Friday, 15 December 2017

VILIO VYATAWALA WAKATI MIILI YA ASKARI WA JWTZ WALIOUAWA DRC IKIWASILI ZANZIBAR

Miili ya Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania {JWTZ} ikiteremshwa kwenye ndege ya JW 8029 katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume ikitokea Mjini Dar es salaam.
Balozi Seif pamoja na Mkuu wa Jeshi la Nchi Kavu Meja General Sharif Sheikh Othman wakitoa heshima wakati Miili ya mwashujaa ikiteremshwa kwenye ndege.
Balozi wa Kuweit Nchini Tanzania Bwana Jassem Alnajem wa kwanza kutoka kushoto akijumuika pamoja na Viongozi wa Kiserikali katika kuipokea Miili ya askari wa Tanzania waliouawa Nchini DRC Wiki iliyopita.
Mawaziri mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakishuhudia kuwasili kwa Miili yaWanajeshi wa Tanzania waliouawa na waasi wa ADF Nchini DRC.
Balozi Seif akiongoza Viongozi na Wananchi wa Zanzibar katika kuipokea miili ya Makeshi ya Tanzania yaliyouawa Nchini Jamuhuri ya Kisemokrasi ya Congo.
Majeshi ya Wananchi wa Tanzania wakiichukuwa Miili ya Askari wenzao wakiwasili katika Viwanja vya Makao Makuu ya Brigedia Nyuki Migombani kwa ajili ya kuagwa rasmi Kiserikali.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitoa salamu za pole kwenye shughuli Maalum ya Kuiaga Miili ya Wanajeshi wa JWTZ hapo Migombani Mjini Zanzibar.

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA MKUTANO MKUU WA CHAMA CHA WALIMU TANZANIA (CWT) MKOANI DODOMA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mamia ya wanachama wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) kabla ya kufungua mkutano huo Mkuu wa (CWT )katika ukumbi wa Chimwaga mkoani Dodoma. Wanachama hao wa CWT walisimama na kushangilia mara baada ya ahadi ya Rais Dkt. Magufuli kuwaahidi kuendelea kutatua kero zao mbalimbali.
Mamia ya Wajumbe wa Chama cha Walimu(CWT) wakishangilia ndani ya ukumbi wa Chimwaga wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akijibu kero zao mbalimbali walizoziwasilisha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na baadhi ya wajumbe wa Chama cha Walimu CWT mara baada ya kuwahutubia katika ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono na viongozi wa muda wa CWT, Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako, Spika wa Bunge Job Ndugai, pamoja na mke wa Rais Mama Janeth Magufuli wakiimba wimbo wa mshikamano pamoja na Wajumbe wote wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) katika ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wakiwa wameshikana mikono wakati wakiimba wimbo wa mshikamano kabla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuhutubia na kufungua mkutano huo wa CWT katika ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma.

MAJALIWA AMWAKILISHA JPM KUAGA MIILI YA ASKARI 14 WA JWTZ WALIOUAWA WAKIWA KWENYE OPERESHENI YA ULINZI WA AMANI CHINI YA UMOJA WA MATAIFA NCHINI DRC

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini, Jenerali Venance Mabeyo baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Upanga jijini Dar es salaam Desemba 14, 2017, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika kuaga miili ya askari 14 wa JWTZ waliouawa wakiwa katika operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa nchini Congo - DRC. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,. Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Upanga jijini Dar es salaam Desemba 14, 2017, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika kuaga miili ya askari 14 wa JWTZ waliouawa wakiwa katika operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa nchini Congo - DRC. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini kitabu cha maombolezo baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Upanga jijini Dar es salaam Desemba 14, 2017, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika kuaga miili ya askari 14 wa JWTZ waliouawa wakiwa katika operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa nchini Congo - DRC. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Upanga jijini Dar es salaam Desemba 14, 2017, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika kuaga miili ya askari 14 wa JWTZ waliouawa wakiwa katika operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa nchini Congo - DRC. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Susan Kolimba baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Upanga jijini Dar es salaam Desemba 14, 2017, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika kuaga miili ya askari 14 wa JWTZ waliouawa wakiwa katika operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa nchini Congo - DRC. Katikati ni Rais Mstaafu wa Awamu wa Nne, Jakaya Mrisho Kikwete na kushoto Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika - SADC. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa wamebeba miili ya askari 14 wa JWTZ waliouwa wakiwa kwenye operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa nchini Congo - DRC,`kwenye viwanja vya Makao Makuu ya JWTZ Upanga jijini Dar es salaam Desemba 14, 2017. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika kuaga miili ya askari hao. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Tuesday, 12 December 2017

TASWIRA KUTOKA JOSIAH GIRL'S SEC SCHOOL ILIYOPO BUKOBA





TASWIRA KUTOKA UWANJA WA NDEGE, JAMCO BLOG TWATETA JAMBO KWA KINA!




