Nusura Yatima ni kituo cha kulea Watoto wadogo mayatima kilichopo kata ya Kashai Manispaa ya Bukoba,Familia ya Jamali Kalumuna ilifika kituoni hapo na kuwachukua watoto wote kushiriki nao Dua ya kumshukuru mwenyezi mungu kuwanusuru katika tukio la kuvamiwa na watu wanaosadikiwa ni majambazi nyumbani mapema mwezi jana.Pamoja na kusoma dua ya shukrani pia familia ilipata chakula cha usiku na watoto hao yatima na kutoa zawadi kidogo kwa watoto hao,Kupitia mtandao huu tunawaomba watu mbalimbali wafike kuwaona mayatima hawa na wanahitaji msaada mkubwa kwani wanatunzwa na Mama Nuru alijitolea kufanya hii kazi ngumu na kubwa kwa kujitolea na bila kuwa na chanzo chochote cha kumuwezesha kusaidia watoto hawa yatima.
Ni Bango la kutambulisha kituo hicho ambalo linaendelea kufutika,lakini pia watoto hawa wanahitaji msaada kutoka kwa wadau mbalimbali,Yawezekana nawe msomaji ni yatima, lakini uyatima unatofautiana,yawezekana wewe ni yatima mwenye uwezo a kujimudu na ni mtu mzima, hawa ni yatima na watoto wadogo sana wanaohitaji msaada wako.
Wakipanda gari kuelekea kwenye dua nyumbani kwa Familia ya Jamal.
Dua ikiendelea, na dua ya mtoto yatima ni makubur, yaani ni bora kuliko ya mtu mzima.
Kulia ni shekhe Idrisa akiwa na mwalimu wa watoto yatima wakiendelea na dua.
Hawa ni yatima jamani tuwasaidie.
Kulia ni Bw Ben Kataruga , rafiki wa familia akishiriki dua.
AMINA YARABI AMINA..
Mwenyezi mungu wahepushe na wabaya viumbe wako.
Badae wakapata maakur.
Pacha akihudumia watoto.
Pacha mkubwa nae akihudumia watoto.
Jamco, baba Right,na Bw Ben Kataruga wakipata supu..
Bw Adamu MUBAGO akipata msosi.
Mama mwenyeji , Mama Jamco akiwa na mwanae Jabir Jamal.
Ukafika wakati wa kueleza nia na madhumuni ya uwepo wa wageni,Jamal Kalumuna akasimama kuzungumza na kuwashukuru wote walioiombea familia na kuwa nao kwa karibu wakati wa matatizo hayo.
Ni Zawadi za nguo , viatu na vitu vingine vilivyotolewa na familia kwa ajili ya matumizi ya watoto yatima wakirejea kituoni.
Bw Ben Kataruga baada ya maelezo akaguswa na akasimama kuongea, kikubwa aliona upo wajibu mkubwa sana wa kusaidia watoto yatima, na akahaidi kufika kituoni na kupeleka msaada wake, na kuwasihi wadau mbalimbali kuwasaidia mayatima.
Jamco family.
Jamcobukoba.blogspot.com kwa habari za uhakika. piga simu 0788-707027 au 0754-757157.
Tuesday, 3 February 2015
Monday, 2 February 2015
TASWIRA WA MISA YA THEONESTINA RWEYEMAMU 1/2/2015 HUKO MT VERNON NEW YORK

ilifanyika tarehe 1 Februari, 2015 siku ya jumapili, kuanzia saa nane mchana mpaka saa kumi na mbili jioni 40 East Sidney Avenue, Mount Vernon NY 10550 (COMMUNITY ROOM).
Mungu wetu azidi kukubariki na wewe.
Sunday, 1 February 2015
BALOZI KAGASHEKI AMVAA WAZIRI MKUU PINDA
![]() |
| Balozi Hamis Kagasheki akishiriki moja ya matukio kwenye jimbo lake la Bukoba Mjini |
![]() |
| Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisisitiza jambo wakati akizungumzia masuala mbalimbali ya Kitaifa |
Mbunge wa Bukoba Mjini kwa tiketi ya CCM, Khamis Kagasheki
amemtuhumu Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuwa ndiye aliyekuza mgogoro wa Bukoba
uliosababisha madiwani wa halmashauri kushindwa kufanya vikao, akidai kuwa
mtendaji huyo mkuu wa Serikali ameshindwa kuchukua hatua. Pinda hakuweza
kupatikana, lakini msemaji wake alisema Waziri Mkuu ameshalishughulikia suala
hilo kwa kiasi kikubwa.
Tuhuma hizo za Kagasheki ni za nadra kwa mbunge huyo wa
chama hicho tawala kuelekeza kwa mtendaji mkuu wa Serikali na mmoja wa wajumbe
wa vikao vya juu vya CCM.
