Friday, 28 November 2014

BAG PARTY YA GEDIOSE .R. MUKULASI YAFANA NYUMBANI KWAO KITENDAGURO BUKOBA.


Kulia ni Mhandisi Gediose Mukulasi akitabasamu akiwa na mdogo wake kwenye Bag Party ya aina yake iliyofanyika nyumbani kwao katika kijiji cha Kitendaguro Manispaa ya Bukoba,Bw harusi mtarajiwa anatarajia kufunga ndoa na Bi Dorise .D. Mboyerwa.
Ni matukio mbalimbali yaliyojiri nyumbani,Olukuri.

Wanafamilia wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya shughuri kuanza.
Kushoto ni Bi harusi mtarajiwa Dorice akiwa na mmliliki wa mojka ya soloon ya kike alikopambwa.
SHANGWE ZIKIENDELEA
Wageni kutoka ukweni ,wazazi wa Bi Dorice wakiwasili nyumbani kwao na Bw harusi .
Murungi kichwabuta akionekana na furaha akipokea wageni kutoka ukweni.
Wageni waalikwa.
Kulia ni Mama Mzazi wa Bi harusi mtarajiwa Mrs Mboyerwa akiwa na mdogo wake.
Wanafamilia ya Mukulasi.
Dada wa Bw  harusi mtarajiwa.
Dada wa Bw harusi mtarajiwa.
Bw harusi mtarajiwa akikaribishwa ukumbini.
Kushoto ni Bi Murungi Kichwabuta akiwa Bi Paskazia Barongo.
Maswala ya burudani
Kulia ni mama Matungwa alihusika katika Mapambo ya ukumbi.
Ndugu wakitete kitu.
Ndafu akahusika,ilikuwa bonge la Bag Party.
Watarajiwa wakahusika kwenye ndafu.
Mtarajiwa katika pozz
Mzee Byorwango akatoa neno kwa upande wa familia ya Mukurasi,mbeni ni mzee Paulo Bashereka.
Mc Kahabuka akifanya yake.
CHAKULA TIME....
Wamarekani wakipata vitu natural.
Kushoto wa kwanza ni katibu wa kamati katika picha ya pamoja na wanafamilia.
Jamcobukoba.blogspot.com tunawatakia kila rakheri katika maisha yenu mapya ya ndoa mnayotarajia kuyaanza.

Wednesday, 26 November 2014

MBRAZIL MPYA WA YANGA ATUA LEO EMERSON DE OLIVERIA NEVES ROUQE

MERSN

Nyota mpya wa Klabu ya soka ya Yanga ya Dar es Salaam, anayekuja kufanya majaribio ya kuziba nafasi ya Mbrazili mwenzake Genlson Santos 'Jaja', Emerson De Oliveria Neves Rouqe akitoa ishara ya dole mara baada ya kuwasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam na kupokelewa na viongozi wa Yanga. Rouque aliwasili na Kocha mkuu wa Yanga, Marcio Maximo pamoja na Nyota mwingine kutoka Brazili Andrew Coutinho.

ESCROW KUSOMWA LEO JION


mvutano uliokuwa unaendelea katika kusomwa na kutokusomwa kwa ripoti ya Esrow bunge halijapokea kwa barua yeyote kutoka katika mahaakama kuu ya Tanzania kwa mujibu wa mwenyekiti wa kikao cha asbuhi cha bunge halijapokea zuio lolote  kujadili  kwa hiyo katika kikao cha jionai ripoti haiyo italetwa mbele ya kikao na kusomwa

Thursday, 20 November 2014

TANGAZO LA RATIBA YA MAZISHI YA MAREHEMU LEONARD MTENSA.

MWENYEKITI KAMATI YA MAZISHI YA MAREHEMU LEONARD MTENSA ANAWATANGAZIA RAIBA YA MAZISHI KAMA IFUATAVYO; TAREHE 21-11-1014 SIKU YA IJUMAA  SAA TISA ALASIRI MWILI WA MAREHEMU UTATOLEWA HOSPITALI YA MKOA WA KAGERA NA KUPELEKWA NYUMBANI KWAKE KYAKAILABWA BUKOBA MANISPAA. NA TAREHE 22-11-2014 JUMAMOSI NDIO SIKU YA MAZISHI. RATIBA ITAANZA KUANZIA SAA SITA MCHANA, CHAKULA NA  IBADA YA MAZISHI.KWA WALE WOTE WENYE MAGARI WANAOBWA  SIKU YA TAREHE 21-11-2014 IJUMAA WAFIKE HOSPITALI YA MKOA WA KAGERA KWA AJILI YA KUUNGANA KWENYE MSAFARA WA KUPELEKA MWILI WA MAREHEMU NYUMBANI KWAKE KYAKAILABWA. ASANTENI.

Tuesday, 18 November 2014

HAFRA FUPI YA UFUNGUZI WA MWEYANJARE BAR & SNACK NYAKATO MWISHO WA RAMI BUKOBA.

 Katika hali ya kusogeza huduma bora kwa watumiaji na walaji,Mkurugenzi wa Mweyanjare Bar & Snack Bw Rwehumbiza na Bi Happiness Rwehumbiza wamewekeza katika  eneo la Nyakato mwisho wa Rami na kufungua Bar & Snack kwa ajiri ya kusogeza karibu huduma bora ambazo wananchi wengi wamekuwa wakiamini huduma bora zinapatikana maeneo ya mijini tu,kitu ambacho Bw  Rwehumbiza ameamua kuonyesha kuwa hiyo dhana si sahihi popote huduma bora zinaweza kupatikana inategemea ni kwa namna gani mtoa huduma amejipanga.Mweyanjare Bar & Snack imefunguliwa maeneo ya Nyakato mwisho wa rami barabara inayokwenda Kashozi Bugabo,Unapokuwa umefika Kata ya Buhembe unaendelea na barabara inayokwenda Nyakato sekondari mwisho wa rami . Ukizingatia Manispaa ya Bukoba inazidi kupanuka , na matawi ya vyuo vikuu kuongezeka,
 Utajipatia chips na nyama choma.
 Karibu sana.
 Eneo la Counter.
 Eneo la ndani.
 Vinywaji vya aina zote vinapatikana.
 Mkurugenzi Bw  Rwehumbiza.
 Sehemu ya store.
 Mama na Baba ni kusaidiana.Mr & Mrs Rwehumbiza wakiwajibika Mweyanjare Bar & Snack karibuni kwa raha mustarehee.
 Wapo wataalam wa kuchoma nyama , kuku, mbuzi, nk.
 Vitu mchanganyiko vinapatikana.
 Mrs Happiness Rwehumbiza ambae ndio meneja mkuu akiwajibika kwa vitendo.
 Eneo hilo limepakana na chuo cha JOKUKO na ni eneo zuri tulivu , salama na huduma za uhakika.
 Watu kwa raha zao.
 Cheers.
 Hakika HAPA HATOKI MTU.
 Mchoma nyama Bw Benjamin akiwajibika.
 Mwendo wa mbilimbili.
 Serengeti kila kona wapo.
Hakika watembelee uone huduma zao. KARIBUNI WOTE.