Friday, 12 July 2013

RAIS KIKWETE AKUTANA NA NAIBU WAZIRI MKUU WA KUWAIT IKULU DAR ES SALAAM LEO JULY 12, 2013

Friday, July 12, 2013

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Naibu Waziri Mkuu wa Kuwait na Waziri wa mambo ya Nje wa Kuwait Mhe Sabah Khalifa aliyemtembelea leo Ikulu Dar es salaam
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Naibu Waziri Mkuu wa Kuwait na Waziri wa mambo ya Nje wa Kuwait Mhe Sabah Khalifa na ujumbe wake aliyemtembelea leo Ikulu Dar es salaam
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata picha ya kumbukumbu na Naibu Waziri Mkuu wa Kuwait na Waziri wa mambo ya Nje wa Kuwait Mhe Sabah Khalifa na ujumbe wake aliyemtembelea leo Ikulu Dar es salaam


AIRTEL YATOA FUTARI KWA WATOTO YATIMA MIKOA MINNE


Friday, July 12, 2013

 Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye hafla fupi ya makabidhiano  ya vyakula vya kufuturisha watoto yatima katika vitu vilivyopo mikoa ya Dar es salaam, Mbeya, Arusha, Mwanza katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani iliyofanyika  katika ofisi za Airtel jijini Dar Es Salam ,akifuatiwa na meneja wa huduma za Jamii wa Airtel bi Hawa Bayumi.
 Meneja  Uhusiano wa Jamii wa Airtel bi Hawa Bayumi  akimkabidhi mwakilishi wa Bakwata Ustadh Hassan Malangali vyakula vya kufuturisha katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani  vilivyotolewa kwa vituo vitatu  vya watoto yatima Dar es Salaam (hawapo pichani)  vituo vitakavyofaidika zaidi ni vya Dar es salaam, Mbeya, Mwanza, Arusha hafla ya makabidhiano iliyofanyika  katika ofisi za Airtel  Morocco jijini Dar Es Salam .
 Meneja  Uhusiano wa Jamii wa Airtel bi Hawa Bayumi  akiwakabidhi Saida Makope mmoja wa wakilishi wa kituo cha watoto yatima mjini Dar Es Salaam  katika  hafla fupi ya makabidhiano  ya vyakula vya kufuturisha katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani  vilivyotolewa kwa vituo vitatu vya watoto yatima jijini Dar Es Salaam  iliyofanyika katika ofisi za Airtel  Morocco jijini Dar Es Salam  akifuatiwa na mwakilishi wa Bakwata ustadhi Ustadh Hassan Malangali .
 Wateja Airtel sasa kupata muda wa dua, nukuu za qurani, mawaidha kwa kutuma neno Ramadhani kwenda 15322 kwa shilingi 153 tu kwa siku.
Kampuni za simu za mkononi za Airtel Tanzania kupitia Kitengo chake cha huduma kwa Jamii wametoa msaada kwa vituo vitatu jijini Dar Es Salaam vya watoto yatima katika mwezi mtukufu wa Ramadhani vikifuatiwa na vituo vingine katika mikoa ya Arusha, Mwanza na Mbeya ili kusaidia watoto wanaolelewa kwenye vituo hivyo.

Msaada huo umetolewa kwa lengo la kuwalenga watoto kutoka mikoa minne ambayo ni Dar Es Salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya kwa watoto hawa wanaohitaji upendo  hususani katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani. Baadhi ya vitu vilivyotolewa ni Mchele,Sukari, maharagwe,unga, mafuta ya kupikia,maziwa, juice, majani ya chai na sabuni vyenye dhamani ya shilingi milioni tano na nusu.

Akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano iliyoandaliwa katika makao makuu ya  Airtel jijini Dar Es Salaam, Meneja uhusiano wa huduma kwa Jamii bi Hawa Bayumi alisema "kwa kutambua umuhimu wa Jamii tunayofanya nayo biashara kampuni ya Airtel tumeamua turudishe kiasi cha faida tunayopata kwa wananchi ili iwasaidie.

Akifafanua alisema kwa muda wa miaka 11 iliyopita tumeweza kusaidia Jamii mbalimbali ya watanzania ndani ya mfungo wa Ramadhani na bila kuacha nyanja za elimu, michezo kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na kukosa huduma mbalimbali za kijamii.

Kwa mwaka huu kupitia Kitengo chake cha huduma kwa Jamii tutarudisha tulichokipata na tutaweza kufikia watoto zaidi ya 300 wa mikoa ya Dar Es Salaam, Arusha , Mwanza na Mbeya na mpaka sasa  kwa mwaka huu Airtel imegharamia zaidi ya shilingi millini 150 katika kukuza kiwango  cha elimu kwa watoto wetu hapa Tanzania," alisema Bayumi.

Bayumi aliongeza kwa kusema kwamba Airtel inapenda kuwatakia kheri na Baraka katika mwezi huu mtukufu na tangu kuanza kwa Mwezi mtukufu wa Ramadhan, wateja wa Airtel wanaweza kufurahia huduma maalumu ya  Ramadhani kwa kutuma neno RAMADHANI kwenda namba 15322 kwa shilingi 153 tu kwa siku. Katika huduma hii mteja atapokea dua, nukuu za qurani, mawaidha na taraweh salat moja kwa moja kwenye simu yake, kila siku.

