Sunday, 25 January 2015

JE UMEWAHI KUFIKA FIOSMIMI HOTEL? KARIBU WAPO BUKOBA MJINI BARABARA YA KASHURA.

 Fiosmimi hotel iko maeneo ya barabara iendayo kashura,ni hotel nzuri iko kilimani ina mazingira mazuri na upepo mwanana kutoka ziwa victoria, unapokuwa umekaa utaweza kuangalia mandhari nzuri ya ukijani uliokolea na kwa mbali kisiwa cha Musira. Fiosmimi hotel inatoa huduma ya malazi, chakula na vinywaji, wanavyo vyumba vya single, double na sute, Pia wanao kumbi mzuri na wa kisasa kwa ajili ya  mikutano, semina, birthday nk. ukumbi unauwezo kwa kuchukua watu kati ya 90 - 100,Wanavyo vifaa vya kisasa kama projectors,Tv . Karibu Fiosmimi hotel kwa huduma bora.
 Unapokuwa Fiosmimi unapata upepo mzuri kutoka ziwa victoria.
 sehemu ya chakula.
 Wanatoa na huduma ya chakula.
 Vyuma vya Double.
 Mkurugenzi wa Fiosmimi hotel Lilian Lwakatare.
 Ni ukumbi wa kisasa wa mikutano.
 Ndani ya ukumbi wa mikutano.
 Mandhari ya nje ya Fiosmimi hotel,ni bwawa la samaki.
 Bwawa la samaki.
 Maeneo yake yanavutia sana.
 Jamco video production wakifanya mahojiano na msimamizi wa Fiosmimi hotel Bi  Tumaini Michael.
 Bi Tumaini Michael ni  bint makini na anaongea kwa kujiamini kwa huduma zinazotolewa Fiosmimi hotel.
Timu nzima ya uongozi na wafanyakazi wa Fiosmimi hotel.
 Huduma ya Internet inapatikana.
 Mkurugenzi akiwa ofisini.
Mkurugenzi akiwa na wafanyakazi wa hotel.

Saturday, 24 January 2015

KAMATI TENDAJI YA KRFA YAFANYA KIKAO NA RAIS WA TFF JAMAL MALINZI ATEMBELEA UWANJA WA KAITABA KUJIONEA MAENDELEO YA UWEKAJI NYASI BANDIA.

 Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu Mkoa wa Kagera (KRFA) Jamal Emil Malinzi akiwa na kamati tendaji wametembelea uwanja wa Kaitaba na kujiona jinsi unavyoendelea kutengenezwa kwa ajiri ya kuwekewa nyasi bandia,mara baada ya kuwasili Bw Jamal ambae pia ni rais wa shirikisho la chama cha mpira wa miguu Tanzania (TFF) alikutana na mtaalamu kutoka FIFA anaesimamia zoezi zima la maandalizi ya uwekaji wa nyasi  bandia Bw  Doron Mommsen alimueleza zoezi linavyoendelea na nini kitafanyika mpaka kufikia hatua ya uwekaji wa nyasi bandia,Baada ya maongezi hayo Bw Jamal alitoa rai kwa viongozi wa serikali na wote watakaokuwa na mamlaka na uwanja wa Kaitaba kuhakikisha mara utakapomalizika kutengenezwa kuutunza na kuusimamia ili uweze kudumu kwa muda mrefu,Amesema uwanja wa Kaitaba kwa asilimia mia moja unagharamiwa na FIFA baada ya yeye (Jamal Malinzi) kuuombea maombi maalumu FIFA na wakakubari kuutengeneza.
 Mapema kabla ya kutembelea uwanja kilianza kikao cha kamati tendaji ya KRFA kikiongozwa na mwenyekiti wake Jamal Malinzi katika ukumbi wa hotel ya Victorius Peach.
 Bw Jamal akiwa na katibu wake Bw Umande Chama,ambae pia ndio mwenyekiti wa wahamuzi TFF.
 Kushoto ni Bw Pelegrius .A. Rutayuga mjumbe wa kamati tendaji KRFA na  pia ni mshauri mkuu wa kiufundi TFF makao makuu.
 Kulia ni Bw Rugeiyamu  Afisa utamadunu Manispaa ya Bukoba.
 Mjumbe kutoka Ngara.
 Bw Jamco na Bw Wily mkurugenzi wa kampuni mpya ya utalii Bukoba Tour wakiteta jambo uwanja wa Kaitaba.

 Kushoto ni blogger wa Bukobasports Faustine Ruta akiwa na Bw Willy.
 Bw WILLY kikazi zaidi akiitangaza kampuni yake kwa mtaalamu wa uwekaji nyasi bandia kaitaba kutoka FIFA.
 Mtaalamu anaesimamia kuweka nyasi bandia akimkaribisha Mwemyekiti wa KRFA Jamal Malinzi na ujumbe aliofuatana nao.
 Akipata maelezo maendeleo ya  utengenezaji uwanja.
 Wanategemea kufikia mwezi wa nne mwaka huu kuwa wamekamilisha uwekaji wa nyasi bandia na miundo mbinu yote ya kuhakikisha maji hayatuami katika uwanja.
 Picha ya pamoja.

 Akasisitiza Jamal Malinzi kuutunza uwanja ukikamilika.
Mwenyekiti wa KRFA Jamal Malinzi  akiwa na baadhi ya wajumbe wa kamati tendaji,katika picha ya pamoja mbele ya kifaa kinachotumika kutengeneza uwanja wa kaitaba.

RAIS ABADILI MAWAZIRI NA MANAIBU WAO, WAPO HAPA WOTE



 
Waziri wa Nishati na Madini mpya, George Simbachawene.
Waziri wa Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe.
Waziri wa Mahusiano na Uratibu, Mary Nagu.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Wiliam Lukuvi.
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Steven Wassira.
 
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Christopher Chiza.
 
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano, Steven Masele.
 
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi, Angellah Kairuki.
 
Naibu Waziri Katiba na Sheria,Ummy Mwalimu.
 
Naibu Waziri Anna Kilango Malecela, Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amebadili mawazini na naibu mawaziri Ikulu leo.
Akitangaza mabadiliko ya mawaziri hao leo, Katibu Mkuu Kiongozi wa Ofisi ya Rais,  Sifue Ombeni alitaja mawaziri hao wapya ambao wanaapishwa jioni hii na wizara zao kwenye mabano kuwa George Simbachawene (Nishati na Madini), Mary Nagu (Mahusiano na Uratibu), Dk. Harrison Mwakyembe, (Afrika Mashariki).
Wengine ni Wiliam Lukuvi (Ardhi, Nyumba na Makazi), Steven Wassira (Kilimo Chakula na Ushirika), Samwel Sitta (Uchukuzi), Jenista Mhagama (Sera na Uratibu wa Bunge) na Christopher Chiza (Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji).
Rais pia ameteua manaibu waziri na wizara zao kwenye mabano kama ifuatavyo: Steven Masele (Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano), Angellah Kairuki (Ardhi Nyumba na Makazi), Ummy Mwalimu (Katiba na Sheria), Anna Kilango Malecela (Elimu na Mafunzo ya Ufundi), Charles Mwijage (Nishati na Madini).