Thursday, 2 October 2014

HATIMAE COSAD KUANDIKA HISTORIA MPYA MANISPAA YA BUKOBA,BALOZI KAGASHEKI ATEMBELEA MIRADI KABLA YA UFUNGUZI RASMI 3-10-2014 IJUMAA

 Wahenga walisema kawia ufike na wengine husema mambo mazuri hayataki haraka, yamedhihirishwa na Cosad baada ya ndoto yao ya muda mrefu ya kuweka miradi mbalimbali katika Manispaa ya Bukoba kwa ajiri ya Jamii kupata huduma na kujikwamua katika wimbi la umasikini uliokithiri kwa kiasi kikubwa katika maeneo mengi nchini.Cosad  ni shirika lisilo la serikali Tanzania wanaweka histori mpya ya kufungua miradi katika upande wa afya kwa kufungua Zahanati katika kata ya Kashai maeneo ya Nyamkazi,Shamba la Mbuzi wa maziwa  kata ya kagondo,Studio ya kurekodi kazi za wasanii(Imuka Recording Studio),Kituo cha Teknolojia na Biashara na Ofisi mpya za makao makuu ya Cosad Nchini.Katika picha ni Uongozi wa Cosad ukimpokea Mbunge wa jimbo la Bukoba Mjini Balozi Khamis Kagasheki katika uwanja wa ndege Bukoba na badae kutembelea maeneo yote ya Miradi kabla ya ufunguzi rasmi 3-10-2014.
 Balozi Kagasheki akipokelewa na Mkurugenzi Mtendaji  wa Cosad Tanzania Bw Smart  Baitan
 Dr Susan McCormick Hadley akisalimiana na Balozi Kagasheki uwanja wa ndege wa Bukoba.
 Hili ndio jengo la  Zahanati itakayofunguliwa maeneo ya Nyamkazi Bukoba
 Bw Smart akitoa maelezo kuhusiana na mradi wa Zahanati  Kwa Mh Mbunge
Kulia mmoja wa wajumbe wa bodi ya Cosad anaehishi Marekani akiwa na wafanyakazi wa Casad Tanzania.
 Eneo la Mapokezi
 Baadhi ya vifaa vya kisasa vitakavyotumika
 Balozi Kagasheki baada ya kuona alikubali na kushukuru kazi kubwa iliyofanywa na Cosad jimboni kwake
 Maeneo ya kupumzisha wagojwa
 Balozi Kagasheki na mmoja wa waandishi na mtangazaji wa Clouds Redio na TV
 Ofisi za Cosad maeneo ya Kashura mlimani.
 Eneo la Mapokezi
 Eneo la mikutano na Mazungumzo
 Eneo la Studio kwa ajiri ya kurekodi kazi za wasanii
 Uongozi wa Cosad wakiwa nyumbani kwa Balozi Kagasheki Maeneo ya Kitendaguro kwa mapumziko mafupi .
 Picha ya pamoja nje ya Nyumba ya Balozi Kagasheki
 Hapa ni Kituo cha Teknologia na Biashara cha Cosad kilichoko Kata ya Kibeta Bukoba Manispaa
 Balozi Kagasheki akisalimiana na Mtoto wa Bw Smart Baitan
 Dr Jessica  Baitan akisalimiana na Balozi  Kagasheki
 Eneo la ndani Kituo cha Teknolojia na Biashara cha Cosad
 Mtoto mdogo wa Bw Smart Baitan.
 Mradi wa mbuzi wa maziwa

 Mbuzi wa maziwa
 Balozi Kagasheki akipewa maelezo jinsi wakina mama wanavyonufaika na mradi huu
 Kushoto ni  kijana anaehudumia mbuzi
 Balozi Kagasheki Live Cloud's Redio akieleza kile alichokiona katika ukaguzi wa miradi itakayofunguliwa rasmi 3-10-2014 jimboni kwake
 Baba ASKOFU Bagonza mmoja wa wajumbe wa bodi ya Cosad
 Baba Askofu Bagonza akisalimiana na Blogger Jamco, na kumpongeza kwa kazi kubwa a
 nayoifanya kuitangaza Bukoba na Kagera.
Blogger's wa Jamcobukoba.blogspot.com na Bukobawadau wakiteta kuhusiana na shughuri za Cosad.Endelea kufuatilia ufunguzi rasmi.

Monday, 29 September 2014

WADADA WAJASILIA MALI (SMALL DADA'S) WA JIJINI MWANZA WAKUTANA NA BALOZI KAGASHEKI

 Balozi Khamis Kagasheki akiongea na kundi la wadada wajasiliamali ambao wanapambana na wimbi la umasikini na kujishughulisha na shughuri za kibiashara,kusaidiana na kukopeshana.
 Katibu wa umoja Bi Frola Binamungu akieleza shughuri mbalimbali wanazozifanya,wa kwanza kulia ni mwenyekiti Bi Anita Zimbihile
 Balozi Kagasheki akimkabidhi mweka hazina wa kundi mchango wake  wa  kukubali kile kinachofanywa na umoja huu katika swala zima la kujikwamua kiuchumi.
Dada huyu aliomba kupiga picha na Balozi Kagasheki kwa kukubali utendaji wake wa kazi na kusimamia haki.

