Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amezindua barabara ya Kyaka Bugene yenye urefu wa km 59.1 yenye kiwango cha lami.Rais Magufuli amesema wakati akiwa waziri wa wizara ya ujenzi katika serikali ya awamu ya nne ulianza ujenzi wa barabara hii na leo akiwa rais anaizindua,amewataka wananchi kuilinda na kutumia fursa ya barabara hii katika uzalishaji mbalimbali na kuwaletea maendeleo.Hafla ya uzinduzi ilifanyika katika mji wa Kayanga Karagwe na kuudhuliwa na mawaziri, makatibu wakuu, wabunge, viongozi wa chama tawala na vyama vya kisiasa,na wananchi.
Mzee Mavunde Mc wa shughuli nzima.
Wednesday, 8 November 2017
Monday, 6 November 2017
RAIS MAGUFULI AZINDUA UWANJA WA NDEGE BUKOBA, UWANJA KUPANULIWA, MELI MPYA YAJA.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amezindua rasmi u kiasi cha wanja wa ndege wa Bukoba leo 6-11-2017, akiongea na wanachi waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza katika viwanja vya uwanja wa ndege , Rais Magufuli amewashukuru wafadhili Benki ya dunia waliofadhili kwa asilimia themanini na seriikali kuchangia zaidi za cha bilioni sita, amewata wananchi kuutumia uwanja huu kwa ajili ya maendeleo kwa wana Kagera, wakati huohuo Rais Magufuli amesema uwanja wa Bukoba utapanuliwa zaidi ili ziweze kutua ndege kubwa za mizigo na itawezesha kusafirisha mazao mbalimbali, na kipato zaidi,wakati huo Rais Mgufuli amesema katika kutekeleza ilani ya uchaguzi ya ccm mwezi Januari mwakani serikali inasaini mkataba wa ujenzi wa meli mpya na Wakorea, katika ziwa victoria na kukarabati Meli ya MV Vctoria na Mv Butihama ili wananchi wananchi waondokane na tatizo la Meli.
Muonekano wa jengo la uwanja wa ndege
Moja ya ndege zinazotua uwanja wa ndege Bukoba.
Muonekano wa jengo la uwanja wa ndege
Moja ya ndege zinazotua uwanja wa ndege Bukoba.
Subscribe to:
Posts (Atom)