Saturday, 9 June 2018

OMURANGILA JUSTUCE RUGAIBULA AFUTURISHA WATOTO YATIMA, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI.

 Ilikuwa ni siku ya pekee sana katika familia ya Omurangila Justuce Rugaibula ya kukutanisha watoto yatima wa kituo cha Nusuru kilichopo Kashai Manispaa ya Bukoba, ndugu ,jamaa na marafiki na kufuturu kwa pamoja,na baada ya hapo ilisomwa dua ya kumshukuru mwenyezi mungu kwa mema na makuu anayoitendea familia,Hafla hii fupi ya kufuturu ilifanyika nyumbani kwa Omurangila Justuce Rugaibula Ibura katika kata ya Ijuganyondo.Kwa niaba ya  Bw Justuce Rugaibura ambae akuwepo yupo safarini nje ya nchi, mama Mzazi Ma Graice alitoa neno la shukrani kwa wageni wote waliofika katika hafla ya kufuturu na watoto yatima, na Ma Graice alitoa wito na kuwaomba wadau mbalimbali kusaidia watoto yatima kwani ni wajibu wa kila mmoja kutambua na kuona kuwa anayobudi ya kusaidia .(katika picha watoto yatima , ndugu na marafiki wakiomba dua.)
 Makazi ya Omurangila Justuce Rugaibula ,.
 Shekhe wa wilaya Bukoba Mjini ,Shekhe kakweke akipata futari na wageni wengine.
 Kushoto Bw Emily Baruti na  Bw Arodi Baruti wakipata Futari.
 Wadau mbalimbali waliobahatika kufika wakipata futari.
 Rais wa Kanda ya ziwa akihakikisha kila mtoto anapata chakula na kinywaji.
 ILIHAM CAFE,Wataalamu wa kupika vyakula mbalimbali katika shughuli mbalimbali ,ndio waliandaa futari.
 Bw Rahim Kabyemela akiwajibika ipasavyo kuhakikisha watoto wanapata huduma.
 Rais wa kanda ya ziwa alilazimika kuwa karibu na huyu mama washirikiane kutoa huduma.
 Kulia Bw Afidhu Karugila,mtu muhim sana aliehakikisha shughuli zinakwenda vizuri. akiwa na Bw  Novatus Nkwama mwenyekiti mstaafu wa ccm Bukoba vijijini.
 Kulia Ma Graice akionekana na furaha.
 Rais wa kanda ya ziwa baada ya shughuli nzito.
 Kijana Rama ,mdau mkubwa aliehakikisha shughuli inafanikiwa.
 MA OGARNAISER.
KWA HABARI ZA KIJAMI, BURUDANI NK TEMBELEA BLOG YETU. AU PIGA SIMU 0788707027 AU 0754757157

UZINDUZI WA PASIPOTI ZA KIELECTRONIKI MKOA WA KAGERA WAFANA.

 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustaph Kijuu amewataka watumishi wa Jeshi la Uhamiaji Mkoa wa Kagera kufanya kazi kwa weredi,uhaminifu na kujituma kuhudumia wananchi katika zoezi la utoaji wa pasipoti za kielectroniki,Akisoma hutuba kwa niaba yake katika uwanja wa Uhuru Bukoba Manispaa ,Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kagera  Mh Deodatus Kinawiro amewataka wananchi wanachi kujitokeza kwa  wingi na kuchangamkia huduma  hii ya pasipoti,huku akitaja faida mbalimbali za kuwa na pasipoti hii. kwa  mujibu wa idara ya Uhamiaji mpaka sasa tayari Jeshi la Uhamiaji limekwisha toa  jumla ya pasipoti 17,598 zikiwemo pasipoti za kawaida, Utumishi, Diplomasia na Diplomasia maalum tangu zoezi hili lilipozinduliwa Rasmi na  Januari 31 mwaka huu, na Mh Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli.(katika picha kushoto mgeni rasmi Kaimu Mkuu wa Mkoa Kagera Deodatus Kinawiro akimkabidhi  pasipoti  ya Kieletroniki Mwenyekiti wa CCM Bukoba Mjini Mh Joas Muganyizi  Zachwa.)
 Kamishna wa pasipoti na  Uraia   Gerlad Kihigi akisalimiana na wageni, wakiwemo viongozi wa dini katika hafla ya uzinduzi wa pasipoti za Kieletroniki.
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bkoba Chief Kalumuna akisalimiana na viongozi wa dini.
 Shekhe wa Mkoa wa Kagera Haruna Kichwabuta akifungua kwa Dua.
 Mwenyekiti wa ccm Bukoba Mjini Joas Muganyizi Zachwa akitoa salamu kwa niaba ya mwenyekiti wa Mkoa ccm.
 Kushoto Kamishna wa Pasipoti na Uraia Gerlad Kihiga akimkabidhi pasipoti ya Mkuu wa Mkoa Kagera iliyopokelewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa Deodatus Kinawiro.
 Baba ASKOF Rwoma akipokea pasipoti yake.
 Mzee Joseph Masabala akitoa neno kwa niaba ya wanachi waliofika katika hafla ya uzinduzi.
Kwa matukio mbalimbali ya kijamii ,burudani nk angalia blog yetu.