Wednesday, 12 July 2017

EVERTON IKIJINOA UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM TAYARI KUIVAA GOR MAHIA

EVERTON IKIJINOA UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM TAYARI KUIVAA GOR MAHIA

 Basi lililobeba wachezaji wa Timu ya Everton ya nchini Uingereza likiwasili katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazoezi leo.
 Baadhi ya viongozi wa wa Timu ya Everton ya nchini Uingereza wakishuka katika basi la timu hiyo mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazoezi leo.
  Mchezaji Wayne Rooney wa Timu ya Everton FC ya nchini Uingereza akielekea kufanya mazoezi na wenzie katika dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es Salam leo.
 Wachezaji wa Timu ya Everton FC ya nchini Uingereza wakiingia katika dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo.
 Wachezaji wa Timu ya Everton FC ya nchini Uingereza wakifanya mazoezi katika dinba la uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo.
 Wachezaji wa Timu ya Everton FC ya nchini Uingereza wakifanya mazoezi katika dinba la uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo.
 Wachezaji wa Timu ya Everton FC ya nchini Uingereza wakifanya mazoezi katika dinba la uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo.
 Wachezaji wa Timu ya Everton FC ya nchini Uingereza wakifanya mazoezi katika dinba la uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo.
 Wachezaji wa Timu ya Everton FC ya nchini Uingereza wakifanya mazoezi katika dinba la uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo.
 Makipa wa Timu ya Everton FC ya nchini Uingereza wakifanya mazoezi katika dinba la uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo.
 Mchezaji Wayne Rooney wa Timu ya Everton FC ya nchini Uingereza akifanya mazoezi na wenzie katika dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es Salam leo.
  Mchezaji Wayne Rooney wa Timu ya Everton FC ya nchini Uingereza akifanya mazoezi na wenzie katika dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es Salam leo.
 Wachezaji wa Timu ya Everton FC ya nchini Uingereza wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya mashabiki wa timu hiyo mara baada ya kumaliza mazoezi katika dinba la uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo.
 Wachezaji wa Timu ya Everton FC ya nchini Uingereza wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya mashabiki wa timu hiyo mara baada ya kumaliza mazoezi katika dinba la uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza jambo na Meneja wa Habari wa Timu ya Everton FC  wakati wa mazoezi ya timu hiyo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Yusuf Omar Singo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza jambo na Meneja wa Habari wa Timu ya Everton FC  wakati wa mazoezi ya timu hiyo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Yusuf Omar Singo.

