Sunday, 31 January 2016

NAIBU WAZIRI WA AFYA AZINDUA DUKA LA DAWA LA MSD JIJINI ARUSHA


Msimamizi wa Duka la MSD Arusha Twaha Kabandika akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Kigwangalla wa namna mfumo unaotumika kwa mauzo unavyofanya kazi.Kulia ni M/Kiti wa Bodi MSD, Prof Idris Mtulia, Mkurugenzi wa MSD Laurean Bwanakunu (Kushoto0 na Mkuu wa Wilaya ya Arusha mjini Fadhili Nkuru.
Naibu Waziri wa Afya akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Prof. Idris Mtulia alipowasili duka la MSD Mount Meru, Arusha kwa ajili ya kulizindua rasmi jana. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Laurean Bwanakunu, akifuatiwa na Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda na Huduma kwa Wateja Bw. Cosmas Mwaifwani.




MAJANGILI YAUA RUBANI BAADA YA KUTUNGUA KWA RISASI NDEGE YA TANAPA



RUBANI wa helikopta ya Doria ya Mamlaka ya Wanyamapori Nchini, (TANAPA), Roger Gower raia wa Uingereza ameuawa baada ya kupigwa risasi akiwa angani na watu wanaosadikiwa kuwa majangili kwenye pori la akiba maswa lililoko wilaya ya Meatu mkoani Simiyu majira ya jioni Januari 30, 2016.
Kamanda wa Upelelezi wa Mkoa wa Simiyu, Jonathan Shana ambaye alikuwa kwenye eneo la tukio, amesema, askari mmoja wa wanyamapori aliyekuwemo ndani ya helikopta hiyo amejeruhiwa.
“Helikopta hiyo haikudunguliwa, bali risasi ilimpata Rubani na hivyo akauawa na helikopta kupoteza mwelekeo na kuanguka.” Alifafanua Kamanda wa Upelelezi Mkoa wa Simiyu, Jonathan.
“Tutawasaka pori kwa pori, pango kwa pango, kijiji kwa kijiji hadi tuwatie mbaroni wahalifu hao. Tumeleta FFU wenye silaha za nkutosha, ili kutekeleza amri ya kamanda IGP, Kamanda DCI na RPC, ndio maana tuko hapa na silaha nzito.” Alisema Mkuu huyo wa upelelezi wa Mkoa wa Simiyu.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Allan Kijazi, walifika eneo la tukio na kushngazwa na tukio hilo ambapo waziri alisema, sasa wahalifu hawa wamefikia kiwango cha juu cha uhalifu hadi kuhujumu teknolojia ya kuhifadhi mazingira, kwa kuwashambulia watendaji wetu, Waziri alisema kwa huzuni na kuongeza kuwa Serikali haitavumilia uhalifu huo na kuahidi kuwasaka popote walipo.
Hili ni tukio la kwanza kwa majangili kutungua kushambulia helikiopta ikiwa angani na kusababisha kifo.
 Waziri Profesa Maghembe, akizungumza baada ya kufika kwenye eneo la tukio. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Allan Kijazi
 Waziri akionyeshwa sehemu risasi ilipopenya kwenye helikopta hiyo
Askari na maafisa wa serikali wakionyeshana sehemu helikopta hiyo ilipopigwa risasi na kuanguka baada ya rubani kuuawa

Friday, 29 January 2016

NYUMBA INAUZWA,IKO KASHAI KASHENYE BUKOBA.

 Nyumba nzuri yenye vyumba vitatu vya kulala na kimoja wapo ni master bedroom,ina sebule kubwa ya kisasa, sehemu ya kulia chakula kubwa na ya kisasa, Jiko, store,public toilet, Bafu ,imeungana na nyumba ya nyuma ambayo unaweza kufanyia matumizi kadri utakavyoamua na uwanja mkubwa kwa ajili ya kuanika nguo au matumizi mengine, Nyumba hii Land; Plot no 159, blok 'AA' Kashai Kashenye Bukoba mjelezoini, Certificate of tittle;9930 Nyumba unaweza kuifanya kwa matumizi yoyote utakavyohitaji iko eneo zuri barabarani  kwa maelezo zaidi wasiliana kwa namba  0713-481813.

 Nyumba iko imara.
 sehemu ya pembeni imeungana na nyumba ya nyuma.
 Hii ni nyumba ya nyuma.
 Sehemu ya mbele ya kuingia ndani.
Kwa mawasiliano zaidi piga no 0713-481813.

DK. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA BALOZI WA UFARANSA, MAKAO MAKUU YA CCM, DAR ES SALAAM

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, anayeshughulika na Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) Ndugu Asha-Rose Migiro, akimkaribisha Balozi wa Ufaransa  Nchini Tanzania, Malika Berak, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam, leo
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, anayeshughulika na Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) Ndugu Asha-Rose Migiro, akizungumza na Balozi wa Ufaransa  Nchini Tanzania, Malika Berak, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam, leo
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, anayeshughulika na Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) Ndugu Asha-Rose Migiro, akizungumza na Balozi wa Ufaransa  Nchini Tanzania, Malika Berak, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam, leo
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, anayeshughulika na Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) Ndugu Asha-Rose Migiro, akizungumza na Balozi wa Ufaransa  Nchini Tanzania, Malika Berak, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam, leo
Balozi akisaini kitabu cha wageni
Balozi akisaini kitabu wa wageni
Mazungumzo yakiendelea
Balozi huyo akimsalimia Ofisa wa Chama katika Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Gift Msuya
Balozi huyo akimsalimia Ofisa wa Chama katika Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Salehe Mhando
Wakijiweka sawa kwaajili ya kuendelea na mazungumzo
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, anayeshughulika na Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) Ndugu Asha-Rose Migiro, akizungumza na Balozi wa Ufaransa  Nchini Tanzania, Malika Berak, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam.

Tuesday, 19 January 2016

MSIBA NYUMBANI KWA MAREHEMU GEORGE SEBO BOWIE, MARYLAND NCHINI MAREKANI


Kushoto ni Abdul Sebo  mtoto wa marehemu akipewa pole na moja ya ndugu, jamaa na marafiki waliofika nyumbani kwa marehemu Bowie kutoa pole na rambi rambi zao kwa wafiwa kutokana na kifo cha mpendwa wao Mzee George Sebo kilichotokea siku ya Jumatatu asubuhi January 18, 2016 katika Hospitali ya Prince George iliyopo Maryland nchini Marekani. Utaratibu na mipango tutajulishwa leo kwa sasa imetengenezwa GOFUNDME ambayo ni www.gofundme.com/8fjvpcns

 Kati ni mke wa marehemu Aunty Grace akipewa pole na moja ya ndugu, jamaa na marafiki waliofika nyumbani kwa marehemu kujumika nao na kuwafariji katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao mzee wetu George Sebo
 Mmoja ya wanaDMV wakijumuika pamoja na kwa kutoa pole na kuwafariji wafiwa katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao. Kushoto ni Salma Moshi.
 WanaDMV na wanafamilia wakijumuika na kuwafariji wafiwa nyumbani kwao Bowie, Maryland nchini Marekani na kutoa pole na rambi rambi zao . Kutoka kushoto ni Sharif, Tuma, Salma, Justa, Aunty Grace na Iska wakiwa na mke wa marehemu Aunty Grace kumpa pole kwenye msiba wa kuondokewa na kipenzi mume wake Mzee George Sebo.
Wana DMV wakijumuika na wanafamilia nyumbani kwa marehemu Bowie, Maryland.