Kampuni ya Utalii Mkoa wa Kagera Kiroyera Tours imekuwa ikiweka jitihada kubwa sana kutangaza vivutio vilivyomo katika Mkoa wa Kagera na kuelimisha jamii kwa ujumla kutambua na kuelewa kuwa Utalii unaweza kuufanya wewe binafsi au Familia si Wazungu tu.Meneja wa Kiroyera Tours Ndugu Willam Ruta(Willy Kiroyera) amekuwa akihimiza jamii kila mara kufanya utalii wa ndani si kusubiri wazungu tu. Haya yamedhihirishwa na Bw Victor Alcard mkazi wa Bukoba anaeishi Jijini Dar ambae amekuja kwa ajiri ya Send off ya mchumba wake wanaotarajia kufunga pingu za maisha 13-9-2014 Jijini Dar, yeye na rafiki zake wamefanya utalii wa ndani kutembelea maeneo mbalimbali katika Manispaa ya Bukoba.
Bw Victor akiwa na swaiba wake wakifurahia hewa safi na kelele za maji katika maporomoko ya kyamunene maeneo ya kata ya Ijuganyondo barabara ya Maruku kwenye msitu wa Kyamunene Bukoba.
Bw Victor akiwa na Jamco mmiliki wa Kampuni ya Jamcovideo production,Jamcobarbershop na blog ya Jamco.
Hakika Victor alijipanga ameambatana na wapiga picha maarufu kutoka Jijini Dar kampuni ya Pixelbase na mwwenye miwani ndio mkurugenzi Bw Abdul Mohamed.wakipeana mikakati ya Send off ya mchumba wa Victor.
Bw Victor na wanae wakiingia Jamcobarber shop kwa ajili ya usafi
Huduma zikiendelea
Kijana wa Pixelbase akiendelea na kazi ya kuchukua matukio.
Kijana Kevin kutoka JAMCO VIDEO PRODUCTION(kushoto) akiwa na mtaalamu Zungu kutoka Pixelbase ya Dar wakishare love
Bw Harusi mtarajiwa akipendezeshwa
Ni Mapozzzzzz
Ni Mikakati tuuuu
Mdau ndani ya msitu wa kyamunene
Victor akiwa katika Msitu wa Kyamunene akifanya utalii wa ndani
Watu wakifanya utalii
Ni eneo muhimu sana ukiwa Bukoba akikisha unafika usisimuliwe
Hali ya hewa safi, upepo mzuri utapenda mwenyewe
Ukafika wakati raha zikazidi na watu wakatunga wimbo na kuimba kyamunene ni balaaaa
Bonge la Tour si mchezooo
UNAONA HIYOOOOO
Wapiga picha crips zikatosha wakataka wapigwe picha na wao
Hapana chezeaa Bukoba wewe...
Bukoba is beautful,tujivunie
Wadau kutoka DAR na wengine wa Bukoba wakifurahia Bukoba.
Mandhari ya Mji
Mshikaji Bukoba ni bonge la vitu hadimu duniani....
Hakika Bukoba ni pazuri,hebu anza wewe kutambua uzuri wa Bukoba na kuitangaza,sie jamcobukoba.blogspot.com tulisjaanza,na tutaendelea kuitangaza Bukoba.Hongera Victor kuwa mmoja wa wadau kutembelea vivutio vilivyopo Bukoba.
Sunday, 31 August 2014
Saturday, 30 August 2014
MTEMVU: CCM ITAUPUKUTISHA UPINZANI TEMEKE UCHAGUZI WA MITAA, SIYO KWA KUTUMIA NGUVU ILA MATUNDA YA UTEKELEZAJI ILANI
Na Bashir Nkoromo
Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu ametamba kuwa, CCM itapukutisha kwa kishindo upinzani wote katika jimbo hilo kwa kushinda mitaa yote katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.
"Wala hatutatumia nguvu bali tutaichukua mitaa yote hata hiyo michache iliyopo sasa chini ya upinzani, kwa kutumia mtaji wa mafanikio makubwa tuliyoonyesha katika utekelezaji wa ilani ya CCM katika kipindi hiki", alisema Mtemvu.
Mtemvu alitoa tambo hizo wakati akihutubia mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Jumuia ya Wanawake Tanzania, Kata ya Azimio, kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Sokoine, katika Kata hiyo, Temeke jijini Dar es Salaam.
Alisema, CCM inao uhakika wa kutwaa viti vyote hadi kurejesha vichache vilivyopo sasa chini ya upinzani kwa kuwa mengi ambayo CCM iliahidi kupitia yeye wakati akiomba kuwa mbunge wa jimbo hilo katika uchaguzi mkuu uliopita yamefanyika.
Mtemvu alitaja baadhi ya yaliyotekelezwa kuwa ni pamoja na ujenzi wa barabara katika maeneo mbalimbali ambazo karibu zote zimeboreshwa kwa kujengwa kwa kiwngo cha lami tofauti na awali ambapo ilikuwa kero kubwa kwa kuwa zilikuwa hazipitiki kutokana na ubovu tena za vumbi.
