Friday, 31 March 2017

MWILI WA MAREHEMU PATRICK PAULO NSHANGE WAPELEKWA KIJIJINI KWAKE KILIMILILE KYAKA KWA MAZISHI

 Ni majonzi na simanzi kubwa kwa familia ya marehemu Patrick Paulo Nshange ambae amefariki dunia tarehe 27-3-2017,KATIKA PICHA NI mwili wa marehemu ukiingia katika kanisa jipya  ambalo halijaisha Kilimilile Kyaka kwa ajili ya kutambua mchango mkubwa wa ufadhili wa ujenzi wa kanisa.
 Mwili wa marehemu ukitolewa Motuary katika hospita ya rufaa Kagera kuelekea kijijini Kilimilile Kyaka.
 Gari iliyobeba mwili kutoka katika moja ya kampuni nchini Uganda inayofanya shughuli za mazishi.
 Msafara kutoka Bukoba mjini kuelekea Kyaka Kilimilile.
 Mjane wa marehemu akilia kwa machungu  baada ya mwili kuwasili kijijini kilimilile kanisani kwa sara maalum.
 Bw Remigius akiwa na viongozi waandamizi wa TRA Kagera wa waliofika kumfariji kwa kufiwa na baba yake mzazi.
 Mjuu wa marehemu Fiti Remigius.
 Ni katika kanisa la Kilimilile ambalo halijaisha, lakini kwa kutambua ufadhili wa marehemu  imebidi  sala maalum ya kumuombea ifanyike hapo.
 Katikati ni Bw Remigius Partrick(Dk Remmy) mtoto wa marehemu Partrick Nshange.
 Katekisti akiendesha sara maalumu kanisani.
Mwenyekiti wa kamati ya mazishi Bw Medard Kaijage akitoa neno  kanisani.
 Mwili ukitolewa kanisani kuelekea nyumbani kwa marehemu
 Mwili ukitoka kanisani  ,Ni kanisa ambalo halijaanza kutumika, ila sara fupi ya kumuombea marehemu ilifanyika hapo kwa kutambua mchango wake mkubwa katika ufadhili.
 Wajukuu wakifanya tukio la kimila.
 Wajukuu wakifanya yao.
Kulia ni Mrs Remigius Nshange ( Dk Remmy) akiwa  na Bi Shubi wakijadili jambo.

Tuesday, 28 March 2017

WANABUKOBA MPYA WAIPONGEZA SHULE YA SEKONDARI KATA HAMUGEMBE ,YAFANYA VIZURI MITIHANI KIDATO CHA NNE MANISPAA YA BUKOBA

 Wana Bukoba mpya wamefurahishwa na matokeo ya kidato cha nne 2016 ya shule ya sekondari ya Hamugembe ambayo imekuwa ya kwanza katika Manispaa ya Bukoba,Mwenyekiti wa  umoja wa Bukoba mpya wakati akiongea na walimu na wanafunzi wa shule ya sekondari Hamugembe Bw Yunus Kabyemela amesema amewakilisha wanaBukoba mpya ambao wanaishi maeneo ,mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi wamefurahishwa na matokeo mazuri ya kidato cha nne 2016 ,na kwa kuzingatia changamoto nyingi zilizo kwenye shule za kata nchini lakini pamoja na changamoto hizo bado shule ya Hamugembe wamefanya vizuri, Bw Yunus Kabyemela aliendelea kusema Wana Bukoba mpya kwa kutambua umuhimu wa elimu wameona walimu wanastaili pongezi kubwa na kutiwa moyo kwa kazi kubwa wanayoifanya .Bw Yusus Kabyemela alikabidhi Tuzo kwa mwalimu mkuu wa Hamugembe sekondari Bw Evodius Rwezahura kama ishara ya kutambua na kuwapongeza kwa ushindi walioupata,pia wana Bukoba mpya walitoa bahasha kwa kila mwalimu wa shule hiyo iliyokuwa na chochote kwa kutambua kazi kubwa inayofanywa na walimu, Bw Yunus alisema kwa upande wa shule wanaBukoba mpya wametoa vitabu vya wanafunzi ambavyo watavitumia katika masomo yao, hafra hiyo fupi pia iliudhuliwa na mstahiki meya wa Manispaa ya Bukoba Mh Chief Kalumuna, makamu Meya Jimmy Karugendo ambae pia ni mwana Bukoba mpya, afisa elimu wa sekondari Manispaa ya Bukoba Bw Wandele Rwakatare, Diwani wa kata Hamugembe  Mh Muhaji Kachwamba,walimu na wanafunzi.(katika picha  mwenyekiti wa BUKOBA MPYA  Bw Yunus Kabyemela akikabidhi Tuzo kwa mstahiki meya,Pia kitaifa katika mitihani ya darasa la nne kitaifa, kidato cha pili kitaifa na kidato cha nne kitaifa Manispaa ya Bukoba imekuwa ya kwanza kitaifa 2016.
 Hii ndio Tuzo.
 Wana Bukoba mpya wakiwasili shuleni.
 Kushoto mwenyekiti wa Bukoba mpya Bw Yunus Kabyemela akiteta na mkuu wa shule.
 Makamu meya MH Jimmy Karugendo.
 Wanafunzi wa Hamugembe sekondari.
 Wimbo wa Tanzania nakupenda ukiimbwa.
 Kushoto Mh Diwani kata ya Hamugembe Muhaji Kachwamba ,afisa elimu sekondari Bw Wandele Rwakatare na makamu meya Jimmy Karugendo.
 Mstahiki Meya Mh Chief Kalumuna akitoa pongezi kwa wana Bukoba mpya kwa kutambua na kuthamini eli,mu na kuwashukuru kwa kitendo cha kiungwana walichokifanya.
 Mwenyekiti wa Bukoba mpya akiongea .
 TUZO
 Baadhi ya vitabu vilivyotolewa na wanaBukoba mpya.
 Mkuu wa shule akifurahi Tuzo na wanafunzi.
 Mwl Mkuuakipokea bahasha yake  ya motisha kwa kazi wanayoifanya .
 Walimu wakipokea bahasha yenye kitu kidogo kutoka kwa wanaBuboba mpya.
 Furaha tele, hapana chezea bahasha weweee.
 Mh diwani wa kata akitoa neno la shukrani.
PICHA YA PAMOJA.

