Thursday, 21 April 2016

EDINA KOKUMANYIKA AFANYIWA SEND OFF BUKOBA CLUB

 Ni Bi Edina Edmund kkatika ubora wake, ilikuwa ni sherehe ya kumuaga iliyofanyika katika ukumbi wa Bukoba club na kuudhuliwa na mamia ya wakazi mbalimbali wa Manispaa ya Bukoba na pande tofauti, Bi Edina anaetarajia kufunga pingu za maisha na kijana David Issaya 22-4-2016 ktk kanisa katoliki la cathedal Bukoba mjini.
 Mwenyekiti Bw Blandes akifungua sherehe.
 Bi Edina akiwa na bw David mme wake mtarajiwa.
 Wazazi wakipokea keki.
 Mkao...
 Macho.. ila ni mtu na mkewe.
 Baba akitoa neno.
 Wanabukoba group wakitoa neno kwa bi harusi mtarajiwa, mwanachama mwenzao, na zawadi pia.
 Mc Rutakwa katika ubora wake.
 Wanakamati.
 Wanakamati.
 Mwenyekiti wa kamati akikabidhi zawadi ya kamati kwa mtarajiwa.
 Bw Edmund akiwa na wapendwa wake.
 Baba mzaa chema akihojiwa na mc Bw Rutakwa.
 Ndugu watatu.
 Mc Baraka wa kwanza kulia akiwa na furaha akiwa na baba mzaa chema.

 Bw Edmund akiwa na mama mzaa chema.
 Mama Mary Kalikawe akiwa na mmewe.
Jamcobukoba.blogspot.com inawatakia maandalizi mema ya ndoa 22-4-2016.

Thursday, 14 April 2016

WAZIRI NAPE NNAUYE AWASILI MKOANI KAGERA LEO


Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akisalimiana na Viongozi mbalimbali kwenye Ofisi za Mkuu wa Mkoa leo

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye leo tarehe 14 April, 2016 akiwa mkoani Kagera ahaidi kuihamishia Wizara yake kwenye mikoa na Halmashauri za Wilaya kwa wadau wanaohusika ili kurasmisha shughuli na majukumu ya wizara hiyo ili iweze kupata ufanisi.

Akiongea na wadau mbalimbali wanaohusika na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo alisema kuwa lengo la ziara yake ni kuja mikoani kujionea changamoto mbalimbali za wizara yake ili aweze kuzifanyia kazi kwa kuishusha wizara kwa wadau wanaohusika ili kutekeleza majukumu yake.

Katika kikao hicho Waziri Nape alisema kuwa sekta nne ambazo ni Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo zimekuwa hazifanyi kazi zake vizuri kutokana na watendaji wake kutokuwa na idara au vitengo vinavyohusika moja kwa moja na kazi zao jambao ambalo linawafanya kujishikiza katika sehemu au idara nyingine.

Waziri Nape akisaini kitabu kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Picha na Faustine Ruta, Bukoba
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Jackson Msome(kushoto) ambaye alikaimu nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera leo akitoa neno.


Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akisikilizwa kwa makini na Wadau wa Maendeleo hapa Bukoba, Picha na Faustine Ruta, Bukoba
Ndugu Willy Bukobatours Rutta,Diwani kata ya Ishozi nae alikuwepo
Kulia ni Bw. Gonzaga Meneja wa Jambo Bukoba Mkoani Kagera
Wakifuatilia jambo kwa karibu
Kaimu wa RAS Bw. Adam Swai akitoa neno
Taswira kamili

Sekta ya Habari
Mhe, Nape aliagiza Halmashauri za Wilaya kuajiri Maafisa Habari katika Halmashauri ambazo hazina Maafisa hao, pili kuwaruhusu Maafisa hao kuingia kwenye vikao vyote vya maamuzi ili kuweza kuzisemea taasisi hizo. Na kutenga bajeti kwa Maafisa habari hao ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ukamilifu.

Kuhusu changamoto ya vitendea kazi Mhe. Nape alisema kuwa Wizara yake imeanza kuwajibika kwa kuto IPad za kisasa kwa Maafisa Habari waliopo Mikoani na katika Halmashauri za Wilaya ili ziweze kuwasaidia kutekeleza majukumu yao kwa ufasaha, kwa mkoa wa Kagera alitoa Ipad tano kwa Maafisa habari.