WANANCHI WAIOMBA SERIKALI IONGEZE MUDA ZAIDI WA KULIPA KODI YA MAJENGO

WANANCHI WAIOMBA SERIKALI IONGEZE MUDA ZAIDI WA KULIPA KODI YA MAJENGO


Zikiwa zimebaki siku tatu kati ya siku 15 zilizoongezwa na Serikali kwa wananchi kulipa kodi ya majengo bila adhabu, baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wameiomba Serikali iongeze muda mwingine zaidi ili watu wote waweze kulipa kodi hiyo bila adhabu kutokana na changamoto mbalimbali zilizojitokeza wakati wa zoezi hilo.
Wananchi hao wamemweleza Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango alipofanya ziara za kushitukiza katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA-Mtaa wa Kipata-eneo la Mnazi Mmoja na Mbagala mkoani Dar es Salaam
Wamesema kuwa mwamko wa wananchi kulipa kodi ni mkubwa hali iliyosababisha foleni kubwa kila mahali nchini kutokana na uhaba wa watumishi wa TRA pamoja na vitendeakazi muhimu kama vile kompyuta na mashine za kielektroniki za kutolea risiti (EFDs).
Waziri wa Fedha na Mipango Dokta Philip Mpango amewataka Watanzania kuwa watulivu na kuendelea kulipa kodi hiyo huku akiahidi kutatua changamoto ya uhaba wa watumishi pamoja na vitendeakazi ili kuwaondolea adha wananchi waliojitokeza kwa moyo kulipa kodi mbalimbali ikiwemo ya majengo.
Ameahidi pia kwamba Serikali itayafanyiakazi maombi ya wananchi ya kutaka kuongezewa muda wa kulipa kodi hiyo na kwamba watajulishwa wakati muafaka  uamuzi wa Serikali kuhusu suala hilo.
Dokta Philip Mpango amesema kuwa Serikali inafarijika kwa kiasi kikubwa na namna wananchi walivyoitikia wito wa Mheshimiwa Rais Dokta John Pombe Joseph Magufuli unao wataka wananchi walipe kodi kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.
Amebainisha kuwa watu wanapolipa kodi wanaipa nguvu Serikali ya kuboresha huduma za jamii kwa wananchi ikiwemo elimu, barabara, maji, afya na kuboresha huduma ya umeme hususan vijijini na kulifanya Taifa kupunguza utegemezi wa misaada kutoka nje ya nchi.
Majuma mawili yaliyopita Serikali iliongeza muda kwa wananchi kulipa kodi ya majengo bila adhabu kwa muda wa majuma mawili hadi Julai 15 mwaka huu ambapo siku hizo zitaisha siku ya Jumamosi huku idadi kubwa ya watu ikiwa bado wanahitaji kulipa kodi hiyo.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akiongea na wananchi waliojitokeza kulipa kodi ya majengo katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)-Ilala Mtaa wa Kipata, na kuwapongeza kwa kuitikia wito huo kwa wingi na kuwaeleza kuwa kwa kulipa kodi kutasaidia upatikanaji wa huduma muhimu kama maji, barabara, umeme  na dawa hospitalini.
 Wananchi waliofika katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Ilala Mtaa wa Kipata, wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) akiwaelezea namna atakavyoboresha huduma kwa walipa kodi za majengo kwa kuwapa kipaumbele walemavu, wazee, wagonjwa na wasiojiweza. Tukio hili litaenda sambamba na kuwawekea sehemu maalumu ya kukaa wakati wakisubiri huduma.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto) akipokea shukrani na pongezi kutoka kwa Bi. Rose Muyalo, kwa utendaji makini wa Serikali ya Awamu ya Tano na kwa kupatiwa huduma bora kutoka kwa wafanyakazi wa TRA.
  Bw. Obedi Hezron Misoji (kulia) ambaye ni mstaafu akimuomba Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), kuongeza muda wa zoezi hili la ulipaji kodi ya majengo kwani watu bado ni wengi na Watanzania wameonesha nia yakujitokeza kwa wingi kulipia kodi hiyo.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) akiongea na wananchi waliofika katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Ilala Mtaa wa Kipata kulipa kodi za majengo na kuelezea furaha yake namna walivyoitikia wito huo.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), akiwasikiliza viongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Ilala Mtaa wa Kipata namna ambavyo wanaweza kukabiliana na changamoto wanazokabiliana nazo katika zoezi hili la ulipaji kodi wa Majengo.  Kutoka kulia ni Meneja Msaidizi Kanda ya Ilala kwa upande wa madeni Bw. Nuhu Ramadhani, Meneja wa Kanda ya Ilala Bw. Abdul Mapembe na Bw. Revelian Kajuna.

 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), akisalimiana na mmoja wa wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)- Mbagala, alipotembelea ofisi hizo kujionea namna zoezi la ulipaji kodi ya majengo unavyoendelea.

 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiwa katika moja ya ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)- Mbagala na kukutana na Mtoto Salma (aliyembeba) ambaye aliambatana na mama yake (hayuko pichani) kwenda ofisini hapo kulipa kodi ya majengo.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto) akiongea na baadhi ya wazee waliojitokeza kulipa kodi za majengo katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)- Mbagala jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto) akiwapongeza vijana waliojitokeza kulipa kodi ya majengo katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) - Mbagala jijini Dar es Salaam.

