Wednesday, 28 August 2013

BONDIA BOTHA ATUA JIJINI DAR


Bondia wa Dunia wa uzito wa juu  Francois Botha akionyesha jinsi ya kupambana kulia ni Yasini Abdalla Rais wa Shirikisho la ndondi nchini ,kushoto ni mdau wa ndondi , uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius  Nyerere  leo  jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya  Michezo Bi.Juliana Yassoda akiwa na  Bondia wa Dunia   wa uzito wa juu Francois Botha alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  leo  jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuzungumzia masuala ya  mchezo wa ndondi utakaofanyika  30 Agosti mwaka huu katika ukumbi wa Diamond.
 Bondia wa Dunia wa uzito wa juu  Francois Botha  akionyesha mmoja ya mkanda alioishinda kwa   muuandaaji wa pambano hilo J Msangi,kushoto ni Rais wa  Shirikisho la Ndondi  Howard Goldberg katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  leo  jijini Dar es salaam
Bondia wa Dunia  Francois Botha akiwa na muuandaaji wa pambano hilo J Msangi,kushoto ni Rais wa  Shirikisho la Ndondi  Howard Goldberg katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius  Nyerere  leo  jijini Dar es salaam.

AUNT EZEKIEL ALIVYOCHABANGWA CHUPA CLUB



MWIGIZAJI wa  sinema za kibongo, Aunt Ezekiel Grayson ‘Gwantwa’ amenusurika kupasuliwa paji la uso kwa chupa baada ya kupigwa mkononi...
 

Usiku wa kuamkia Jumatatu, nje ya Ukumbi wa Billicanas, mwanamke aliyejulikana kwa jina moja la Yvonne alimpiga Aunt kwa chupa tupu ya bia na kumpasua mkono wa kushoto.

Watu walioshuhudia tukio hilo wamedai  kuwa, wakati Yvonne anatekeleza ukatili huo, Aunt alikuwa amesimama na marafiki zake waliotajwa kwa jina moja moja, Sajenti na Rehema. 
 “Ndani ya ukumbi shoo ilikuwa ikiendelea, Aunt, Rehema na Sajenti walisimama nje, ghafla alitokea Yvonne akiwa na chupa mkononi, akailenga kwenye paji la uso la mwenzake, bahati nzuri Aunt aliiona na kukinga mkono,” kilisema chanzo.

Kikaendelea: Vurugu kubwa ilizuka, ilibidi shoo ndani isimame ili kushughulia suala hilo. Aunt alikimbizwa Aga Khan, Yvonne akapelekwa msobemsobe Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Dar ambapo anashikiliwa.

Baada ya taarifa hizo, juzi mchana, mwandishi wetu  alifika  nyumbani kwa Aunt, Mwananyamala na kumkuta ambapo alikuwa na haya ya kusema:

“Ishu ni kweli kama mlivyosikia, lakini kule Agha Khan sikutibiwa, niliambiwa daktari hayupo mpaka saa mbili asubuhi na muda huo ilikuwa saa kumi alfajiri.

“Ilibidi niende kutibiwa kwa Dokta Mvungi, Kinondoni Hospitali ambako nilishonwa nyuzi sita.”

mwandishi: Madai ya Yvonne ni nini hasa?
Aunt: Yaani hata mimi sijui, nilishangaa sana. Kwanza lengo lake lilikuwa kunijeruhi kwenye uso, lakini niliiona chupa nikaikinga na mkono ndiyo maana ikaniumiza.

 mwandishi: Siku za nyuma uliwahi kuingia kwenye mzozo na Yvonne kwamba unamchukulia mpenzi wake aitwaye Joff, siyo kwamba ndiyo kisasi?
 
Aunt: Yale mambo yalipita, yeye ana maisha yake na mimi nina yangu.

