Tuesday, 29 July 2014

SHEKHE WA MKOA WA KAGERA AKEMEA VIONGOZI WA DINI NA SIASA WANAOHATARISHA AMANI YA WATANZANIA

 Shekhe wa Mkoa wa Kagera Alhaji Haruna Kichwabuta amekemea viongozi wa kidini na siasa kuwa waangalifu na kauli zao kwa wananchi  zinazoweza kuhatarisha amani nchini.Akiongea na waislamu walioswali katika msikiti wa Jamia Manispaa ya Bukoba leo katika kuazimisha sikukuu ya Edd el-ftr,Shekhe Haruna amesema si busara na haitakiwi kabisa viongozi wa dini au siasa kuchochea na kuhatarisha amani ya nchi hii kwa masilahi yao binafsi.Pia katika salamu zake za Idd amewataka wabunge wa bunge la katiba waliosusia kikao watambue kuwa wapo pale kwa ajiri ya wananchi hivyo kususia Bunge si Busara kwani wenye kauli ya mwisho ni Wananchi wa Tanzania na si wao, hivyo ni vema wakarejea Bungeni kuendelea na vikao.
 Waumini wakisikiliza mawaidha ya Idd
 Hali ya usalama iliimarishwa ili waumini waweze kuswali kwa amani na utulivu
 Mc Baraka ndani ya kanzu lake akitinga msikitini
 Ni furaha tu za Idd
 Shekhe Kakwekwe akieleza jambo
 Mapacha hao
 Maurana akiwa na wanae
 mtaani baada ya swala
 Seneti nako tukapita, hali ilikuwa hivi.
 Familia mbalimbali baada ya kuswali
 Mama na wanae akataka atokelezee kwenye blog.
 Pilika lango kuu la soko.
 Akataka apate picha,nasi bila hiyana tukapiga.
 Ni benz ya zamani ya Marehemu Rostamal Radha likiwa na mjuu wake mtaani wakitokea msikitini
 Ni kuwahi sokoni


 Ni pilika baada ya swala ya Idd
 Kifamilia zaidi
Mr Mohamed Remdin akiwa na mke wake Rehana wakifurahi na camera yetu mitaa ya Miembeni baada ya swala ya Idd

Monday, 28 July 2014

KAGONDO FC WATINGA NUSU FAINALI KWA KUIFUNGA IJUGANYONDO KWA MIKWAJU YA PENATI 4-3 KAGASHEKI CUP 2014.

Wachezaji wa Timu ya Kagondo Fc wakipongezana mapema kipindi cha pili baada ya kuifunga bao la pili na kufanya 2-1 dhidi ya Timu ya Ijuganyondo amabao ndio walikuwa wamewatangulia kwa bao 1-0 tangu kipindi cha kwanza.Wachezaji wa Timu ya Kagondo FC wakipongezana baada ya Kipa wa Ijunganondo Fc Yassin Issa kujifunga bao kwa Uzembe  wa kudaka mpira na kumponyoka na kuingia langoni mwake na Mwamuzi wa pembeni kuliona na kudai bao na hatimaye Timu ya Kagondo kufanya itangulie kwa bao 2-1.
Uwanjani ilikuwa mshike mshike!!! Kagondo tangu kipndi cha pili walikuwa wanausongo wa kuwafunga wenzao Ijuganyondo!
Mchezaji wa Ijuganyondo akikimbizwa na wachezaji wawili wa Kagondo Fc
Baadae katika kipindi cha pili mwishoni Timu ya Ijuganyondo ilifanya Mabadiliko na kufanikiwa kusawazisha baada ya Straika wao kukatiza mbele ya Mabeki wa Kagondo Fc na kusawazisha bao na kufanya bao kuwa 2-2 na mtanange kumalizika kwa dakika 90 kwa kutoshana nguvu kwa sare ya 2-2. Mikwaju ndio iliamua nani anakwenda hatua ya Nusu Fainali kati ya Kagondo Fc na Ijuganyondo Fc. Timu ya Ijuganyondo ilikosa penati mbili na timu ya Kagondo Fc kukosa mmoja ambapo timu ya Kagondo iliibuka na Ushindi kwa  Mikwaju ya penati 4-3 na kujikatia tiketi ya kwenda Nusu fainali katika Michuano hii ya Ligi ya Kagasheki.
Mpaka sasa katika timu nane tayari timu 3 zimeishatinga hatua hiyo ya Nusu Fainali ambazo ni Mabingwa watetezi Bilele Fc, Miembeni Fc, Kagondo Fc. Kesho ni kati ya  Rwamishenye vs Kitendaguro kutafuta timu ambayo itakamilisha timu nne za kucheza Nusu Fainali. Ambapo Mshindi wa Kesho anatarajiwa kucheza na mshindi wa leo Kagaondo Fc.