MASHABIKI WA MUZIKI NCHINI WAZISUBIRI KOLABO MATATA ZA COKE STUDIO KWA SHAUKU



Wakati uandaaji wa onyesho la muziki la Coca-Cola Coke Studio msimu wa tano unaendelea jijini Nairobi nchini Kenya linalojumisha kolabo za wanamuziki wa kitanzania kwa kushirikiana na wanamuziki wa nje, washabiki wa muziki nchini wamezisubiri kwa shauku kolabo hizo.
Burudani za onyesho hili ambalo limepata umaarufu mkubwa nchini kutokana na kufuatiliwa na wapenzi wengi wa muziki kupitia luninga litaanza kurushwa mapema mwezi Septemba na kwa upande wa Tanzania wasanii ambao wako ndani ya nyumba ni Rayvanny, Izzo Bizness na Nandy.
Katika onyesho la Coke Studio msimu mwa mwaka jana wakali wa muziki nchini ambao walishiriki walikuwa ni Ally Kiba,Vanessa Mdee,Ben Pol na Fid Q ambao walishirikiana na wanamuziki Wangechi, Maurice Kirya, Victoria Kimani na 2Face.
Katika msimu wa Coke Studio wasanii wanaoshiriki wanatokea katika nchi za Kenya,Afrika ya Kusini, Uganda, Tanzania, Rwanda, Ethiopia, Nigeria, Ghana, Angola, Zimbabwe, Togo, Cote d’Ivoire, Madagascar, Mauritius, Mozambique, DRC na Cameroon wakisindikizwa na mwanamuziki nguli wa kimataifa kutoka nchini Marekani Jason Derulo.
Mbali na wasanii kutoka Tanzania wakali wengine wa muziki kutoka nchi za Afrika wanaoshiriki msimu huu ni Khaligraph Jones na Band Becca (Kenya),Sami Dan (Ethiopia),Bebe Cool, Eddy Kenzo , Sheebah, Ykee Benda ( Uganda).
Wengine ni Nasty C, Busiswa, Mashayabhuqe kutoka Afrika ya Kusini, Youssoupha kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Runtown na Yemi kutoka Nigeria, Dji Tafinha kutoka Angola, Laura Beg kutoka Mauritius,Jah Prayzah na Slapdee kutoka Central Africa Republic,Bisa Kdei na Worlasi kutoka Ghana
Taarifa kutoka kampuni ya Coca-Cola ambayo iliyotolewa hivi karibuni imeeleza kuwa onyesho la Coke Studio ambalo umaarufu wake umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka msimu huu utakuwa na burudani za aina yake kutoka kolabo za wasanii nguli barani Afrika kuanzia Afrika Magharibi mpaka Afrika ya Kusini na litarushwa na vituo vya luninga kwenye nchi zaidi ya 30 barani Afrika na kuzidi kuifanya Afrika izungumze lugha moja tu ya muziki.
Imelielezea zaidi kuwa onyesho hilo kuwa lina lengo la kukusanya pamoja wasanii na kuonyesha uwezo na vipaji vya muziki vilivyopo Afrika ikiwemo kutoa fursa kwa wasanii chipukizi kufanya kazi na baadhi ya wasanii na watayarishaji wa muziki wa kimataifa,vilevile Kuwakusanya wasanii wanaofanya aina tofauti ya muziki, wanaotoka katika nchi tofauti za Kiafrika kuwawezesha kutengeneza sauti ya Afrika kupitia burudani ya muziki
Coca Cola Coke Studio pia inaleta burudani kubwa kwa washabiki wa muziki wa kiafrika na kuwaunganisha waafrika hususani vijana kupitia muziki.
Msanii Rayvanny (katikati) akiwa na wasanii wenzake wakifanya moja ya Mashup hivi karibuni

Mwanamuziki Izzo Business akiwa amepozi ndani ya studio jijini Nairobi

Baadhi ya wasanii nguli waliopo kwenye matayarisho ya Coke Studio msimu wa tano wakiwa katika picha ya pamoja jijini Nairobi hivi karibuni.