Aidha, Mhe. Nape aliwahakikishia Waandishi wa Habari kuwa maslahi yao yataboreshwa chini ya usimamizi wake kama Waziri mwenye dhamana ambapo alisema kuwa Serikali ipo kwenye mchakato wa kukamilisha Mswada wa huduma kwa vyombo vya habari ambao utazingatia mahitaji na maslahi ya waandishi wa habari.

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye kwa makini akisikiliza Hoja.
Mkurugenzi wa Radio Kasibante FM 88.5 ya Mjini Bukoba Richard Leo akitoa Mada
(Kushoto) ni Mkurugenzi wa Radio Vision FM Ngd. Valelian na kulia ni Mr. Teso Boy Msanii wa hapa Mjini Bukoba, Picha na Faustine Ruta, Bukoba
Mkurugenzi wa Kiroyera tours Bi Mary Kalikawe akisikiliza kwa makini.
Chief Kalumuna(kushoto) Mea wa Mji wa Bukoba akitolea ufafanzi Jambo mbele ya Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akitoa iPad kwa ajili ya Maafisa habari


Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akitolea ufafanuzi jambo

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye na Viongozi wengine walipata nafasi wakatembelea Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba kuona unavyoendelea.

Waziri akipata ufafanuzi wa Umaliziaji wa Uwanja wa Kaitaba kupitia simu ya Mkononi wakati alipotembelea Uwanja huo. Picha na Faustine Ruta, Bukoba

Sekta ya Michezo
Katika sekta ya Michezo Mhe, Nape aliwakumbusha Makatibu Tawala wa Mikoa wao kama Wenyeviti wa kamati za michezo za mikoa kutembelea na kukaa na viongozi wa vyama vya michezo kuwakumbusha majukumu yao na kupitia mara kwa mara mipango kazi yao ya kazi aidha, kusimamia upatikanaji wa viongozi wenye wajibu katika michezo na siyo vibarua wa kuingia kuwatumikia baadhi ya watu Fulani.

Aidha, alimuagiza Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba na Wenyeviti wa Halmashauri kuhakikisha wanasimamia urudishwaji wa viwanja vilivyoporwa na kutopitisha ramani za mipango miji zisizozingatia utengwaji wa maeneo ya wazi ya michhezo.

Sanaa
Mhe. Nape alisema kuwa Serikali inakusudia kuirasmisha sanaa kuwa shughuli za uchumi badala ya kuwa shughuli za burudani tu kwasababu kwasasa sanaa inaonekana kuwa ni kuburudisha tu wakati imekuwa ikitoa ajira kwa vijana wengi. Aidha, Serikali inakusudia kuwasimamia wasanii kuondokana na matapeli wanaonufaika kupitia kazi zao nao kubaki hoi hae.

Katika Sekta ya Utamaduni Mhe, Nape alisema Serikali inakusudia kutumia utamaduni kama nyenzo ya utalii katika taifa la Tanzania
Ili kutatua changamoto zinazoikabili Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo zilizopo katika mikoa na Halmashauri za Wilaya Mhe. Nape alisema Wizara yake imeanza kufanya mazungumzo na Ofisi ya Rais TAMISEMi ili kuanzisha vitengo au idara katika Mikoa na Halmashauri za Wilaya.

Baada ya kuongera na wadau Mhe. Nape alitembelea Uwanja wa Kaitaba na kujionea maendeleo ya ukarabati wa uwanja huo ambapo amewahakikishia wadau wa michezo wa Mkoa wa Kagera kuwa atahakikisha anamsukuma mkandarasi ili akamilishe uwanja huo mapema iwezekanavyo.

Sehemu ya Uwanja wa Kaitaba ambao unaendelea kujengwa ambapo Waziri Nape amegusia pia kuhusu umaliziaji wa Uwanja huo na kutolea ufafanuzi wa Vifaa ambavyo vilikuwa vimekwamia bandarini na sasa vipo njiani tayari kwa umaliziaji wa Uwanja huo.

