Tuesday, 15 July 2014

TBC YAFANYA HAFLA YA KUHITIMISHA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw. Clement Mshana (kulia) akiwakaribisha wageni walioalikwa katika hafla ya kuhitimisha michuano ya kombe la dunia 2014 iliyofanyika jana Julai 12, 2014 katika ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam. 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante ole Gabriel, akiongea machache katika hafla ya kuhitimisha michuano ya kombe la dunia 2014 iliyofanyika jana Julai 12, 2014 katika ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante ole Gabriel, akimkaribisha Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Mhe. Juma Nkamia ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kuhitimisha michuano ya kombe la dunia 2014 iliyofanyika jana Julai 12, 2014 katika ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam. 
Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia akiongea akiongea katika hafla ya kuhitimisha michuano ya kombe la dunia 2014 iliyofanyika jana Julai 12, 2014 katika ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam. 

Mshehereshaji wa Hafla hiyo Elisha Elia akiongea machache.
Rais wa Bongo Movie, Steve Nyerere akitoa shukrani zake kwa niaba ya wasanii katika hafla ya kuhitimisha michuano ya kombe la dunia 2014 iliyofanyika jana Julai 12, 2014 katika ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Ommy Dimpoz akiongea machache hafla ya kuhitimisha michuano ya kombe la dunia 2014 iliyofanyika jana Julai 12, 2014 katika ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam. 
Kutoka kushoto ni Mboni Masimba, Mbunge wa Temeke Mh. Abbas Mtemvu pamoja na mchambuzi wa Mpira Manara katika hafla ya kuhitimisha michuano ya kombe la dunia 2014 iliyofanyika jana Julai 12, 2014 katika ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam. 
Wasanii walioalikwa wakipakua chakula (futari) iliyoandaliwa katika hafla hiyo.
Wasanii mbali mbali walioungana katika hafla hiyo wakipata futari.
Wafanyakazi wa TBC hawakuwa nyuma kujipongeza kwa kazi nzuri waliyoifanya.
Wasanii wakifurahia jambo na Mchambuzi wa Mpira, Mw. Kashasha.
Msanii JB akiongea na Mchambuzi wa Mpira wa Miguu, Mwl. Kashasha.
Wasanii wakijadili mambo.
Dokta Cheni akishow love.
Mw. Kashasha nae alikuwepo.
Meza kuu kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw. Clement Mshana, Mbunge wa Temeke Mhe. Abbas Mtemvu, Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia pamoja na Mdau mkubwa wa Michezo, Juma Kipingu wakifuatilia mpira wa fainali ya kombe la dunia 2014, kati ya Argentina na Ujerumani
Wasanii wakifuatilia kwa makini mpira huo.
Wafanyakazi wa TBC nao hawakuwa nyuma.
Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wakipongezwa kwa kazi waliyoifanya.
Picha ya pamoja ya viongozi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)  na wakurugenzi wa bodi.

.NAIBU WAZIRI WA MAJI, AMOS MAKALLA AWANASA WEZI WA MAJI DAR NA KUTANGAZA KUFILISI MALI ZAO


Meneja Mkuu wa Kampuni ya ufyatuaji matofali ya Ujenzi Solutions, ya Kimara kwa Msuguri, Dar es Salaam, Rahim Hamis na mfanyabiashara wa kampuni isiyo na jina, Credo Rajab (kulia) wakiwa chini ya uliznzi wa Polisi huku wakiwa wamevishwa pingu baada Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla kuamuru kuwakamata alipokagua viwanda vyao vya ufyatuaji na kugundulika kuwa wanatumia maji isivyo halali kwa kujiunganishia kwenye bomba kuu la Mamlaka ya Maji Safi na Taka Dar  ws Salaam (DAWASA).

 Makalla ambaye alifanya ziara ya kukagua maendeleo ya upanuzi wa Matambo wa Maji wa Ruvu Juu, Mlandizi, mkoani Pwani , pia alifanya msako wa kushitukiza kwa kampuni hizo.
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (kulia) akijaribu kuendesha katapila la Kampuni ya Ujenzi ya VA Tech Wabag Ltd, alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya upanuzi wa Mitambo ya Maji ya Ruvu Juu, Mlandizi, mkoani Pwani .Katikati ni Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaa na Meneja Mradi wa kampuni hiyo, Pintu Dutta.
Askari wa FFU wakilinda doria katika kiwanda cha ufatuaji tofali cha Ujenzi Solutions, Kimara Dar es Salaam
Moja ya mabomba linalodaiwa kuunganishwa kiholela kwenye bomba kuu la Ruvu Juu linaloleta maji  mjini na kampuni ya Ujenzi Solutions eneo la Kimara
Makalla akizungumza mbele ya Lori la Maji lililokamatwa likijazwa maji yanayodaiwa kuwa ya Dawass, katika kiwanda cha matofali cha Ujenzi Solutions
Pumpu iliyonaswa na Dawasa ikinyonyonya maji kutoka bomba kuu la Ruvu Juu eneo la Ubungo, Dar es Salaam
Makalla akiondoka katika kiwanda cha matofali cha Moto ambacho alisitisha shguli zake baada ya kubainika wakiiba maji ya Dawasa eneo la Ubungo.
Ramani ya upanuzi wa Mtambo wa Maji wa Ruvu Juu, eneo la Mlandizi, Pwanik.
Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaa akijaribu kuendesha katapila la Kampuni ya Wagani ambayo imepewa tenda ya upanuzi wa Mtambo wa Maji wa Ruvu Juu.
Makalla (wa pili kushoto) Mbunge wa Kihaha Vijijini, Hamoud Jumaa ( wa pili kulia) na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Halima Kihemba kulia, wakikagua ujenzi wa upanuzi wa mtambo huo. Picha na Richard Mwaikenda