Tuesday, 11 July 2017

Ujumbe wa Tanzania washiriki Mkutano wa 36 wa SADC



Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Emmanuel Kolobelo unashiriki  Mkutano wa 36 wa Mawaziri wa Nishati na Maji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), nchini Swaziland.
Mkutano huo uliofunguliwa na Waziri Mkuu wa Swaziland, Dkt. Sibusiso Dlamin umehudhuriwa na nchi mbalimbali ikiwemo  Tanzania, Malawi, Zambia, Zimbabwe, Lesotho, Swaziland, Botswana, Msumbiji, Namibia, Seychelles, Botswana, Madagascar na Mauritius.
Mkutano huo umeanza tarehe 8 Julai, 2017 na utamalizika tarehe 11 Julai, 2017.
 Waziri Mkuu wa Swaziland, Dkt. Sibusiso Dlamin akifungua Mkutano wa 36 wa Mawaziri wa Nishati na Maji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika nchini Swaziland.
Ujumbe wa Tanzania unaoshiriki  mkutano wa 36 wa Mawaziri wa Nishati na Maji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), nchini Swaziland, kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji,

TCAA yapiga marufuku kununua, kurusha ‘drones’ bila kibali maalum

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imepiga marufuku urushwaji angani wa vifaa vya kieletroniki visivyo na rubani (drones) bila kupata kibali maalum.

Kupitia tangazo lake kwa umma, TCAA imesema kuwa kwa taasisi au mtu binafsi kufanya majaribio au kurusha drones, ni lazima apate idhini ya Wizara ya Ulinzi na Usalama pamoja na Mamlaka hiyo.

“Ifahamike kuwa kuanzia sasa, taasisi au mtu binafsi anayetaka kununua, kufanya majaribio au kurusha angani vifaa hivyo visivyotumia rubani anapaswa kupata idhidi ya Wizara ya Ulinzi na Usalama pamoja na kibali kutoka TCAA,” imeeleza taarifa ya Mamlaka hiyo.

Taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari imefafanua kuwa uendeshaji wa shughuli zote za anga nchini uko chini ya Mamlaka hiyo kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizopo.

Tangazo hilo linakuja wakati ambapo kumekuwa na urushwaji wa drones unaofanywa na watayarishaji wa video za muziki kwa lengo la kuchukua picha za juu, pamoja na taasisi mbalimbali zinazochukua matukio husika hasa yanapofanyika katika maeneo ya wazi.

Drones zilitumika zaidi katika uchaguzi wa mwaka 2015 ambapo mikutano ya kampeni za wanasiasa ilikuwa ikipigwa picha za juu kuonesha umati uliohudhuria.

Monday, 10 July 2017

HONGERA EVODIUS RUGEIYAMU NA AGNETHA EVODIUS KWA KUFUNGA PINGU ZA MAISHA.

 Maandiko matakatifu yanasema mwanamke utamuacha baba na mama yako utaambatana na mmeo, maandiko haya matakatifu Bi Agnetha ameyatimiza mapema wiki mbili zilizopita, baada ya kutamka bila chenga mbele ya waumini, ndugu, jamaa na marafiki waliojitokeza kushuudia ibada takatifu ya ndoa yake na Bw EVODIUS RUGEIYAMU katika kanisa katoliki la Cathedral Bukoba Mjini, na badae bonge la party katika ukumbi wa Bukoba club.
 Baba harus Bw Rugeiyamu akiwa kanisani.

 Wakila kiapo.
 Tarumbeta.
Hongereni sana maharusi.

KARIBUNI KWENYE MJUBURO(KITCHEN PARTY) YA JARIA EMIRY MNYONGE ,UKUMBI WA LINA'S 16-7-2017 JUMAPILI SAA TISA ALASILI.

 Hidaya Mnyonge, maarufu( mama Achi) anawakaribisha akina mama wote, wadada,wabibi kutoka maeneo yote ,siku ya tarehe 16-7-2017 Jumapili, kuanzia saa tisa alasiri kwenye ukumbi wa Lina's kwenye Mjuburo (Kitchen party) ya mtoto wake Jaria Mnyonge, , Mc kutoka jijini Mwanza aliebobea katika maswala ya mafundisho ya akina mama (Mama  Stivin)atatoa somo na kurudisha upendo na mapenzi katika mahusiano yako na mmeo, mpenzi nk, hii si yakukosa.Mama Achi anawakaribisha woteeeee.
Bi Jaria Mnyonge