Monday, 17 November 2014

NI MIAKA SABA SASA TANGU UTUTOKE MAMA YETU MPENZI OMUGENZI MA AULELIA KOBULUNGO MUGANDA,MISA YA SHUKRANI YAFANYIKA KASTAMU BUKOBA MJINI.

 Ni Picha ya marehemu Ma Aulelia Kobulungo Muganda wakati wa uhai wake, imefanyika misa ya shukrani kwa ajiri ya kumshukuru mungu na kumuombea marehemu, Ibada ya misa imefanyika nyumbani kwa marehemu Kastam Bukoba Mjini na kuudhuriwa na ndugu,jamaa na marafiki,Wakati huo pia Ibada ya misa ya shukrani imefanyika jijini Dar nyumbani kwa mtoto wa marehemu James Rugemarila maeneo ya Makongo Dar.
 Mzee Robert Bahati na wazee wengine wakati wa ibada ya misa ya shukrani.
 Mama Victor (kushoto) akiwa katika Ibada.
 Kwaya ya Mt Telesia ikitumbuiza wakati wa Ibada.
 Bw Rahim Kabyemela akiwa na Bi Tunu kuhakikisha shughuri zote zinafanikiwa.
 Chakula Time.
 Mama Achi ndio alisababisha watu wakashibaaaa.
 Padri akitoa neno la bwana kwa kondoo wake.
 Mwanga wa milele umwangazie ehe bwana Ma Aulelia Kobulungo Muganda.
 Mzee kijana huyo....
 Mzee Robert Bahati akitoa neno la shukrani  kwa niaba ya familia na kwa niaba ya mzee James Rugemarila .
 Wakati wa ngoma.
 Windhock ndio ilikuwa mpango mzima..
 Kila mmoja ni kinywaji cha Windhock , hapana chezea kampuni ya Mabibo Wine chini ya mkurugenzi wake Mama James Rugemalira.
 Windhock ikawafanya wachangamke zaidi.
 Bojo Windhock nenura ushaga ensenene,chonka Ta James Rugemalirila yakolaaa.
 Tunu akifurahi na camera yetu.
 Wanafamilia picha ya ukumbusho.
 Picha ya pamoja Wanafamilia.

Pumzika kwa amani  Ma Aulelia Kobulungo Muganda.

Sunday, 16 November 2014

MAREHEMU KHERI JUMA SUED KAGASHEKI AZIKWA MAKABURI YA KISHENGE MANISPAA YA BUKOBA LEO.

  Ni Mwili wa marehemu Kheri Sued Juma Kagasheki ukitolewa  katika msikiti wa Ijumaa Manispaa ya Bukoba ukipelekwa katika makaburi ya Kishenge kwa ajiri ya mazishi. Marehemu alifariki jana katika hospitali ya Mkoa  wa Kagera Majira ya jioni.
 Mstahiki Meya Manispaa ya Bukoba Mh Ngalinda akiwa msibani.
 Bw Medard akisalimiana na Mh Khamis Kagasheki.
 Bw Jumanne Bingwa akiwa na Alhaj Adam nyumbani kwa Mzee Sued Kagasheki Rwamishenye kwenye msiba.
 Jeneza la mwili wa maerehemu likiwa mbele ,marehemu akiswaliwa.
 Waumini wa dini ya kiislamu wakimswalia marehemu  katika msikiti wa Ijumaa Bukoba kabla ya kwenda kuzika katika makaburi ya kishenge.
 Marehemu akiswaliwa.
 Umati mkubwa ukiwa kwenye makaburi ya kishenge.
 Mazishi yakiendelea.
 Shekhe wa Mkoa Kagera Alhaj Haruna Kichwabuta akitoa mawaidha baada ya mazishi.
 Alhaj Abuba Kagasheki akitoa shukrani kwa niaba ya familia.
 Bw Abdul Kagasheki akitoa shukrani baada ya mazishi na kutoa utaratibu unaofuata.
 Bw Yakub akisalimiana mh Kagasheki.
 Mh Kagasheki akiwa na Mhandisi Chakindo.
 Mh Kagasheki akisalimiana na mkurugenzi wa  shule ya Kemibos Bw Kareju.
 Bw Rahimu  Kabyemera akiwa maeneo ya makaburi ya kishenge baada ya mazishi.
 Bw Amidu akiwa na Mh Diwani  Ibrahimu Mabruki baada ya mazishi.
 Alhaj Adam Kagasheki akiwa na rafiki yake baada ya mazishi.
 Balozi Khamis Kagasheki akitroti maeneo ya kishenge baada ya mazishi.
 Balozi Khamis Kagasheki akisalimiana na Mama Rubi na Bi Hawa Hasani baada ya mazishi .
 Dk Omary akiteta na ndugu yake.
Jamcobukoba.blogspot.com inatoa pole kwa ndugu,jamaa na marafiki wote.