 Na Richard Mwaikenda
NAIBU Waziri wa  Maji, Amos Makalla amezifungia kampuni tatu za ufyatuaji tofali kuendesha shughuli baada ya kubainika  kujiunganishia isivyo halali maji kutoka kwenye bomba kuu la Mamlaka ya Maji Safi na Taka (DAWASA), wakati wa ukaguzi wa kushitukiza alioufanya leo katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Makalla aliamuru viongozi wa kampuni  hizo wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa hatua zaidi, ambapo pia aliagiza mali zote za kampuni hizo zifilisiwe ili zitumike kulipa fidia kwa hasara kubwa iliyoingizia Serikali.
Akiwa katika ukaguzi huo, Makala aligundua madudu mengi yanayofanywa na kampuni hizo, ambazo zimejiunganishia maji kwa ajili ya kufyatulia matofali na kuuza kwa kutumia malori. 
Kampuni alizozikagua leo na kukutwa na dhahama hiyo ni; Moto iliyopo mita chache kutoka Makao Makuu ya Wizara ya Maji, Ubungo Dar es Salaam, Ujenzi Solutions iliyopo Kimara kwa Msuguri pamoja na kampuni isiyo na jina iliyopo pia Kimara kwa Msuguri.
Kabla ya kufika katika kampuni hizo, ulinzi wa Polisi wenye silaha ulikuwa umeimarishwa, ambapo Makalla alitoa agizo kwamba wasiondoke katika maeneo hayo ili wahusika na wafanyakazi wao wasiendelee na kazi yoyote.
Katika kampuni ya Moto, ilikutwa pampu ikiendelea na kazi ya kuvuta maji ambapo Msimamizi wa kampuni hiyo, Frederick Tarimo alikana kuiba maji kwenye bomba la Dawasa na kudai kwamba maji hayo wanayatoa kutoka kwenye mto. 
Tarimo alisema kuwa hutumia lita 3000 za maji kwa siku, ambapo hufyatua matofali kati ya 1500 na 2000 kwa siku. Pia huuza kwa siku kiasi cha matofali kama hayo. Kila tofari huuzwa kati ya sh. 800 na 1000. Alisema kuwa endapo hatofanya kazi kwa muda wa mwezi mmoja ataingia hasara ya sh. mil. 90, hivyo kila siku kupata hasara ya sh. mil. 3.
Naye Meneja wa kampuni ya Ujenzi Solutions, Rahim Hamis, alikana katakata kwamba maji wanayoyatumia wameunganisha kutoka kwenye bomba la Dawasa, bali wanatumia maji kutoka kwenye bwawa dogo lililopo jirani na kampuni yao. Pia katika eneo hilo lilikamatwa lori  aina ya Isuzu namba 957 AJK likijazwa maji. 
Viongozi waliokamatwa ni Frederck Tarimo ambaye alijitaja kuwa msimamizi wa kampuni ya Moto, Meneja Mkuu wa kampuni ya Ujenzi Solutions, Rahim Hamis na Credo Rajab mmiliki wa kampuni aliyodai haina jina.
Makalla, alisema ili kupambana na wezi wa maji, haina budi sasa kupeleka mswada bungeni ili watungiwe sheria ya uhujumu uchumi pamoja na kutoa adhabu kali ikiwemo ya kutaifisha mali zao, tofauti na adhabu wanayopewa sasa ya kulipishwa faini ya sh, mil 2.
Katika ziara hiyo pia alifanya ukaguzi wa matanki ya kuhifadhia maji ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambapo alijionea jinsi maji yalivyopungua kwenye matanki hayo ambayo pia yapo kwenye maandalizi ya kufanyiwa ukarabati mkubwa ili yafae kwa ajili ya hifadhi ya maji kutoka bomba la Ruvu Chini ambalo upanuzi wake umekamilika.
Pia alitembelea kuona maendeleo ya upanuzi wa Mtambo wa Maji wa Ruvu Juu, Chalinze, Mkoa wa Pwani. kesho anaendelea tena na ziara kama hiyo katika Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.

Sunday, 13 July 2014

UTENGENEZAJI WA VIDEO YA WIMBO WA KIPI SIJASIKIA WA PROF JAY NA DIAMOND UNAENDELEA CHINI YA NEXT LEVEL


 Msanii mkongwe kwenye game la Bongo Fleva anajulikana kwa jina la Prof Jay leo mchana alikuwa akishoot video yake mpya aliyomshirikisha Diamond inaitwa KIPI SIJASIKIA. Video hiyo iliyokuwa ikishutiwa pale Sinza Makaburini ilipo Mahakama. Video imesimamiwa wa Dir Adam Juma kutoka Next Level
 Diamond kama wakili wa Profesa J