"Zamani nilikuwa kila nikisimama jukwaani mnaniolea matatizo na kero lukuki hasa kuhusu hizi barabara, sasa leo hatuzungumzii matatizo ya barabara, tunazungumzia tu sasa kuboresha taa kwenye mitaa na barabara hizi", alisema Mtemvu.
Alisema, kuanzia mwezi huu Septemba, taa zote katika barabara na mitaa kwenye jimbo hilo zitawaka ambapo sasa zinafanyiwa maboresho ili zitumie nishati ya jua (solar) ili kupunguza changamoto ya gharama za malipo ya umeme wa taa hizo.
Mtemvu alisema, kukamilika kwa taa hizo itakuwa janga kwa vibaka ambao wamekuwa wakitumia fursa ya giza kujificha wakati wakivizia kuiba kwenye nyumba za watu na pia kukwapua wapitanjia nyakati za usiku.
Alisema mbali na kuboresha barabara CCM pia kupitia uongozi wake imeweza kuboresha hali za wananchi hasa kina mama na vijana kwa kuviwezesha vikundi vyao vya ujasiriamali kwa kuwakopesha fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali ambapo sasa zaidi ya vikundi 100 vimenufaika.
Mtemvu aliahidi kuendelea kushirikiana na wabunge wengine wa Temeke na mkoa wa Dar es Salaam kwa jumla kuhakikisha watendaji wabovu serikalini wanakabwa koo ili wawajibike ipasavyo kutumikia wananchi.
Pia aliahidi kuhakikisha anaedelea kupigania kupatikana kwa mazingira bora ya kufanya kazi zao mamalishe na bodaboda kwa kuwa wana mchango mkubwa katika maendeleao ya jamii.
"Najua haiwezekani bodaboda zote zikaingia mjini, lakini tunachofanya ni kupigania kuhakikisha unakuwepo utaratibu mzuri utakaowezesha baadhi kufika mjini bila kuharibu taratibu na sheria zilizopo. Pia Mamalishe kwa kuwa lazima waendelee na shughuli zao tunawatafutia utaratibu bora kufanya shughuli zao kwa amani badala ya kukimzwa kimbizwa na mgambo kila mara", alisema Mtemvu.
Katika mkutano huo, uliosheheni burudani mbalimbali ikiwemo msanii Omari Tego kuimba wimbo maalum wa CCM ambao ulikonga nyoyo za waliohudhuria, Mtemvu aligawa kadi kwa wanachama wapya 45 wa UWT.
HABARI KATIKA PICHA KUHUSU MKUTANO HUO
Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu akihutubia mkutano wa hadhara uliofabyika kwenye Uwanja wa shule ya Sokoine, Temeke jijini Dar es Salaam, jana, Agosti 30, 2014.
Mtemvu akishangiliwa wakati akihutubia mkutano huo wa hadhara
Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu akimpa kadi ya Uanachama wa UWT Maridha Rajabu wakati wa mkutano huo, wanachama wapya 45 wa jumuia hiyo walipewa kadi
Mbunge wa temeke, Mtemvu akimtuza msanii Omari Tego baada ya kukunwa na msanii huo kwa kuimba wimbo maalum wa CCM wakati wa mkutano huo
Mbunge wa temeke, Mtemvu akimpongeza baada ya kumtuza msanii Omari Tego baada ya kukunwa na msanii huo kwa kuimba wimbo maalum wa CCM wakati wa mkutano huo
Umati wa wananchi ukiwa umefurika wakati wa mkutano huo
Mwenyekiti wa UWT Kata ya Azimio, Tatu Hassan akifungua mkutano huo, kwenye Uwanja wa Sokoine Temeke kabla ya kuhutubiwa na Mtemvu
Diwani wa Kata ya Azimio, Hamisi Mzuzuri akieleza utekelezaji wa ilani ya CCM katika kata hiyo wakati wa mkutano huo
Ofisa Kutoka Makao Makuu ya CCM, Idara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Gifti Isaya akipata picha kupitia simu yake kwenye mkutano huo
Waalikwa wakiwa kwenye mkutano huo. Wapili walioketi kulia ni Ofisa katika Idara ya Mambo ya Nje Makao Makuu ya CCM, Gift Isaya akifuatilia kwa makini pamoja na wenzake
Msanii Yusuf Peter wa Kikundi cha hamasa Temeke, akionyesha vimbwanga vyake mbele ya mke wa Mbunge wa Temeke Mama Mtemvu (kulia)
Msanii Ahmadi Juma wa kikundi cha hamasa Temeke, akionyesha uhodari wa 'kula' moto wakati kikundi hicho kikitoa burudani wakati wa mkutano huo
Mtemvu akiwatuza wasanii waliotia fora uwanjani wakati wa mkutano huo.
Subscribe to:
Posts (Atom)











.jpg)

