Wednesday, 27 May 2015

MWILI WA MAREHEMU SAMWELI RUANGISA KUWASILI 1-6-2015 JUMATATU KUTOKA NEW YORK NA KUZIKWA 3-6-2015 JUMATANO.

 Mwili wa marehemu Samweli Ruangisa utawasili Uwanja wa ndege  wa Entebe 1-6-2015 Jumatatu majira ya saa saba mchana ukitokea New york Marekani na kupokelewa na Gari maalumu(Ambulence) na kusafirishwa kwa njia ya barabara mpaka Bukoba.Kwa mujibu wa habari hizi kutoka  kwa mwanafamilia Majid Kichwabuta mazishi yatafanyika 3-6-2015 Jumatano nyumbani kwa marehemu Kitendaguro,Marehemu aliaga dunia huko New york Marekani tarehe 25-5-2015 majira ya saa tano asubuhi kwa saa za huko.(katika picha ni Balozi Kagasheki akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu Kitendaguro.) Ratiba ya mpangilio mzima wa mazishi itatoka.
 Mdogo wa marehemu.
 Mdogo wa marehemu.
 Ma Yustina dada wa marehemu.
 wa pili kulia Jackline Kichwabuta mtoto wa marehemu, mzee Rujwangana, na Yunis Ruangisa.
 Murungi Kichwabuta mtoto wa marehemu akiwa na Bw Deus Mutakyawa

 PICHA YA FAMILIA WAKATI WA UHAI WA MAREHEMU.
Ratiba   ya mazishi itatoka badae.

Monday, 25 May 2015

BURIANI MZEE SAMWELI NTAMBALA LWANGISA,AFARIKI DUNIA HUKO NEW YORK MAREKANI.

 Mwanasiasa mkongwe katika nchi ya Tanzania na muasisi wa chama cha mapinduzi  Mzee Samwel Lwangisa ameaga dunia leo majira ya saa tano asubuhi kwa saa za marekani,kwa hapa kwetu  ni saa kumi na mbili jioni.kwa mujibu ya maelezo ya mwana familia Bw Majid Kichwabuta taratibu  na mipango ya kusafirisha mwili  zinafanyika na taarifa rasmi zitatolewa, akiongea kwa njia ya redio Kasibante Mbunge wa jimbo la Bukoba Mjini Balozi Khamis Kagasheki ametoa pole kwa ndugu , jamaa na wanajimbo wote kwa kumpoteza kiongozi ambae anahistoria kubwa katika Taifa la Tanzania, Marehemu alikuwa kwenye matibabu nchini Marekani.
 Katika picha ni hivi karibuni  mwezi mmoja uliopita Mh Kagasheki alimtembelea  marehemu akiwa New york Marekani.
 Marehemu akiwa na mwanae Murungi  huko Marekani.
Mzee Lwangisa ni miongoni mwa viongozi wa kwanza waliofanya kazi na mwl Nyerere akiwa mkuu wa Mkoa wa kwanza wa Ziwa magharibi kwa sasa Mkoa wa Kagera. Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihidimiwe.

Sunday, 24 May 2015

ZOEZI LA UANDIKISHAJI DAFTARI LA WAPIGA KURA MANISPAA YA BUKOBA LAENDELEA.

 Katibu tawala wa wilaya (DAS) Bukoba akiwa katika kituo cha Airport Bukoba kata ya Miembeni mtaa wa Pwani akijiandikisha.
 Waandikishaji wakiwa kazini.
Viongozi wakisubiri kujiandikisha.
 Mmoja ya Mzee akijiandikisha,
 Ni Mratibu  wa Uandikishaji Mkoa wa Kagera Bw Seif Hussen akifanya mahojiano na vyombo vya habari kuhusiana na zoezi la uwandikishaji.
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba akiongea na vyombo vya habari kuwaomba wananchi wajitokeze kwa wingi.
 Wananchi wakiwa kwenye foleni.
Jamcobukoba.blogspot.com inawasisitiza wanachi wajitokeze kwa wingi kujiandikisha, muda ni mchache, jitokezeni.