Wednesday, 18 November 2015

NI MWAKA MMOJA LEO TANGU MAREHEMU LEONARD MTENSA AFARIKI,ANGALI BAADHI YA MATUKIO KATIKA MAZISHI YAKE

 Nakumbuka ilikuwa ni mstuko mkubwa katika kila kona ya Manispaa ya Bukoba na maeneo mengine pale mtu alipopata taarifa za msiba wa Mtensa,watu wengi walionekana kutoamini taarifa hiyo kwani wapo waliokuwa na marehemu masaa machache kabla ya kifo akiwa mzima, wapo wa siku moja nk,lakini yote hayo ni maneno tu ya mwanadamu kwani tarehe ikifika hakuna kizuizi,Mtensa leo ni mwaka sasa hatuko nawe tunakukumbuka kwa mahusiano yako mazuri katika jamii kwa ujumla,Unakumbukwa na familia yako,ndugu , jamaa na marafiki, Kipekee umoja wako wa Pamoja group unakukumbuka sana,tunaamini kimwili hatuko wote bali kiroho tuko pamoja, Pumzika kwa amani Leornard Mtensa Mkurugenzi wa Lina's.Siku ya jumamosi tarehe 21-11-2015 itakuwepo misa ya kumkumbuka nyumbani kwake Kyakairabwa aliko zikwa.





 Mr Ernest Nyambo akiweka shada la maua.
 Rafiki kipenzi wa marehemu Mr Bube.
 Wafanyakazi wote wa Lina's wakimuaga bosi wao.



Hakika wanapamoja kama vile hawaamini kile killichokuwa kinafanyika.

Sunday, 15 November 2015

WAHITIMU DARASA LA SABA NA KIDATO CHA NNE WAAGWA KEMEBOS,MONGELLA MGENI RASMI.

 Mahafari ya tano ya darasa la saba na mahafari ya tatu ya kidato cha nne yamefanyika katika shule ya Kemebos yenye Chekechea,Shule ya msingi, sekondari na kidato cha tano na sita na mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera John Mongella,Akiongea na hadhara iliyohudhuria Mh Mongella amesema Kemebos ni shule iliyopiga hatua kubwa kitaaluma na imeiletea sifa kubwa  Mkoa wa Kagera kwa kuongoza Kitaifa mitihani.(Katika picha kushoto ni Meneja wa shule Bw Katiti, Mkurugenzi wa shule Bw Kareju, Mkuu wa Mkoa John Mongela, Diwani Kata Ijuganyondo Almasoud Kalumuna(Kamala) na Mjumbe wa bodi.


 Baadhi ya wahitimu darasa la saba.
 Wahitimu kidato cha nne.
 Mh Diwani Kamala akisalikmiana na wahitimu.
 Mgeni rasmi Kushoto akiwasili.
 Mgeni rasmi akipata maelezo kwenye moja ya chuma maalumu kwa ajili ya masomo ya Jografia.
Maabara ya kisasa.
 Wanafunzi katika ukakamavu.
 Keki kwa ajili ya wahitimu na waalikwa.