BASI LA HOOD LAGONGA NA KUUA MMOJA PAPO HAPO


HABARI ZILIZOUFIKIA MTANDAO HUU HIVI PUNDE ZINASEMA KUWA MTU MMOJA ANAYEKADILIWA KUWA NA UMRI WA MIAKA (45) AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA BASI LA HUD LILILOKUWA LINATOKEA KILOMBERO KUJA JIJINI DAR, ENEO LA KIEMBENI MIKESE.
IMEELEZWA KUWA KATIKA AJALI HIYO WATU WENGINE 15 WAMEJERUHIWA WAKATI BASI HILO LILIPOKUWA LIKIJARIBU KUMKWEPA MTU HUYO NA KUINGIA PORINI NA KISHA KUPINDUKA MIGUU JUU.
AIDHA IMEELEZWA KUWA DEREVA WA BASI HILO LILILOSABABISHA AJALI HIYO KUTOKANA NA MWENDO KASI, ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA HASSAN MBEGA, AMETOROKA NA JESHI LA POLISI LINAENDELEA NA ZOEZI LA KUMTAFUTA ILI KUMFIKISHA MBELE YA SHERIA.
MAJERUHI WAMEPELEKWA KATIKA HOSPITALI YA MKOA WA MOROGORO KWA MATIBABU.

VIJIMAMBO VILIVYOJILI FIESTA 2013 SINGIDA NA TABORA


WALIMU WAWILI NA WAKULIMA WAWILI WAIBUKA WASHINDI WA PROMOSHENI YA AIRTEL YATOSHA


Washindi wa siku wa shilingi milioni moja wa promosheni ya Airtel yatosha bwana Thomasi Joackim Chali na Abdallah Omari Muhomba kwa pamoja wakionyesha furaha mara baada ya kukabithiwa zawadi za pesa
taslimu baada ya kuibuka washindi wa siku wa promosheni ya Airtel yatosha.
Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando akiongea na moja ya washindi wakati Airtel ilipochezesha droo ya saba ya washindi wa shilingi milioni moja kila siku wa promosheni ya Airtel yatosha
ambapo mpaka sasa zaidi ya shilingi million 44 zimeshatolewa. Akishuhudia ni Msimamizi wa bodi ya michezo ya Bahati nasibu.
 *   Zaidi ya shilingi million 39 bado kushindaniwa.
 *   Na washindi wa wiki ya sita wakabidhiwa zawadi zao.

Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel imetangaza  washindi wake saba wa wiki ya saba ya  Airtel Yatosha  promosheni na kukabidhi zawadi za  washindi wa wiki ya sita wa promosheni ya  Airtel Yatosha.

Airtel imechezesha droo ya wiki ya saba ya promosheni ya Airtel yatosha Jana  katika ofisi za makao makuu ya Airtel morocco jijini Dar es saalam ambapo wateja saba  wameibuka washindi wa kitita  cha
shilingi million 1 kila mmoja.

Washindi hao ni pamoja na Theresia Martine Komba wa Morogoro -Mkulima, John Kimoro wa kondo Dodoma -Mwalimu, Yohanna Masunga Zengo wa Maswa Shinyanga -Mkulima, Isabellah Joseph wa Chamwino Dodoma  -Mwalimu, Nassor Mohammed Nassor  wa Kariakoo DSM -Mfanyabiashara, Modest Laurian Mussa wa Bukoba Kagera  -Mfanyabiashara na  Masanja Mwanamenda
wa Nkyala Singida -Mfanyabiashara.
Wakati huo huo Airtel imeendelea kuwazawadia wateja wake kupitia promosheni ya Airtel Yatosha ambapo washindi wa wiki ya sita nao walikabidhiwa zawadi zao ambapo kila mmoja aliondoka na shillingi
milioni moja.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo katika ofisi za makao makuu ya  Airtel  bwana Abdallah Omari Muhomba  mmoja wa washindi  wa million  1 alisema, "nashindwa jinsi ya kuongea lakini nawashukuru sana Airtel kwa kuweza kunizawadia shilingi milioni 1 ambazo kwangu  nikama ndoto.
 Nategemea kutumia pesa hizi kujiendeleza kiuchumi na maaendeleo ya familia yangu. Binafsi nachukua fursa hii kuwaasa watanzania kushiriki katika promosheni hizi za Airtel na kwa hakika wataamka washindi kama
mimi hivi leo".

