Wednesday, 9 September 2015

MKAPA ASEMA USHINDI KWA CCM NI LAZIMA,NI KATIKA UFUNGUZI WA KAMPENI JIMBO LA BUKOBA MJINI.

 Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin William Mkapa akiwa kwenye mkutano wa kampeni ya uzinduzi Mkoa wa Kagera akimkabidhi Irani ya uchaguzi ya ccm 2015-2020 mgombea ubunge jimbo la Muleba Kaskazini Charles Mwijage kwa niaba ya wagombea ubunge wote Mkoa wa kagera,Mh Mkapa amesema ushindi wa ccm ni lazima kwa sababu imefanya mengi na kuleta maendelea katika Taifa la Tanzania.
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera John Mongella akiwa na katibu wa ccm mkoa Kagera wakiteta kwenye uwanja wa ndege Bukoba.
 Mzee Mkapa akiwasili uwanja wa ndege.
 Mzee Mkapa akisalimiana na Balozi Kagasheki.
M
 Mzee Mkapa akisalimiana na mh Mwijage.
 Mh Kagasheki akisalimiana na mh Karamagi.


 Mzee Mkapa akiingia uwanja wa uhuru plat form
 Balozi Diodorus Kamala mgombea ubunge jimbo la Nkenge.
 Mgombea jimbo la Karagwe kayanga.
 Mgombea jimbo la Kyerwa



Tuesday, 8 September 2015

MWILI WA MAREHEMU JOSEPH MSHUMBUSI WAWASILI DAR,KUZIKWA NYUMBANI KWAKE BUKOBA KANAZI 11-9-2015 IJUMAA.

 Mwili wa marehemu Joseph Mshumbusi umewasili Dar jana usiku tarehe 9-10-2015 Jumatano majira ya saa tatu usiku kutokea Dubai ambako mauti yalimkuta akiwa safarini akitokea Hong kong China,Marehemu Mshumbusi ataagwa na ndugu na jamaa wa Dar leo kuanzia saa saba mchana katika kanisa la Last Mt.akw Martha Mikocheni,Baada ya misa mwili utapelekwa kulala uwanja wa kimataifa Dar na siku ya Alhamisi saa tatu asubuhi mwili utapelekwa Bukoba kwa ndege ya kukodi,Kwa mujibu wa msemaji wa mipango ya mazishi ndugu Protas Ishengoma amesema marehemu Mshumbusi atazikwa siku ya Ijumaa nyumbani kwake kijiji cha Rulongo Kanazi kwa kutanguliwa na Ibada ya mazishi itakayoanza saa saba mchana,Marehemu katika uhai wake amekuwa karibu sana katika shughuli za kidini na hasa kanisa katoriki, hivyo inatarajiwa maaskofu, mapadre, waumini, na jamii kwa ujumla kujitokeza kwa wingi sana kumzika.
Marehemu Mshumbusi katika uhai wake akiwa na mkewe, Pumzika kwa amani Mzee Mshumbusi, mtu wa watu.utakumbukwa daima kwa upendo wako, utani wako, ucheshi wako, ukarimu wako katika jamii.

Sunday, 6 September 2015

RAIS MSTAAFU MZEE BENJAMIN MKAPA KUZINDUA KAMPENI ZA CCM KATIKA JIMBO LA BUKOBA MJINI 8-9-2015 UHURU PLATFORM

 Rais mstaafu wa awamu ya  tatu mzee Benjamini William Mkapa atazindua kampeni za Ccm Kimkoa katika jimbo la Bukoba Mjini siku ya jumanne 8-9-2015 majira ya saa tisa alasiri katika uwanja wa mashujaa Uhuru platform.Mh Mkapa pia atazindua kampeni rasmi za jimbo la Bukoba mjini kwa kumnadi mgombea Ubunge Balozi Khamis Sued Kagasheki na wagombea wa majimbo mengine manane katika Mkoa wa Kagera.
 Kushoto ni Balozi Kagasheki akiwa na  mgombea urais Pombe John Magufuli.
 Mgombea Ubunge Jimbo la Muleba Kusini Prof Anna Tibaijuka
Wananchi wote mnaobwa kujitokeza kwa wingi.

MAGUFULI AITEKA MOROGORO MKUTANO WAKE WAWEKA HISTORIA MOROGORO


 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa Jamhuri tayari kuhutubia wakazi wa Morogoro mjini kwenye mkutano wa kampeni za CCM.
 Wananchi wakimkaribisha Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
 Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wakifurahia ujio wa mgombea wa Urais wa CCM Dk.John Pombe Magufuli.
 Mwenyekiti wa CCM ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa CCM Ndugu Innocent Kalogeresi na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Alhaji Abdalla Bulembo kwenye mkutano wa kampeni za CCM  uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri.
 Mwenyekiti wa CCM ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa CCM Ndugu Innocent Kalogeresi na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Alhaji Abdalla Bulembo kwenye mkutano wa kampeni za CCM  uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri.
 Wananchi wakiwafurahia wasanii wa Tanzania wanaounda umoja unaofahamika kama Mama Ongea na Mwanao.

 Mzee Yusuph Makamba akisalimiana na Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa Jamhuri, kulia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.
 Wananchi wakiwa wamefurika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kwenye mkutano wa Kampeni
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Alhaji Abdallah Bulembo akiwahutubia wakazi wa Morogoro mjini kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa Mgombea wa CCM amejitosheleza kuongoza nchi yetu.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakazi wa Morogoro mjini ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa mchakato wa kumpata Mgombea wa Urais ulikuwa wa haki na kila mjumbe alipiga kura.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakazi wa Morogoro mjini ambapo aliwaambia wananchi hao hana mashaka na mgombea urais wa CCM na kuwataka wananchi  hao kumpigia kura siku ya oktoba 25.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akipanda ngazi za jukwaa kwa kukimbia mbio tayari kwa kuhutubia wakazi wa Morogoro mjini.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Morogoro mjini kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri.

 Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika uwanja wa Jahmuri.
 Mzee Yusuph Makamba akipanda ngazi za jukwaa tayari kuhutubia wakazi wa mji wa Morogoro.
 Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Yusuph Makamba akizungumza na wananchi wa mkoa wa Morogoro wakati wa mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea wa urais kupitia chama hicho Dk. John Pombe Magufuli uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
 Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Yusuph Makamba akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea wa urais kupitia chama hicho Dk. John Pombe Magufuli uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro