Sunday, 13 March 2016

WAZIRI MKUU ATEMBELEA MRADI WA MAJI BUWASA,WANANCHI WA KIFUNGWA KAHORORO KULIPWA FIDIA.

 Waziri mkuu Kassim Majaliwa ametembelea mradi mkubwa wa kusambaza maji katika manispaa ya Bukoba unaogharimu zaidi ya bilioni 30,mradi huu unaotarajiwa kukamilika mapema mwezi wa nne mwaka huu,pia waziri mkuu ameahidi kushughulikia kwa haraka madai ya wananchi wa Kifung wa kata ya Kahororo zaidi ya bilioni moja,wanayoidai Buwasa kwa ajia fidia ya maeneo yao.
Kushoto mkurugenzi wa Buwasa mhandisi Chagaka akiteta  jambo na waziri mkuu.

KASSIM MAJALIWA AWASILI BUKOBA,AWATAKA MAAFISA WA UHAMIAJI KUACHA MCHEZO MCHAFU.

 Mh Mkuu mkuu wa mkoa wa Kagera(Ambae kaamishiwa mkoa wa Mwanza) akimkaribisha waziri mkuu 
 Kassimu Majaliwa katika uwanja wa ndege wa Bukoba.Mbali na mambo mengi aliyoongelea amewataka maafisa uhamiaji kuacha mchezo mchafu wa kutoa vibari vya waamiaji haramu, na hasa kwenye ranch za Missenye na zingine  na kusababisha hatari ya usalama wa mipaka ya nchi yetu.

 Viongozi mbalimbali wakiwa uwanja wa ndege.
 Viongozi wa dini wakiwa uwanjani.
 Naibu waziri wa mambo ya ndani Mh Masaun  akisalimiana na maafisa wa magereza.
 Mh Mbunge wa jimbo la Nkenge balozi Dr Diodorus Kamala  akisalimiana na waziri mkuu.
 Waziri mkuu Kassim Majaliwa akizungumza jambo na meneja wa mfuko wa pensheni  wa PPF kanda ya ziwa  Meshach Bandawe alipowasili uwanja wa ndege  mjini Bukoba kwa ziara ya kikazi.
 Kikundi cha kakau bendi kikitumbuiza.
 Wananchi wakiwa uwanja wa ndege kwa nje kumpokea waziri mkuu.
 Mwenye miwani Bw Said Mtanda, mshauri wa waziri mkuu.
 Kushoto ni mwandisi wa maji Kijigo,Dk Mugula na  DAS BiharamuBi Agnes.
viongozi mbalimbali.
 Mwenye shati nyekundu mstahiki meya wa manispaa ya Bukoba Chief Kalumuna akirifa ya mkoa.. taamsikiliza mkuu wa mkoa akitoa
 Viongozi wa kidini wakiwa Ikulu ndogo Bukoba.
mkuu wa mkoa wa Kagera John Mongella (Ameamishiwa mkoa wa Mwanza)akisoma taaarifa ya mkoa.

Friday, 11 March 2016

KASSIMU MAJALIWA KUTUA BUKOBA JUMAPILI 13-3-2016,MONGELA AKUTANA NA WAANDISHI.ABADILISHA RATIBA GHAFLA KWA MANISPAA YA BUKOBA


 Waziri mkuu Kassimu Majaliwa anategemea kuwasili siku ya jumapili katika uwanja wa ndege wa Bukoba na kuanza ziara ya siku  tatu, Mkuu wa mkoa kagera John Mongella akiongea na waandishi wa habari alisema Mh waziri mkuu mara baada ya kuwasili atakwenda kufungua kiwada cha maji Bunena, na siku ya Jumanne kuelekea wilaya ya Missenye kutembelea Lanchi  ambazo zimekuwa kwenye mgogoro wa muda mrefu sasa, na baada ya hapo ataelekea wilaya ya Ngara,Mara baada ya taarifa hiyo,badae jioni ratiba ikabadilika ,na kutolewa maelezo mapya, mh waziri mkuu atatembelea kujionea maendeleo ya mradi wa maji  mkubwa unaoendelea kujengwa,baada ya hapo ataongea na watumishi wa manispaa ya Bukoba na Wilaya ya Bukoba kwenye ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa Kagera,na baada ya hapo atakwenda kwenye mkutano wa hadhara uwanja wa uhuru platform kuzungumza na wananchi.
 Aliesimaa ni Afisa habari ofisi ya mkuu wa Mkoa Bw Silvester akimkaribisha mkuu wa mkoa kuzungumza na waandishi.
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera  John Mongera akizungumza na waandishi.
 Msaidzi wa mkuu wa mkoa.