Kwa upande wake bwana Thomas Joachim Chali ambaye pia ni Mshindi wa wiki ya sita alisema, "anawashukuru Airtel kwa kuanzisha promosheni yaAirtel Yatosha , na kuahidi kuzitumia pesa zake kuendeleza na kupanua biashara kwa kuwa hiyo ndio shughuli kubwa anayoifanya"

Akiongea wakati wa makabidhiano hayo kwa washindi hao Meneja uhusiano wa Airtel bwana Jackson Mmbando alisema, "leo tunao washindi saba waliojishindia shilingi milioni 1 kila moja katika droo ya wiki.
Tumeendelea kushuhudia watanzania na wateja wetu wakiibuka mamilionea kila siku na kila mwezi kupitia promosheni hii ya Airtel Yatosha.

Tunaahidi kuendelea kuwazawadia wateja wetu huku tukiboresha huduma zetu , na kuwapata wateja wetu huduma bora zenye gharama nafuu kupitia huduma yetu poa ya Airtel Yatosha inayomuwezesha mteja kuwasiliana na mitandao mengine ya simu za mkononi kwa bei poa na kupata vifurushi
vya maongezi bila kulipia gharama ya ziada". Aliongeza Mmbando.

Promosheni ya Airtel Yatosha bado inaendelea na wateja wetu wa Airtel Yatosha bado wananafasi ya kuendelea kujishindia pesa taslim na Nyumba  mbili za kifahari zilizopo Kigamboni  bado kushindaniwa.

Droo itakayomchagua mshindi wa nyumba kwa mwezi huu inatarajiwa kuchezeshwa tarehe 5/9/2013 saa tano asubuhi. hii itachagua mshindi mmoja kati ya wateja wote waliotumia huduma ya Airtel yatosha kwa
mwezi huu.

Ili mteja wa Airtel aweze kushiriki  anatakiwa kujiunga na vifurushi vya Airtel Yatosha kwa kupiga *149*99# na kujiunga na vivurushi vya Airtel Yatosha. Kila unapojiunga na kifurushi unaingia moja kwa moja
kwenye droo ya kushinda.

GRAND MALT YAMWAGA VIFAA LIGI KUU ZANZIBAR

 Mwakilishi wa timu ya KMKM ya unguja  Said Mfaume akipokea jezi toka kwa Waziri wa habari,utalii na michezo Zanzibar Said Mbarouk tayari kabisa kwa kuanza kwa ligi kuu ya Grandmalt Zanzibar,Kulia ni meneja masoko wa GrandMalt Fimbo buttala na Rais wa ZFA Ravia Faina
 Mwakilishi wa timu ya Mafunzo  ya pemba  Khamis Ally akipokea jezi toka kwa Waziri wa habari,utalii na michezo Zanzibar Said Mbarouk tayari kabisa kwa kuanza kwa ligi kuu ya Grandmalt Zanzibar,Kulia ni meneja masoko wa GrandMalt Fimbo buttala na Rais wa ZFA Ravia Faina
 Mwakilishi wa timu ya jamhuri  ya pemba  Abdallah Abeid  akipokea jezi toka kwa Waziri wa habari,utalii na michezo Zanzibar Said Mbarouk tayari kabisa kwa kuanza kwa ligi kuu ya Grandmalt Zanzibar,Kulia ni meneja masoko wa GrandMalt Fimbo buttala na Rais wa ZFA Ravia Faina.
KINYWAJI kisicho na kilevi cha Grand Malt, walio wadhamini wa Ligi Kuu ya Zanzibar maarufu kama ‘Grand Malt Premier League’ jana walikabidhi rasmi vifaa kwa timu 12 zinazoshiriki ligi hiyo katika hafla iliyofanyika hoteli ya Bwawani, mjini hapa.
 