KAGASHEKI MGENI RASMI MAHAFARI KIDATO CHA NNE BWERANYANGE GIRL'S SCH KARAGWE

 Akizungumza mbele ya mgeni rasmi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Bukoba mjini CCM Balozi Khamis Kagasheki, katika mahafali ya tano ya kidato cha nne katika shule inayomilikiwa na KKKT ya Bweranyange, askofu Bagonza amemwomba mbunge huyo kumsaidia kukamilisha usajili wao ili wasikwame kufundisha katika shule za kanisa hilo kunusuru wanafunzi wa sayansi.

Amesema kuwa alienda Sri Lanka kufanya mazungumzo, na kukubaliana na walimu kadhaa ambao kwa mujibu wake anataka kubadilisha mawazo na mtazamo wa elimu ya tanzania kupitia walimu kutoka nje, huku akisema kuwa walimu wa ndani waache kushinikiza mishaara mikubwa, kisa wanafundisha sayansi.

Katika mhafali hayo, wanafunzi 67 wa kike wamehitimu kidato cha nne, huku shule hiyo ikikabiliwa na mapungufu ya kompyuta, huduma ya maji na umeme, ambavyo mh. Kagasheki amesema ankwenda kuzungumza na rafiki zake, ili kuona jinsi ya kusaidia vitu hivyo, huku akiomba apewe bajeti yake.

Balozi Kagasheki, akifanyiwa utabiri na mwanafunzi kutaja na ni kitu gani ameshika mkononi wakati wa mchezo wa kuigiza..

Mgeni rasmi katika mahafali hayo Balozi Kagasheki akikabidhi cheti kwa moja ya mwanafunzi muhitim.

Askofu Bagonza kushoto, akiongozana na Balozi Kagasheki katika ukaguzi wa mazingira ya shule hiyo ya wanafunzi wa kike,ambapo hatahivyo balozi ameoneshwa maabara ya shule hiyo inavyofanya kazi.

MANISPAA YA BUKOBA HATARINI KUKUBWA NA MAFURIKO.

  

 Mvua zilizonyesha jana katika mji huo na viunga vingine mkoani Kagera, imesababisha nyumba kadhaa kuzingirwa na maji, ambapo sababu kubwa inachangiwa na kuziba kwa mitaro, mito, pamoja na ujenzi holela, hasa katika kujenga kado kando ya mto Kanoni, unaokatiza katika mji huo.
Ni eneo la Miembeni, mkabala na ukumbi wa Disco Linas.

Ni mkabala na CRDB, chini ya Baa ya Oxygen katikati ya mji.

Hapa ni katika paking ya bank CRDB
Kituo cha mfuta Camel barabara ya Kashozi nacho ndani ya maji.

Daraja katika barabara ya Kashozi liko eneo la Migera.

Sunday, 28 September 2014

MARAFIKI WAZIDI KUMTEMBELEA MH DAUDA KALUMUNA KUMJULIA HALI BUGANDO

 Kapten Mwasa akiwa hospital ya Bugando akiongea na mzee Kalumuna kuhusiana na maendeleo ya matibabu na afya yake kwa ujumla.
 Vijana maarufu wanaotambulika kwa jina la Kanyaga mafuta waliyakanyaga mpaka hospital ya Bugando kwenda kumjulia hali mzee Kalumuna hakika wahaya wanamsemo wao Bayoreka engozi za mazima.
 Wakiingia lango kuu la Bugando.
 Katika hali ya kuweka kumbukumbu sawa ikabidi  kanyaga mafuta washuhudishe vibao vya Bugando.
 USO KWA USO na Mzee Kalumuna,palikuwa hapatoshi mzee alipata nguvu ghafla.
 Wamezoea kumuita mzee wa CPA , Ilikuwa ni soga kwa kwenda mbele.
 Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi Geita Mh Maduhu,Mwenyekiti baraza la Ardhi Mkoa wa Kagera Renatus wakiwa na mzee Kalumuna Hospitalini Bugando.
Kuilia Bw Spidion Njunwa maarufu kama Obama  akiwa na mzee Kalumuna na Rehema Kalumuna.
Mzee Dauda Kalumuna akielezea maendeleo ya afya yake inavyozidi kuboreka kwa jamaa waliofika kumuona hospitalini Bugando.

Friday, 26 September 2014

MCHUNGAJI ATUMIA SADAKA KUSAIDIA UJENZI WA MAABARA BUKOBA

Mchungaji James

Hatahivyo mashirika, Taasisi na watu binafisi mkoani Kagera wameombwa kuendelea kuchangia katika miradi mbalimbali ya Maendeleo .


Wito huo umetolewa na mmoja wa wadau wa maendeleo manispaa ya Bukoba, MCHUNGAJI KING JAMES wa kanisa la ukombozi manispaa ya Bukoba wakati wa hafla ya kukabidhi mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya maabara unaondelea kwa sasa.

Mchungaji JEMES  amesema kuwa amewiwa kutoa mchango huo, katika shule za manispaa zinazoendelea na ujenzi huo ili kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha elimu hususan masomo ya sayansi.

Kulia ni mkuu wa wilaya ya Bukoba Bi ZIPORAH PANGAN

Kutoka kushoto ni mkurugenzi manispaa, naibu meya Ngalinda, mchungaji James, mwenyekiti wa ccm wilaya, na afisa tarafa Abdon Khawa.



Ameongeza kuwa juhudi za serikali pekee hazitoshi katika kuwaletea wananchi maendeleo bali ni kushirikiana na wadau wote.

Akisoma risala wakati wa kupokea msaada huo mkurugenzi wa manispaa ya Bukoba, ADOH MAPUNDA amesema kuwa msaada huo, umetolewa kwa wakati muafaka na kutaka msaada huo kutumika kwa malengo yaliyokusudiw