Naye katibu mkuu wa Bakwata Sheikh Suleiman Lolila  ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema mbali ya hafla hiyo makabidhiano ya chakula imetoa fursa kwa waislam kutoka maeneo mbalimbali kukutana pamoja na kukumbushana juu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Aidha Lolila licha ya kuishukuru Airtel Tanzania kwa misaada inayotoa kwa Jamii alisema jambo hilo linahitaji pongezi na kutaka liungwe mkono na kuigwa na kampuni zingine hapa nchini.

CAMERA YETU IJUMAA YA KWANZA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI,MSIKITI WA IJUMAA NA BILELE USWAHILINI BUKOBA LEO

                                           ni ijumaa ya kwanza ya mfungo wa ramadhani
                                    waumini wamejaa mpaka nje na wengine wamesimama
                                                              watoto nao wakiwa msikitini
                                                          wakati wa swala umefika
                                                          mzee waziri akiwa msikitini
                                               shehe jamada(kulia) na shekhe kassimu
                                                           waumini wakisikiliza mawaidha
                                             waumini walijitokeza kwa wingi na wengine waliswalia nje ya msikiti
                                          ramadhani kambunga na ndugu yazid wakiwa msikiti wa ijumaa
                                               hapa ni waumini msikiti wa ijumaa wakitoka
                                                                 waumini wakitoka msikitini
                                                        bwana subira akitoka msikitini
             shekhe akiwataka waumini kutoa swadaka zao katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu
 shekhe kichwabuta akiwasisitiza waumini kuchangi kununua rangi ya kupiga msikiti wa bilele leo
                                                     salamu alkhum,ijumaa kareem
                                           wamama wamejitanda ushungi na nguo ndefu
                                              akina mama wakitoka msikitini bilele
Waumini wakiwa wamemaliza kuswali  swala ya ijumaa kaika msikiti wa bilele,jamcobukoba.blogspot.com tunawatakia mfungo mwema

KAGASHEKI CUP 2013: IJUGANYONDO 0 vs BAKOBA 11, AIBU YAIKUMBA TIMU YA IJUGANYONDO YACHAKAZWA BAO BILA HURUMA!!!

Bakoba wakicheza kwa kujiamini na kucheza mchezo wa kuwashtukizia wenzao Ujuganyondo leo kwenye Kagasheki Cup 2013, Uwanja wa Kaitaba wameishindilia jumla ya mabao 11-0 timu ya Kata ya Ijuganyondo bila kujitetea!!!
Mchezo huu mpaka kipindi cha kwanza kinaisha Bakoba walikuwa mbele ya bao 6-0 dhidi ya kibonde Ijuganyondo. Kipindi cha pili Bakoba waliendeleza ubabe wao wa kuziona nyavu na kweza kufunga bao 5 na huku wakikosa mabao mengi na ya wazi.
Benchi la Timu ya Bakoba
Benchi la ufundi na viongozi wa Bakoba wakiendelea kuangalia timu yao ikimenyana na timu ya Ijuganyondo
Kocha wa Ijuganyondo hakuweza kukaa maana alikuwa na jukumu la kuwahamasisha wachezaji wake nao waweze kufika kwenye lango la wenzao japo hawakuweza kufurukuta hata kidogo hata kusogea eneo la kipa.
Mchezo uliopigwa saa nane kamili mchana na timu ya Bakoba ikaibuka kidedea kwa bao 11-0 na kujiwekea historia ya pekee tangu Kagasheki ianze, Na kumbuka hawa Ijuganyondo juzi walicheza na Kashai na kufungwa bao 4-0 hivyo timu hii unaweza ukajionea mwenyewe kwa lugha nyingine unaweza ukasema ni kibonde!!!, Kwa kukujuza zaidi nakumbuka kwa haraka timu iliyowahi kufungwa mabao 11-0 ni ya mwaka 2011 Septemba 2 wakati timu ya uholanzi ilipoifunga bao 11-0 timu ya San Marino, Robin Van Persie mchezaji wa United alipoifunga bao nne mwenye na leo hii kuna mchezaji wa Bakoba kafunga bao tano mwenyewe!!!
Wachezaji wa Bakoba wakiwatoka wachezaji wa Ijuganyondo na kwenda kufunga.
Mashabiki jukwaa kuu walikuwa wakishangilia vilivyo baada ya kuona Mabao yaingia bila shida ya kukabwa na huku timu ya Ijuganyondo ikionekana kuzidiwa kila kitu!!

Mashabiki wakishangilia jukwaa kuu
Wadau wakifatilia soka wengine wakiponda kibonde Iujuganyondo

Furaha ikatanda kwa Mwinyi kushoto hapa!!! akiwa na wachezaji wa akiba

Mashabiki wakiwa hawana hamu!!! wengine wakisikitika kwa kile kinachoendelea na wengine wakisikitika kuona Bakoba wanaendelea kukosa mabao kadhaa kwenye goli la Ijuganyondo!!!
Shabiki akipuliza Vuvuzela la asili kuashilia soka hapa!!

wakati wa mapumziko Bakoba wakipongezwa kwa kazi nzuri!
Kiongozi mwinyi akiwapongeza wachezaji wa Bakoba

Mashabiki

Patashika za hapa na pale kwenye goli la Ijuganyondo!

Kikosi cha Bakoba

Bakoba wakijiachia kwenye kamera

Baada ya mechi kuisha Bakoba wakipongezana na kuomba kwa kile walichokifanya uwanjani Kaitaba cha kuwazaba Ijuganyondo bao 11-0


Patashika mchezaji wa Ijuganyondo aliumia kichwani baada ya kukogana kichwa na mwenzake

Kipa wa Ijuganyondo hoi!!!

Hoi!!!!!!!!! kibano cha 11-0!!............hakunaga!