Mbali na kumwaga vifaa hivyo, Grand Malt pia wameamua kufanya kweli zaidi kwa kuongeza udhamini wao kwa waamuzi na uendeshaji wa ligi, ambapo msimu huu watatoa kiasi cha Sh milioni 200 kutoka Sh milioni 140 za msimu uliopita.
 
Hafla hiyo maalumu ya kukabidhi vifaa na kutangaza kiasi hicho kipya cha uendeshaji wa ligi,  ilihudhuriwa na viongozi na wanamichezo mbalimbali wakiongozwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Saidi Ali Mbarouk.
 
Akizungumza katika hafla hiyo, Mbarouk alisema wamefurahishwa mno na Grand Malt kwa kuongeza udhamini wao pamoja na kutoa vifaa bora vya michezo kwa timu zote zishiriki.
 
“Tuna uhakika sasa soka ndani ya Zanzibar itazidi kusonga mbele, ombi lenu kwenu ZFA (Chama cha Soka Zanzibar), pamoja na wadau wote kutumia fursa hii kuhakikisha tunafika kule tunakokutaka.
 
“Nawasifu zaidi Grand Malt kwa kuendelea kudhamini Ligi Kuu ya Zanzibar nah ii inadhihirisha tuko nao pamoja kwa mambo mengi, nasi pia tunapaswa kuwaunga mkono kwa kutumia kinywaji chao,” alisema.
 
Mkurugenzi wa Masoko wa Grand Malt, Kushillah Thomas naye alisema, kinywaji hicho kitaendelea kushirikiana na watu wa Zanzibar katika kuhakikisha wanafanikiwa kwenye malengo yao.
 
“Udhamini huu ni mwanzo tu na tunaamini utasaidia kwa kiwango kikubwa kufanikisha malengo ya soka ya Zanzibar,” alisema.
 
Viongozi wa ZFA nao walikiri kufurahishwa na udhamini huo na kusema, wanaamini Ligi Kuu ya Grand Malt msimu huu itakuwa na ushindani mkubwa zaidi.
 
KMKM ndio waliofanikiwa kutwaa ubingwa huo msimu uliopita, wakiwa ni mabingwa wa kwanza toka kuanza kwa udhamini wa Grand Malt.
 
Mbali na KMKM timu nyingine zinazoshiriki ligi hiyo ni Fuoni, Chuoni, Polisi, Malindi (Bandari), Zimamoto, Mafunzo, Jamhuri, Chipukizi, Kizimbani, Mtende na Miembeni.
 
Kinywaji cha Grand Malt kisicho na kilevi ndio walioingia mkataba wa kudhamini ligi hiyo, hivyo kujulikana kama Ligi Kuu ya Grand Malt.

Tuesday, 27 August 2013

KAMATI KUU CCM YABATILISHA UAMUZI WA HALMASHAURI KUU YA CCM BUKOBA




 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi  wa CCM, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uamuzi wa kamati kuu wa kubatilisha kufukuzwa kwa madiwani wa Bukoba nje ya ukumbi wa NEC.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa imejadili na kutolea maamuzi pamoja na mambo mengine suala la Madiwani wanane waliotangazwa kufukuzwa uanachama na Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera.

Katika maamuzi yake, Kamati Kuu imebatilisha uamuzi uliofanywa na Halmashauri Kuu CCM ya Mkoa wa Kagera Agosti 13, 2013 wa kuwafukuza uanachama Madiwani hao. Hivyo Madiwani hao wanane ni wanachama halali wa CCM.