Sunday, 26 March 2017

HUMPHREY POLEPOLE AFAFANUA KWA KINA MAGEUZI YA CCM

Mabadiliko

HUMPHREY POLEPOLE AFAFANUA KWA KINA MAGEUZI YA CCM

ya Katiba ya CCM 2017 yamegusa maeneo gani?
Hivi karibuni kumekuwapo maneno ya upotoshwaji juu ya Mabadiliko ya Katiba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) yaliyofanyika tarehe 12 Machi 2017. Napenda kufafanua kwa uchache maeneo ambayo yamefanyiwa Mabadiliko ili kuanzia sasa ieleweke bayana kwamba msingi wa Mabadiliko haya ni Mageuzi Makubwa ambayo yanafanywa na Chama chetu ili kuongeza tija, ufanisi, uwajibikaji, kupunguza gharama za uendeshaji, kupiga vita rushwa na ubadhirifu wa mali za umma.

Mageuzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) yanalenga kutizama Uongozi (Leadership), Muundo/Mfumo (Structure/System) na Utawala (administration). Chama chetu kimetimiza miaka 40 mwaka huu (2017) tangu kuanzishwa kwake na kipindi hiki tumeazimia kwa kauli moja kukiimarisha, kukijenga na kukifanya madhubuti. Kazi hii ya Mageuzi ya CCM ilianzishwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM iliyokaa katika Mkutano wake wa mwenzi Desemba 2016 na baadaye kupitishwa kwa sauti moja na Mkutano Mkuu Maalum wa Machi 2017.

Ikumbukwe kwamba mabadiliko haya ya Katiba yangaliweza kupendekezwa na kuanza kutumika pasina ya kuitisha Mkutano Mkuu, lakini hekima ya Uongozi wa Chama chini ya Mwenyekiti Ndugu Magufuli na Katibu Mkuu Ndugu Kinana ikatuongoza kwamba Mabadiliko haya ambayo yanajenga msingi wa Mageuzi ya Chama chetu lazima yashirikishe wanachama wetu.

CCM kama chama cha siasa ili kifanye kazi yake vizuri na yenye matokeo makubwa chanya, ilikusudiwa lazima kihuishwe ili kiweze kwenda na wakati na kutekeleza matakwa ya wanachama, kwa kuzingatia ukweli kuwa lengo kuu la chama chochote cha siasa ni kushika dola.

Mabadiliko ya Kikatiba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) yana lengo la kukiimarisha chama chetu ili kuziteka hisia, mioyo na fikra za watanzania wengi, kwa nia ya kukiunga mkono katika lengo lake la kushika dola na kuleta maendeleo endelevu kwa watanzania.

Katiba ya CCM imekuwa ikifanyiwa marekebisho mara kwa mara tangu ilipotungwa mwaka 1977, kwa madhumuni ya kuiboresha ili iendane na wakati uliopo. Kwasababu hiyo, yamekuwepo matoleo 12 ya Katiba hii hadi mwaka 2012. Katiba ambayo imepitishwa na Mkutano Mkuu Maalum tarehe 12 Machi 2017 jijini Dodoma, inakuwa toleo la 14.

Mabadiliko haya yanalenga kurekebisha Muundo, Mfumo, Uongozi, Utendaji na mengineyo.