Kagasheki, ambaye alikuwa Waziri wa Maliasili na Utalii,
alitoa tuhumu hizo wakati wa mahojiano maalumu na gazeti hili wiki iliyopita,
akisisitiza kuwa ni makosa kuutazama mgogoro huo kuwa ni kati ya yake na meya
na akataka ijulikane kuwa kinachoendelea Bukoba ni suala la wizi.
Mgogoro huo wa kisiasa, ambao umedumu kwa takriban miaka
miwili na unaotishia kugawanyika kwa CCM, umekolezwa na kufunguliwa kwa kesi
tatu ambazo zimezuia utekelezaji wa shughuli za maendeleo na umekuwa
ukihusishwa na vita vya ubunge baina ya Kagasheki na Meya wa Manispaa ya
Bukoba, Anatory Amani.
“Hii ni mara yangu ya kwanza kupata nafasi ya kuzungumzia
suala hili. Hakuna unafiki hapa, hili nitalisimamia mahali popote na nitalisema
mahali popote kuwa Pinda, ndiye tatizo katika mgogoro huu ulioinyima Bukoba
maendeleo,” alisema Kagasheki.
“Lakini hiyo hainizuii kusema kuwa Tamisemi ndiyo tatizo,
ingawa waziri wake ni Hawa Ghasia. Pinda ndiye msimamizi na bungeni alisema
Amani siyo meya tena, lakini hakuna lililofanyika hadi leo na wananchi wanakosa
maendeleo,” aliongeza akirejea kauli ya Pinda bungeni kuwa meya huyo alijiuzulu
halafu siku chache baadaye Amani akaibuka na kukanusha habari za kuachia kiti
cha umeya.
Alisema kuwa awali wakati mgogoro huo unafukuta, uongozi wa
juu CCM uliagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Fedha za Serikali (CAG) kwenda Bukoba,
naye akaenda kufanya utafiti, akamaliza na akatoa kila kitu.
Kagasheki alieleza: “ Nilikwenda katika kikao cha CCM, Pinda
yupo ndani ya chama, kikaagiza madai hayo yafanyiwe kazi, lakini mpaka leo
Takukuru hawajafanya chochote. Ndiyo maana nasema, Pinda akija kuomba kura (za
urais) Bukoba, pale mjini, hali ni ngumu kwelikweli, atapata shida sana.
“Huu siyo mgogoro, ni wizi wa fedha na ripoti ya CAG ipo
wazi lakini wahusika walio chini ya Waziri Mkuu hawataki kuifanyia kazi…Jambo
hili lisipofanyiwa kazi, lazima itakuwa ajenda katika Uchaguzi Mkuu.”
Mbunge huyo wa Bukoba Mjini alisisitiza akisema: “Unajua
kuna vitu vinaumiza, maana vile siyo vitu vyangu ni taarifa ya CAG na kwa kweli
huyu CAG aliyeondoka ungekuwa unamuuliza ukweli, angekwambia amegundua mambo
mengi ndani ya Serikali ambavyo hayafanyiwi kazi. Wizi usio na kifani, upotevu
wa fedha na jambo zuri ni kuwa ile kazi aliyokuwa akafanya CAG ipo kikatiba.”
Alisema kuwa CCM ilitoa maelekezo na kupitia Serikali
ikayapeleka Tamisemi, lakini hadi sasa hakuna pendekezo hata moja la CCM wala
CAG lililofanyiwa kazi, lakini Waziri Mkuu yupo kimya.
“Tunapozungumzia Tamisemi, tunazungumzia Waziri Mkuu, bahati
nzuri yeye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM. Uamuzi wa Kamati Kuu, Pinda
hakufanya hata moja na hapo ndipo mgogoro ukapamba moto,” alidai.
Alitoa mfano wa jinsi wananchi wa Bukoba wanavyokosa
maendeleo kutokana na mgogoro huo akisema kuwa kwa msaada wa Rais Jakaya
Kikwete, Benki ya Dunia ilitoa fedha kwa ajili ya kutekeleza mradi wa maji
katika jimbo hilo, lakini mradi haujatekeleza kwa sababu hakuna vikao vya
baraza la madiwani vinavyofanyika huku Tamisemi ikiwa kimya.
“Yapo mengi, lakini sasa tupo katika mazungumzo na Tamisemi
kuomba watusaidie kupata fedha za huo mradi wa maji kabla ya mwaka wa fedha
haujaisha na fedha kurudishwa kwa wafadhili,” alisema.
Akizungumzia tuhuma hizo, Irene Bwire, msemaji wa Pinda,
alishangaa kwamba vyombo vya habari vinaandika habari hizo kwa upendeleo na
kuongeza kuwa Waziri Mkuu alishashughulikia suala hilo kwa kiasi kikubwa.