KIWANDA CHA SARUJI TANGA (SIMBA CEMENT) YATOA MIFUKO 760 KUCHANGIA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA SHULE YA MSINGI PONGWE JIJINI TANGA


Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akipanga tofali kwenye msingi wa ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya msingi ya wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi (Albino) na wasioona ya Pongwe Jijini Tanga ambapo Kampuni ya Simba Cement imetoa mifuko 760 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa vyumba hivyo

Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart kulia akijenga tofati katika vyumba vipya vitatu vya madarasa kwenye shule ya Msingi ya
ya wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi (Albino) na wasioona ya Pongwe Jijini Tanga ambapo Kampuni ya Simba Cement imetoa mifuko 760 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa vyumba hivyo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa

Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart kulia akiweka tofati katika vyumba vipya vitatu vya madarasa kwenye shule ya Msingi ya
ya wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi (Albino) na wasioona ya Pongwe Jijini Tanga ambapo Kampuni ya Simba Cement imetoa mifuko 760 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa vyumba hivyo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa



Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart kulia akiweka sawa tofati katika msingi wa moja ya vyumba vipya vitatu vya madarasa kwenye shule ya Msingi ya ya wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi (Albino) na wasioona ya Pongwe Jijini Tanga ambapo Kampuni ya Simba Cement imetoa mifuko 760 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa vyumba hivyo

Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart kulia akimuelekeza jambo mmoja wa wakandarasi watakaojenga vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya wanafunzi wenye maahitaji maalumu ikiwemo wasiona na wenye ulemavu wa ngozi (Albino) ya Pongwe Jijini Tanga ambapo Kampuni ya Simba Cement imetoa mifuko 760 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa vyumba hivyo



Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart kulia akiweka sawa tofati katika msingi wa moja ya vyumba vipya vitatu vya madarasa kwenye shule ya Msingi ya ya wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi (Albino) ya Pongwe Jijini Tanga ambapo Kampuni ya Simba Cement imetoa mifuko 760 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa vyumba hivyo

Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akizungumza katika halfa hiyo iliyofanyika leo kwenye shule ya Msingi Pongwe Jijini Tanga



Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi huo leo



Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Pongwe Yahaya Mafita mara baada ya kutoa hotuba fupi katika uzinduzi huo leo ambapo Kampuni ya Simba Cement imetoa mifuko 760 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa vyumba hivyo ambapo aliishukuru kampuni hiyo kwa kuthamini juhudi za kuinua elimu

Diwani wa Kata ya Pongwe(CCM),Mbaraka Sadi akizungumza katika uzinduzi huo ambapo Kampuni ya Simba Cement imetoa mifuko 760 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa vyumba hivyo



Afisa Uhusiano wa Simba Cement Noor Mtanga akizungumza katika uzinduzi huo leo kwenye shule ya Msingi Pongwe ambapo Kampuni ya Simba Cement imetoa mifuko 760 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa vyumba hivyo


Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart kushoto akipongezwa na Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Pongwe Yahaya Mafita mara baada ya kutoa hotuba fupi katika uzinduzi huo leo ambapo Kampuni ya Simba Cement imetoa mifuko 760 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa vyumba hivyo
Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart katikati akifuatilia uzinduzi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa kwenye shule hiyo uliofanywa leo na Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa kushoto ni Afisa Uhusiano wa Simba Cement Noor Mtanga

KIKAO CHA KUJADILI HALI YA USALAMA BARABARANI NCHINI CHAFANA MJINI DODOMA

Na WAMJW - Dodoma
Madereva nchini wamepongezwa kwa kuanza kubadilika na kutii sheria bila shuruti katika kukabiliana na ajali za barabarani na hivyo kupungua kwa ajali pamoja na vifo vitokanavyo na ajali kwa uendeshaji unaofuata taratibu na sheria za barabarani.


