Thursday, 5 February 2015

BI SOPHIA AHMAD ASHEREKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA, KAMA HARUSI,SI MCHEZO.....

 Ilikuwa ni bonge la Birthday ya Bi Sophia Ahmad au Mrs Nuru Galiatano kama wanavyoonekana kwenye picha,Sherehe iliyosheheni  watu takribani  150 ilifanyika katika pande za Lake Hotel Bukoba na muonekano wake kuonekana kama harusi kutokana na maandalizi yake kuwa tofauti na birthday tulizozoea, Hongera Bi Sophia kwa kutimiza miaka kadhaa.
 Bi Sophia akiwa na mumewe wakitinga katika ukumbi wa tukio.
 Wakisalimia wageni.
 Mc Rutakwa akifanya yake.
 Mama Shukuru akikaribisha wageni.
 Keki.
 Mtoto akikata keki kwa mbali laazizi wake akishuhudia na kutabasamu.
 Bi shukuru akisaidia kuvikata vipande vidogo.
 Akamlisha mwanae.
 Karibuni keki.
 Akamtambulisha mume wake mbele ya kadamunasi iliyohudhuria.
 N mumewe akasalimia wageni.
 Ikakatwa keki maalumu ya miaka saba  ya ndoa yao.wanasema wahenga unaua ndege wawili kwa jiwe moja.
 Ikawa nilishe nikulishe tuonyeshe tunavyopendana, hakika ilikuwa poa sana.
 Cheers.
 Dah hii birthday si mchezo.
 Bi shukuru kitengo cha mipango na maandalizi yote ya shughuli hii.
 Babu Rweyemamu akitoa burudani.
 Wageni walitokelezea.
 Ni vijimambo tu katika shughuli.
 Wa mjini utawajua,hapa na soft drinks tu.
 Wewe picha zako ni nzuri, kauli ya mama shakira.
 Rangi adimu wanasema,
 Burudani.
 Kamati ikitoa zawadi.
 Mama Erick akitoa zawadi na wenzake.
 Wafanyakazi wenzake na mtoto alizaliwa wakileta zawadi,
 Mama hongera, ni mtoto akimpongeza  mama yake.
 Wa mama wakipata chakula.
Mawifi nao wakatoa zawadi na picha ya pamoja.

BARAKA KIZUGUTO ATUA TFF



Baraka Kizuguto sasa ndiye atakuwa msemaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).


Mara ya mwisho, Kizuguto alikuwa msemaji wa klabu ya Dar Young African.

Habari za uhakika kutoka ndani ya TFF, zimeeleza Kizuguto amewapiga kumbo zaidi ya wasemaji kumi kushinda nafasi hiyo.

Pamoja na kuwa na taaluma ya uandishi wa habari Kizuguto ni mtaalamu wa masuala ya website.

Tuesday, 3 February 2015

BEN KATARUGA AGUSWA NA KITUO CHA NUSURU YATIMA,KUJENGA BWENI MOJA,ATOA LAKI TANO CASH KWA MAHITAJI YA WATOTO.

Mfanyabiashara maarufu anaeishi jijini Dar mzaliwa wa kijiji cha Gera Bukoba vijijini  Bw Ben Kataruga ameguswa na kuwiwa kusaidia watoto yatima wa kituo Nusuru yatima kilichopo Kata Kashai Bukoba Manispaa,Mara baada ya kufika katika kituo hicho alitembezwa kujionea mazingira ya kituo hicho na kujionea namna watoto hao wanavyoishi,Kimsingi Bw Ben alibaini mazingira magumu wanayoishi watoto hao kwani mlezi na msimamizi wa kituo hicho Mama Nuru hana chanzo chochote cha kutunza watoto hao yatima.Bw Ben Kataruga akaguswa na kuamua kujenga bweni kubwa la kisasa litakalokuwa na nafasi ya kutosha na hewa ya kutosha ili watoto waweze kulala vizuri zaidi kuliko wanavyo lala kwa sasa.
Ben akipokelewa na watoto yatima alipowasili katika kituo hicho.
Watoto walifurahi walipoona wageni.
Ben akiangalia moja ya bweni lililojengwa na wafadhili.
Ben akikagua maeneo wanayolala watoto.
Akipata maelezo kutoka kwa mlezi, kwa nje ni ng'ombe waliopewa na waziri mkuu kwa ajili ya maziwa ya watoto,Kwa sasa imekuwa mzigo mkubwa kwani hawana uwezo wa kuajiri mtu wa kutunza ng'ombe hao kitu kilichosababisha afya ya mifugo kuzoofika kwa kutopata lishe bora na maana halisi ya kuwa na ng'ombe hao kupotea.
Mlezi akiendelea kutoa maelezo ya kina.
Mc Baraka akakabidhi kiai cha shilingi laki tano kilichotolewa na Bw Ben Kataruga kusaidia mahitaji mbalimbali ya watoto yatima.
Mlezi akishukuru.
Mmoja wa yatima anaetunzwa kituoni hapo,wadau tafakari na jiulize maswali mengi juu ya yatima wa umri huu na nachukua hatua.
Bw Ben aliambatana na rafiki yake Mchungaji Deo ambae nae amehaidi kusaidia.
Mara watoto wakasoma dua kuombea ugen uliofika kuwaona.
Aminaaaa.
Jamco, Bushira, Shafi ni miongoni wa waliomsindikiza Bw Ben.
Baada ya shughuli nzito msafara ukaelekea airport Bukoba, Bw Ben akiteta na Bw Hafidhu Karugila.
Jamcobukoba.blogspot.com inatoa shukra za pekee kwa Bw Ben Kataruga, kwani  baada ya blogger Jamal kumueleza habari ya kituo hiki alikubali kuwatembelea na kujionea hali halisi,Asante sana Bw Ben kwa moyo wako wa huruma na upendo, wewe ni mfano wa kuingwa na mungu akutangulie katika shughuli zako, umetambua watu wenye matatizo na mahitaji.