Tuesday, 17 February 2015

VALENTINE DAY ILIKUWA POA KIWANJA CHA LINA'S.BARNABA BOY NA AMIN WARIBURUDISHA WATU WAKAPENDANA.

 
 Ni washindi wa zawadi katika kundi la familia,hakika walipendeza na muda wote mezani walionyesha kutulia na kuongea kwa karibu, na simu zao hawakuwanazo kabisa,ni moja ya tatizo kubwa liliwakumba wana ndoa siku hiyo walionekana busy na whassap na kushindwa  kuka uli mkao wa bwana na bibi,hivyo kwa hawa vigezo jaj aliridhika navyo.

 Kulia ni muandaaji wa shughuri nzima Regina Muganyizi kutoka Zachwa investment akiwa na Bw Jerry kutoka Shemeji Investmet walioshirikiana kuandaa.
 Ni kifamilia zaidi.
 Bw Nyamoni na mkewe bi Enjoey wakiongea.
 Kijana Alpha katika pozz.
 Ni  katika lile red capet kwa ajili ya picha za kumbukumbu,lililoandaliwa na Nyumbani studio.
 Mkurugenzi wa Zachwa Investment Bw Muganyizi.
 Ni siku ambayo mwenzi wako umvuta karibu, na wengine upata faraja ya kuwa na wepenzi wao hadharani mara moja kwa mwaka.
 Lakini pia siku hii marafiki upata nafasi ya kukutana na kuongea na kuonyeshana upendo.
 Na wengine uvaa nguo nzuri na kupendeza.
 Na mikao huwa tofauti na siku zingine.
 Barnaba boy akicharaza gita live, ilikuwa poa sana.

 Amin na Barnaba wakifanya yao.
 Kijana sambamba na mamaa.
 Hapo sasa,mie nimefika huko wapi mpaka saa hizi.
 Hii ipo poa.
 Bi Lydia anaeishi  sweden akicheka na camera yetu sambamba na Bw Nico.
 Mahaba niuweee....
 Mtoto wa Jinzi katulia mwenyewe hataki mambo mengi.
 Nilishe nikulishe,hii mpaka mwakani tena utakutana nayo.
 Bw Avit na mkewe ilikuwa ni shidaaaa.
 Bw na Bi Chakindo,wakipeana vitu adimu.
 Hawa kweli walistaili kuwa washindi.
 Jerry na pacha wake Aman katika stage.
 Bw Bube Jaji , aliekuwa makini kuhakikisha vigezo na mashariti vinazingatiwa.
 Dada alieshinda zawadi ya single lady,
 Akiwa na Jaji baada ya ushindi
 Sued Kagasheki, mzee wa baltika.

 Anamaanisha peace  & Love.

 Mama Nice na single lady.

 Siku hiyo unawekewa kinywaji.

Ilikuwa poa sana Hongera sana Zachwa Investment na shemeji investment kwa kufanikisha.

Monday, 16 February 2015

KAMANDA WA UVCCM MKOA WA KAGERA DIONIS MALINZI ASIMIKWA,NAPE ATEMA CHECHE.

 Katibu wa Itikadi , siasa na uenezi Taifa ccm Bw Nape Nnauye akimvisha joho kama ishara ya kumsimika kamanda wa uvccm Mkoa wa Kagera Bw Dionis Malinzi katika uwanja wa uhuru plat form Bukoba.Katibu wa uvccm Mkoa wa Kagera Bw  Didas Zihimbile akisoma taarifa .
 Bw Shafi akiweka mambo sawa.

 Ni Maandamano ya pikipiki na magari kueleke uwanja wa uhuru,baada ya mapokezi ya Nape.
 Bw Nape akiwa kwenye gari maalumu la wazi akiwa na Bw Dionis Malinzi.
 Saida Kaloli akifanya yake.


 Umati mkubwa ulioudhuria.
 Kushoto ni Bw Juliasi Rugemalila mjumbe wa mkutano mkuu wa Taifa ccm ,akiwa na mwenezi wa Bukoba mjini Ramadhani Kambuga.
 Kushoto ni Katibu wa ccm Mkoa wa Kagera  akiwa na Mbuge wa jimbo la Bukoba Mjini Balozi Khamis Kagasheki.
 Mnec wa Bukoba Mjini Abdul Kagasheki akimtunza mtoto aliekuwa akicheza nyimbo za saida kwa ufasaha mkubwa ukilinganisha na umri wake.

Balozi Kagasheki akiongea na wananchi, kikubwa amesema,Nimechaguliwa na wananchi ili niwatetee, niwasemehe na kusimamia,katu hatomuonea aibu yeyote atakae taka kudhulumu haki za wananchi, akaongeza kuwa Siku zote unapowatetea wanyonge wapo watu wachache watakuzushia na kusambaza uongo, lakini yeye daima msimamo wake atabaki na wengi.
 Mwenyekiti wa uvccm Mkoa wa Kagera Bw Yahya Kateme akiongea na wananchi, akizungumzia swala zima la uchaguzi , amesema vijana wako imara watasimamia na kushiriki kikamilifu katika uchaguzi na ushindi utapatikana kwa kishindo.
 Mh Mkuu wa Mkoa wa Kagera John Mongella.
Siku zote wanawake uonyesha mapenzi ya kweli.

 Mh Dionis Malinzi akiwa ameshasimikwa,Bw Nape akiongea na wananchi wa amesema wananchi anawashukuru kwa kuendelea kukiamini chama cha mapinduzi,na kwa hali ilivyo bado itaendelea kushika dora, amewataka viongozi  wa serikali Mkoa kuweka mambo yao sawa na hasa katika mgogoro wa Manispaa ya Bukoba, na amesisitiza kuwa wale wote waliohusika katika kuhujumu wananchi  hivi karibuni watapelekwa kwenye vyombo vya sheria,Pia akawashukuru wananchi wa Bukoba kwa kumuamini Mbunge wao Balozi Kagasheki na akasema ccm Taifa inatambua na kuthamini kazi kubwa anayoifanya Kagasheki na bado wanamuhitaji sana katika kulitumikia Taifa .