Hayo yamesemwa na Kamanda wa Kikosi cha Barabarani Tanzania Fotunatus Mselemu –Kamishana Msaidizi Mwandamizi wa Polisi(SACP) wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa kupokea maoni ya sheria kuhusu ajali za barabarani unaojumlisha mashirika yasiyo ya Kiserikali
Kamanda Mselemu alisema tatizo la ajali barabarani bado ni kubwa kwani watu wengi wanafariki na kujeruhiwa kutokana na ajali barabarani”sisi sote ni wahanga wa usalama barabarani hivyo hatuna budi wadau wote kushirikiana katika kukabiliana na suala hili na kila mmoja anayo nafasi ya kuchangia ili usalama wa barabarani uimarike na kuboreka zaidi”Alisema.


Alisema hivi sasa watu wengi wameanza kubadilika hususan madereva wengi ambapo kuna wakati inabidi jeshi la polisi kutumia nguvu nyingi ili kuweza kuepuka ajali zinazoweza kuepukika na nguvu hizi zimetumika kwa nia nzuri ili watanzania kuwa salama wanapotumia vyombo vya moto
Akitolea mfano kwa hali ya usalama barabarani kwa siku ya jana (juzi) nchi nzima kulikua na ajali nne ambazo zimesababisha vifi viwili na majeruhi nne,hivyo ni hatua nzuri.


Hata hivyo aliwataka wadau hao kuhakikisha wanatoa maoni mazuri ambayo yatasaidia kupata sheria ambayo haitamkandamiza mwananchi na ambayo itakua salanma na kupunguza ajali za barabarani nchini na kuwa na sheria inayotekeklezeka kwa kupunguza ajali kwa asilimia 50 kama
“Serikali ya awamu ya tano inapenda kulinda maisha ya watanzania,serikali inatengeneza uchumi wa kati na viwanda kwa kuboresha miundombinu ikiwemo barabasha hivyo jukumu letu kushirikiana na serikali kuilinda miundombinu yote inayotengenezwa”


Aidha,Kamanda Mselemu aliwataka wananchi waondoe dhana kwamba ajali zinatokana na nmapenzi ya Mungu “hii siyo kweli ila matatizo yote ya ajali ni sisi wenyewe tunasababisha kutokana na mwendo kasi na kutotii sheria za barabarani.


Alitaja takwimu za ajali barabarani kwa Tanzania kwa mwezi Julai hadi Septemba mwaka 2016 ilikua 639, vifo 923 na majeruhi 2,469 na kwa mwaka 2017 kuanzia Julai hadi Septemba ajali za barabarani zilikuwa 1,376, vifo 655 pamoja na majeruhi 1,469.


Naye Mwakilishi toka shirika la Afya Dunia Mery Kessy alisema zaidi ya asilimia 90 za ajali zinazotokea katika nchi zinazoendelea ingawa ni asilimia 10 tu nchi hizo zinamiliki vyombo vya moto na hiyo ni kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo miundombinu,mazingira pamoja na tabia.


Alisema wahanga wakubwa wanaopata ajali na vifo ni vijana kati ya miaka miaka 15 mpaka 29 kwani umri huu wanakuwa kwenye hatari kubwa ya kusababisha ajali na hivyo ajali hizo kuchukua zaidi ya asilimia 3 za pato la Taifa kwani serikali inaingia gharama kubwa kutibu majeruhi katika sekta ya afya.

Kamanda wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Nchini SACP Fortunatus Musilimu aliyesimama akiongea na wadau mbalimbali wa usalama barabarani hawapo pichani wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama barabarani nchini kilichofanyika leo mjini Dodoma.

Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Bi. Mary Kessy akiongea na wadau mbalimbali wa usalama barabarani hawapo pichani wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama barabarani nchini kilichofanyika leo mjini Dodoma.

ASP Deus Sokoni wa kwanza kulia akiongea na wadau mbalimbali wa usalama barabarani hawapo pichani wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama barabarani nchini kilichofanyika leo mjini Dodoma, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Wizara ya Mambo ya Ndani Bi. Marlin Komba anayefuata ni Kamanda wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Nchini SACP Fortunatus Musilimu.

Katibu Mkuu wa Shirikishi wa vyama vya Walemu nchini Bw. Felicina Mkude aliyesimama akiongea na baadhi ya wadau mbalimbali wa usalama barabarani hawapo pichani wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama barabarani nchini kilichofanyika leo mjini Dodoma.



Baadhi ya wadau mbalimbali wa usalama barabarani wakimsikiliza kwa makini Kamanda wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Nchini SACP Fortunatus Musilimu hayupo pichani wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama barabarani nchini kilichofanyika leo mjini Dodoma.

Kamanda wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Nchini SACP Fortunatus Musilimu katikati waliokaa akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa usalama barabarani wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama barabarani nchini kilichofanyika leo mjini Dodoma.