Tuesday, 29 July 2014

SHEKHE WA MKOA WA KAGERA AKEMEA VIONGOZI WA DINI NA SIASA WANAOHATARISHA AMANI YA WATANZANIA

 Shekhe wa Mkoa wa Kagera Alhaji Haruna Kichwabuta amekemea viongozi wa kidini na siasa kuwa waangalifu na kauli zao kwa wananchi  zinazoweza kuhatarisha amani nchini.Akiongea na waislamu walioswali katika msikiti wa Jamia Manispaa ya Bukoba leo katika kuazimisha sikukuu ya Edd el-ftr,Shekhe Haruna amesema si busara na haitakiwi kabisa viongozi wa dini au siasa kuchochea na kuhatarisha amani ya nchi hii kwa masilahi yao binafsi.Pia katika salamu zake za Idd amewataka wabunge wa bunge la katiba waliosusia kikao watambue kuwa wapo pale kwa ajiri ya wananchi hivyo kususia Bunge si Busara kwani wenye kauli ya mwisho ni Wananchi wa Tanzania na si wao, hivyo ni vema wakarejea Bungeni kuendelea na vikao.
 Waumini wakisikiliza mawaidha ya Idd
 Hali ya usalama iliimarishwa ili waumini waweze kuswali kwa amani na utulivu
 Mc Baraka ndani ya kanzu lake akitinga msikitini
 Ni furaha tu za Idd
 Shekhe Kakwekwe akieleza jambo
 Mapacha hao
 Maurana akiwa na wanae
 mtaani baada ya swala
 Seneti nako tukapita, hali ilikuwa hivi.
 Familia mbalimbali baada ya kuswali
 Mama na wanae akataka atokelezee kwenye blog.
 Pilika lango kuu la soko.
 Akataka apate picha,nasi bila hiyana tukapiga.
 Ni benz ya zamani ya Marehemu Rostamal Radha likiwa na mjuu wake mtaani wakitokea msikitini
 Ni kuwahi sokoni


 Ni pilika baada ya swala ya Idd
 Kifamilia zaidi
Mr Mohamed Remdin akiwa na mke wake Rehana wakifurahi na camera yetu mitaa ya Miembeni baada ya swala ya Idd

Monday, 28 July 2014

KAGONDO FC WATINGA NUSU FAINALI KWA KUIFUNGA IJUGANYONDO KWA MIKWAJU YA PENATI 4-3 KAGASHEKI CUP 2014.

Wachezaji wa Timu ya Kagondo Fc wakipongezana mapema kipindi cha pili baada ya kuifunga bao la pili na kufanya 2-1 dhidi ya Timu ya Ijuganyondo amabao ndio walikuwa wamewatangulia kwa bao 1-0 tangu kipindi cha kwanza.Wachezaji wa Timu ya Kagondo FC wakipongezana baada ya Kipa wa Ijunganondo Fc Yassin Issa kujifunga bao kwa Uzembe  wa kudaka mpira na kumponyoka na kuingia langoni mwake na Mwamuzi wa pembeni kuliona na kudai bao na hatimaye Timu ya Kagondo kufanya itangulie kwa bao 2-1.
Uwanjani ilikuwa mshike mshike!!! Kagondo tangu kipndi cha pili walikuwa wanausongo wa kuwafunga wenzao Ijuganyondo!
Mchezaji wa Ijuganyondo akikimbizwa na wachezaji wawili wa Kagondo Fc
Baadae katika kipindi cha pili mwishoni Timu ya Ijuganyondo ilifanya Mabadiliko na kufanikiwa kusawazisha baada ya Straika wao kukatiza mbele ya Mabeki wa Kagondo Fc na kusawazisha bao na kufanya bao kuwa 2-2 na mtanange kumalizika kwa dakika 90 kwa kutoshana nguvu kwa sare ya 2-2. Mikwaju ndio iliamua nani anakwenda hatua ya Nusu Fainali kati ya Kagondo Fc na Ijuganyondo Fc. Timu ya Ijuganyondo ilikosa penati mbili na timu ya Kagondo Fc kukosa mmoja ambapo timu ya Kagondo iliibuka na Ushindi kwa  Mikwaju ya penati 4-3 na kujikatia tiketi ya kwenda Nusu fainali katika Michuano hii ya Ligi ya Kagasheki.
Mpaka sasa katika timu nane tayari timu 3 zimeishatinga hatua hiyo ya Nusu Fainali ambazo ni Mabingwa watetezi Bilele Fc, Miembeni Fc, Kagondo Fc. Kesho ni kati ya  Rwamishenye vs Kitendaguro kutafuta timu ambayo itakamilisha timu nne za kucheza Nusu Fainali. Ambapo Mshindi wa Kesho anatarajiwa kucheza na mshindi wa leo Kagaondo Fc.

Kipa Yassin Issa wa Ijuganyondo akidaka kwa uzuri kona
Mashabiki Jukwaa kuu furaha tupu baada ya timu zote kutoshana nguvu ya 2-2
Kamera Jukwaa kuu ikitafuta tamasamu za mashabiki

Habari zifike na Nyumbani

Taswira jukwaa Kuu wakitazama soka
Wakati huo zikiwa 2-2 hakuna aliyetaka mpira utue chini...
Wachezaji wa Timu ya Kagondo Fc wakimpongeza mchezaji wao aliyewapa ushindi wa kwenda hatua ya Nusu fainali Abdallatifu Khamis juu kwa juu.
Ilikuwa Shangwe leo, Huku mashabiki wa Ijuganyondo Fc wakibaki midomo wazi kuona Timu yao inaondolewa katika Michuano hii ambako walikuwa wanaipa Matumaini tangu kipindi cha kwanza kusonga hatua ya Nusu Fainali.
Mashabiki wa Kagondo Fc wakiwa wamembeba aliyewapeleka katika hatua ya Nusu Fainali
Ushindi raha tupu!!