Kipa Yassin Issa wa Ijuganyondo akidaka kwa uzuri kona
Mashabiki Jukwaa kuu furaha tupu baada ya timu zote kutoshana nguvu ya 2-2
Kamera Jukwaa kuu ikitafuta tamasamu za mashabiki

Habari zifike na Nyumbani

Taswira jukwaa Kuu wakitazama soka
Wakati huo zikiwa 2-2 hakuna aliyetaka mpira utue chini...
Wachezaji wa Timu ya Kagondo Fc wakimpongeza mchezaji wao aliyewapa ushindi wa kwenda hatua ya Nusu fainali Abdallatifu Khamis juu kwa juu.
Ilikuwa Shangwe leo, Huku mashabiki wa Ijuganyondo Fc wakibaki midomo wazi kuona Timu yao inaondolewa katika Michuano hii ambako walikuwa wanaipa Matumaini tangu kipindi cha kwanza kusonga hatua ya Nusu Fainali.
Mashabiki wa Kagondo Fc wakiwa wamembeba aliyewapeleka katika hatua ya Nusu Fainali
Ushindi raha tupu!!


Sunday, 27 July 2014

KASHAI FC WATUPWA NJE KWA MIKWAJU YA PENATI (5-4) NA TIMU YA MIEMBENI FC KAGASHEKI CUP, MIEMBENI WASONGA HATUA YA ROBO FAINALI!

Na Faustine Ruta, Bukoba
TIMU ya Kashai Fc maarufu kama Abanyaruganda imetupwa nje ya Mashindano ya Ligi ya Kagasheki leo kwenye Hatua ya Robo fainali baada ya kutoshana nguvu ya bao 1-1 na timu ya Miembeni. Kipindi cha kwanza kilimalizika ya bila kufungana. Timu ya Kashai ndio ilianza kupata bao katika kipindi cha pili kupitia mchezaji wake Shamte Odilo na wao Miembeni kusawazisha bao kupitia kwa Rashid Mandawa katika kipindi hicho hicho cha pili na mtanange kumalizika kwa dakika 90 kwa sare ya bao 1-1 na hatimaye Mtanange kwenda kwenye Mikwaju ya penati ambayo timu ya Miembeni imeibuka kidedea kwa penati 5-4. Ushindi huu wa Timu ya Miembeni unawakutanisha na Mabingwa watetezi Bilele Fc walioshinda jana bao 1-0 timu ya Kahororo na sasa watakutana katika Nusu Fainali wiki Ijayo kati ya Bilele Fc na Miembeni walioshinda leo.

Patashika kwenye lango la Miembeni Fc

Jackson (kulia) akimwesabu Msengi Gerard wa Kashai katika kipindi cha kwanza

Hapa hukatizi!

Mchezaji wa Miembeni Jackson Kanywa kwenye mbio za kutaka kumtoka mchezaji wa Kashai Fc.

Kipindi cha pili lango la Timu ya Miembeni liliandamwa sana na kupata bao lao

Mtanange ulikuwa wa kasi sana kipindi cha kwanza kila timu ikipania kumfunga mwenzake, Kitu ambacho katika kipindi hicho cha kwanza hakuna aliyeliona lango la Mwenzake.Ilikuwa ni Ngoma na Nyimbo kwa Mashabiki hawa wa Kashai maarufu AbanyarugandaMizuka ya Mashabiki wa Kashai Fc wakiipamba timu yao leo kwenye mchezo wake wa Robo Fainali dhidi ya timu ya Miembeni FcViongozi wakiwa Jukwaa Kuu wakitazama Mtanange kati ya Kashai Fc vs Miembeni Fc, wa pili kutoka kulia ni Bw. Ernest Nyambo.Mashabiki Jukwaa kuu wakitazama Mtanange!Mashabiki wa Kashai wakiishangilia timu yao leo hii ambayo imetupwa nje kwa mikwaju ya penati baada ya kuchezea sare ya 1-1 za dakika 90.Kisa Mwamuzi Mshika kibendera alinyanyua kuashiria kuotea huku wachezaji wa Miembeni wakipingana nae!!kabla ya Timu ya Mimbeni hawajapata bao walikwaruzana na Mwamuzi wa pembeni mshika kibendera..Wachezaji wa Miembeni wakishangilia bao lao la kusawazisha lililotiwa kimiani na Rashid MandawaWachezaji wa Miembeni wakicheza Muziki baada ya kusawazisha bao katika kipindi cha pili kwa kufanya 1-1 ndani ya dakika 90.Ilikuwa ni staili ya aina yake kushangilia Nyomi ya Mashabiki Uwanjani Kaitaba wakitazama Mechi ya leo hii kati ya Kashai Fc na MiembeniMashabiki wa Timu ya Kashai wakitokelezea!! Mashabiki wakitazama Kipute cha leo hiiKatika Michuano hii ya Ligi ya Kagasheki 2014 Kata ya Kashai ndio huwa na Mashabiki wengi