Monday, 6 July 2015

BW EUNIAS NTANGEKI RAIS MPYA ROTARY CLUB BUKOBA,JOHN MONGELLA MGENI RASMI.

 Wa pili kushoto ni Bw Eunias Ntangeki akikabidhiwa vifaa vya kazi kama rais mpya wa rotary club Bukoba,Ni katika hafla fupi iliyofanyika katika hotel ya Fiosimim iliyoko barabara ya Kashura,hafla hiyo ilihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo wajumbe wa rotary club Bukoba,waalikwa mbalimbali na mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Bw John Mongella,Katika picha kulia ni rais mstaafu aliemaliza muda wake na kukabidhi kijiti Bw Archard Ngemela, rais wa Cosad Tanzania Bw Smart Baitan na mwisho ni Rtn Mashasi.
 Bw Bube Mkurugenzi wa shule ya watoto wadogo Leoleo akiteta na Bi Briltany Leitch Afisa mipango wa Cosad Tanzania.
 Mkurugezi wa Fiasmim Lilian Rwakatale akiongea na waalikwa waliofika katika hotel yake.
 Bw Archar Ngemela rais mstaafu akiongea na wadau kueleza mambo mbalimbali yaliyofanyika katika kusaidi jamii kupitia  rotary club Bukoba.
 Wageni waalikwa.
 Mzee Mashasi mjumbe wa muda mrefu sana katika rotary club Bukoba akiongea neno kwa wajumbe na waalikwa.
 Rais mpya akikabidhiwa mikoba.
 Akila kiapo.
 Kulia ni mzee Rutabingwa Rtn akiwa na Rtn Mashasi,maswaiba wa muda mrefu sana.
 Hongera rais.
 Rtn mpya nae akachukua kipaza sauti na kunena.
 Mzee mashasi akamvisha begi Bi Hapiness Esau kutambua ujumbe wake mpya wa rotary club Bukoba.
 Rtn mpya Bi  Brigitter Karg nae akapongezwa na rais mpya.
 kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera Bw John Mongella(mgeni rasmi) akiwa na rais wa Cosad Tanzania Bw Smart Baitan.
 Wadau mbalimbali wakapata fursa ya kupiga picha na mgeni rasmi.
 Hapo bwana ni sleng kwa kwenda mbele.
 Waalikwa.
 Mrs Rais mstaafu.
 Dr Jesca Baitan akitabasamu.
 Bw Mutusi, katika pozz.
Mrs Masabara.
Mc Baraka na Walter katika pozzzz.

Saturday, 4 July 2015

NMB BUKOBA YAKUTANA NA WAFANYABIASHARA(NMB BUSINESS CLUB)VIONGOZI WAANDAMIZI WA NMB WATOA SOMO.

NMB Bukoba imekutana na wafanyabiashara na wateja wao kwa lengo la kukaa pamojakuzungumza maswala mbalimbali ya kibiashara na namna ya kupeana mafunzo na uboreshaji wa biashara,Mkutano huuo ulihudhuriwa na viongozi waandamizi wa NMB makao makuu, kanda na viongozi wa Nmb tawi la Bukoba,Wafanyabiashara walipata fursa ya kueleza maoni yao mbalimbali  namna ya kufanya biashara.(Katika picha ni mmoja ya mfanyabiashara(mama  Edgar) akitoa maoni yake.)
Wafanyabiashara wakiwa ukumbini.
Wakifurahia mafanikio na NMB.
Unaweza kuangalia salio katika account yako kwa kutumia simu yako ya mkononi, kama wanavyofanya hawa.
Sura za furaha na muonekano wa bashasha na NMB.
Kulia ni Meneja wa tawi la NMB  Bukoba Victorine Kimario akiwa na  afisa  wa huduma  kwa wateja NMB Bukoba Bw Sadick Mkakile wakiteta jambo kabla ya mkutano kuanza.
Kushoto nimwenyekiti wa Business club tawi la Bukoba  Faustine Karugendo akiwa na  meneja kanda ya ziwa NMB  bw Abraham Agustino.
Meneja NMB tawi la Bukoba  bw Victorine Kimario akitoa maelezo kwa wafanyabiashara.
Kushoto ni Meneja mwandamizi NMB makao makuu Bi Suzan Shuma,Meneja mahusiano biashara kutoka makao makuu na Bw Adam karazani.
Bw Mugisha akitoa maoni yake.
Bi Penina Nyoni Afisa mikopo NMB Bukoba.
Bi Rukia Mawenya (KUSHOTO) akiangalia salio.
Bw Stephen Manji Afisa Mahusiano biashara NMB makao makuu akitoa somo.
Punga mikono , ni maafisa wa NMB Bukoba.
Kushoto ni Bi Shida Maingu Afisa  mikopo midogo na ya kati NMB Bukoba.
Afisa mikopo NMB Bukoba Bi Janet Aloya akitoa somo.
Bw Peter Afisa mikopo NMB Bukoba.
Mwenyekiti wa Business club Bukoba Faustine Karugendo akiongea na wafanyabiashara.
Bw Borando Chacha ( Bima)
Bw Adam Kazarani akitambulisha zao la  NMB  Master card.
Meneja mwandamizi  makao makuu Bi Suzan shuma akielezea maboresho ya huduma, maboresho ya mikopo na kujibu maoni mbalimbali yaliyotolewa na wafanyabiashara.
NMB NDIO MPANGO MZIMA KWA MAISHA BORA NA UHAKIKA.