Alisema Pinda alidiriki hata kuchukua wahariri wa habari
kwenda nao Bukoba kwa ajili ya kushuhudia jitihada zake za kutatua mgogoro huo
na kwamba mengi ameshayafanya. Bwire alitaka baadaye apelekewa maswali, lakini
hakupatikana.
Oktoba mwaka jana, Waziri Pinda alikwenda Kagera na katika
kikao chake na viongozi wa mkoa aliwataka kutumia busara kumaliza mgogoro huo
kwa kuwa unakwamisha shughuli nyingi za maendeleo, ukiwamo mradi wa maji ambao
ulifadhiliwa Sh18 bilioni na Benki ya Dunia, lakini haujatekezwa kwa sababu ni
lazima matumizi hayo yaidhinishwe na Baraza la Madiwani.
Katika kikao hicho, Pinda alisema ni viongozi wa mkoa
wakubaliane kufuta kesi zilizopo mahakamani ili kazi za kusaidia wananchi
zifanyike.
Alisema anaumizwa na hali ya viongozi wa mkoa kukosa uchungu
kwa wakazi wa manispaa hiyo wa kukosa maendeleo kwa ajili ya mtu mmoja, ambaye
amefungua kesi mahakamani kuzuia shughuli za manispaa.
Katika mkutano huo, Mkuu wa Mkoa wa Kagera wa wakati huo,
Fabian Masawe alimweleza Pinda kuwa shughuli za kisiasa zinakwamisha maendeleo
na kwamba hadi wakati huo kulikuwa na kesi tatu mahakamani, ambazo zina zuio.
Alizitaja kesi hizo kuwa ni Namba 02/2014 iliyofunguliwa na
Amani ya kutaka Mkurugenzi wa manispaa amtambue kuwa ni meya iliyopo Mahakama
ya Hakimu Mkazi wa Bukoba na ambayo hakimu ametoa zuio la shughuli za
halmashauri lilitolewa. Amani pia alifungua kesi Mahakama dhidi ya CAG na
Mwanasheria Mkuu akitaka mambo kadhaa yaliyomo kwenye taarifa ya ukaguzi,
yaenguliwe.
Kesi nyingine imefunguliwa na Yusuf Ngaiza na wenzake watano
dhidi ya Chifu Kalumuna na Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba wakipinga kuvuliwa
udiwani.
Akizungumzia mgogoro huo ulivyoanza, Kagasheki alisema: “Ule
mgogoro siyo wangu, wala siyo suala la mgogoro, ni suala la wizi. Sisi
Watanzania ni mahodari wa kubadilisha maneno.”
Alisema anashangazwa na wanaomtaja kuwa ana mgogoro na meya
huyo wa Bukoba na kukumbusha kuwa Meya Amani ni mtu ambaye Serikali
ilishamwondolea uraia, hivyo hakuwa na nafasi yoyote ndani ya CCM wala
Serikali.
Ni mfanyabiashara na kilichotokea ni kuwa sisi watu wa
Bukoba tulisema tunahitaji maendeleo. Mimi ndiyo nilikuwa kinara wa kutaka
Amani atusaidie, wenzangu wote walikataaa, wakasema huyu mtu ana rekodi mbaya
na kwamba ndiyo maana alinyang’anywa uraia na hivyo hafai. Nikapambana akawa
diwani, alipopata udiwani ikabaki kazi ya madiwani kumpitisha, nikawashawishi
kuwa ‘jamani, huyu ni mfanyabiashara atatusaidia’, kweli akapita akawa Meya.
“Mimi ningekuwa na ubaya na Amani? Aliyemleta pale ni mimi,
nitakuwa mtu wa ajabu sana au kichaa, nimlete mtu halafu baada ya miezi sita
nimkatae. Lakini kutokana na agenda yake nyingine tofauti na ile
tuliyomchagulia, alichofanya akaamua kuwanunua viongozi.”
Aliongeza kusema: “Akamtumia Mkuu wa Mkoa, katibu na
mwenyekiti wa CCM mkoa wakati huo, wakakubaliana kujenga soko jipya, uamuzi
ambao ulipingwa na baadhi ya madiwani. Mimi nikatengwa na nilipomuuliza Amani,
ugomvi ukaanzia katika mambo ya miradi.
“Sasa walichofanya wakaamua kuwafukuza wale madiwani
waliokuwa wanapinga na kutetea haki za matumizi ndani ya halmashauri kwa madai
kuwa ni madiwani wa Kagasheki, uamuzi uliopingwa na chama (CCM) na kuamua
kuwarejesha.”
Alisema kutokana na kushindwa kutatuliwa kwa mgogoro huo,
maendeleo hayawafikii wananchi wa Bukoba, hali aliyosema inawasababishia mateso
makubwa.Chanzo gazeti la Mwananchi Jumapili
Subscribe to:
Posts (Atom)

