Saturday, 8 August 2015

ILIKUWA NI SHANGWE BW HUSEIN THALHA NA BI HAMIDA,BW SHARIFU KACHWAMBA NA BI FATMA TWALHA KUFUNGA NDOA

Kushoto ni Bw Husein Twalha na mkewe Hamida Munisi wakiwa na katika picha ya pamoja na maharusi wenzao Bw Sharif Kachwamba na Bi  Fatma Twalha..
kulia ni Shekhe wa Mkoa wa Kagera Haruna kichwabuta.
Bw optat Katibu.
Mc Saad Katoma akiwajibika.
Mulid ikisomwa.
Bw Husein Twalha akiwa na mkewe.
Bw Harusi nae akaonyesha ujuzi wake katika kupiga lika.
Kushoto shekhe Mustaph akisalimiana na shekhe Kichwabuta.
Bw Rashid Twalha(KULIA)
Mwanamke smiling

Shekhe Haruna akitoa somo kuhusu ndoa na mapana yake.
Bw Rashid soma la shekhe likamgusa.
Ikafungushwa nikkah ya bw Sharif Kachwamba na Bi Fatma Twalha.
karibu raazizi wangu.
Karibu mutima wangu.
Bibi akimpongeza mjukuu.
Familia.
Zawadi time.


Bi Ashura katika ubora wake, kapata wifi.

Monday, 3 August 2015

MKUU WA MKOA KAGERA AWATAKA WAJASIRIAMALI KUWA NA NIDHAMU NA PESA ZA MIKOPO,ESAURP NA FSDT WAENDESHA MAFUNZO YA WAJASIRIAMALI BUKOBA.

 Zaidi ya wajasiriamali 150 wa Bukoba wanaojishughulisha na utalii na shughuli nyingine za biashara wameanza mafunzo ya ujasiriamali kwa ajiri ya kujenga uwezo wa kuhuisha biashara zao.Mradi  URPhuu unaofadhiliwa na taasisi ya ukuzaji sekta ya fedha nchini (FSDT) na  kutekelezwa na program ya utafiti ya vyuo vikuu vya nchi za mashariki na kusini mwa Afrika (ESAURP) ni mwendelezo wamradi  huo uliotekelezwa mwaka 2013 na ESAURP ambapo safari hii unalenga kufikia mikoa kumi ya Arusha, Kilimanjaro,Mbeya,Iringa,Kagera, Mtwala, Kigoma, Singida, Morogoro na Dodoma.
 Washiriki wa mafunzo..
 Kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa ESAURP Prof  Ted Maliyamkono akiwa na mkuu wa Mkoa wa Kagera Ndugu John Mongella.
 Msimamizi wa ESAURP Bukoba Bw Mutakyahwa Ruta.
 Meneja wa ESAURP Bi Flolentina .C. akieleza namna wanavyofanya kazi katika kujenga uwezo wajasiriamali.
 Prof Ted Maliyamkono amesema kazi kubwa wanayofanya kama ESAURP katika Mradi   unalenga kusaidia biashara  ndogo ndogo na za kati zinazoendeshwa katika mfumo usio rasmi kupata uwezo na maarifa ya kusaidia kukua na kuwa sekta rasimi,kupata huduma za kifedha,pia kufahamu benki washiriki ili kutengeneza mabadiliko ya tamaduni za kibenki namna ya kusaidia miradi ya sekta isiyo rasimi katika miradi inayotafuta huduma za kibenki na hasa mikopo.Bw Christian Mpalanzi  Mtaalamu mshauri wa huduma za Fedha kwa wajasiriamali(FSDT) taasisi ya ukuzaji sekta ya fedha nchini.
 Mkuu wa mkoa wa Kagera John Mongella akifungua mafunzo ya ujasiriamali,amewsaataka washiriki kuzingatia mafunzo na kuheshimu na kuwa na nidhamu na pesa za mikopo.
 Wajasiriamali 150 walishiriki mafunzo katika ukumbi wa St Francis Bukoba.
 Mmoja wa washiriki.

Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na waandaaji wa mafunzo.
 Mgeni rasmi akiwa na wajasiriamali.
Endelea kufuatilia jamcobukoba.blogspot.com.

Sunday, 2 August 2015

CCM BUKOBA MJINI YATANGAZA MATOKEO YA KURA YA MAONI UBUNGE.

 Mwenezi wa ccm  Bukoba mjini Bw Ramadhani Kambuga akitangaza rasmi matokeo ya kura za maoni za Ubunge na madiwani Manispaa ya Bukoba, Wagombea walikuwa wanane,Balozi Kagasheki kura 6971, Amani Anatory kura 944, George Lubeiyukya kura 113, Bw Kaijage kura 71, Kataraiya kura  53,Katabazi kura 34, Rwezahura kura 29,Elieth Lukomoka kura 19.
 Haya ndio matokeo.
 Katibu wa ccm Bukoba mjini  Bw Mwadalu akiongea na waandishi wa habari.
 Waandishi wa habari wakichukua matokeo katika ofisi za chama.
 Kituo cha NHC Kashai.
 Balozi Kagasheki akiteta jambo na na Bw Samora Lyakurwa alieshida kura za maoni katika kata ya Kashai kwa kura za kishindo.
Ni katika kituo cha matopeni Kashai.