Shule ya awali ya Kanisa la AICT (Africa Inland Church Tanzania) Pastoreti ya Kahama Mjini.ambapo baadae aliendesha Harambee ya Kuchangia Ujenzi wa Shule ya Msingi ya Kanisa hilo.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipanda Mti katika eneo la Kanisa hilo.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipokea Michango Mbali Mbali kutoka kwa Marafiki zake.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipokea zawadi ya kitabu cha Mungu (Biblia) kutoka kwa Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT (Africa Inland Church Tanzania) Dayosisi ya Shinyanga,Dkt. John Kanon Nkola mara baada ya kuendesha Harambee ya Kuchangisha fedha kwa ajili ya Ujenzi wa Shule ya Msingi ya Kanisa la AICT (Africa Inland Church Tanzania) Pastoreti ya Kahama Mjini.ambapo zaidi ya Shilingi Milion 212 zilipatikana zikiwemo na ahadi.

PRISCA CLEMENT ATWAA TAJI LA VIPAJI MISS TANZANIA 2013

Mrembo Prsica Clement, kutoka Kitongoji cha Sinza (katikati) akipunga mkono kwa furaha baada ya kutangazwa mshindi wa shindano la Redd's Miss Talent kwa mwaka 2013, na kufanikiwa kupata tiketi ya kuingia hatua ya 15 bora ya shindano la Redd's miss Tz mwaka huu.
Washiriki wa shindano la kumtafuta mshiriki wa kuingia katika hatua ya 15 bora ya Shindano la Redd's Miss Tanzania kwenye shindano la Redd's miss tz Talent 2013 wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutangazwa washindi wa hatua ya tano bora.

 Mrembo Prisca Clement ambaye ni mwakilishi kutoka Sinza na Kanda ya Kinondoni usiku wa kuamkia leo alifanikiwa kuwabagwa warembo wenzake 26 kati ya 30 wanao wania taji la Miss Tanzania mwaka huu na kufanikiwa kuwa mrembo wa 3 kuingia Nusu Fainali ya Mashindano hayo baada ya kutwaa taji hilo dogo.
Shimdano hilo lilifanyika katika Hoteli ya Giraffe Ocean View ambako ndiko Kambi ya Warembo hao ilipo.
 Prisca akipita jukwaani mara baada y.a kutajwa kuwa ndio mshindi
 Prisca Clement (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washindi wenzake aliyeshika nafasi ya pili Joyce Shayo (kushoto) na Lucy Tomeka aliyeshika nafasi ya tatu.
 Mambo yalikuwa hivyo kwa baadhi ya washiriki
 Lucy Tomeka akifanya vitu vyake
 Huyu ni kama Lil Bow Wow!!
 Huyu ni balaaaa
 Hapa jee
 Weeeeee
 Prisca alikula moto kama hana akili nzuri na kuibuka mshindi
 hii we acha tu...
 Huyu alitoka hivi...na twist kali aliicheza