Mambo muhimu ambayo yamezingatiwa katika marekebisho haya ni yafuatayo; -

MFUMO WA CHAMA
Mfumo wa Chama, una sura ya serikali na utawala na kuwa na ngazi nyingi ya vikao vya uamuzi. Hali hii inafanya gharama ya kukiendesha Chama kuwa kubwa, vikao haviitishwi na maamuzi ya chama hayawafikii walengwa. Hivyo basi yafuatayo yanazingatiwa,

Kupunguza wingi wa vikao vya nadharia na badala yake kuwa na vikao vichache vinavyofanyika, vyenye maamuzi yenye tija na kujenga uhai wa chama.

Kupunguza idadi ya wajumbe au wawakilishi ili wawe wachache lakini wenye umakini na uwezo wa kusimamia sera, itikadi, maamuzi ya chama pamoja na kuondoka urasimu na kupunguza gharama za uendeshaji pasina kuathiri ubora wa uwakilishi.

Muundo wa Wilaya za Chama uendane na uundo wa sasa wa wilaya za Serikali

Uztio mkubwa umewekwa katika kuimarisha chama katika ngazi ya shina, eneo ambalo ndilo waliko wapiga kura. Kwa kufanya hivyo, chama kitakuwa karibu na watu na watakiona kuwa ni chama chao.

Uendeshaji wa shughuli zote za jumuia za chama na mali zake uwe chini ya usimamizi wa Chama cha Mapinduzi na Baraza la Wadhamini la Chama cha Mapinduzi.

VIONGOZI

Viongozi wachache wamekuwa na tabia ya kujilimbikizia nafasi nyingi za Uongozi, utendaji na uwakilishi katika Chama na Serikali. Hali hii hushusha ufanisi na kupunguza tija. Nafasi nyingi kwa mtu mmoja ni kushindwa kuleta ufanisi katika vikao husika.

Hapa imezingatiwa kuwa; ukiacha wale wanaolazimishwa kikatiba kuwa na nafasi zaidi ya moja kwa mujibu wa mamlaka yao, kuanzia sasa nafasi za Uongozi katika chama zitakuwa si zaidi ya moja.

KURA YA MAONI
Mfumo wa kura za maoni hukusudia kuimarisha demokrasia ndani ya chama na kuashiria nafasi ya mgombea anayeonekana kukubalika zaidi. Hata hivyo, eneo hili limekuwa na matokeo mabaya ya kukithiri kwa rushwa na kupata viongozi wasio na imani ya kweli ya chama wanaosaka maslahi, wafanyabiashara wenye malengo binafsi na mamluki.
Mapendekezo ya kuimarisha udhibiti wa kura za maoni; -

Katiba ya CCM ya Mwaka 1977 Toleo la 2012 Ibara ya 61A(1-3) inaelekeza kura za maoni za ubunge na uwakilishi zitapigwa kwenye mikutano mikuu ya jimbo na si kwa wanachama wote matawini kama ilivyofanyika mwaka 2015.

Imependekezwa ili kudhibiti taratibu za kura za maoni jimboni, kuepusha migawanyiko, kuziba mianya ya rushwa na kuepusha wapiga kura mamluki, inapendekezwa kufanya mabadiliko ya upigaji kura za maoni za ubunge na uwakilishi pamoja na kufuata utaratibu ufuatao wa kuwajadili wanaogombea;

Wagombea ubunge/uwakilishi watachukua fomu na kurudisha kwa Katibu wa CCM wa Wilaya inayohusika. Fomu zote za wagombea ubunge/uwakilishi zitajadiliwa na kutolewa mapendekezo katika ngazi ya wilaya, mkoa na Taifa kabla ya kupigiwa kura za maoni.

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa itateua majina yasiyozidi matatu ambayo yatawasilishwa mbele ya Mkutano Mkuu wa Jimbo kwa ajili ya kupigiwa kura za maoni. Mkutano Mkuu wa Jimbo utapiga kura za maoni kumpendekeza mwanachama mmoja awe mgombea wa ubunge/uwakilishi katika jimbo hilo.

Mara ya baada ya kura za maoni, mapendekezo ya uteuzi yataanzia kwenye Kamati ya Siasa Jimbo (kwa Zanzibar), Kamati ya Siasa ya Wilaya (Tanzania Bara), Mkoa, Kamati Maalum (Kwa Zanzibar), Kamati Kuu na hatimaye Halmashauri Kuu ya Taifa itafanya uteuzi wa mwisho.

Utaratibu huu hautawapa fursa wagombea kutengeneza makundi na kutoa rushwa kwasababu hakuna anayejua kama atakuwepo kwenye orodha ya wagombea. Wale wana CCM wenye tabia ya kujiandaa na vyama zaidi ya kimoja, kwa utaratibu huu hawataweza kujiandaa mapema kuhamia vyama vingine. Utaratibu huu pia utasaidia kuondoa urasimu na migawanyiko isiyokuwa na sababu.

Aidha, utaratibu huu utahakikisha anapatikana mgombea mwenye msimamo thabiti wa Chama na ni utaratibu halisi kwa chama kuusimamia ipasavyo.