Thursday, 7 April 2016

RAIS DKT. MAGUFULI ASHIRIKI SHUGHULI ZA KUMBUKUMBU YA MAUAJI YA KIMBARI (KWIBUKA) KIGALI NCHINI RWANDA




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli wameungana na wananchi wa Rwanda kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 22 ya tangu kutokea kwa mauaji ya kimbari yaliyosababisha vifo vya watu takribani milioni 1.

Maadhimisho hayo yamefanyika katika eneo la Gisozi Mjini Kigali, yalipo makumbusho ya mauaji ya Kimbari ambapo Rais Magufuli na Mkewe wakiwa na mwenyeji wao Rais Paul Kagame wa Rwanda na Mkewe Mama Janeth Kagame wameweka shada la mauaji katika eneo walipouawa idadi kubwa ya wananchi wa Rwanda na pia wakawasha mwenge wa matumaini kwa walionusurika katika mauaji hayo na kwa Taifa zima la Rwanda.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakisali mbele ya makaburi ya watu waliouwawa katika Mauaji ya Kimbari nchini Rwanda mwaka 1994. Kulia ni Rais wa Rwanda Paul Kagame pamoja na Mkewe Janeth Kagame na mtoto.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame wakiwasha mwenge wa matumaini kuashiria kutotokea tena kwa mauaji ya Kimbari nchini Rwanda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame, mama Janeth Magufuli, Mama Janeth Kagame wakisikiliza historia ya jinsi mauaji ya kimbari yalivyotokea katika eneo la kumbukumbu ya mauji hayo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame, mama Janeth Magufuli, Mama Janeth Kagame wakiwa wamesimama kutoa heshima kwa watu waliofariki katika mauaji hayo ya kimbari.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiangalia kwa uchungu mafuvu ya watu waliopoteza maisha katika mauaji hayo ya kimbari.
............................................................
Pamoja na kupata historia ya mauaji hayo ya kimbari, Rais Magufuli akiongozwa na mwenyeji wake Rais Kagame ametembelea jumba maalum lililohifadhi kumbukumbu ya watu waliopoteza maisha, ambapo amepata maelezo kutoka kwa wahifadhi wa makumbusho hiyo, na pia kujioonea picha na mabaki ya mifupa na mafuvu ya binadamu waliouawa.

Akizungumza mara baada ya kutembelea jumba hilo la makumbusho Rais Magufuli ameelezea kusikitishwa kwake na mauaji hayo na kusema tukio hilo halipaswi kurudia.

"Haitatokea tena, hatuwezi kubadilisha yaliyopita lakini tunaweza kubadilisha mambo ya sasa na yajayo, mauaji haya hayapaswi kutokea tena" Amesema Rais Magufuli. 

Wageni mbalimbali waliofika kwenye kumbukumbu hizo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia picha za watoto waliouwawa kinyama katika eneo la Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbari  Gishozi Kigali nchini Rwanda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitabu katika Jengo la makumbusho ya mauaji ya Kimbari Gishozi Kigali nchini Rwanda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea kitabu chenye maelezo mbalimbali kuhusu mauaji hayo ya kimbari.
Rais wa Rwanda Paul Kagame akimpokea Rais Magufuli katika viwanja vya Gishozi kabla ya kwenda kuweka mashada ya maua kwenye makaburi ya watu waliouwawa katika mauaji ya Kimbari.
Rais wa Rwanda Paul Kagame akiwa na Rais Magufuli pamoja na Mama Janeth Magufuli, Janeth Kagame wakielekea kwenye makaburi ya halaiki katika makumbusho ya mauaji ya Kimbari, Gishozi Kigali nchini Rwanda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakisali mbele ya makaburi ya watu waliouwawa katika Mauaji ya Kimbari nchini Rwanda mwaka 1994. 

Rais Magufuli ambaye aliingia nchini Rwanda jana tarehe 06 April, 2016 ikiwa ni ziara yake ya kwanza nje ya nchi tangu aingie Madarakani Tarehe 05 Novemba, 2015 ameondoka Mjini Kigali jioni hii na kurejea Jijini Dar es salaam.