Kamati Kuu imetoa uamuzi huo, baada ya kubaini kuwa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera haikuzingatia Katiba ya CCM ya 1977 Toleo la 2012 Ibara ya 93 (15). Ibara hiyo inasomeka kuwa moja ya kazi ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa ni:-
“Kumwachisha au kumfukuza uongozi kiongozi yeyote ambaye uteuzi wake wa mwisho unafanywa na Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa, isipokuwa kwa suala la kumvua uanachama au uongozi Diwani lisifanyike hadi Kamati Kuu imearifiwa na kutoa maelekezo”.

Aidha, Kamati Kuu imewaonya Madiwani wa CCM wa Manispaa ya Bukoba, Mbunge wa Bukoba Mjini na Meya kwa kusababisha kukosekana kwa utulivu, mshikamano na amani katika Manispaa na Chama.

Kamati Kuu pia imeitaka Serikali kumwagiza mdhibiti na mkaguzi mkuu wa serikali(CAG) kufanya ukaguzi maalum wa haraka wa mambo yanayolalamikiwa dhidi ya Meya ili ukweli ujulikane na matokeo ya uchunguzi huo yasilishwe kwenye baraza la madiwani ili hatua stahiki zichukuliwe kwa mujibu wa sheria na taratibu zinazoongoza Serikali za Mitaa.

Wakati tuhuma hizo dhidi ya Meya zikichunguzwa; Kamati Kuu inawataka Madiwani wa CCM  kurejesha utulivu kwenye Manispaa na Chama kwa ujumla ili kufanikisha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuwaletea maendeleo wananchi wa Bukoba.

Imetolewa na:-

Nape Moses Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM
ITIKADI NA UENEZI
27/08/2013

MATUKIO MBALI MBALI NJE YA UKUMBI WA NEC



 Mwenyekiti wa Mkoa wa Kagera Constansia Buhiye akizungumza na aliyekuwa Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Hamis Suleiman Dadi nje ya ukumbi wa NEC, Dodoma leo, kushoto ni Katibu wa Mkoa wa Kagera Avelin Mushi.

 Meya wa Bukoba ndugu Anatory Amani akizungumza na Mwneyekiti wa UVCCM nje ya ukumbi wa NEC mara tu baada ya kutoka kwenye mahojiano na kamati kuu ya CCM.
Watumishi wa Makao Makuu CCM, kutoka kushoto ni Suleiman Serera,Adam Soud, Katibu Mpya wa  CCM Mkoa wa Morogoro ndugu Romuli  John na Annamringi Macha wakibalishana mawazo nje ya ukumbi wa NEC ,Dodoma.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari juu ya uamuzi wa kamati kuu kubatilisha uamuzi wa kufukuzwa madiwani wa Bukoba.

WEMA SEPETU ATAMBULISHA WASANII WAKE



wema2
mirror
barnaba
Wasanii wanaokuja kwa kasi katika muziki wa Bongo flava hapa Tzee Mirrow pamoja na Asali jana waliweza kukonga nyoyo za mashabiki wao walipopanda Jukwaani.
Mirrow na Asali ni wasanii wanatoka katika kampuni ya Endless Fame ambayo ipo chini ya Mwanadada mahiri Wema Sepetu.
Katika uzinduzi huo wasanii wa Endeless Fame walitambulisha nyimbo zao mpya ambazo ziliwagusa mashabiki waliofika katika Club ya Bilicanas, pamoja na uzinduzi huo CEO wa Endless Fame Wema Sepetu alipanda Jukwaani kwa ajili ya kunena na mashabiki wake, ili waweze kuwapokea wasanii wanaotoka katika kampuni yake.
Uzinduzi wa nyimbo mpya za Mirrow na Asali ulisindikizwa na wasanii mbalimbali kama vile, Mwana FA, H.Baba, Country Boy, Barnaba, Mao, TID, Nyandu Tozi, Hassani Mapenzi.